FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,530
- 46,614
Alama za vidole imesajiliwa hiyo line?
Mazungumzo ya Tapeli Na Mwalimu aliyetaka kuhama kituo Cha kazi.
Tapeli:Hallo,wewe ni Mwalimu Fulani bin Fulani Na unataka kuhama
Mwalimu:Ndiyo nina uhitaji sana wa kuhama huku niliko.
Tapeli:Mimi nipo Tamisemi kuna mtu hapa nipo naye Ana uwezo wa kukusaidia tatizo lako ndani ya muda mfupi
Mwalimu:Nitashukuru sana kama nitafanikiwa.
Tapeli:Ila huyu mheshimiwa anahitaji ya maji kidogo ili aweze kufanya zoezi lako la kukuhamisha.
Mwalimu:Anataka kiasi Gani Na lini?
Tapeli:Anataka kiasi Fulani (Ziatajwa laki kadhaa) Fanya haraka Sasa hivi maana nafasi ni chache Na wahitaji ni wengi.
Mwalimu:Kwa Sasa hivi kupata hela ni ngumu maana hela ipo benki Na muda huu hakuna magari Na kwa bodaboda nauli haitoshi.
Tapeli:Mchukue bodaboda uende naye mjini utamlipa ukifika benki.Ufanye hima Mwalimu
Mwalimu: Oooh umenipa wazo zuri nachukua bodaboda nitamlipa nikifika mjini.(Mwalimu anampanga bodaboda kuwa aseme hawezi mpeleke town Bila kuweka advance ya shilingi elfu kumi,nyingine atamalizia akifika town)
Tapeli:Fanya haraka ukichelewa ofisi zitafungwa Na utakuwa umekosa nafasi
Mwalimu:Nimeongea Na bodaboda amekataa kunipeleka Bila kuweka advance hela ya mafuta labda uongee naye wewe umshawishi anipeleke.
Tapeli anaongea Na bodaboda,bodaboda anagoma kumpeleka mwalimu,Bodaboda anamshauri Tapeli amkopeshe mwalimu hela halafu ye ndo atalipwa Na Mwalimu.Tapeli anaingia kingi anatuma elfu kumi kwa bodaboda.Bodaboda Na Mwalimu wanatoa fasta ile elfu kumi halafu Mwalimu anapiga simu kwa Tapeli.
Mwalimu:Ndugu yangu umeniokoa,nimeshaanza safari ya mjini.
Masaa kadhaa yanapita.
Tapeli:Vipi mmeshafika mbona kimya.
Mwalimu:Mkuu sio kila siku unatapeli tu watu nawe siku moja Moja ukitapeliwa siyo vibaya.
Tapeli🙁Anatukana matusi yote Na anagundua kuwa naye kaliwa)

Hawa jamaa hovyo sana...waliwahi nipigia wakanambia wana deal za visima wako Katavi sasa wanahitaji dawa ya kutibu maji...kwa kua ninawafahamu nikajitoa akili ili nione mwisho wao...hawa wamejipanga baadhi wanajifanya wazungu hawajui kiswahili nikaenda nao mawasiliano masaa 2...mwisho wakasema basi tuma laki 5...nikawaambia subiri naenda kutoa pesa natuma baada ya saa 1 nikawachana kua huo utapeli kwa sasa umepitwa na wakati.. ..jamaa akacheka sana.
Na Mimi wlinfanyia km hivo..... Ila hapo kwenye KATAVI wakaweka SERENGETI..... Nikawauliza mnachimba VISIMA mbugani.... Nyie SIMBA na CHUI wajomba zenu? Walitaka laki 5! Nilikuwa mitaa karibu na BUGURUNI POLICE, kuna pot mwanafunzi wng nikampa simu aongee nao! Yule anaejifanyaga mzungu hajui kiswahili aliongea Kiswahili kushinda Manara!

Dogo acha kupenda mitelemko!!Na wazazi wangu sijawambia hadi Leo sijui pakuanzia kuwaambia kuwa nimetapeliwa.
Acha tu ndugu yangu Kuna mengine acha tu yapite kimya kimyaKuna baba mmoja na mama mmoja walitudanyanga kuwa wamehamia Dodoma na wakajitangaza sana kuwa sasa wako Dodoma wanamsubiri boss wao lakini kila siku wako Dar. Je huo sio utapeli?
Acha tu ndugu yangu Kuna mengine acha tu yapite kimya kimya

