Ukweli wa video hii ni upi? Je, mauaji haya ni kweli yalitokea Zanzibar?

Swadakta mkuu,unaweza kusaidia kuongezea nyama kuhusu yaliyojiri baada ya yale mapinduzi japo kwa muktasari?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiitizama hiyo video unamsikia muelezaji anayechukua anataja mpaka tarehe ilikua kwenye 18-20 jan. Nakumbuka niliitizama Africa Addio yenye English Subtitle mana ilikua ya lugha ya kitaliano.
Tatizo kuu la mapinduzi yale hayakuwa na mwenyewe. Wanamapinduzi halisi (au waliojiona wanamapinduzi) walipinduliwa siku hiyo yamapinduzi yenyewe. Kassim Hanga, Mdungi Ussi, Saddala, Abudu Mmasai na wengine ambao kwa uhalisia wao ndiowaliokua ma plnner wayale mapinduzi ndani ya Zanzibar. Kina Okello na Genge Lake ambalo lilitokea Tanga pamoja na Jeshi la Mwalimu wali take-over kila kitu. Na ndio Karume akatangzwa kua raisi Kwa matakwa ya Nyerere huku Hanga akibakia kutoa macho tu. Hanga alitangazwa waziri mkuu baada ya siku tatu akabadilishwa cheo akawa Makamo wa Raisi.
Huku kilichokua kinaendelea nyuma ni kuwaua kila aliekua mfuasi wa vyama vya Z.P.P.P na Z.N.P
Kwa miaka mingi tumelazimishwa kuaminishwa kama vyama vya Z.N.P na Z.P.P.P vilikua ni vyama vya waarabu tu. Wakati Walikuepo Waafika wengi sana ndani ya hivyo vyama kuanzia ngazi za wanachama mpaka viongozi. wametutengenezea dhana za kibaguzi ili tuwasuport kwa kupitia asili zetu. Lakini Mwisho wa ubaya ni aibu. Picha za wazi zinaonesha walivokua wakiwaua Waafrika wenzetu.
 
Unajibu kama kwamba mimi ndiye nilihitaji kujua. Elezea kile unachokijua kuhusu hayo mapinduzi na hiyo clip iliyowekwa hapo. Mambo ya Nyerer na Sultani hayatuhusu kwani wao hawapo kwenye picha hii. Tunacho bishania hapa ni huyo aliyeiweka hii clip kuwa ati ni watu wa Zanzibar walikuwa wanauliwa. Halafu kaweka clip ambayo ilikuwa inachukuliwa na mtu aliyekuwa kwenye chopa. Jamani, hebu tuambieni; Alikuwa mwandishi wa habari wa channel gani huyo ambaye mwaka 1964 alikuwa na uwezo wa kuchukua hizo picha kwa kutumia chopa??
Acheni kuwaharibu watoto wetu kihivyo. Malkia alipokuja Kenya unajua alikuja kwa ndege gani?? Iwezekaneje mwandishi wa habari atembelee chopa?? Acheni uongo huu. Historia ya Zenj mmeshaiharibu vya kutosha wala hakuna tena awezaye kujielewa ni lipi lilitokea.

Mtoto wako hajaharibiwa, Mkuu wewe ndie ulieharibiwa akili.
jaribu itafute uipitie documentary hii Africa Addio. Hii documentntry ipo tokea 1965. siyaleo mkuu. Na imerokodiwa na Wazungu nasio CUF au Waarabu mkasema kwamba wanapinga matunda ya Chama Tawala.
 
Mtoto wako hajaharibiwa, Mkuu wewe ndie ulieharibiwa akili.
jaribu itafute uipitie documentary hii Africa Addio. Hii documentntry ipo tokea 1965. siyaleo mkuu. Na imerokodiwa na Wazungu nasio CUF au Waarabu mkasema kwamba wanapinga matunda ya Chama Tawala.

Hii hapa mkuu wasije wakasema hawajaiona,sakata la zanzibar linaanzia kwenye 1:00:00

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajibu kama kwamba mimi ndiye nilihitaji kujua. Elezea kile unachokijua . Halafu kaweka clip ambayo ilikuwa inachukuliwa na mtu aliyekuwa kwenye chopa. Jamani, hebu tuambieni; Alikuwa mwandishi wa habari wa channel gani huyo ambaye mwaka 1964 alikuwa na uwezo wa kuchukua hizo picha kwa kutumia chopa??
.

