Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Natumaini nikimaliza mwezi wa tatu bila kilaji ndio nimeacha hivyo, kuna mdau humu alitoa ushauri mzuri sana juu ya pombe, me bado naiongele na nakaa na walevi sema sigusi kabisa nakula maji tu lengo baada ya muda nione kitu cha kawaida na hakina maana kabisa. Pombe ni mbaya sana nilikosea watu heshima na kuwa mtu wa hovyo sana. Uzi mzuri sana huu.
Mkuu upo kwenye maumivu kama yangu,ila nimeanza kuzoea nakaa na wanywaji muda mrefu naona kitu cha kawaida,japo siku za mwanzo ilikua shida nilikua nashinda na marafiki wasiokunywa pombe,kwa sasa nashinda na walevi tunakula wote nyama mpaka usiku sana mi ni juisi na maji
 
1.Timotheo 5:23
"Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara "
HILO NDILO NENO LA BWANA HALLELUYAH!!!!
 
Naandika ujumbe huu kwa msukumo mkubwa baada ya uchunguzi nilioufanya na kujiridhisha.
Vifo vingi vya vijana au wababa walio chini ya miaka 50 vinadababishwa na tabia hizi kuu 2 ambazo ni ulevi na uesherati au uzinzi.
Kijana mzinzi au mhesharati ana asilimia kubwa sana ya kufa mapema zaidi ya kijana ambaye ni mwaminifu katika ndoa yake au ni rahisi kijana mzinzi na mhesharati kufa mapema kuliko kijana ambaye hayuko ndani ya ndoa ila anaulinda mwili wake, hapa simaanishi kuwa anaulinda kwa kutumia kondomu.
Wengi wamekufa kwa magonjwa na wengine wamekufa kwa sababu zingine ila chanzo ni uzinzi na uesharati.
Tabia ya pili inayoua vijana kwa kasi ni ulevi, ulevi wa pombe na starehe zingine zinazofanana na ulevi. Nimeona vijana wengi wakifa kwa ajali, kupigana hadi kifo n.k kwaajili ya ulevi.
Nathubutu kusema kuwa kama ulevi na uzinzi kijana unavifanyia fahari jua kuwa uko katika mstari mwekundu na kinachosubiriwa ni zamu tu.
Simuhukumu mtu humu na wala sijipendekezi kwa mtu yeyote kwani hakuna anayenijua humu na hakuna ninayemjua au kumfahamu, ila ninachokifanya ni kuonyesha upendo kwa vijana wenzangu.
Asante kwa wewe unayesoma na kwa utakayeleta kejeli mimi nakusihi endelea na tabia hizo ila usisahau kuwa zamu yako i karibu.
Moderator mmeuhamisha na kuunganisha uzi wangu na uzi huu, uzi wangu umebeba 2 themes(ulevi na uzinzi) while huu umebase kwenye ulevi tu deeply.
Mbona nyuzi nyingi za Dr. Shika na matukio mengine yanayofanana zinakuwaga nyingi tu.
Sio poa, mtuache tutumie jukwaa hili. Jf mbona tamu sana ila kuna wachache mnaibana kana kwamba hamna ndoto
kuifanya internationally.
Mimi huo mwingine
Twende kazini.
 
mbona umetaja hasara tuu,BY THE WAY WALEVI NDIO HUISHI MIAKA MINGI KULIKO UPANDE WA PILI ,jiongeze acha kujibania rahaaa za dunia mkuu PIGA KWA AFYAA YAKOOO
Ulevi hauna faida achana nao.
 
Mkuu upo kwenye maumivu kama yangu,ila nimeanza kuzoea nakaa na wanywaji muda mrefu naona kitu cha kawaida,japo siku za mwanzo ilikua shida nilikua nashinda na marafiki wasiokunywa pombe,kwa sasa nashinda na walevi tunakula wote nyama mpaka usiku sana mi ni juisi na maji
Wasaidie marafiki zako nao waache pombe.
 
Hata maji Yana madhara. Hivi wasiokunywa pombe hawaugui figo, maini, kisukari au kupata ajali? Akili za kiCCM hizi.
 
1.Timotheo 5:23
"Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara "
HILO NDILO NENO LA BWANA HALLELUYAH!!!!
Umelielewaje we mwanakwaya?
 
Hivi watu wakiacha pombe wakati pombe ni sehemu ambayo serikali yetu tukufu inategemea kodi yake hapo ili kuendesha serikali mnataka serikali ipate wapi kodi sasa??
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] sikuwahi kuwaza kama itatokea nyie Kaka zangu wa kuleee [emoji12] [emoji12] muiseme vibaya hii kitu aiseee.

Hivyo kodi itakosekana si eti eee. Hahahaaaa.
 
Mkuu upo kwenye maumivu kama yangu,ila nimeanza kuzoea nakaa na wanywaji muda mrefu naona kitu cha kawaida,japo siku za mwanzo ilikua shida nilikua nashinda na marafiki wasiokunywa pombe,kwa sasa nashinda na walevi tunakula wote nyama mpaka usiku sana mi ni juisi na maji
Safi sana kiongozi hii kitu sio nzuri kwa afya ya akili na mwili, mimi niligombana sana na wachumba coz akigusia tu kuacha pombe namuona hafai. Now hata nikienda batani anajua nipo vizuri na nnarudi bila vurugu.
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] sikuwahi kuwaza kama itatokea nyie Kaka zangu wa kuleee [emoji12] [emoji12] muiseme vibaya hii kitu aiseee.

Hivyo kodi itakosekana si eti eee. Hahahaaaa.
Hahahaa kabisaa serikali itakosa mapato dada! Karibu sana krismass nyumbani zitakuepo za kutosha.
 
Back
Top Bottom