X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,117
Mapenzi tumeyakuta, lakini ubaya ni kuwa hakuna mtu aliye wahi kufundishwa somo la mapenzi wengi watakubaliana nalo hilo kuwa hakuna somo la mapenzi, lakini hali ni tofauti somo la mapenzi lipo lakini kipindi kile unapokuwa unafundishwa hilo somo akili huwa inajua kuwa upo kwenye somo lakini upeo unakuwa hauelewi.
ni wengi tumesha wahi kulia kwa ajili ya mahusiano, yupo yule kijana mtanashati/mrembo ulimpenda, ulimvumilia kwenye shida leo amepata amekuacha ukiwa bado unampenda, umekaa ndani unalia hakuna wakukufuta machozi. moyo wako unakuuma ukikumbuka raha na shida mlizopitia pamoja kiasi mkaapiana kuwa kamwe kifo ndicho kitakacho watenganisha imekuaje leo sheteni mbaya ameingilia kati mahusiano yenu?
somo kubwa tunalopata kwenye mahusiano ni maumivu, mtu hupitia kwenye maumivu kama vile mtoto anapopokea adhabu ya viboko kwaajili ya kosa fulani alilolifanya. hivyo maumivu katika mahusiano huja kama somo ukifaulu vyema hutapata tena maumivu.
lakini wengine hufeli huu mtihani wa maumivu ya mapenzi wengi hujikuta wamezizuru nafsi zao kwa kujinyonga hadi kupoteza uhai, au pengine kunywa sumu,
maumivu ya mapenzi yanauma vibaya asikwambie mtu, na mtu aliye katika maumivu haya uwa kwenye hali ya kupungukiwa akili {ukichaa}, kichaa wa mapenzi ni kicha mbaya zaidi ya vichaa wote, hato msikia baba, mama wala ndugu yeyote.
mimi nilishawahi kuumizwa kwenye mapenzi, niliferi vibaya mitihani yangu kisa mapenzi sikuwahi kuamini kuwa yule niliyempenda kweli mbali na mimi ameenda...? nilijifunza kumsahau nikaidanganya akili yangu akili imekubari kuwa yule si msichana wa kunifaa lakini nimejikuta nashindwa kumsahau kabisa
ni miaka mitano sasa imepita...uwezi kuamini kuwa kipindi hiki chote cha miaka mitano sina mawasiriano naye lakini bado naamini kuwa ipo siku atarudi,
nilianza kusoma vitabu mbali mbali, nilijifunza kuimba na kusikiliza mziki, nilijifunza kuogelea niliituma akili yangu kuwaza mafanikio, nilitumia muda wangu mwingi sana kutembelea mitandao mbali mbali hiyo yote niliifanya ili tu nitoke kwenye ukichaa wa mapenzi, kwa kuwa sijamsahau na bado naamini atarudi hivyo nahisi sijapona,
Niliumizwa kwa muda mrefu kidogo na yote ilikuwa ni kwa sababu nilikuwa nikimpenda ex wangu kwa dhati kabisa kwa kuwa ni mtu aliyenitoa mbali sana kwa kipindi niko kwenye wakati mgumu sana yeye pekee ndiye aliyenishika mkono bila kujali nini wala nini. sitaacha kuukumbuka wema wake mpaka nafukiwa kaburini nasema kweli na Mungu ananiona ingawa aliniumiza mno kuliko mtu mwingine yeyote katika maisha yangu. amenipitisha kwenye maumivu makali ambayo sikuwahi kutegemea kama nitakuja yapitia siku moja. jamani nikisema kumpenda mtu kwa dhati kabisa halafu anakuumiza nafikiri kwa anaejua hiyo situation anajua nini namaanisha.
maana nilikuwa nae kwa miaka mingi kidogo na sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine yeyote akati nipo nae.nilikuwa mwaminifu sana kwake kwa kuwa nilimpenda kuliko kawaida.ingawa ameniumiza lakini haki yake nampa.'amenionyesha mwanga mkubwa sana katika maisha.
Huwa sijutii kumfahamu hata kwa bahati mbaya. ingawa kabla sijafikia uamuzi wa kusema sijutii kumfahamu,nilikuwa nikimchukia kuliko mtu mwingine yeyote. unajua kwanini niliamua kuyafuta machukizo yote, nikwa sababu niliamua kukimbilia kanisani ingawa nilikuwa nikikumbana na changamoto za baadhi ya marafiki zangu kuwa niende kwa waganga wa kienyeji. kweli ilikuwa kidogo kuchanganyikiwa lakini niliamini Mungu pekee ndiye mwenye kunijua mimi na hatma yangu na kwanini nayapitia haya. na ili nizungumze na Mungu na kuyajibu maombi yangu ilikuwa ni lazima kumsamehe ingawa ilikuwa ni ngumu mnooo..lakini nilimsamehe.