Mi siwalaumu sana nyie wazee,brainwashing mliyofanyiwa na bwana Mchonga ilikuwa vere effective,kama wewe na utu uzima wako pamoja na uwapo wa google unaweza kusimama kifua 'mbere' ukatoa hiyo statement hapo juu basi haina hata maana ya kuendeleza mjadala na wewe,miaka ya stini major powers zilikuwa zinashindana kwenye space race mambo ya kuexplore anga,wewe eti unashangazwa na waandishi kutumia chopa,hivi unafahamu kuwa vita ya pili ya dunia iliyoisha mwaka 1945 ilikuwa well documented kwa picha za video tena za aina zote ikiwamo hizi aerial?,ingia youtube tafuta docuseries inaitwa APOCALYPSE.WORLD WAR 2 ndo utaelewa nini namaanisha

Hapa naorodhesha baadhi ya helicopter za miaka ya 60
Hyo iliyobeba ndege inaitwa boeing. CH-47 chinook imetoka mwaka 1962
640px-Ah-1cobra_1.jpeg
341px-Chinook_airlifting_an_F-15_(2).jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu Cha mwalimu Nyerere (the influence of Nyerere ), cha mwaka 1995 (uk-172) kina sema .. uhuru wa Zanzibar ulipatikana alhamisi ya December 10 .1963.sultan akiwa mkuu wa nchi ya Zanzibar nakupewa mamlaka ya kumteua mrithi wake "..
Mapema mwaka huo huo Mwalimu Julius Nyerere . Aliionya serikali ya uingereza kwamba ikiwa itatoa .mamlaka kwa chama cha watu wachache " Kina-choongozwa na waarabu cha ZNP "... Maamuzi hayo yataifanya Zanzibar kuwa sehemu ya Mashaka ..

Ndani ya Majuma ma-5 tu serikali hiyo ilipinduliwa na masiha mjinga .Ambaye ni kiongozi wa wanaharakati (JOHN OKELLO)

Baada ya kipindi kifupi cha vurumai na mauaji (OKELLO) alisimika baraza la mapinduzi chini ya Uongozi wa Abeid aman karume ....

Kwa hiyo mkuu kwa kukujibu tu swali lako " Hayo mauaji Yalitokea kipindi cha vurugu za mapinduzi yaliyo asisiwa na Bwana john okello na rafiki wake wa karibu shekhe abeid aman karume .... ni mauaji Ambayo yaliua takribani ya watu 1.2000.

Nadhani nitakuwa nimekujibu ..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini umemuita masiha mjinga mkuu
 
Bado hujaelewa mkuu mbona majibu ni mazuri sana unataka utajiwe na majina ya marehem mkuu?
Mkuu shukrani kwa jibu lako,lakini ningependa kujua zaidi kuhusu yanayoendelea kwenye hii video,kwanini hawa watu waliuwawa,waliouwawa ni akina nani,na nani aliwauwa,nani alitoa amri,na hawa waliokuwa wakirekodi hii footage ni akina nani na kwanini hawakuchukua hatua yoyote,kwanini hili jambo halizungumziwi wala kufundishwa mashuleni etc etc,maswali ni mengi

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTEJ
 
Mi siwalaumu sana nyie wazee,brainwashing mliyofanyiwa na bwana Mchonga ilikuwa vere effective,kama wewe na utu uzima wako pamoja na uwapo wa google unaweza kusimama kifua 'mbere' ukatoa hiyo statement hapo juu basi haina hata maana ya kuendeleza mjadala na wewe,miaka ya stini major powers zilikuwa zinashindana kwenye space race mambo ya kuexplore
Kwa hivyo wakazileta Zenj kuja kuchukua picha za wazalendo wakiuawa. Yaani hata script ya senema huwezi itofautisha?? Ulimwengu huo ulikaa kimya kwa sababu watu waliuliwa na maji au mizinga?? Pathetic
 
Kwa hivyo wakazileta Zenj kuja kuchukua picha za wazalendo wakiuawa. Yaani hata script ya senema huwezi itofautisha?? Ulimwengu huo ulikaa kimya kwa sababu watu waliuliwa na maji au mizinga?? Pathetic
Mzee wangu twende taratibu,kwanza tumekubaliana pasipo shaka kuwa uwezo na rasilimali na vitendea kazi vya kuweza kuchukua ile aerial footage kutoka kwenye chopa ulikuwapo mwaka 1964?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi,

Kuna hii video ipo youtube kitambo kidogo, inaonesha watu wakiuawa kwa mamia, wengine kwenye plots na wengine fukwe. Video inadaiwa kuchukuliwa Zanzibar mwaka 1964.

Kwa wataalamu wa historia, wachambuzi na Wajuzi tujuzane, ni kweli hii ni Zanzibar? Je, nini kilikuwa kinaendelea mpaka watu hawa kuuawa kama kuku, kama sio Zanzibar ni wapi?

Ujue kama ni upotoshaji tuiripoti hii video youtube iondolewe kwa "kuchafua taswira" ya visiwa vyetu pendwa na wahusika waliyoipandisha wapelekwe Mahakamani.



Sent using Jamii Forums mobile app

Video hiyo si ya kweli, hakukuwepo na kamera za video wakati huo pia picha zilizopigwa wakati huo hazikuwa za rangi.
 
Angalia Documentary Africa Addio,ina kipande kinaonyesha mauaji hayo mwanzo mwisho.
Kuna muitaliano alikua anarekodi matukio yote baada ya uhuru Africa.
Bongo nyerere walikula ubwabwa wazungu wakapewa hadithi wakapanda zao meli haoo na matarumbeta wakapigiwa ya kuagwa pale feri ikulu.
Huyu jamaa muitaliano na rafiki yake wamedocument matukio mengi sana. Walifika mpaka congo. Kule nigeria ile vita ya Biafra waliireport vzuri sana. Kule youtube unaipata video yote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu twende taratibu,kwanza tumekubaliana pasipo shaka kuwa uwezo na rasilimali na vitendea kazi vya kuweza kuchukua ile aerial footage kutoka kwenye chopa ulikuwapo mwaka 1964?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama ulikuwepo lakini usingeliweza kutumika Zanzibar kwa sababu; Kwanza ilikuwa dola changa sana ambayo pia uhuru wake ulikuwa na mushkeli. Pili; Haikuwa ni Zanzibar kwa sababu mauaji hayo kama yangelitokea, lazima yangepigiwa kelele na wakoloni kwani ndio kwanza tu wamewapa uhuru. Sultani alikuwa hata hajajiandaa kujiunga kokote. Tatu; Sutani alikuwa na undugu na Oman wdhani ndugu zake wasingelipiga kelele?
Nasema, sikatai walikufa watu ila sio kwa umati ule. Waarabu wale walikuwa hata hawajajua ni nini maana ya kujitawala.
 
Hata kama ulikuwepo lakini usingeliweza kutumika Zanzibar kwa sababu; Kwanza ilikuwa dola changa sana ambayo pia uhuru wake ulikuwa na mushkeli. Pili; Haikuwa ni Zanzibar kwa sababu mauaji hayo kama yangelitokea, lazima yangepigiwa kelele na wakoloni kwani ndio kwanza tu wamewapa uhuru. Sultani alikuwa hata hajajiandaa kujiunga kokote. Tatu; Sutani alikuwa na undugu na Oman wdhani ndugu zake wasingelipiga kelele?
Nasema, sikatai walikufa watu ila sio kwa umati ule. Waarabu wale walikuwa hata hawajajua ni nini maana ya kujitawala.
Mkuu sitaendelea mbele nahuu mjadala mpaka tukubaliane kwanza kuwa aerial videography kutokea kwenye chopa ama ndege ilikuwa ni kitu cha kawaida mwaka 1964,hata huko zanzibar.

Exhibit #2


Hiyo ni exerpt kutoka kwenye muvi ya mwaka 1954 zaidi ya miaka 10 kabla ya mapinduzi ambayo sehemu iliigiziwa zanzibar,angalia kuanzia sekunde ya 12 hadi 20.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom