Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Ulevi wa pombe ni hatari kwa afya yako

Usitupangie cha kunywa mkuu. Walio na afya mbovu si wanywaji wa pombe tu.

[emoji482] [emoji482] [emoji482]
Walio na afya mbovu zaidi ni walevi kama wewe, pona yako ni kuacha kunywa.
 
Nadhani mleta mada ungekuja na hoja nzito na ya msingi kushawishi viwanda vya pombe vyote vifungwe, hio ingekuwa solution, haya mengine uliyoandika ni kelele za bahari haziwezi kuzuia safari ya mashua.
Hakuna kelele hapa, bali nimeleta hii kitu kuonya
walevi.
Kuhusu viwanda, haviwezi kuacha Ama kuzuuliwa kuzalisha kwa kuwa serikali hupata fedha nyingi kutokana na ushuru wa mauzo.
 
Utakufa kabla ya wakati ukiwa Mlevi.
Kwani kuna wakati sahihi wa binadamu kufa?..... hivi unafahamu kuwa wanaokunywa pombe kwa * kiasi* huishi maisha marefu yenye furaha na afya njema kuliko wasiokunywa kabisa pombe?

Tunashauriwa tunywe kwa kipimo, ...... na kipimo cha pombe kila mtu ana chake kadili ya afya ya mnywaji, mfano binafsi", mimi huwa naweza kunywa castle light tano+ konyagi ndogo moja na nikadrive, mwingine kwa kipimo hicho unaweza mkuta mtaroni.
 
Nashukuru Mungu ni mwezi wa nne sasa tangu niache kunywa shetani nilikuwa na duka la kuuza pombe za jumla nashukuru nimemkataa shetani pamoja na kwamba nimeyumba Mungu ataninyanyua ki vingine PUMBAFU POMBE NENDA ZAKO KUZIMU
Ilo duka lutakua makunduchi zenji
 
Ulevi wa pombe ni ugonjwa unaoathiri watu wengi duniani. Kwa ulimwengu mzima,mamilioni ya watu wameathirika kwa njia moja ama nyingine kutokana na tatizo hili la ulevi wa pombe.

Pombe hupendwa na watu wengi na kuwepo kwake kumeanza tokea enzi za wahenga. Masimulizi ya pombe hupatikana ktk vitabu mbalimnali na hata Biblia imezungumzia na kuonya kuhusu ulevi wa pombe.

KWA NINI WATU
WANAVUTIKA KUNYWA
POMBE?

Sababu kubwa hasa huwa ni kutoa burudani kwa mtumiaji awapo ktk starehe zake za kila mara.
Ni kweli pombe isiponywewa kwa wingi ni kiburudisho, inaliwaza na kumfanya mtu achangamke, wakati mwingine watu hujiamini baada ya kunywa pombe.

POMBE IKINYWEWA
HUFANYA NINI MWILINI?

Pombe ikinywewa huingia tumboni, na baada ya muda hufika kichwani kwa kupitia kwenye mishipa ya damu. Matokeo Yale mtu huanza kuwa na furaha na kujiamini kwa muda.
Jinsi pombe inavyozidi kuingia tumboni ndivyo inavyozidi kuingia kwenye damu. Damu ikiwa na pombe nyingi hudhoofisha sehemu ya ubongo ambapo humfanya mtu kushindwa kupambanua jema na baya hata kumfanya aweze kujisaidia hadharani, kumtemea mate mwenzake nk.

AINA ZA POMBE.

Pombe zimegawanyika ktk sehemu tatu

1. Pombe Kali kiasi _ kama
bia, mbege nk.

2. Pombe Kali sana _ kama
vile divai.

3. Pombe Kali zaidi _ kama
vile whisky, gongo na
konyagi.

MADHARA YA ULEVI.

_ Kuugua magonjwa kama
kisukari, ugonjwa wa moyo,
utapiamlo , ini, kudhoofu akili,
na mwili, kusababisha ajali nk

Ni vizuri kutokunywa pombe kama hujaanza.
Na kama wewe ni mnywaji mahili tafuta msaada mapema.

Nawasilisha.
Ni kweli kabisa
 
Kwani kuna wakati sahihi wa binadamu kufa?..... hivi unafahamu kuwa wanaokunywa pombe kwa * kiasi* huishi maisha marefu yenye furaha na afya njema kuliko wasiokunywa kabisa pombe?

Tunashauriwa tunywe kwa kipimo, ...... na kipimo cha pombe kila mtu ana chake kadili ya afya ya mnywaji, mfano binafsi", mimi huwa naweza kunywa castle light tano+ konyagi ndogo moja na nikadrive, mwingine kwa kipimo hicho unaweza mkuta mtaroni.
Mtengeneza pombe amekuonya usidrive ukiwa chakali, halafu we unakiuka masharti?
Afanaleki kufa hakuna breki, endelea kushupaza shingo tukuzike mapema.
 
Mtengeneza pombe amekuonya usidrive ukiwa chakali, halafu we unakiuka masharti?
Afanaleki kufa hakuna breki, endelea kushupaza shingo tukuzike mapema.
Nimesema nagonga c- light tano mixing konyagi ndogo moja. Siwi chakali mkuu, ila stimu zinakaa vizuri.. .. au hukunielewa?
 
Weeeee ni hatari kuzidi Ahmada. Halafu nimekumisi balaa mkuu wangu, naja huko muda si mrefu!
Hahahahaha yaani mkuu kwa jinsi ulivyonifanya AMMADA ndiyo maana umeniita...
Nimekumiss sana jamanii
 
Weeeee ni hatari kuzidi Ahmada. Halafu nimekumisi balaa mkuu wangu, naja huko muda si mrefu!
Njoo boss wangu .
Sikukuu hii nimedoda.
I love you boss.
Hahaha pale I love zinapozidi kipindi cha sikukuu
 
Njoo boss wangu .
Sikukuu hii nimedoda.
I love you boss.
Hahaha pale I love zinapozidi kipindi cha sikukuu
Dadeq, hizi "Nakulavlav" hizi nilkuwa nashangaa mbona nyingi sana, kumbe leo tarehe 21!!!!
 
Back
Top Bottom