Ukweli wa Polepole Usipuuzwe kwa Sababu ya Hulka

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Ni ukweli kwa 100%, ni vigumu sana kumwunga mkono jambazi akisema kuwa ujambazi ni mbaya. Lakini ukweli hautabadilika kuwa alichosema jambazi ni sahihi ingawa yeye mwenyewe hakiishi.

Kuna kauli kadhaa alizozitoa bwana Polepole ambazo zinaishi. Ni kauli za kweli, japo Polepole mwenyewe licha ya kuujua ukweli wa kauli zake, hakuweza kuupigania wala kuuishi.

CCM KWENYE UCHAGUZI HURU NA WA HAKI, HAIWEZI KUSHINDA-Polepole
Nani anaweza kuikataa kauli hii? Kila mwanaCCM mwenye akili anaujua ukweli huu. Kikwete anayesadikika kufinyanga matokeo yaliyompa ushindi rafiki yake wa damu, anaujua ukweli huu. Siro anaujua ukweli huu. Bashiru anaujua ukweli huu. Mahera anaujua ukweli huu. Mzee Mangula anaujua ukweli huu. Lakini Polepole, ni mwanadamu, ana tumbo, ana ndugu, na anastahili kuishi. Akateuliwa kuwa kiongozi wa chama ambacho chini ya uchaguzi huru na haki hakiwezi kushinda lakini kwa sasa kina kila nyenzo, pamoja na kumhakikishia maisha ya raha na starehe. Je, akatae? Mbona makocha huwa wanakubali kwenda kufundisha timu ambazo wanajua hazitashinda?

WAKUU WA WILAYA NA MIKOA WALIKUWA NI VIBARAKA WA WAKOLONI WILAYANI NA MIKOANI. KWA SASA HAWANA KAZI-Polepole
Nani ataukataa ukweli huu? Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa, wana kazi gani? Kikubwa tunachoambiwa, eti ni wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama. Lakini kiuhalisia, ndiyo wavurugaji wakubwa wa usalama na amani kutokana na kutaka kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama kwa manufaa ya CCM. Hivi kwa nini wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama, asiwe OCD na RPC? Baada ya muda, Polepole aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya, nafasi ambayo hakuna kazi zaidi ya kuwa kibaraka. Polepole mlitaka akatae? Akatae wakati inampa uhakika wa maisha? Kumbukeni wapo wanaolima tumbaku lakini wanaamini kabisa kuwa tumbaku ni sumu. Lakini wafanye nini, kama tumbaku ndiyo itakayomfanya aitwe baba wa familia?

KATIBA MPYA NI HITAJI LA WATANZANIA-Polepole
Nani mwenye akili anayeweza kupinga kauli hii ya Polepole? Mwalimu mwenyewe baye ni Baba wa Taifa letu aliwahi kutamka kuwa katiba yetu inamfanya Rais kuwa dikteta. Kwa mantiki hiyo marais wote wa Watanzania walikuwa madikteta kwa mamlaka yao ya kikatiba. Tofauti yao ilitokana na hulka binafsi na siyo maelekezo ya katiba. Polepole alipoteuliwa kuwa katibu mwenezi, akapewa kazi maalum, kazi ya manunuzi. Aliifanya kwa ufanisi, japo alijua siyo hitaji la Watanzania, lakini afanyeje, wakati ndiyo kazi aliyoipata na ndiyo inampa uhakika wa maisha? Hivi wale wafanyakazi wa kusafisha vyoo mahospitalini, mnadhani wanaifurahia ile kazi? Kama hawaifurahii, kwa nini wanafanya?

TUSIPOKUWA MAKINI KUNA KIKUNDI KINAWEZA KUIPOKA SERIKALI MAMLAKA, NA SERIKALI IKABAKIA KUWA MWANASESERE-Polepole
Nani anapinga ukweli wa kauli hii? Lisu naye katamka kauli inayofanana na hii, akisema amepewa taarifa toka kwa watu serikalini. Naye Rais Samia kasema kuwa miezi 6 alitulia kuwasoma mawaziri. Wengine wakaanza kufanya yao. Polepole anayasema haya akiwa mbunge wa kuteuliwa, akishiriki kwenye bunge bandia lililopatikana kwa matakwa ya mtu mmoja. Lakini tulitaka akatae uteuzi wa kwenda kwenye bunge bandia wakati hapo patampa uhakika wa maisha?

Hongera Polepole kwa kauli sahihi, japo umeshindwa kuziunga mkono kwa vitendo. Kuziishi kwa vitendo, labda uwe na ujasiri na uzalendo wa hali ya juu kama wa Tundu Lisu. Na kwa nchi hii, ukimwacha Hayati Maalim Sefu, Freeman Mbowe, Ben Saanane, Sugu, Mchungaji Msigwa, Askofu Mwamakula, Askofu Niwemgizi, Askofu Shayo, Askofu Bagonza, wale mashujaa wa Zanzibar, sidhani kama kuna mtu anayeweza kuukaribia ujasiri, uzalendo, weledi na ukweli wa nafsi wa Tundu Antipasi Lisu, ndiyo maana sisi wengine tumebakia kuwa warriors wa kwenye mitandao. Hivyo hatuna haki ya kukulaumu Polepole, japo, kwa hakika, unaweza kukataa kuutumikia udhalimu kwaajili ya kutetea haki kama umeamua kuwa mkweli wa kauli, nafsi na matendo kwa nia ya kuzipa nguvu kauli zako.
 
Huyu anatafuta cheo ili asiendelee kuongea hana lipya. Vilevile anavyoongea havipo TZ katiba yetu Raisi ni mfalme
 
Mwanasesere😁😁😁

0AIS-7z.jpg
 
Anatafuta kuwekwa jikoni tu, hizo nyingine zote kelele, kama kweli analna CCM imepoteza muelekeo aondoke.
 
Polepole hana jipya,kwani kaifanyia Nini nchi hii kilicho na manufaa? Polepole anajua kuwa 2020 yeye na Dr Bashiru waliahiriki kuwatapeli wagombea ubunge na udiwani wa CCM kwenye kura za maoni.Ni ushahidi usio na Shaka kuwa waliahiriki kuingiza madarakani serikali dhalimu ya ccm 2020. Leo polepole hapaswi kuwatisha watu Wala kututoa kwenye mstari wa KATIBA MPYA.Yeye aendelee kuhunika na makahaba mambo ya taifa letu tutayaweka sawa wenyewe.Tupo tunapigania KATIBA MPYA Kama anaweza aamka hata saa tisa usiku aungane na sisi.Mbowe Kwanza polepole atusu irie.
 
Heshimu mamlaka iliyopo kwani nawe ulikuwa kwenye mamlaka iliyopita na hukusema hayo unayo yasema sasa kumbuka pia kuwa Kila kitabu na zama zake zama zile za vitisho na jeuri zishapita hizo Kaa mguu sawa na unyamaze kabisa kwani wengi japo sio wote tunafurahia uhuru tulio nao"KAZI IENDELEE HASWA"
 
Kumbuka pia ww ni mteule wa rais hayo majivuno na maneno ya hovyo hovyo unayatoa wapi na kiburi hicho unakitoa wapi cha kuongea maneno hayo ya upuuzi ulio pitiliza unataka kutuaminisha mambo ambayo hayaaminiki.Bado tuna imani na rais wetu wa JMT na kumbuka pia usichukilie poa Kwa mamlaka iliyopo na kumbuka pia rais ni taasisi pia,Kwa hiyo usijitoe ufahamu kuonekana hamnazo
 
Back
Top Bottom