July 7,2005

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
2,987
9,322
ANGALIZO: Yote yaliyoandikwa humu yatabaki kuwa ni maoni binafsi ya mwandishi wa makala ambayo baada ya kukamilika hii habari references na citations zitawekwa. Kutokana na maada hii kuwa controversial kwa kugusa imani za watu, hivyo nimejaribu kufanya summary ya baadhi ya vipengele kadhaa ili kuondoa ukakasi kwa kadiri niwezavyo kwenye kazi original ya mwandishi ili kushare baadhi ya matukio yaliyoikumba dunia kwenye kipengele cha usalama.


"Religion does three things effectively: divide people, controls people and deludes people". UNKNOWN.


Ilikuwa ni majira ya saa Tatu asubuhi ,ambapo raia wa uingereza waliamka na kukutana na taarifa mbaya zaidi kwenye vyombo vya habari. Ni siku hii ambapo serikali ya uingereza haikuamini ni nini kimetokea kwenye ardhi yake yenyewe.

Hii ni baada ya milipuko kadhaa ya mabomu kutokea. Treni zinazopita underground ililipuliwa ,na baadaye basi la abiria Tena likasambaratishwa vipande vipande kwenye eneo la Bloomsbury square. Hali ya maeneo haya yalitisha haswa eneo ilipolipuliwa treni baada ya shughuli ya kukusanya mabaki ya miili ya watu kutoka kwenye treni hiyo kuharibiwa vibaya.

Wiki mbili baadaye majaribio mawili yalifanyika katika kulipua mabasi na pia treni zile zinazofanya safari katikati ya mji lakini kwa bahati nzuri mabomu hayo yalifeli kulipuka . Kutokana matukio haya yaliyotokea kwa mfululizo , uingereza haikuamini ni nini kimetokea kwenye ardhi yake ,huku raia wakiwa wapo kwenye panic kutokana na matukio haya. Ilionekana Sasa ni rasmi nchi hii ilikuwa kwenye kampeni dhidi ya mashambulizi ya kigaidi ya kujitoa mhanga ,huku maeneo ya umma walipo raia wengi yakilengwa zaidi.

Serikali haikutegemea kama wahusika wa matukio haya ya kigaidi ni raia wa nchi hiyo. Imekuwaje raia wa uingereza anaamua kujitoa mhanga na kuua raia wenzake?. Baadaye ilikuja kuvuja mkanda wa video ikimuonyesha kijana mmoja Raia wa uingereza mwenye asili ya Asia ambaye ni mmoja wa wahusika wa bomu la kujitoa mhanga , ulimuonyesha kijana huyu akijinasibu kwa kusema njia pekee ya kuwasilisha masahibu wanayopitia waislamu wakazi wa mji wa Yorkshire kwa serikali ya uingereza ni kujitoa mhanga peke yake .

Baada ya mkanda huu wa video kuvuja na kutapakaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari, serikali ilikuwa Haina jinsi zaidi ya kuukubali ukweli mchungu na kujiuliza inakuwaje raia kama huyu ,aliyesomea uingereza,na kupata kazi nzuri na kukulia kwenye familia Bora iliyostaarabika anaamua kugeuka gaidi na kujitoa mhanga kwa kujilipua na kufa na Raia wengine wasiokuwa na hatia?. Nini alikikosa Hadi imfanye kuwa gaidi?

Ilisemekana nchi ya uingereza wakati huo (ripoti za takwimu za mwaka 2005 kurudi nyuma)ilikuwa na takribani raia milioni 60 huku millioni mbili wakiwa ni waislamu. Maswali mengi watu wakajiuliza Je ni vijana wangapi raia wa uingereza wamekuwa radicalized na kupata mafunzo yenye itikadi Kali ikiwemo ya kujitoa mhanga na kuwaua wenzao? Na wengine wakiamini uislamu ni dini ya kuhubiri amani na upendo kwenye jamii Nini kinaendelea?.

Maswali yalikuwa mengi kuliko majibu. Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali nchini uingereza za wakati huo ilionyesha kwamba takribani raia 16,000 wa nchi hiyo ambao ni waislamu wanajihusisha moja kwa Moja au wanasapoti shughuli za kigaidi na jihadi. Pia Ripoti ilisema kwamba zaidi ya raia 3000 wafuasi wa dini hiyo , wamewahi pita kwenye kambi mbalimbali za mafunzo za Al Qaeda kabla ya kuhamia uingereza,na mamia kati Yao wakiwa wanaamini uingereza ni target kwa ajili ya jihadi.

Kutokana na takwimu hizi , zilionyesha Kuna mahali kama serikali ya uingereza ilikosea na vyombo vya usalama vya nchi hiyo vilikuwa vimelala . Lakini wengine walienda mbali na kusema matokeo haya yote ni uingereza kuulea ugaidi uliokuwa umezaliwa ndani ya nchi hiyo Sasa matunda yake inaanza kuyala .sera Yao ya kuukubali uhamiaji ni dhambi iliyoanza kuwatafuna.

IPO HIVI
Jiji la London ndilo Jiji kubwa zaidi nchini uingereza lenye kila aina ya raia wa nchi mbalimbali wanaoongea lugha tofauti tofauti,ikiwa ni ushahidi tosha kwamba Jiji Hilo ni kitovu Cha Raia wengi wahamiaji kutoka nchi nyingi duniani. Na sehemu kubwa iliyokuwa na idadi kubwa ya wahamiaji ni kusini mashariki mwa Jiji Hilo.

Lakini kwa mtu ambaye ni mdadisi akaamua kukatiza mitaa ya Jiji hili haswa kwenye maeneo ya wahamiaji wengi atagundua kitu kingine zaidi tofauti. Lazima angekutana na kina mama wamevalia mahijabu ,scarf pamoja na nikabu mavazi ambayo yanawafunika mwili mzima na kuacha tu sehemu ya macho . Wanaume wakiwa kwenye kanzu. Wengine wakiamini ni sehemu ya utamaduni wa kiislamu . Huku wengine wakiamini ni zaidi ya jambo lingine linafichwa.

Kwa kadiri mtu angetoka katikati ya Jiji Hilo na kwenda kwenye miji ya pembeni ya Oldham, Bradford na Burnley angekutana na misikiti ,maduka ya vitabu vya kiarabu,bidhaa mbalimbali ikiwemo mavazi na vyakula vya asili ya Asia. Na mtu angekatiza mitaa ya miji hii angehisi yupo katikati ya mji mojawapo ndani ya nchi za Asia ,huku lugha zao ikiwa ni tofauti kabisa na kingereza kimatamshi.

Miji hii lugha iliyotawala ni kiarabu. Na zaidi mtu angegundua wakazi Hawa wenye asili ya Asia wengi wakiwa wahamiaji ,wamejitenga mbali na Raia wengine wenyeji ,kuanzia muundo wa makazi Yao na pia kimavazi. Na wengi wao wakiishi maisha Yale ya communal. Na raia wa uingereza walipendelea kuwaita Asians kuliko kuwaita waislamu. Hii ni kwa sababu raia wengi wa uingereza huepuka mikwaruzano ya kidini , Maana waliamini kuwaita waislamu ni kama jina la kiubaguzi wa kidini dhidi yao.

Zaidi ya Hilo ni kwamba nchini humo ilionekana kwa wakati huo uislamu ulikuwa ukikuwa kwa Kasi kuliko ukristo. Waislamu wengi walizingatia ibada kuhudhuria misikitini kuliko wakristo walivyokuwa wanahudhuria makanisani. Ripoti zilionyesha dini ya uislamu ilikuwa inakua kwa Kasi ndani ya uingereza kukikadiriwa kulikuwa na waislamu milioni 1.6. Ikiwa dini ya pili kwa ukubwa baada ya ukristo.

Miongo miwili iliyopita ,nchi ya uingereza ilikuwa ni center ya imani mbalimbali za kiislamu barani ulaya nje ya mashariki ya kati. Uingereza iliwavutia wengi na ikapelekea kukua kwa imani mbalimbali ikiwemo wasuni ,washia na pia waisimailia. Vilevile London ilikuwa ni makao makuu ya vyombo kadhaa vya habari ikiwemo magazeti yenye ushawishi kama Al-hayat na Al-quds al-arabi.

Na vilevile Middle East broadcasting Company (MBC) pamoja na machapisho mengine yalikuwa London. Yote haya yakiwa yanafadhiliwa na makundi ya kijihadi huko mashariki ya kati.

Ukweli mchungu ni kwamba kwenye haya maduka ya Hawa raia wenye asili ya Asia kulikuwa kunauzwa pia vitabu ,majarida na machapisho mbalimbali ambayo yalikuwa yamepigwa marufuku sehemu nyingi duniani.

Hususan kwenye nchi za ulaya na marekani na pia kwenye Baadhi ya nchi za Asia. Hii ni kutokana na ukweli kwamba machapisho haya yalikuwa yanahamasisha na pia kuunga mkono harakati za kijihadi na ugaidi kwenye nchi ambazo zilikuwa ni adui kwa kwa kile walichokiita maadui wa imani ya kiislamu. Kwa mfano maduka haya yalikuwa yanauza vitabu kama vya mein-kampf Cha misimamo ya Hitler dhidi ya wayahudi na kingine kikiwa kinaitwa the protocols of the elders of Zion.

Machapisho mengine yalikuwa ni kama vile filisteen Al muslima(Muslim Palestine )ambacho kilikuwa kina glorify ugaidi dhidi ya Israel na vilevile kilihamasisha raia wa Palestina kuwa na chuki dhidi ya Israel kutokana na kuwakalia kimabavu. Chapisho hili lilikuwa linafadhiliwa na kundi la itikadi Kali la hamas la Palestina. Pia gazeti la Al- sunah lilikuwa linauzwa ,na lilikuwa likitoa ujumbe kwa jamii za waislamu kuungana katika kumpiga adui wa uislamu ambaye alikuwa ni marekani na nchi za ulaya kwa njia yoyote ile. Gazeti hili lilijulikana kama Risalat-al ikhwan(message of brotherhood).

Na Moja ya nukuu kwenye gazeti hili ilisema kwamba "Active resistance {muqawamah) to the occupation and the use of any available means to resist it are a religious Moslem duty, a national duty and a natural right anchored in both international law and the United Nations Charter."..

Watafiti na wachambuzi wa historia wanasema kwamba kuwepo kwa hayo machapisho yenye itikadi Kali yalikuwa tu ni tone la maji kwenye bahari. Inasemekana kwamba mikakati mingi ya ugaidi yalikuwa yalifanyika jijini London, ikiwemo kuchangishana michango kwa makundi ya kigaidi Ili kufanya recruitment na pia kuwezesha kufanikisha vitendo vya kigaidi. Ukitoa Afghanistan , Jiji la London lilikuwa ndio kama makao makuu ya shughuli za kigaidi kwa bara la ulaya. Na inasemekana harakati za kundi la Al Qaeda zilikuwa kwa Kasi jijini hapo. Kwa mfano machapisho mengi ya fatwa ya Osama bin laden yalichapishiwa uingereza .

Kuanzia miaka ya 1980 Hadi 1990 makongamano mengi ya makundi ya kiislamu yenye itikadi Kali pamoja na wanaharakati wa jihad yalifanyika uingereza. Wawakilishi wa makundi Kama hamas na Hezbollah walifanya vikao vyao vingi nchini humo kwa ajili ya kupanga mikakati Yao. Lakini yote Tisa , Je mamlaka za nchi ya uingereza zilikuwa wapi kipindi hiki Ili kuweza kubaini hizi harakati za haya makundi yenye mfungamano na ugaidi.?

uingereza iliamini kwamba hakuna Abaya . Kwa mfano baada ya kupigwa kwa majengo ya WTC na pentagon ,tukio la 9/11 Marekani ilianza kuwa vigilant na harakati zote za makundi ya kigaidi duniani na bunge la congress likaidhinisha bajeti kubwa ya kiulinzi kupambana na joka la ugaidi . Lakini uingereza kama mshirika wa marekani haikuona haja ya kujizatiti kiulinzi dhidi ya harakati za ugaidi..... A fatal mistake...

Hata baada ya mlipuko wa bomu wa London mwaka 2005, mamlaka za nchi hiyo hazikuweza kuamini kwamba hao waliojitoa mhanga ni raia wa nchi hiyo ambao walikuwa radicalized na makundi ya kigaidi. Na Wala hawakutaka kushutumu waislamu kwa tukio hili kutokana na kwamba lingezusha chuki za kidini nchini humo baina ya waislamu na wakristo au makundi mengine ya imani tofauti. Uingereza walijichanganya sana . Kwa kifupi hawakuwa siriazi kwenye vita ya ugaidi .

Kuna nadharia kama mbili hivi zinaelezea kwanini harakati za ugaidi zilishika Kasi sana nchini uingereza. Nadharia ya kwanza inaeleza kwamba makundi ya kigaidi yenye msimamo mkali kutoka afrika kaskazini na mashariki ya kati yalijipenyeza Hadi uingereza Ili kupata mazingira Salama kuendesha harakati zao. Nadharia ya pili inasemwa kwamba makundi ya raia kutoka nchi kama Pakistani, Bangladesh na Kashmir walioingia uingereza Miaka hiyo ya kuanzia 1980 kama wakimbizi ilichangia kwa kiasi kikubwa raia Hawa kujishughulisha na kusapoti ugaidi wakiwa nchini uingereza.

Makundi kadhaa yalikuwa yameamua kuutetea uislamu popote duniani kwa gharama zozote zile .
Wataalamu wa mambo wanasema kwamba Hizi harakati za kuutetea uislamu zilianza tokea karne ya ya kwanza ikidaiwa kwamba wanaharakati na wafia dini waliamini uislamu upo kwenye vita na makafiri hususan wa nchi za kimagharibi hivyo ingebidi kupambana kwa namna yoyote ile Ili kuilinda imani hii.

Kundi la kwanza la harakati la kuutetea uislamu lilikuwa linaitwa Tablighi jamaat lenye chimbuko lake nchini India na Pakistani . Hawa waliamini kwamba waislamu inawalazimu warudi kuishi kwenye misingi ya kiislamu na vilevile wajitenge na wasio waislamu . Kundi la pili lilitwa Muslim brotherhood lenye chimbuko lake nchini misri likiongozwa na Hassan Al banna na Sayed Qutb wenyewe Hawa walikuwa wamejikita zaidi kwenye mafundisho ya chuki dhidi ya wayahudi na misimamo Yao mikali ilikuwa inaitwa salafi. Kundi la tatu liliitwa Jamaat Al -islami likiongozwa na Sayed abu al maududi lenye makao yake huko nchini Pakistani haya yote yalikuwa na harakati sawa za kuutetea uislamu kwa gharama yoyote ile.

Kwa mfano kundi la Muslim brotherhood lilipotimuliwa kutoka nchini misri ,lilihamia Saudi Arabia Ili kuendeleza harakati zake na viongozi wake walipata uungwaji mkono kutoka kwa wahabi amabao ni kundi kubwa la waislamu nchini Saudi Arabia na Pakistani. Makundi haya yalijipenyeza mpaka uingereza kupitia raia wa kigeni wa nchi hizi kama wakimbizi au raia wahamiaji.Swali kubwa likabaki kuulizwa Je Hawa raia wa kigeni walikuwa wanasapoti harakati za ugaidi wakiwa uingereza? Maana raia Hawa mpaka wanahamia uingereza ni kwamba walihitaji maisha ya amani kama wengine wanavuohitaji , na Je inakuwaje makundi haya yanasapoti harakati za ugaidi kwa jina la uislamu?

Mkanganyiko miongoni mwa wanazuoni na wanahistoria walikuwa na mjadala mzito sana kutokana na haya maswala ya ugaidi. Wengine wakajiuliza inakuwaje maimamu wa kiislamu wanahubiri amani na upendo kwa nje lakini kwa upande mwingine wanahubiri chuki dhidi ya umagharibi na imani nyingine za kidini? Na wengine wakadai inakuaje makundi mengi ya kigaidi kama Hezbollah na hamas wanapata uungwaji mkono kutoka kwenye nchi za kiislamu kama Saudi Arabia na Pakistani?

Wengine waliamini huenda harakati za ugaidi ulijipenyeza kupitia hao hao wahamiaji na mbaya zaidi uingereza haikuwa makini katika kujishughulisha katika kuchunguza imani hizi za kidini kuepusha mgongano na migogoro . Inadaiwa kwamba mipango mingi ya ugaidi iliyofanyika kwenye nchi kama ;Pakistani, Afghanistan, Kenya, Tanzania, Iraq, Israel, Morocco, Russia, Spain na marekani ilikusukwa na magaidi waliokuwa wamekita kambi uingereza kwenye Jiji la London na maeneo mengine.

Kwa mfano gaidi aliyemuua mwandishi wa habari Daniel pearl aliyejulikana kama Ahmed Omar saeed sheikh alikuwa na connection kutoka London maana alikuwa na asili ya Pakistani mwenye uraia wa uingereza. Wengine amabao walikuwa ni wanachama wa Al Qaeda inasemekana kwamba walikuwa wanasuka mipango ya kulipua taasisi za kifedha kama mabenki nchini marekani. Hawa walikuwa ni Dhiren barrot, Nadeem tarmohammed na Qaisar shaffi. Wote Hawa walikuwa na uraia wa uingereza.

Mwingine alikuwa ni Muhammad billal mkazi wa Birmingham aliyeendesha gari lililojaa mabomu Hadi kwenye kambi ya polisi huko Kashmir...........

Wengine ni kama Richard Reid raia wa uingereza aliyesilimu na Sajid badat mkazi wa Gloucester Hawa wawili walipanga kulipua ndege ya shirika la ndege la American airline iliyokuwa inafanya safari kutoka uingereza Hadi miami nchini marekani bahati nzuri mabomu waliyokuwa wameficha kwenye viatu yalifeli kulipuka na walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Walipewa jina la shoe bombers. Pia walikuwepo raia wawili wa uingereza Omar Khan sharrif na asif Mohammed hanif waliolipua baa Moja mjini tel Aviv na kuua raia watatu wa uingereza mwaka 2003. Pia list hii ya magaidi waliokuwa na connection jijini London ilimhusisha raia mmoja aliyeitwa Azahar husin a.k.a demolition man aliyekuwa anajihusisha na kundi la jemaah islamiya lenye mfungamano na Al Qaeda.

Huyu alikuwa ni injinia raia wa Malaysia aliyesoma chuo Cha Reading fani ya uhandisi nchini uingereza na alipata mafunzo yake ya kuunda mabomu yale ya kujitoa mhanga miaka ya 1990 huko Afghanistan . Huyu alikuwa ni mastermind kwenye mashambulizi ya mabomu yalioua raia kadhaa kwenye visiwa vya Bali huko Indonesia . Inasemekana baada ya kufanya tukio lile na kuanza kufukuziwa na maafisa wa polisi wa Indonesia aliamua kujilipua mazima na bomu kuliko kukamatwa.

Pia inadaiwa kwamba mipango ya kufanya mashambulizi ya kigaidi marekani ikiwemo Yale ya 9/11 kwa sehemu ya mipango hiyo ilifanyika London.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye idara ya mahakama ya marekani ilisema kwamba Osama bin laden alianzisha kile walichokiita Media information office huko uingereza . Lengo la hii ofisi ilikuwa ni kuweka mipango yote ya Osama ya kigaidi kwenye vitendo na vilevile kufanya recruitment ya Al Qaeda members na pia kutoa funds kwa ajili ya hizo harakati zake. Kwa kifupi ofisi hii ilikuwa kama ni center ya Al Qaeda kwa nchi za magharibi ikipokea taarifa zote na kutuma kutoka kwa Osama .

Kikundi kingine ambacho kilikuwa ni sehemu ya Al Qaeda kiliitwa committee for defense and legitimate rights (CDLR) lilikuwa likijihusisha katika kutangaza harakati zote za Al Qaeda na kutetea propaganda. Kundi hili lilianzishwa na Mohammed Al massari raia wa Saudi Arabia aliyepigwa ban nchini kwake na kuhamia uingereza kutokana na kuhusishwa na maswala kadhaa ya ugaidi nchini humo. Huyu bwana mwaka 2004 aliwahi andika kwenye tovuti ya CDLR kwamba angetaka George bush rais wa marekani na tony Blair pamoja na washirika wake wauawe kutokana na mauaji ya raia yaliyokuwa yanafanyika nchini Iraq baada ya uvamizi wa marekani katika kampeni ya kupinga utawala wa Saddam Hussein iraq na ugaidi huko Afghanistan iwe kama ni collateral damage.

Kwa kifupi huyu alikuwa ni kama mwana propaganda aliyetumiwa na Al Qaeda katika ku justify na kutetea harakati zote za Al Qaeda. Hili CDLR lilihusishwa katika harakati za makundi ya kigaidi kwenye chi za afrika mashariki, Morocco , Algeria na maeneo ya mashariki ya kati. Ukweli mchungu ni kwamba harakati nyingi za makundi ya kigaidi yalifanya nchi ya uingereza kama base camp katika kufanya coordination za harakati na mipango yote na vilevile kuwezesha kifedha na pia kukusanya michango yote kutoka kwa wafadhili wa ugaidi. Nchi ya uingereza haikuweza kupata Intel yoyote kutokana na harakati za makundi haya. A fatal mistake.......

Inasemekana kwamba makundi kadhaa ya kidini ya msimamo mkali na yanayojihusisha na ugaidi yaliyopigwa marufuku kwenye nchi za kiarabu yalipata nguvu yakiwa nchini uingereza kutokana na mamlaka za nchi hiyo kutojihusisha katika ku monitor harakati za makundi ya kidini hususan yalitojiita ya kiislamu kwa kile walichokiita freedom of worship hivyo hawakutaka kuingilia dini za watu.

Kwa mfano kundi la Muslim brotherhood lilikuwa na mtandao mpana kwenye nchi za Palestina, Syria,misri,Libya na Iraqi. Kwenye nchi hizo kundi la Muslim brotherhood lilikuwa Lina operate kwenye kichaka Cha taasisi na asasi za kidini au kiraia. Kwa mfano kulikuwa na Muslim association of Britain, The Muslim welfare trust,the Palestine return center,Institute of Islamic Political Thought, Mashreq Media Services na zingine nyingi. Zote hizi zilikuwa na mkono wa support kutoka kwa Muslim brotherhood ambao walijikita nchini uingereza.

Pia kundi la wanaharakati la dhehebu la kiislamu la wahabbi la Ahle Hadith lililokuwa linapata support kutoka serikali ya Saudi Arabia lilihusishwa katika kuendesha mafunzo ya itikadi Kali kwenye madrassa huko Kashmir na Pakistani. kikundi hiki kilikuwa na vituo kama vinne nchini uingereza vilivyokuwa vinasimamia madrassa Kadhaa sehemu mbalimbali nchini humo. Mfano kwenye tovuti Yao waliwahi andika nanukuu"Be different from the Jews and Christians. Their ways are based on sick or deviant views concerning their societies.". Kutokana na misimamo yake mikali ya kundi hili,lilipigwa marufuku kwenye nchi nyingi za kiarabu hususan za kiislamu.

Kundi lingine la kidini ambalo pia lilikuwa na mafundisho yenye msimamo mkali lililopigwa marufuku liliitwa Hizb ut Tahrir lilikuwa na makao yake nchini uingereza. Kundi hili lilikuwa linahubiri kwamba kuwe na nchi za kiislamu na waongozwe na sharia law. Makundi mengine ni kama al-Muhajiroun, Al-Muntada al-Islami. Mfano kundi hili la Al muntada lililokuwa na makao yake mjini Leicester liliwahi kutuhumiwa na polisi nchini naijeria kujihusisha na ku support makundi yaliyolenga mashambulizi kwa wakristo na makundi mengine huko naijeria kaskazini.
Makundi haya yote yalikuwa yamejichimbia kambi uingereza.

Swali likabaki Je mamlaka za uingereza zilikuwa wapi mpaka haya makundi hatari yenye asili ya mashariki ya kati na Asia yaliyopigwa marufuku sehemu mbalimbali kushamiri nchini uingereza,?


LET'S DIG DEEPER
Inadaiwa kwamba mpaka haya makundi ya kidini yapate kukua kwa Kasi na kushamiri nchini humo kulianzia miaka ya 1970.

Inadaiwa kwamba wahamiaji kutoka Bangladesh, India na Pakistani walianza kuhamia uingereza na walikuja kwa ajili ya kufanya kazi kwenye viwanda vya kuchakata pamba na vya nguo kwenye miji ya Oldham, Burnley , Rotherham na Bradford kama cheap labor. Kutokana na uchumi wa dunia kuhamia kwenye viwanda na pia ushindani , viwanda vingi vilipunguza wafanyakazi huko uingereza na wengi wa Hawa wahamiaji wakawa kwenye Lindi la kukosa ajira. Ilitarajiwa Hawa wahamiaji watengeneze pesa Kisha warudi kwao lakini haikuwa hivyo.

Inadaiwa kwamba wahamiaji Hawa walikuwa pia wanapitia ubaguzi wa rangi kutoka kwa wenyeji na hali hii ikafanya wajitenge kivyao vyao huku wakiukumbatia utamaduni wa nchi zao . Na wengi ya Hawa wahamiaji walikuwa wametoka kwenye jamii maskini Zaidi hivyo kutokana na kukosa ajira wakaamua tu ku settle nchini uingereza kwa kuwa hakuna namna wangeweza kurudi kwenye nchi zao. Kwa mfano wengi wa wahamiaji Hawa walikuja uingereza ambapo walikuwa wanakimbia sheria Kali za kidini kwenye nchi zao hususan Pakistani.

Na hata walipofika nchini humo Japo walikuwa Wanafanya ibada za kawaida ambazo hazikuwa na misimamo mikali ,ni kwamba makundi fulani ya kidini ya msimamo mkali yalipata kujipenyeza. Kwa mfano kundi la kidini la Jamaat al-Islami lilianzisha misikiti kwenye miji ya Leicester. Na hapo ndipo baadhi ya waislamu wahamiaji taratibu wakaanza kuingizwa kwenye mafundisho yenye itikadi Kali haswa Yale ya kuanzisha nchi ya kiislamu na yenye Sheria za kiislamu a.k.a sharia law.

Na hapo ndipo mafunzo ya kidini yenye itikadi Kali yalianza kujipenyeza kwa Kasi sana kiasi kwamba Sasa ikawa ni tatizo jingine. Ikumbukwe Kipindi Cha kuanzia 1980 Hadi 1990 dunia ilikuwa inapigana vita baridi . Russia ilipoivamia Afghanistan kwa mara ya kwanza miaka 1980 , marekani na uingereza waliamua kusimama na wapiganaji wa kiislamu wa mujahedeen kwa kuwapa silaha na mafunzo Ili waweze kupigana na WA Russia. Lakini u.s na uingereza hawakujua wanaanza kumwagilia maji mti ambao ungekuja kutoa matunda ya sumu ya ugaidi ambayo yangekuja kuwadhuru wenyewe marekani na uingereza. Na hapo kupitia kikundi hiki Cha mujahedeen ambacho kilikuwa tayari kina itikadi Kali kikawa kinaamini kinapigana vita takatifu ya kiislamu ..

Viongozi wa kundi hili waliamini wanapigana na wapagani ambao hawakutaka uwepo wa dini ya kiislamu nchini Afghanistan. Ikumbukwe Russia wao wanaamini hakuna kitu kinaitwa Mungu,hivyo hii sababu inatumiwa na Hawa mujahedeen kupigana vita ya kiislamu dhidi ya makafiri. Wao uingereza na marekani wakiamini wanapigana na Russia kumkomoa kupitia Hawa mujahedeen kumbe Hawa wenyewe wanapigana vita walioamini ni ya kuutetea uislamu. Na hapo mafunzo ya kidini yenye itikadi Kali yalianza kubadilika na kuwa vita ya jihad na ikawa mojawapo ya nguzo ya imani.

Kikundi hiki Cha mujahideen waliamini kwamba nchi za magharibi hazitaki uwepo wa imani ya kiislamu hivyo ingewapasa kupigana vita ya jihadi, marekani na uingereza wasijue kwamba wao ndio next targets baada ya Russia. Lakini baada ya viongozi Kadhaa wa kikabila waliopinga utawala wa kiislamu nchini Afghanistan kufukuzwa /exiled miaka ya 1980, baadhi Yao walionya nchi za magharibi ikiwemo marekani kwamba nanukuu "For God's sake, you're financing your own assassins." Kutokana na kuwapa support kikundi Cha wapiganaji wa kiislamu wa mujahedeen.

Kwa mfano mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979 yaliyomweka ayatollah Khomeini madarakani yalipata uungwaji mkono na waislamu ambao walikuwa wakiishi Nchini uingereza. Punde tu baada ya ayatollah kuingia madarakani aliibadilisha Irani kuwa Islamic state na dini ya kiislamu ikawa ni kama political ideology ya kuiongoza nchi hiyo. Nchi za magharibi ikiwemo uingereza taratibu zikawa zinajipalia makaa ya moto .

Hii ni kutokana na mapinduzi haya kuzalisha mgogoro mwingine wa kitamaduni baina ya nchi za kiislamu na nchi za magharibi. Nchi za magharibi zikionekana hazijastaarabika na ni maadui wa uislamu. Kwa mfano ilitokea kisa kimoja Mwaka wa 1989 ambapo mwandishi wa riwaya wa uingereza aliyeitwa Salman Rushdie alichapisha riwaya Moja iliyoitwa SATANIC VERSES.

Riwaya hii ilikuwa ni kama dhihaka au tunasema satire kwa maana ilikuwa inakashifu uislamu. Kibongo bongo tungeweza kusema ni kama ile stori ya Kaptula La Marx au NCHI YA KUSADIKIKA zilizokuwa zinapinga siasa za ...... Anyway tuachie hapo.

Baada ya kitabu hiki kuingia mtaani kilileta shida sana kwa wenye imani zao na kupelekea maandamano makubwa ya waislamu huko Pakistani kupinga riwaya hii. Na hapo ndipo ayatollah Khomeini wa Iran alipotangaza fatwa ya kumhukumu Salman Rushdie popote atakapoonekana. Huyu bwana Rushdie aliamua kuishi maisha ya kificho kwa miaka mingi kuepuka kifo. Kama mnakumbuka huyu bwana Salman Rushdie mwaka 2022 nadhani alinusurika kuuawa huko marekani kwa kuchomwa na kisu . Hukumu yake bado inamfuatilia Japo ilitamkwa tokea Miaka ya 1980.

Maana kipindi hicho ilitangazwa yoyote angepeleka kichwa chake huko angepata zawadi nono na angepata thawabu..

Baada ya kutangazwa fatwa ya huyu bwana Rushdie , jamii ya waislamu waliopo nchini uingereza ilikuwa alerted na walililipinga hili adharani kwa kuandamana huku wakichoma vitabu vyake mtaani . Hili pia liliungwa mkono na aliyekuwa secretary wa Bradford council of mosques nchini uingereza aliyeitwa Sayed Abdul Quddus. Huyu bwana Alikiri adharani kwamba Rushdie amedhalilisha uislamu hivyo anastahili kinyongwa. Aliongea haya mbele ya waandamanaji na akaenda mbali zaidi na kusema nanukuu:"Muslims here would kill him and I would willingly sacrifice my own life and that of my children to carry out the Ayatollah's wishes should the opportunity arise."

Viongozi wa kidini pia wa Iran walipinga hili la hiki kitabu hadharani na kutoa misimamo mikali ya hatua kichukuliwa dhidi ya huyu Rushdie. Lakini haya yote na kauli za Hawa viongozi wa kidini kutamka waziwazi kwamba Rushdie anapaswa kuuawa ,lakini hakuna yoyote alitechukuliwa hatua za kisheria na mamlaka za serikali ya uingereza kuhusiana na hili la kuhamasisha mauaji. Lakini kama kawaida ya wanasiasa , waliamua kujichukulia umaarufu kutokana na hili sakata la Rushdie. Kwa mfano mbunge wa chama Cha labour wa Leicester bwana Keith vaz aliungana na waandamanaji zaidi ya 3,000 waliopinga sakata la Rushdie na kitabu chake . Hapo ikaonyesha unafiki wa wanasiasa.

Inadaiwa kwamba baada ya Rushdie kuandika hiki kitabu , raia wa uingereza ambao walikuwa ni waislamu walianza kufundishwa kwamba wapo hatarini katika kushambuliwa au kudhihakiwa na kile walichokiita makafiri. Sakata hili lilichukua sura mpya ya kidini. Na hata baada ya Khomeini kufariki , washirika wake walishikilia msimamo uleule kwamba Rushdie alipaswa kuuawa .

Na mbaya zaidi vita ya Bosnia ilipelekea waislamu wengi wa uingereza kuwa radicalized na kuwa wenye misimamo mikali. Kwa mfano waliamini kwamba kwenye hii vita ya Bosnia waislamu walikuwa wananyanyaswa na wenzao wakristo na mbaya zaidi haya yalikuwa yakitokea katikati ya bara la ulaya ambalo ni multi cultural society. Hivyo walihisi wao ni victims ...... Na kutokana na vita ya Bosnia , uingereza haikuchukua hatua yoyote kuingilia hii vita na hapo British Muslims wakaamini kwamba wao ndio walengwa. Hii ikasababisha baadhi Yao kujiunga na wapiganaji huko Bosnia kama sehemu ya kupigana jihad dhidi ya makafiri wa ulaya.

Na ni kipindi hiki makundi ya itikadi Kali za kiislamu kutoka nchi za Algeria , Libya na misri yalianza kuingia uingereza baada ya kufukuzwa nchini mwao kutokana na harakati zao za itikadi Kali na wakapata uungwaji mkono na waislamu wenzao nchini uingereza. Na wengi ya Hawa walipigana vita ya Afghanistan na Soviet. Na hapo wakaanza harakati zao za kuwafundisha wenzao harakati za itikadi Kali katika kupinga umagharibi kwamba utamaduni wa nchi za ulaya zipo against na mwenendo wa sheria za kiislamu.

Kwa mfano mwandishi wa habari wa Algeria aliyeitwa reda Hussaine aliyekuwa kwenye payroll za mashirika ya kijasusi ya ufaransa na uingereza kwa kutoa Siri za haya makundi ya kijihadi aliwahi kusema kwamba nanukuu ;They came to the UK, the only country that gave asylum and didn't ask a lot of questions........Thousands and thousands came, wave upon wave, saying they were being repressed in Algeria........" Huyu bwana alisema kwamba wengi ya makundi baada ya kufika huko uingereza walianza kuji organize dhidi ya kupinga umagharibi na wangetaka ulaya yote iwe chini ya sharia law.

Kwa mfano Afghanistan ilimtuma mhubiri aliyeitwa Abu Qatada Hadi London kwenye msikiti Finsbury Park mosque. Na mhubiri yake yalijikita zaidi katika fatwas ambazo zililenga kuwaua wale wote waliokuwa against na itikadi za kiislamu. Huyu Qatada alikuwa ni kama kiongozi wa kiroho wa kundi la mujahedeen jijini London na alikuwa pia anafadhili kichapishwa kwa gazeti la Algerian Terrorist group la GIA . Na vilevile huyu bwana alichukuliwa kama balozi au mwakilishi wa Osama bin laden huko ulaya.

Mahubiri ya huyu bwana Qatada yaliwavutia watu kama Zacarias Moussaou ambaye alikuwa kwenye jopo lililosuka mpango mkakati wa kuilipua WTC 9/11. Na mikanda ya video ya mafunzo ya huyu muumini wa Qatada , ilikutwa kwenye jengo alilokuwa anaishi bwana Mohammed atta huko Hamburg baada ya upekuzi . Atta ambaye alikuwa ndio the RING LEADER wa wale walioteka ndege zile zilozoenda kugonga WTC..........

Baki hapa tutaendelea
 
Huo ni ugaidi, si msingi wa jihadi, kujitoa muhanga ni kosa, kuua mtu asiye na hatiani kosa. Kufata dini kwa mihemko bila fikra huru lazima upotoke sehemu.

Lazima tu some dini.. Na hili ndilo la kwanza kwa mtume, alikazaniwa asome,
Vita ya kwanza mtume alipigana baada ya kuhama makkah ambao walikua wanakataza kuabudu, wanateswa, akahamia madina alikopata hifadhi, watu wa makkah hawakuridhika, wakawa wanawavizia njiani, wanapora misafara, choko choko haziishi, ndio mtume kuzichapa, sababu ya uonevu kuzidi.
Sasa wewe mtu unaswali kwa uhuru, unafanya kila jambo, jihadi ya nini.. Unakuta mtu wanakimbilia jihadi ila hata swala ambayo ndio nguzo kuu ya uislamu haifanyi... Mtu anakua brainwashed anapigana jihadi kumbe mzinifu, mzurumati.. Huu sio uislamu.

Enzi za mtume(nazungumzia himaya yake) kulikuwa na mayahudi, manaswara(wakristo) je aliwachinja, au waliishi kwa amani mradi tu hawavunji sheria za pale?

Kama mayahudi na manaswara ni wabaya mbona kulikuwepo sheria(ruhusa) kuwaoa hao watu wa kitabu(ahlul kitabu) mtu mbaya utapewa ruhusa umuoe.

Jihadi kubwa kabisa iliyobaki ni mtu na nafsi yake, labda kwa wale wanaoteseka na kunyanyaswa, hawa wana haki ya kupigana, kujitetea.
 
Huo ni ugaidi, si msingi wa jihadi, kujitoa muhanga ni kosa, kuua mtu asiye na hatiani kosa. Kufata dini kwa mihemko bila fikra huru lazima upotoke sehemu.

Lazima tu some dini.. Na hili ndilo la kwanza kwa mtume, alikazaniwa asome,
Vita ya kwanza mtume alipigana baada ya kuhama makkah ambao walikua wanakataza kuabudu, wanateswa, akahamia madina alikopata hifadhi, watu wa makkah hawakuridhika, wakawa wanawavizia njiani, wanapora misafara, choko choko haziishi, ndio mtume kuzichapa, sababu ya uonevu kuzidi.
Sasa wewe mtu unaswali kwa uhuru, unafanya kila jambo, jihadi ya nini.. Unakuta mtu wanakimbilia jihadi ila hata swala ambayo ndio nguzo kuu ya uislamu haifanyi... Mtu anakua brainwashed anapigana jihadi kumbe mzinifu, mzurumati.. Huu sio uislamu.

Enzi za mtume(nazungumzia himaya yake) kulikuwa na mayahudi, manaswara(wakristo) je aliwachinja, au waliishi kwa amani mradi tu hawavunji sheria za pale?

Kama mayahudi na manaswara ni wabaya mbona kulikuwepo sheria(ruhusa) kuwaoa hao watu wa kitabu(ahlul kitabu) mtu mbaya utapewa ruhusa umuoe.

Jihadi kubwa kabisa iliyobaki ni mtu na nafsi yake, labda kwa wale wanaoteseka na kunyanyaswa, hawa wana haki ya kupigana, kujitetea.
Kuua mtu asiye na hatia ni kosa!! Kwahiyo mwenye hatia ni sawa kuuwawa? Na huyu mtu mwenye hatia ni mtu wa aina gani?
 
Huo ni ugaidi, si msingi wa jihadi, kujitoa muhanga ni kosa, kuua mtu asiye na hatiani kosa. Kufata dini kwa mihemko bila fikra huru lazima upotoke sehemu.

Lazima tu some dini.. Na hili ndilo la kwanza kwa mtume, alikazaniwa asome,
Vita ya kwanza mtume alipigana baada ya kuhama makkah ambao walikua wanakataza kuabudu, wanateswa, akahamia madina alikopata hifadhi, watu wa makkah hawakuridhika, wakawa wanawavizia njiani, wanapora misafara, choko choko haziishi, ndio mtume kuzichapa, sababu ya uonevu kuzidi.
Sasa wewe mtu unaswali kwa uhuru, unafanya kila jambo, jihadi ya nini.. Unakuta mtu wanakimbilia jihadi ila hata swala ambayo ndio nguzo kuu ya uislamu haifanyi... Mtu anakua brainwashed anapigana jihadi kumbe mzinifu, mzurumati.. Huu sio uislamu.

Enzi za mtume(nazungumzia himaya yake) kulikuwa na mayahudi, manaswara(wakristo) je aliwachinja, au waliishi kwa amani mradi tu hawavunji sheria za pale?

Kama mayahudi na manaswara ni wabaya mbona kulikuwepo sheria(ruhusa) kuwaoa hao watu wa kitabu(ahlul kitabu) mtu mbaya utapewa ruhusa umuoe.

Jihadi kubwa kabisa iliyobaki ni mtu na nafsi yake, labda kwa wale wanaoteseka na kunyanyaswa, hawa wana haki ya kupigana, kujitetea.
Mkuu!Tulia kwanza.Pia ishu za dini utolewa kwa dalili.
 
Kuua mtu asiye na hatia ni kosa!! Kwahiyo mwenye hatia ni sawa kuuwawa? Na huyu mtu mwenye hatia ni mtu wa aina gani?
Vizuri, mfano, mtu aliye kuja kuiba nyumbani kwako Tena na silaha akiwa anataka kukudhuru, ruksa kumuua, mtu anataka kuanza kukudhuru(kukuua) ruksa kumaliza.

Vibaya kuanza wewe, mtu kajikalia zake, hana hili wala lile na wewe unapiga bisu, au kujilipua kufa nae ni kosa. Mmebishana, ama mmetofautiana mitazamo, ubishi wa vitu tofauti ndio umuue, ni kosa.
 
Back
Top Bottom