Bohari ya Dawa (MSD) yashusha shehena ya dawa ya kuacha pombe

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,020
Reaction score
6,858
#𝗠𝗦𝗗 𝗬𝗔𝗜𝗡𝗚𝗜𝗭𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗡𝗜 𝗦𝗛𝗘𝗛𝗘𝗡𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗪𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗗𝐮webp-1.webp

Bohari ya Dawa (MSD) imeingiza nchini shehena ya kwanza ya Naltrexone, dawa inayotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa watu wenye tatizo hilo.

Uingizaji wa dawa hiyo umefanyika kupitia ushirikiano kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, katika mpango wa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya zinazotumika kudhibiti uraibu wa pombe nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya MSD iliyotolewa leo, Septemba 23, 2026, na Meneja Mawasiliano wa taasisi hiyo, Etty Kusiluka, Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Amesema MSD itaendelea na ununuzi wa dawa hiyo kwa ajili ya taasisi hiyo ili kuhakikisha inapatikana kwa wanaohitaji huduma.
#𝗠𝗦𝗗 𝗬𝗔𝗜𝗡𝗚𝗜𝗭𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜𝗡𝗜 𝗦𝗛𝗘𝗛𝗘𝗡𝗔 𝗬𝗔 𝗞𝗪𝗔𝗡𝗭𝗔 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗪𝗔 𝗬𝗔 𝗨𝗗𝐮webp.webp

Soma Pia: Dawa kuacha pombe kuwasili Tanzania

Naltrexone ni miongoni mwa dawa zinazotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe na inaweza kusaidia kupunguza hamu ya kunywa kwa baadhi ya wagonjwa inapotoa pamoja na ushauri nasaha na huduma nyingine za kitabibu.
 
View attachment 3676489

Bohari ya Dawa (MSD) imeingiza nchini shehena ya kwanza ya Naltrexone, dawa inayotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa watu wenye tatizo hilo.

Uingizaji wa dawa hiyo umefanyika kupitia ushirikiano kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, katika mpango wa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya zinazotumika kudhibiti uraibu wa pombe nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya MSD iliyotolewa leo, Septemba 23, 2026, na Meneja Mawasiliano wa taasisi hiyo, Etty Kusiluka, Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.

Amesema MSD itaendelea na ununuzi wa dawa hiyo kwa ajili ya taasisi hiyo ili kuhakikisha inapatikana kwa wanaohitaji huduma.
View attachment 3676490

Soma Pia: Dawa kuacha pombe kuwasili Tanzania

Naltrexone ni miongoni mwa dawa zinazotumika katika matibabu ya uraibu wa pombe na inaweza kusaidia kupunguza hamu ya kunywa kwa baadhi ya wagonjwa inapotoa pamoja na ushauri nasaha na huduma nyingine za kitabibu.
Dawa ni mtu mwenyewe akiamua izo dawa nikama external factors tuu mtu akishindwa kwa izo dawa anaweza kuwa sugu kabisa wa pombe
 
Back
Top Bottom