Ninamshukuru sana kwa kuniumiza.*ninakushukuru sana kwa kuniumiza na kunipitisha katika yale maumivu*.wapendwa,maumivu yake yamenijenga mno!yamenifanya niwajue watu,yamenifanya nimjue Mungu kuliko nilivyokuwa nikimjua kuwa yupo katika maisha yetu anaishi ni sisi kumkaribisha tu.
Back to the point kuwa nilifanyaje kwa mwenye uzi..niliukimbilia msalaba.natumai nimekujibu.asante.
Mnajuwa Nature is the RIGHT answear! siku zote ukiona sehemu kuna milima basi ujuwe kuna sehemu nyingine kuna mabonde, ukiona mtu ana faraja basi elewa kuna mwingine anayo huzuni, ukiona leo umepata wa kukupoza moyo fahamu kuna mtu ameumizwa kwa raha kama hiyo unayoipata kwa wakati huo upande wake. Nature huwa ina balance all of these things.Ukiumizwa jipe muda kwani ujuwe kuna mtu bora anajiandaa kuja kwako ila wewe unamchelesha kwa kung'ang'ania mtuuu ambaye tayari hayuko kichani kwako. VUMILIA ILI UPATE MEMA.
Huwa sitaki hata kukumbuka
sijawahi kuumia kama wakati ule
Nililia mfululizo kwa miezi 9 kila siku natoa chozi
Niliisha kwa mawazo
Nilipauka kama naumwa
Nakumbuka kaka aliniita akanambia mdogo wangu ni takribani mwaka sasa kila siku kilio Kwanini?
Hivi unajua kama hata ukilia yeye haoni chozi lako
Kwanini ulie kiasi hiki?
NiliShukuru Mungu nikafuta machozi
Kisha nikajipanga upya
Kuna watu wanafiwa na bado wanasahau
Nilipata nguvu mpya nikaona ni kweli natakiwa kumove on
Nimezoea na maisha yanasonga
Mkuu songa mbele... mimi yalinikuta kama yako ila mimi nimeweza kupotezea na kuendelea na maisha...
Nilikuwa nae kwa miaka saba tangu 2009... ila ilipofika 2013 mwishon akapata kazi mkoani mimi nikiwa bado hapa mjini...
Mapenzi yaliendelea lakini yakaanza ukakasi wa dharau na u busy usio na maana.. tukaloweka chini... tukaongea akaelewa kosa akaniomba msamaha nikamsamehe..
Ila tabia ni ngumu kubadilika... akawa msiri sana wa vitu vyake hata simu yake bila mimi kumuomba unaona kabisa anaificha au kuizima tukiwa pamoja.
Ilipofika 2016 nikatangaza kumchumbia, yani mahari na kila kitu... hapo ndo mwenzagu akaniambia nisijisumbue maana muda mrefu aliniomba tufunge ndoa mimi sikuwa tayari na yeye tayari kashampata mwengine hukohuko mkoani na tayari nyumbani kwao kashawaambia kuwa amesha achana na mimi na ana mtu mwengine.
Kwa kweli niliumia sana plus wanasema hakuna mwanaume asiye na mchepuko...ila mimi sikuwa hivyo..
Hivyo nikavumilia ingawa nilipata mshituko sana maana nilijiandaa kweli kweli nikitegemea mwezi wa tatu 2017 namuweka ndani... maana kipindi namwambia kuhusu engangement tayari nilishanunua jiwe la tanzanite kwa ajili ya pete yake...
Ila now niko poa namshukuru Mungu, sala, mazoezi na u busy wa kazi vimenipa tena amani... hivyo ipo siku utapata akupendae kwa dhati na huyo utamsahau kabisa...
"There is no a song which doesn’t have a dancer"
je wewe ulitumia mbinu gani kukabiliana na amaumivu ya Mapenzi...? kidonda chako cha mapenzi ulikitibu kwa dawa gani...?
je kilipona kabisa au bado kina maumivu kila kikitoneshwa...?
je kumebaki kovu ambalo kila ukiliona huwa huishi kumkumbuka yule aliye kuumiza..?
changia mawazo yako wengine wajifunze...