Ulifanyaje kukabiliana na maumivu ya mapenzi?

Ulifanyaje kukabiliana na maumivu ya mapenzi?

Haswaa nimepona.
Kwanza ni kukubaliana na matokeo.
Pili, me nilifuta access zote asinipate hewana wala kuniona japo tupo mbalimbali.
Tatu, nilijenga mtazamo na dhana mpya kuwa kuna wenzake waliomzidi ktk mambo mengi na kwamba nitakutana nao.
Pia niliwaza,huwezi jua Mungu amekuepusha na nini.
Haya ni baadhi
sawa....nimekuelewa mkuu....ila nakuomba utuhadithie kilichotokea...
 
samahani kaka nimeona juu hapo kuna mdada...keshapatikana changamkia si ajabu siku za usoni katualika...mimi nitachangia tena kadi yangu nataka iwe maalum VIP
[emoji50] [emoji50] [emoji50] [emoji50] yan ushaenda hadi kwenye mrejesho wa tatu.... Mmmh[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mkuu songa mbele... mm yalinkuta kama yako ila mm nimeweza kupotezea na kuendelea na maisha...
Nilikuwa nae kwa miaka saba tangu 2009... ila ilipofka 2013 mwishon akapata kazi mkoani mimi nikiwa bado hapa mjini...
Mapenz yaliendelea lakini yakaanza ukakasi wa dharau na u busy usio na maana.. tukaloweka chini... tukaongea akaelewa kosa akaniomba msamaha nikamsamehe..
Ila tabia ni ngumu kubadilika... akawa msiri sana wa vitu vyake hata simu yake bila mimi kumuomba unaona kabisa anaificha au kuizima tukiwa pamoja.
Ilipofika 2016 nikatangaza kumchumbia, yani mahari na kila kitu... hapo ndo mwenzagu akaniambia nisijisumbue maana muda mrefu aliniomba tufunge ndoa mm sikuwa tayar na yy tayar kashampata mwengine hukohuko mkoan na tayar nyumban kwao kashawaambia kuwa ameshaachana na mm na ana mtu mwengine.
Kwa kweli niliumia sana plus wanasema hakuna mwanaume asiye na mchepuko...ila mimi sikuwa hivyo..
Hivyo nikavumilia ingawa nilipata mshtuko sana maana nilijiandaa kweli kweli nikitegemea mwez wa tatu 2017 namweka ndani... maana kipind namwambia kuhusu engangement tayar nilishanunua jiwe la tanzanite kwa ajili ya pete yake...

Ila now niko poa namshukuru Mungu, sala, mazoezi na u busy wa kazi vimenipa tena amani... hivyo ipo siku utapata akupendae kwa dhati na huyo utamsahau kabisa...
"There is no a song which doesnt have a dancer"
..Pole Sana Mkuu,..
 
Mkuu eddy ni hatariiii,nikikusimulia utalia huo mkasa wangu.
Nililazwa na kupigwa drip sita wakati sina ugonjwa wowote.
Lakini ulifika muda nikaona upuuzi tu.Nikasonga na maisha yng na nimesimama ingawa anapiga sn simu.
AMINI INAWEZEKANA KABISA KUSAHAU HATA KAMA ULIKUWA UNAMPENDA KIASI GANI.
..Tamuu weka ile Avatar yako ya Zamani,..
 
Kile unachotakiwa ujifunze kuhusu mapenzi ni kutouweka moyo wako rehani,kupenda ni jambo zuri lakin huwa ni baya pale ambapo umpendae anapoanza kuleta pozi
Hivyo njia ilio bora nikujiandaa mapema kisaikolojia
Anza kufikiria namna unavyoweza kuishi bila yeye wakati bado mapenzi yako motomoto hii itakusaidia kutokupata maumivu sana pindi mtakapoachana,maana uliandaa mazingira mapema.....
Don't be a mad of love....you will regret forever...
 
Kiukweli Mimi nlikabiriana na maumivu ya mapenzi kwa kuanza kupiga,nyeto,kuvuta bhangi kunywa Pombe na jioni kufanya mazoezi then narudi ghetto napika msoc wa nguvu huku naskiliza music kwa mbaaali then naoga nazama kitandani kushtua asubuhi hiyo nlifanya hivi kwa mwezi mmoja nkamsahau yule mwanamke na tangu hapo nimepambana Sana na maumivu ya mapenzi na nimeshinda mara zote
Duh sasa huku si kujitesa??
 
1.Nilikuwa na marafiki wacheshi na supportive,aina ya marafiki ambao unaweza kuwaambia matatizo yako wakakupa ushauri na kukuliwaza,kukuchangamsha na kukufanya usijiskie mwepeke.
2.Kukubali hali halisi.mapenzi samtaimz ni upofu,ukishapenda mtu ile too much,hata akili inashindwa kufanya reasoning na logical thinking.Unakuta mtu hakutaki na kashaonyesha dalili zote za kutaka kutengana na wewe chaajabu wewe hutaki kukubali ukweli hapo ndipo maumivu yanapoanzia.Mimi nliamua kukubaliana na hali halisi kwamba sina changu na wala hakuna haja ya kupoteza muda kufosi mapenzi
3.Bangi.Kwenye mjani kuna kemikali inaitwa "dont give a damn",aisee ukiwa na stelesi ukanyonga highgrade yako ya kibabe ukawasha, ukableiz uka inhale kisha uka exhale basi matatizo yoote yanakuwa trivial.unalala usingizi mwororo kama katoto kadogo.
3.Moving on.nliamua kujikeep busy na mambo mengine ya msingi,sikujiruhusu kuwa idle hata dakika moja mchana mishemishe nkitoka naingia gym,ama basketball court napiga hoops zangu za kutosha na one to one nkitoka hapo hoi kulala.baada ya muda nkatafuta kiburudisho chengine kika kaimu nafasi.
Ila yule mwanamke nilimpenda jamani,yaan nkijifikiria najiona nlikuwa zuzu sema ndo hivyo haikuwa fungu langu and I have no regrets.kila kitu kinatokea kwa sababu maalumu.
 
80f2cbaa8f05cf523cd439c32252dbe2.jpg
 
Sitasahau 5/12/2014 cku ya ijumaa saa 5 ucku ckumbuki na dakika ngapi naongea nae namuuliza "ndio hunitaki tena? anajibu kwa kujiamini kabisa " sikutaki na sikupendi" hpo anaongea ypo ghetto kwa jamaa aliyetoa barua kwao enzi hzo nimemaliza chuo no direction miaka 3 nimesugua mtaani napga dili ndogo ndogo tu kilikuwa kpnd kigumu kiukweli ila kwa mwanaume rijali its not ishu sana huja na kupita alikaa mwaka 1 tu hakuna ndoa wala nn 2015 akantafuta anataka kurudi hpo keshapata taarifa nimeajiriwa mkoa flan yaani nnachomfanya hata ibilisi hapendi kuna watu tunajua visasi bhana!
Mkuu nimeipenda hiyo
 
Nyimbo yangu kubwa ilikuwa "miss u die" ya psquare nauskiza kutwa nzma nalia tu ghetto nkitoka nje naongea fresh nacheka nkirudi ndani navuta picha ule mshepu na michezo alokuwa ananipa ile ina maana ndio anampa jamaa saa hz? bc dah...chozi linateremka bila kutaka simsahau yle mtt mungu amjaalie kila la kheri hko aliko sitafurahia nkimkuta ana hali mbaya kimaisha nlimpenda sana dua zng na zimfikie kuachana co vita!
Huo ndo uanaume
 
Nimeshaumia sana kwenye mapenzi, lakini namshukuru Mungu huwa nasahau haraka sanaa, halafu na take it easy though siyo rahisi kihivyo lakini naiaminisha nafsi yangu kwamba i deserve much better, N maisha siku zote yanatupa nafasi nyingine ya kufanya vizuri zaidi hivyo nitapata mpenzi mwingine bora zaidi, mimi ni muumini wa ku let it go, hivyo i don't waste time pleasing sm1 nikiona drama mapema naku ignore, baba yangu alinijenga hivyo Mpende mtu lakini pia ipende nafsi yako zaidi na kuamini utapata kilicho bora, kwangu mbinu rahisi ya kumsahau mpenzi ni pale hisia zinapotaka kurudi najaribu kukumbuka mabaya yake tu aliyowahi nifanyia, hivyo na kuona hakuna haja ya kurudi nyema tena kwani hanifai
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom