Ule utapeli wa kijuha umeanza tena...

Ule utapeli wa kijuha umeanza tena...

Habali ya leo.mimi MICAEL KUYUNGA.samahani kuna boc wangu yupo serengeti mbuga ya wanyama poli yupo na wageni wake ni wazungu.watalii.wanataka kununua vitu vya kitamaduni kama vinyago vya kuchonga na mti wa mpingo,mabatiki,mashuka ya kimasai na vitu vingine vingi.kaniomba nimtafutie mtu naemjuwa na mwaminifu amsaidie kwenye manunuzi ya hivyo vitu.kama uko tayali nimpatie namba zako akupe maelekezo zaid.mimi naumwa matonses na kifua nimebanwa sauti imenikauka.uwe unanitumia sms kwa mawasiliano zaidi.

Namba iliyotumika ni 0621 375081
Hii message ni ya zamani....nimewahi tumia mwaka 2015
 
KWELI haisee ilikua tarehe 26 mwez wa 7 dah hapa nimefurugwa nitaanzaje kuwaambia wazazi na ilikua ada ya shule.
Nakushauri siku nyingine usichezee ada ya shule maana hizo siyo pesa zako ni za aliyekupa na aliyetakiwa kuzipokea kutoka kwako. Subiri uchezee mshahara wa ajira yako au faida kwenye biashara yako hizo ndiyo pesa zako.
 
Learned a hard way
 
Hawa jamaa na mie wametaka kuniliza mpigaji akidai kuna ma boss wa kizungu wanataka viatu vya kimasai na vitu vya kitamaduni kama shanga ila kuna mama ambae hua wanachukua kwake ambae kwa sasa ni mgonjwa hivyo me niwe mbadala wake anipe no za mwenye kiwanda cha viatu ataniuzia kwa bei mdogo baada ya kuchukua mzigo nimpigie yeye nikiwa na mzigo ili aje na hao wazungu kuchukua mzigo kwangu kwa bei ya juu namba aliotumia ni 0787068453
 
Mimi niliwahi kuwatapeli hao jamaa 5000Tsh maana nilikuwa sina MB's.

Hawakujua sina hata mia,
Wakanipigia simu kunipa deal hilo nawachora tu mwisho wakanipa namba za mtu mwingine nimtumie hela 150000/- nikakubali ila ndo nikamwambia nina 146000 tu ngoja nitafute iyo 5000 ndo nitume kumbe mi nimelala zangu sina hata mia,

Yule bwana si akaona nachelewa kutuma hela maana alikuwa anapiga sana simu, nikamuambia anitumie iyo 5000 mpesa halafu nitume kwenye ile namba alonambia tuchukue mzigo.

Akatuma mi nikaunga bando.
 
Hawa jamaa nusura wanirambe mil 2 Wamenisomesha mpaka nikaenda bank Mlimani City ilikuwa tukutane Mwenge Coke cola. Wazungu kutoka Manyara walikuwa wananisubiri Sea Cliff Hotel.

Ghafla nikabadili mawazo nikaenda Mwananyamala nikamshirikisha jamaa yangu mmoja ambaye naye walishampigia wakijifanya wanahitaji madawa kwenye kambi za wakimbizi Kigoma.

Nikageuza na hela zangu kurudi nyumbani
 
Ungedhani kwamba pamoja na taarifa hizi kusambaa kila siku basi watu wataelimika lakini wapi bana! Juzi tu si kapigwa mafao yule mwalimu? Yaani watu wa kuingizwa mjini hua hawaishi na hawa jamaa wataendelea kupiga pesa kwa miaka mingi tuu kwa mbinu hizi hizi..
 
Bro hili jambo liliwahi kutokea mwaka jana kwangu mwezi November kuna mama mmoja mfanya biashara wa vifaa vya hospital nimezoeana nae kama mama angu maana mtoto wake best yangu.Huyo mama aliibiwa simu na vibaka na hao vibaka wakaanza kuitumia ile simu kupata hela walitumia hiyo mbinu na kwakua yule mama anaheshimika na watu wengi so walifanya kama alivyoagiza kwenye sms sijui walifanye wale wezi hawakiushtukiwa mapema wakaweza kutapeli kiasi cha 2.8 milioni ndani ya siku moja kupitia namba ya mama.Wezi wakawa wamenifikia na mimi almanusura niingie mkenge maana nikawa nikipiga simu haipokelewi nikabidi nimpigie simu best yangu ambaye mwanae ndo akanieleza habari za kuibiw la simu na hao watu wanatafutwa Mungu mwema walipatikana.
Habali ya leo.mimi MICAEL KUYUNGA.samahani kuna boc wangu yupo serengeti mbuga ya wanyama poli yupo na wageni wake ni wazungu.watalii.wanataka kununua vitu vya kitamaduni kama vinyago vya kuchonga na mti wa mpingo,mabatiki,mashuka ya kimasai na vitu vingine vingi.kaniomba nimtafutie mtu naemjuwa na mwaminifu amsaidie kwenye manunuzi ya hivyo vitu.kama uko tayali nimpatie namba zako akupe maelekezo zaid.mimi naumwa matonses na kifua nimebanwa sauti imenikauka.uwe unanitumia sms kwa mawasiliano zaidi.

Namba iliyotumika ni 0621 375081
 
Eti nafasi za jeshi
Screenshot_20190808-152942.jpeg
 
Back
Top Bottom