[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Rafiki yangu aliibiwa simu akiwa anasafiri, mara nikatumiwa ujumbe kuwa simu yake imeharibika na anasafiri ila amepatwa na shida kidogo hivyo nimtumie laki moja na namba ikatumwa ya kutumia hela. Nikampigia akakata na kutuma ujumbe kuwa simu mbovu hatutoelewana.
Nikiwa njiani kuelekea kwa wakala nafsi ikasita, nikampigia mama yake bahati nzuri nae(rafiki) ndio alikuwa amefika, kumueleza akastuka kweli, ikabidi aanze mchakato wa kuwajulisha alioweza kuwa ameibiwa simu. Ila kuna mjomba wake alikwishatuma pesa.