Ha ha ha njaa mbaya sana yule jamaa ambae anasambaza picha za nyuki wakiwa wamejaa kwa MTU au kifaa kilichoibiwa anajiita mzee wa nyuki kumbe nae tapeli tu
Ni hivi juzi kati aliibiwa dogo laptop yake sasa katika pitapita face book na wasap kakuta hizo picha akajaa kumbe mzee wa nyuki kamwambia atume salio na majina matatu dogo salio kakwama ikabidi anistue nikamwambia huyo atakuibia akagoma nikamwambia amwambie huyo mganga amfanyie kwanza akipata kifaa chake ndio tumlipe tukiingia mitini hizo nyuki atume kwetu,,
Mzee nyuki kuambiwa hivo matusi kama yote eti nyuki wangu nawatoa kwa gharama basi toeni hata hela ya kiti basi.
Dogo kapiga kimya kama siku mbili cha ajabu mzee nyuki ye ndio anapiga simu kila Mara kuulizia hela inatumwa au vp, nikamwambia dogo unaona yaan aliyeibiwa amepozi lkn mganga anakomaa kupiga simu kama mpiga debe akitafuta abiria.