Ukweli wa video hii ni upi? Je, mauaji haya ni kweli yalitokea Zanzibar?

Kweli hakuna mapinduzi yasiyo mwaga damu lakini yale ya Zenj hakukuwa na umwagikaji mkubwa kihivyo wa damu. Sultani alidhani yuko peponi na ukichanganya tena dini yake ilikuwa ndiyo imeshika hatamu alijiona salama kabisa.
Zilitumika jambia 2 to na panga tatu nne hivi. Okello mwenyewe alikuwa hajui kutumia bunduki hivyo alipoipewa akaijaribia kwa kijana wa kiarabu. Walipouona ubongo wake, kila mtu alizimia na waliokuwa na nguvu kidogo wakamwabudu Okelo.
Kweli Karume alikuwa Dar lakini aliitwa haraka sana asubuhi kurudi kwani Sultani kiishaikimbia Ikulu hivyo akaja kutawala. Hakukuwa na mauaji hayo ila waliotaka kutoroka nchi walikuta mashua zote zimeondoka kuelekea Oman.

Watu zaidi ya 20,000 waliuwawa halafu unasema hakukua na umwagaji wadamu mkubwa?
 
Mkuu umeeleza vzr sana. .. sorry kwa maswali zaidi. ..
Nataka kujua kwann John okello hakuweza kugombea?
Huyu okello inasemekana ni mganda aliingiaje zenj na kuweza kuongoza mapinduzi?
Na aliondoka zenj kwasababu zipi?

Swali gumu sana hilo kwa wafuasi feki wa Okello.
 
Okelle ikabidi aingilie yale maongezi na kisha akawaambia kwamba yeye anapajua sehemu ya kupata dawa ambayo itawasaidia kwenye plan yao kufanya mapinduzi dawa ambayo watakapo itumia itakuwa kama inawapumbaza serikali hata kama ikitokea wakasikia kwamba kuna vugu vugu la wazanzibar kudai ukombozi wa puuzie ... okello na genge lake la wadai mapinduzi waka bebana mpaka kenya kwa mau mau wakapatiwa hizo dawa ..kisha wakaanza sasa kujipanga kufanya mapinduzi baada ya kurudi ... (nime jaribu kueleza kwa kifupi ).... Mgirik

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hizo ni porojo ambazo utazikuta kwenye kitabu chake tu Okello na hutozikuta pengine.
 
Historia ya mapinduzi inaonyesha kuwa hakukutumika nguvu kubwa kwa kina okelo kuyafanikisha na kutwaa nchi sasa hawa watu waliuwawa kwa sababu gani wakati tayari wanamapinduzi walishachukua nchi?.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hayo mauaji yalitokea baada ya mapinduzi. Usiku wa Mapinduzi watu waliokufa hawakufika hata 100. Lakini kuanzia siku ya pili nakeundelea mwezi mzima ndipo yalipofanyika mambo kama hayo.
 
-Video inaweza kuwa imechukuliwa na yoyote,jw,ama hata wazungu.
--Haja ya kujua ipo,sababu inahusiana na historia ya nchi na uhai wa watu wengi uliopotea bila ya sababu zinazokubalika na binaadamu wenye utu.
-Sikuwepo duniani mwak 1964 lakini ni wajibu wangu kujua historia yangu,ya watu wangu na dunia kwa ujumla
-unajustify mauaji ya watu wote hao kwa sababu ya kipuuzi ya wazee kupata wake za hao waliowauwa?.Kama mtu mzima na akili zako unahitaji kuuwa mtu ili uweze kupata mwanamke basi wewe ni khabith,psychopath,sick and an animal,mshenzi na sheitwani,wala sio ushababi huo,wanaume wa kweli wanatongoza na kutumia njia za kistaarabu na kiungwana kuwapata wanawake wawatakaoo,sio kufanya genocide/ethnic cleansing.na unayesapoti hyo mentality na yeyote unakuwa kwenye kundi hilohilo.
-Sina nia mbaya Lengo la kufukua hili kaburi ni kujaribu kujifunza historia ya nchi yangu ambayo ni pwani nzima ya afrika mashariki pamoja na visiwa vyake.Kumekuwa na upotoshaji ama kufichwa kwa historia ya mwafrika,na hili linaturudisha nyuma,usipojua historia yako huwezi kuendelea na maisha yanakuwa magumu zaidi kwahyo ni muhimu kujua.Nia sio kutoa lawama ama kunyooshea watu vidole.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu tungelianzia hapa. Kwanza mapinduzi ya Zanzibar Yalifanywa na Nyerere na sio mwengine yoyote. Na aliyafanya hayo akiwa na backup kutoka kwa mataifa makubwa ya. (U.S, U.K, Israel)
Sultan wa Zanzibar alikua ni kibaraka tu wa waingereza na wala hakuwa na athari yoyote kwao, walikua na uwezo wa kumendesha wanavotaka wao, Ila Z.N.P au Hizbu ndio ilikua tatizo kwa hayo mataifa makubwa. Hawakumtaka Ali muhsin atawale Zanzibar, Pamoja na Abrahman Babu ambaye katika kipindo hicho cha mapinduzi walishagawana mbawa kutokana na tafouti zao za kisiasa. Kwaiyo mapinduzi yale yalikua nikwaondoa Hizbu na sio Sultan kama tunavoaminishwa. Na ndiomana jiulize Sultan kipi alipata kwenye hayo mapinduzi? Nyerere ndio aliemuhifadhi kwa kutii amri ya Muengereza na baadae akelekea Uengereza akiwa salama yeye na ukoo wake wote.
Sasa watafute hao viongozi na wanachama wa chama cha Hizbu yaliowakuta ndio hayo. Viongez wengi walikula viteso wakaishia majela kwa zaidi ya miaka 10 na zaidi.
Sasa hizi porojo nyengine tunazokaririshwa ni za uchaa tu, Na tunazidi kuwa wajinga tunapozidi kubebe vitu visivoingia akilini.
Labda tungeuliza hivi mfano leo kukitokea mapinduzi India ni nani atakua aliyepinduliwa Ram Nath Kovind au Narendra Modi? au Ujerumani Frank-Walter Steinmeier au Angela Merke? naomba nijibu hili ili tuendelee mkuu.

Tupo pamoja mpaka hapo mkuu?
 
Mkuu punguza kusambaza uwongo.
Babu sina muda wakubishana na wewe ...tuko hapa kwaajili Ya kusambaza elimu " na waungwana huwa wanapingana kwa hoja ..kama unazo hoja zenye mantiki ziweke hapa ili watu wapate kuelimika na sio wewe kuanza kukashifu watu nakuwaita waongo.... hiyo sio desturi ya muungwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babu sina muda wakubishana na wewe ...tuko hapa kwaajili Ya kusambaza elimu " na waungwana huwa wanapingana kwa hoja ..kama unazo hoja zenye mantiki ziweke hapa ili watu wapate kuelimika na sio wewe kuanza kukashifu watu nakuwaita waongo.... hiyo sio desturi ya muungwana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sijakukusudia kukukashifu ila nimekusudui kupinga unachoeleza. Samahani kama nimekukera.

Mkuu lamwanzo ningependa unambie. Revolution ilikua ni idea kutoka kwa nani kutokana na ufahamu au ueleo wako?
 
Hapana hakuwahi ila baada ya Yale mapinduzi alipewa cheo cha u-field Marshall ...na alopofukuzwa na kwenda uganda alikuja kupewa cheo Jeshini ila kwakuwa kilikuwa ni cheo kidoho hakuridhika nacho ..idd amin baada ya kusikia history ya jamaa kuwa aliwahi kufanya mapinduzi ya nchi akawa ana muogopa ... wakampangia mpango wakamuua ... wakajifanya kumwambia wanamuhamishia kazi mpakani ili aende kuwa kiongozi wa kuilinda boda ya uganda na kenya .... baada ya kufika huko wakamuua "

Sent using Jamii Forums mobile app
Tupe source maana nina uhakika hukuwepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
-Video inaweza kuwa imechukuliwa na yoyote,jw,ama hata wazungu.
--Haja ya kujua ipo,sababu inahusiana na historia ya nchi na uhai wa watu wengi uliopotea bila ya sababu zinazokubalika na binaadamu wenye utu.
-Sikuwepo duniani mwak 1964 lakini ni wajibu wangu kujua historia yangu,ya watu wangu na dunia kwa ujumla
-unajustify mauaji ya watu wote hao kwa sababu ya kipuuzi ya wazee kupata wake za hao waliowauwa?.Kama mtu mzima na akili zako unahitaji kuuwa mtu ili uweze kupata mwanamke basi wewe ni khabith,psychopath,sick and an animal,mshenzi na sheitwani,wala sio ushababi huo,wanaume wa kweli wanatongoza na kutumia njia za kistaarabu na kiungwana kuwapata wanawake wawatakaoo,sio kufanya genocide/ethnic cleansing.na unayesapoti hyo mentality na yeyote unakuwa kwenye kundi hilohilo.
-Sina nia mbaya Lengo la kufukua hili kaburi ni kujaribu kujifunza historia ya nchi yangu ambayo ni pwani nzima ya afrika mashariki pamoja na visiwa vyake.Kumekuwa na upotoshaji ama kufichwa kwa historia ya mwafrika,na hili linaturudisha nyuma,usipojua historia yako huwezi kuendelea na maisha yanakuwa magumu zaidi kwahyo ni muhimu kujua.Nia sio kutoa lawama ama kunyooshea watu vidole.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeshapandwa na hasira ma hili litakuzuia kujadili vizuri. Swali ni Je; Kwa nini usiamini kuwa huenda hizi zilikuwa ni photo za senema flani hivyi?
Tuliokuwa dar enzi hizo tunajua kuwa kulikuwa na mawasiliano mazuri tu baina ya Zanzibar na bara. Iweje tusikie na kuyaona ya John Okello na alivyowaweza waarabu lakini tusisikie hivyo vifo vya halaiki??
Jiulize, Zanzibar ilikuwa na watu wangapi kipindi hiyo halafu wafe wengi kihivyo dunia isitikisike?? Ndio sijakataa kuwa walikufa watu, hata bara pale Magomeni Mapipa alikufa mwarabu. Lakini sio vifo vingi hivyo.
Unataka kujua historia ya nchi yako ya Zenj?? Hutakaa uipate kwani waliivuruga kumchafulia Okello asijewadai mafao
 
Watu zaidi ya 20,000 waliuwawa halafu unasema hakukua na umwagaji wadamu mkubwa?
Acheni kukuza mambo. Tuambie, walikuwa weusi, waarabu au?? Hivi wajua population ya Zanzibar kipindi hicho walikuwa watu wangapi? Wajua leo wapo watu wangapi? Acheni kuvuruga watu. Tumepigika vya kutosha mfukoni msitupe stress zaidi.
Swali chokonozi tu; Wajua Sultani alikimbilia wapi?? Iweje Uingereza ije kuisaidia Tanganyika kuyazima yale mapinduzi ya 1964?? Nadhani mna kitu mnakitafuta lakini tafuteni vizuri msitumie wengine. Tena wengi wao wesharehemeka
 
Siku zote ndio ulimwengu ulivyo hivyo " Mashujaa huwa wana hofiwa ...

Refer kisa cha Samson ... samson alikuwa ana hofiwa na watawala kutokana na uwezo wa nguvu zake za asili alizo nazo .... walikuwa wanapata hofu ..kuwa ipo siku anaweza kuzitumia nguvu zao kwaajili ya kuwaondoa katika vyeo walivyo navyo ...

Hata sababu ya yesu kuandamwa ili kuwa ni hofu ya watawala ...kwa sababu alikuwa akiitwa/akijiita mfalme na watu walikuwa wana mkubali --wakati katika nchi anayoishi palikuwa na mfalme anayefahamika kwa jina la Caesar ..
Watawala wakaingiwa na hofu kuwa anaweza kuutumia ushawishi wake kwaajili ya kuupindua utawala uliopo madarakani " ...

BTW -- SINA UHAKIKA NA MASIMULIZI HAYA KAMA YALIWAHI KUTOKEA KWELI. LAKINI HATA KAMA NI YA KUTUNGWA YANA JAMBO LA KUTUFUNDISHA ..

Sent using Jamii Forums mobile app
Hats lissu watawala wanamhofia hadi wanataka kumtoa roho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana hakuwahi ila baada ya Yale mapinduzi alipewa cheo cha u-field Marshall ...na alopofukuzwa na kwenda uganda alikuja kupewa cheo Jeshini ila kwakuwa kilikuwa ni cheo kidoho hakuridhika nacho ..idd amin baada ya kusikia history ya jamaa kuwa aliwahi kufanya mapinduzi ya nchi akawa ana muogopa ... wakampangia mpango wakamuua ... wakajifanya kumwambia wanamuhamishia kazi mpakani ili aende kuwa kiongozi wa kuilinda boda ya uganda na kenya .... baada ya kufika huko wakamuua "

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kuwa Okello aliuwawa na Idd Amin lakini sababu haikuwa kumuogopa kwa sababu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sababu hasa ni kuwa Okello alikuwa amejiunga na kundi la Obotte lililokuwa Tanzania. Katika harakati hizo Amin akawa amepata taarifa na Wakamwekea mtego wakamnasa na kumuua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acheni kukuza mambo. Tuambie, walikuwa weusi, waarabu au?? Hivi wajua population ya Zanzibar kipindi hicho walikuwa watu wangapi? Wajua leo wapo watu wangapi? Acheni kuvuruga watu. Tumepigika vya kutosha mfukoni msitupe stress zaidi.
Swali chokonozi tu; Wajua Sultani alikimbilia wapi?? Iweje Uingereza ije kuisaidia Tanganyika kuyazima yale mapinduzi ya 1964?? Nadhani mna kitu mnakitafuta lakini tafuteni vizuri msitumie wengine. Tena wengi wao wesharehemeka

Population ya zanzibar ilikua 350,000. Na ndiomana ukaambiwa hayakuwa mauaji ya kawaida.

Uingereza ilikuja kuyazuia mapinduzi ya 64 ya Tanganyika kwa sababu hawakuyataka. Nyerere alikua ni kibaraka wao.
Lakini Zanzibar Waengereza hawakuwata ZNP na ndio mana yakafanyika mapinduzi yale. Hakuna yoyote angelithubutu kufanya mapinduzi kama muengereza asingiridhia kile kitu. Na Sultan ambaye pia alikua kibaraka wa Waengereza naye ndio mana akafika salama Uingereza na alihifadhiwa na huyo Nyerere.
 
Basi unafiki ndio ulikuwa unatawala kumbe!! Muingereza hamtaki ZNP hivyo akaamua Sultani apinduliwe, akamwita aende kukaa kwake. Nyerere akamsaidia aondoke asije uliwa. Huku nyuma Nyerere akatuma chopa kwenda kuwapiga picha waswahili wakiliwa huko Zenj.
Kweli hadithi nyengine jifunzeni kuzitunga muingizemo na viungo ili tusiokuwepo tusigundue uongo wenu. Fikiria, watu 20000 wauliwe mchana. Asichupoke hata 1 tu wa kwenda kueleza yaliyowakuta wenzie?? OK yu can believe whatever ila usiwaaminishe wengine
 
Kitabu Cha mwalimu Nyerere (the influence of Nyerere ), cha mwaka 1995 (uk-172) kina sema .. uhuru wa Zanzibar ulipatikana alhamisi ya December 10 .1963.sultan akiwa mkuu wa nchi ya Zanzibar nakupewa mamlaka ya kumteua mrithi wake "..
Mapema mwaka huo huo Mwalimu Julius Nyerere . Aliionya serikali ya uingereza kwamba ikiwa itatoa .mamlaka kwa chama cha watu wachache " Kina-choongozwa na waarabu cha ZNP "... Maamuzi hayo yataifanya Zanzibar kuwa sehemu ya Mashaka ..

Ndani ya Majuma ma-5 tu serikali hiyo ilipinduliwa na masiha mjinga .Ambaye ni kiongozi wa wanaharakati (JOHN OKELLO)

Baada ya kipindi kifupi cha vurumai na mauaji (OKELLO) alisimika baraza la mapinduzi chini ya Uongozi wa Abeid aman karume ....

Kwa hiyo mkuu kwa kukujibu tu swali lako " Hayo mauaji Yalitokea kipindi cha vurugu za mapinduzi yaliyo asisiwa na Bwana john okello na rafiki wake wa karibu shekhe abeid aman karume .... ni mauaji Ambayo yaliua takribani ya watu 1.2000.

Nadhani nitakuwa nimekujibu ..

Sent using Jamii Forums mobile app
John okelo ni Mkristo ilikuaje akawa na nguvu Zanzibar ya sultan wa kiarabu?

Kuna kitu natamani kujifunza ukinijibu nitakuwa na maswali mengi inaonekana una Mambo mengi unafahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom