Kiongozi kila jambo lazima lina angle za kidini ndani yake? Mi nimeona kinachozungumziwa hapa ni ukwepaji kodi na mahakama zipo kama pana shaka yoyote mahakama itatoa haki. Embu tuache haya makitu ya udini na ukanda kwenye mambo serious ya kitaifa kama haya
Mkuu hili ni tatizo kubwa sana bapa Tanzania.
Kwa muda mrefu tumekua tukiibiwa na kudhulumiwa kwa kutumia dhana za udini.
Kuna kundi la watu kazi yao ni kufanya mafyongo halafu wanapobanwa wanaleta dhana ya udini. Ooh nimefukuzwa kwa sababu ya dini yangu na blah blah nyingi utafikiri walitumwa na dini kuiba.
Magufuli awakatae hawa watu wenye mirengo ya kidini serikalini.
Futa misamaha yote ya kodi bila kujali hawa makuadi wa matajiri na wanyonyaji kwa mirengo ya kidini.
Hata misamaha ya kodi feki kwenye taasisi za dini zina makuwadi wake.Zinapoguswa wanajitokeza kwa nguvu kubwa kutetea ukwepaji wa kodi huku wananchi wengi wakiumia bila kujali dini zao.
Historia inaonyesha pia kuwa maajenti au mawakala wa ukoloni walikua ni watu wa dini. Mpaka leo kuna watu na akili zao hawatambui na hawataki kuelewa au kuelezwa kuwa Mengi ,MO ,Bakhressa ,Sas Abood na wengine hawa ni mabepari na wafanya biashara ,wanachoangalia ni kupata faida kubwa na kushika soko kwa namna yoyote na wasipodhibitiwa basi wanawashika wanasiasa na kukwepa kodi. Hawa sio mitume au manabii wa kidini. Hawa ni mitume na manabii wa kipepari. Hawa wanatambuana dunia nzima katika harakati zao za Kibepari bila kujali dini zao. Wanawatumia waumini wenzao wenye kulewa ushabiki wa kidini kufanya uhujumu wakijua mashabiki wao watapoteza malengo kwa kuibua hoja dhaifu za udini.
Hali hii imejitokeza sana kwenye biashara zote haram. Mtu akikamatwa wanaangalia dini yake na nguvu yake ndani ya dini na makuadi wao wanajitokeza na kuanza kulalamika kuwa ameonewa kwa sababu ya dini yake.
Ndio maana hata maeneo yenye wabunge wafanya biashara yanakua na huduma duni sana kwa wananchi na umaskini ni mkubwa sana.
Kampeni zikifika blah blah za udini zinawarudisha madarakani kwa kupitia makuwadi wao wa kidini kufanya ushawishi ya huyu ni muumini mwenzetu na anatusaidia kwenye misiba n.k. huku wanafunzi wa maeneo hayo wengi wakikaa chini.
Kwa kweli inefikia mahali kila mtu achukizwe na huu ujinga wa kuwatetea wezi kwa sababu tu ni muumini wa dini au dhehebu lake.