Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

madabadaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2017
Posts
288
Reaction score
178
Ulevi wa pombe ni ugonjwa unaoathiri watu wengi duniani. Kwa ulimwengu mzima,mamilioni ya watu wameathirika kwa njia moja ama nyingine kutokana na tatizo hili la ulevi wa pombe.

Pombe hupendwa na watu wengi na kuwepo kwake kumeanza tokea enzi za wahenga. Masimulizi ya pombe hupatikana ktk vitabu mbalimnali na hata Biblia imezungumzia na kuonya kuhusu ulevi wa pombe.

KWA NINI WATU
WANAVUTIKA KUNYWA
POMBE?

Sababu kubwa hasa huwa ni kutoa burudani kwa mtumiaji awapo ktk starehe zake za kila mara.
Ni kweli pombe isiponywewa kwa wingi ni kiburudisho, inaliwaza na kumfanya mtu achangamke, wakati mwingine watu hujiamini baada ya kunywa pombe.

POMBE IKINYWEWA
HUFANYA NINI MWILINI?

Pombe ikinywewa huingia tumboni, na baada ya muda hufika kichwani kwa kupitia kwenye mishipa ya damu. Matokeo Yale mtu huanza kuwa na furaha na kujiamini kwa muda.
Jinsi pombe inavyozidi kuingia tumboni ndivyo inavyozidi kuingia kwenye damu. Damu ikiwa na pombe nyingi hudhoofisha sehemu ya ubongo ambapo humfanya mtu kushindwa kupambanua jema na baya hata kumfanya aweze kujisaidia hadharani, kumtemea mate mwenzake nk.

AINA ZA POMBE.

Pombe zimegawanyika ktk sehemu tatu

1. Pombe Kali kiasi _ kama
bia, mbege nk.

2. Pombe Kali sana _ kama
vile divai.

3. Pombe Kali zaidi _ kama
vile whisky, gongo na
konyagi.

MADHARA YA ULEVI.

_ Kuugua magonjwa kama
kisukari, ugonjwa wa moyo,
utapiamlo , ini, kudhoofu akili,
na mwili, kusababisha ajali nk

Ni vizuri kutokunywa pombe kama hujaanza.
Na kama wewe ni mnywaji mahili tafuta msaada mapema.

Nawasilisha.
 
Muhudumu ongeza glass, maisha ndio haya haya! kwani uliumbwa uishi milele?
Je hizo figo, maini na firigisi unaenda nazo kaburini?
kama vipi si utoe uwape wanaohitaji?
Mhudumu ongeza glass weka wine, whisky, brand, banana, gongo weka mezani!
 
Pombe ni janga linalofungiwa macho na watu wengi Ila linaua vijana wengi sana na limeingiza wengi kwenye umasikini mkubwa wengi pia wamepoteza kazi au biashara zimefilisika Kwa ajili yo pombe.ikikukolea ni addiction mbaya Sanaa Ila inavituo vichache vya kusaidia waathirika
 
Natumaini nikimaliza mwezi wa tatu bila kilaji ndio nimeacha hivyo, kuna mdau humu alitoa ushauri mzuri sana juu ya pombe, me bado naiongele na nakaa na walevi sema sigusi kabisa nakula maji tu lengo baada ya muda nione kitu cha kawaida na hakina maana kabisa. Pombe ni mbaya sana nilikosea watu heshima na kuwa mtu wa hovyo sana. Uzi mzuri sana huu.
 
Natumaini nikimaliza mwezi wa tatu bila kilaji ndio nimeacha hivyo, kuna mdau humu alitoa ushauri mzuri sana juu ya pombe, me bado naiongele na nakaa na walevi sema sigusi kabisa nakula maji tu lengo baada ya muda nione kitu cha kawaida na hakina maana kabisa. Pombe ni mbaya sana nilikosea watu heshima na kuwa mtu wa hovyo sana. Uzi mzuri sana huu.
Pole mkuu...I can feel your pain
 
Hili bwege na halinacha zake hapa,hivi huo mshahara unaolipwa unatoka kwa baba yako?? Tbl ni mlioa kodi mkubwa hapa ila mnawapiga vita kila uchwao,muwaache kila mtu na starehe zake mbona wewe zinzi hatusemi au wewe huogopo ukimwi?? Mxuuu!! Shwain
 
Usitupangie cha kunywa mkuu. Walio na afya mbovu si wanywaji wa pombe tu.

[emoji482] [emoji482] [emoji482]
 
Muhudumu ongeza glass, maisha ndio haya haya! kwani uliumbwa uishi milele?
Je hizo figo, maini na firigisi unaenda nazo kaburini?
kama vipi si utoe uwape wanaohitaji?
Mhudumu ongeza glass weka wine, whisky, brand, banana, gongo weka mezani!
Kweli we pilipili kichaa [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Nadhani mleta mada ungekuja na hoja nzito na ya msingi kushawishi viwanda vya pombe vyote vifungwe, hio ingekuwa solution, haya mengine uliyoandika ni kelele za bahari haziwezi kuzuia safari ya mashua.
 
Hakuna kitu kisicho na madhara pale ukitumiapo pasipo kiasi, hivyo pombe ni sehemu ya vitu vingi sana vyenye madhara makubwa pale uvitumiapo pasipo mipaka.
Kweli mkuu, vyakula vyenyewe vinasababisha magonjwa vitumiwa vibaya.
 
Back
Top Bottom