Usiseme nenoNdio maana kwenye cm hutakiwi kusave majina kama mama yangu, sjui baba yangu au mke wangu, mume wangu au kaka angu yaaani mtu akiiba cm yako wa kwanza kuwa taperi hera ni hao uliowasave kama ndugu zako wa karibu na lazima watume
Rafiki yangu aliibiwa simu akiwa anasafiri, mara nikatumiwa ujumbe kuwa simu yake imeharibika na anasafiri ila amepatwa na shida kidogo hivyo nimtumie laki moja na namba ikatumwa ya kutumia hela. Nikampigia akakata na kutuma ujumbe kuwa simu mbovu hatutoelewana.
Nikiwa njiani kuelekea kwa wakala nafsi ikasita, nikampigia mama yake bahati nzuri nae(rafiki) ndio alikuwa amefika, kumueleza akastuka kweli, ikabidi aanze mchakato wa kuwajulisha alioweza kuwa ameibiwa simu. Ila kuna mjomba wake alikwishatuma pesa.
Kidogo wanipune hela ya pango maana nilikuwa na miadi ya kuituma kesho yake baadae nikapokea msg kutoka namba mpya kwamba nitume pango la nyumba namba fulani fasta nikawekza pesa kwenye laini yangu tiyari kwa kutuma shida ikaja simu ikawa haipokelewi nami nikasita tuma ndo pona yangu nikawa nimewachania mkeka
Ukapone mkuu vp hujachinja kuku au mbuziHawa jamaa nusura wanirambe mil 2 Wamenisomesha mpaka nikaenda bank Mlimani City ilikuwa tukutane Mwenge Coke cola. Wazungu kutoka Manyara walikuwa wananisubiri Sea Cliff Hotel.
Ghafla nikabadili mawazo nikaenda Mwananyamala nikamshirikisha jamaa yangu mmoja ambaye naye walishampigia wakijifanya wanahitaji madawa kwenye kambi za wakimbizi Kigoma.
Nikageuza na hela zangu kurudi nyumbani
Hichi kitu kimenitokea Leo. Kuna brother nilikua nataka mtumia pesa akaniambia nitumie pesa. Baada ya dakika tano SMS ikaingia hiyo Pesa itume kwa Namba hii nilishindwa kijua natuma kwa Namba ipi ikabidi ni hakikiile itume kwenye namba hii angekula hela yangu sema kuweka neno 'itume haraka' alikosea
kuna bwana mdg nilitakiwa mtumia hela na nilimwahidi siku iyo mara msg ya itume kwa namba hii iyo hapo ila nikashangaa bwana mdg anasema itume haraka nikakausha kumbe ni bwana tapeli.

kuhakiki nikajua nataka lupigwa. Hii issue watu wa mitandao wanajuaNdio maana kwenye cm hutakiwi kusave majina kama mama yangu, sjui baba yangu au mke wangu, mume wangu au kaka angu yaaani mtu akiiba cm yako wa kwanza kuwa taperi hera ni hao uliowasave kama ndugu zako wa karibu na lazima watume
Hapo ndipo nikapata mashaka na kwa kujiridhisha zaidi nikachukua namba zao na kusearch majina yao kwa kutumia mpesa yule mmoja ambaye alijiita Frank namba yake ilisoma kwa jina la Hamis,na yule aliyejiita Odeso namba yake ikatokea kwa jina la Tatu Suleiman.Mimi mwenyewe leo walinikosakosa nimetumiwa meseji na namba ya Bosi wangu wa zamani akisema anataka kuniunganisha na mjomba wake Kuna biashara ya haraka haraka tuipige,kwa hiyo namba yangu anampatia huyo mjomba wake anipe maelekezo.
Baada ya dakika 3 akanipigia huyo mjomba yake akajitambulisha kwa jina la Frank na akasema yupo kwenye miradi ya serikali ya fummigation,kwa hiyo anasema Kuna wageni wamekuja dar na wanahitaji madawa/kemikali za fummigation kwa hiyo anataka Mimi niisimamie hiyo biashara ili tupate faida ya juu.
Baada ya hapo akasema ananiunganisha na Sales manager wa kiwanda Cha Shelys pharmaceuticals Mwenge anaitwa Odeso yeye ndio atahusika na kutoa hizo bidhaa.
Basi akanipa namba za huyo meneja nikampigia na kuongea naye Kisha nikaulizia Bei za hizo dawa nikaambiwa zinauzwa laki mbili kwa box moja.
Baada ya hapo nikamrudia yule aliyenipa maelekezo(frank) nikampa feedback ya Bei ambayo ni laki 2 Kisha akaniambia sisi itabidi tuuze laki 3 kila box moja.
Akasema hatua inayofuata anipe namba za wateja ambao alidai wako kwenye hotel maeneo ya Sinza ili niwape Bei halaf wakiafiki nikaonane nao tumalize biashara na kupata mahela na alidai hao wateja Wana uwezo wa kuchukua hata box 50.
Jamaa akanitumia namba zao hao wateja,lakini kwa bahati nzuri machale yakanicheza nikasema ngoja kabla sijaongea na hao wateja ili nianze kutoka home na kusogea maeneo ya mwenge ngoja kwanza nijiridhishe na kuconfirm Kama Kuna ukweli.
Nilichofanya nikampigia mtu wa Mwanzo kabisa ambaye namba yake naifaham Kama ya Bosi wangu isije ikawa amepoteza simu halaf imeokotwa na wahuni.
Nilivyompigia akapokea lakini akawa hataki kuongea sana na akawa ananong'ona kwa sauti ya chini na kuongea maneno machache yafuatayo,"nipo kwenye kikao nitakupigia baadae" kwa sauti ya kunong'ona.
Hapo ndipo nikapata mashaka na kwa kujiridhisha zaidi nikachukua namba zao na kusearch majina yao kwa kutumia mpesa yule mmoja ambaye alijiita Frank namba yake ilisoma kwa jina la Hamis,na yule aliyejiita Odeso namba yake ikatokea kwa jina la Tatu Suleiman.
Nikagundua kwamba ni matapeli nikaishia kucheka peke yangu,na hadi Sasa hivi hawajanitafuta tena.