DOKEZO Ukwepaji kodi kupitia EFD ni mkubwa kweli mpaka nimeona uchungu Kariakoo leo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,649
20,988
Am very sorry, I was misled the information written were not true, tuzipuuze kwani hazina ukweli wowote and am sorry endapo kama thread hii imepelekea kuleta usumbufu wowote, infact all that written here are not truly.

N. B: TUJITAYARISHE KWA SENSA AMBAYO ITAFANYIKA TAREHE 23 MWEZI HUU WA NANE, AIDHA TUACHE KUMBUKUMBU NA VIELELEZO SAHIHI KWA AJILI YA SENSA

Tarehe za watoto za kuzaliwa, idadi kamili na halisi ya wanafamilia.
THANK YOU ALL

KUOMBANA RADHI NDIO UUNGWANA WA KITANZANIA.
Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

Umuhimu wa kipekee wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na:-
  1. Kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;
  2. Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;
  3. Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
  4. Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
  5. Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
  6. Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.
"EWE MTANZANIA , JIANDAE KUHESABIWA"
 
natamani ungejua jinsi biashara inavyokwenda... kwa sasa watu wanalipa zaidi ya hiyo 6m yako maana.. pia kumbuka hela tukilipa tunafaidisha wengine tu.. bora tufaidi wote kitu cha milioni nilipe laki nane nipite hivi
Na ma risiti kanjanja pia yamekuwa mengi yapo copyright na original, sorry kuna watu wataumia au kuchukizwa na uzi huu maana naaribu ugali wao.
 
Tra wana mambo mengi na watumishi wachache hawawezi kuwa na ufanisi hata kidogo.

Napendekeza TRA wajikite kwenye kodi tu

Mambo ya magari na usajili na maleseni yawe chini ya taasisi nyingine itayosimamia mambo yote ya magari.

Tra wajikite kwenye kodi tu waweke sera nzuri za kuhakikisha kodi inalipwa kwa kuzingatia maslahi ya pande zote, rushwa itungiwe sheria ya kunyongwa😂
 
Unanunua kitu cha laki tisa unapewa risiti ya laki 4 tena niyakusindikizia mzigo, unapofika home, unarudisha risiti maana kuna kijana unakuwa umepewa ili akaichukuwe.
Kwa maoni yangu mfumo wa zamani wa risiti urudishwe ispokuwa maduka yote kariakoo nzima yafanyiwe sensa maalumu yajulikane, pili yote yapatiwe namba maalumu(unique) utambukisho wa mmiliki wa duka pamoja na kitambulisho chake uraia, ikibidi GPS ya eneo la duka and then serekali urudishe utaratibu wa ukadiriaji kwa awamu 4 kwa mwaka, nikiwa naamini hakuna duka ambalo litakadiriwa chini ya million 6 kwa mwaka, it should be 6 ml, and above, infact to 20ml P.a,kwa akili za wafanyabiashara wa kariakoo ndilo litakuwa jibu sahihi unless otherwise ni shida they are so tricky! Maduka haya yakishaingizwa kwenye database na faini zikawa nzito kwa mcheleweshaji zikiambatana na vifungo na kutafutwa na vyombo vya doll kwa watakaojaribu kukwepa itasaidia sana kwa mtazamo wangu kwa jinsi nilivyoiona hali halisi.
WASALAAM.
N. B, Mashine hizi ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa jamii iliyostaarabika.
Tuanze na wewe unayepewa risiti ya laki 4 badala ya laki 9, na tena unairudisha akapewe mwingine kusindikizia mzigo wake..!!! Kwanini usitoe taarifa panapohusika?
 
Halafu mnataka maji,barabara,umeme na kadhalika bila kulipa kodi,we nawe mhujumu uchumi tuu.Umetoa laki 9 unapewa risiti ya laki 4 mmh
 
Unanunua kitu cha laki tisa unapewa risiti ya laki 4 tena niyakusindikizia mzigo, unapofika home, unarudisha risiti maana kuna kijana unakuwa umepewa ili akaichukuwe.
Kwa maoni yangu mfumo wa zamani wa risiti urudishwe ispokuwa maduka yote kariakoo nzima yafanyiwe sensa maalumu yajulikane, pili yote yapatiwe namba maalumu(unique) utambukisho wa mmiliki wa duka pamoja na kitambulisho chake uraia, ikibidi GPS ya eneo la duka and then serekali urudishe utaratibu wa ukadiriaji kwa awamu 4 kwa mwaka, nikiwa naamini hakuna duka ambalo litakadiriwa chini ya million 6 kwa mwaka, it should be 6 ml, and above, infact to 20ml P.a,kwa akili za wafanyabiashara wa kariakoo ndilo litakuwa jibu sahihi unless otherwise ni shida they are so tricky! Maduka haya yakishaingizwa kwenye database na faini zikawa nzito kwa mcheleweshaji zikiambatana na vifungo na kutafutwa na vyombo vya doll kwa watakaojaribu kukwepa itasaidia sana kwa mtazamo wangu kwa jinsi nilivyoiona hali halisi.
WASALAAM.
N. B, Mashine hizi ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa jamii iliyostaarabika.
Ata ww unaekubali upewe risiti ya laki 4 ni MZEMBE ...mm huwa nakomaa nawaamniagankabisa risiti isome pesa niliyo lipa na huwa sirudishigi mm ... Huwa nakuwaga bandidu kweli kweli
 
Unanunua kitu cha laki tisa unapewa risiti ya laki 4 tena niyakusindikizia mzigo, unapofika home, unarudisha risiti maana kuna kijana unakuwa umepewa ili akaichukuwe.
Kwa maoni yangu mfumo wa zamani wa risiti urudishwe ispokuwa maduka yote kariakoo nzima yafanyiwe sensa maalumu yajulikane, pili yote yapatiwe namba maalumu(unique) utambukisho wa mmiliki wa duka pamoja na kitambulisho chake uraia, ikibidi GPS ya eneo la duka and then serekali urudishe utaratibu wa ukadiriaji kwa awamu 4 kwa mwaka, nikiwa naamini hakuna duka ambalo litakadiriwa chini ya million 6 kwa mwaka, it should be 6 ml, and above, infact to 20ml P.a,kwa akili za wafanyabiashara wa kariakoo ndilo litakuwa jibu sahihi unless otherwise ni shida they are so tricky! Maduka haya yakishaingizwa kwenye database na faini zikawa nzito kwa mcheleweshaji zikiambatana na vifungo na kutafutwa na vyombo vya doll kwa watakaojaribu kukwepa itasaidia sana kwa mtazamo wangu kwa jinsi nilivyoiona hali halisi.
WASALAAM.
N. B, Mashine hizi ni nzuri sana lakini ni nzuri kwa jamii iliyostaarabika.
TRA waweke doria kwenye malango ya kuingilia na kutokea Kariakoo na waende kwenye vijiwe vya kupakilia mizigo hasa kidongo chekundu...waache kula AC watoke ofisini. Nchi inajengwa kwa kodi mbona wafanyikazi wanalipa kodi
 
Back
Top Bottom