Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

..kuna kitu kinaitwa " WORKING LANGUAGE " ambacho Watz lazima tufahamu maana yake.

..working language maana yake ni lugha rasmi zinazotumika ktk shughuli na mawasiliano ya shirika fulani la KIMATAIFA.

..tunapotafuta kazi ktk MASHIRIKA NA TAASISI ZA KIMATAIFA ni lazima tuwe na uwezo wa kuwasiliana ktk working languages zinazotumika ktk mashirika hayo.

..Ni vizuri kuipenda na kuienzi lugha yetu ya Kiswahili, lakini tuzingatie ukweli huo hapo juu.

cc Chige, Nguruvi3, Masanja
Mkubwa, sidhani kama Kiswahili linazuia mtu kujua lugha nyingine hasa katika zama hizi

Wahindi wana lugha zao na utamaduni wao lakini bado wanazungumza lugha kama ya kiingereza kwa ufasaha

Nchi za nje wanajifunza Kiswahili licha ya kuwa lugha zao ni kubwa.

Katika 'working language' hili ni sehemu moja ya umuhimu, lakini pia kuna suala la maarifa.
Maarifa mengi yamefichwa katika lugha zingine, na ili tuweze kupiga hatua lazima tujifunze

Hivi kwanini Wajaluo wanazungumza lugha tatu na isiwe sisi Watanzania? Ndivyo wawemba walivyo n.k.

Kiswahili ni lugha yetu, lakini katika dunia ya leo 'working language' n.k. zinahitajika
 
Ndo suala ambalo mara kwa mara nimekuwa nikiwahoji Wakenya kwamba, Uhuru ana exposure kubwa sana, amekulia maisha mazuri sana kuliko majority of Kenyans lakini anaongea Kiswahili vizuri sana, na ni mara chache sana utamkuta anatumia Kiingereza mbele ya hadhira kubwa ya Wakenya!!

Leo hii kama utapanga orodha ya viongozi wa Kiafrika hapa Afrika Mashariki na kati, sina shaka Uhuru ndie anaongoza kwa kutoijua kabisa shida!!

Ndipo nawahoji, inakuwaje nyie watoka shamba huko, tena kwenye familia duni, lakini mkishafika tu Nairobi ndo mnajifanya hamkijui Kiswahili!!! Hili swali bado sijawahi kujibiwa
Wakenya walio wengi Wana tabia za kimarekani, wao wako proud Sana na Kwa bahati mbaya Sana ukoloni uliwaingia Hadi kwenye Damu, Kwao kutumia lugha ya kimombo Kwa ufasaha ni ishara ya kuelimika,wao ushindana kuongea vocabularies nyingi na kwenye TV programs zao nyingi zimekaa Kwa style ya Debates ili kuonesha umahiri wa kuongea lugha ya Malkia..SASA Kwa mentality aliyokuwa nayo Baba yake Uhuru towards ukoloni, sidhani kama brains za watoto wake zimekuwa programmed kuamini kwamba vya wazungu ndio bora.. But ata baadhi ya wafanyabiashara wa kitanzania waliowekeza katika sekta ya utalii wanawasifia Sana wahudumu wa kikenya na kuwapendelea kuwapa ajira dhidi ya watanzania wenzao Kwa kigezo cha kuongea lugha ya kiingereza, hivyo basi ili mkenya haonekane Yuko juu ataongea Kiingereza muda wote ili kujitofautisha na walio wengi(swahili speakers) ili kupata recognition au upendeleo wa KAZI au priveledge.
 
5 May 2021
Nairobi, Kenya

TANZANIA BUSINESS MOGUL MR. ROSTAM AZIZ THROWS TOUGH QUESTIONS AT UHURU & SAMIA'S MEETING IN NAIROBI !!​



Source : Kenya Digital News
 
Kwahiyo huwezi kufanya diplomasia bila kizungu? Ona jinga hili!

Wachina na warusi mbona wamekupiku kwenye kila jambo pamoja na hicho kiingereza chako cha kuokoteza?

Ati diplomacy sijui nini nini!

Umejipiiindaa mwenyewe unaandika uharo mtupu!

5 April 2021
Nairobi Kenya

LIVE! PRESIDENT UHURU & TANZANIA PRESIDENT SAMIA SULUHU MEETING KENYA & TANZANIA BUSINESS PEOPLE!


Source : Kenya digital news
 
Mkubwa, sidhani kama Kiswahili linazuia mtu kujua lugha nyingine hasa katika zama hizi

Wahindi wana lugha zao na utamaduni wao lakini bado wanazungumza lugha kama ya kiingereza kwa ufasaha

Nchi za nje wanajifunza Kiswahili licha ya kuwa lugha zao ni kubwa.

Katika 'working language' hili ni sehemu moja ya umuhimu, lakini pia kuna suala la maarifa.
Maarifa mengi yamefichwa katika lugha zingine, na ili tuweze kupiga hatua lazima tujifunze

Hivi kwanini Wajaluo wanazungumza lugha tatu na isiwe sisi Watanzania? Ndivyo wawemba walivyo n.k.

Kiswahili ni lugha yetu, lakini katika dunia ya leo 'working language' n.k. zinahitajika
Safi sana. Wapashe wapashike. Watu wasichukulie kutopenda/kutoelewa Kingereza kama sababu ya kukatisha tamaa matumizi yake sehemu mbali mbali. Kingereza kina nafasi kubwa kwenye biashara za kimataifa na mahusiano ya kisiasa na kidiplomasia.
 
Back
Top Bottom