Ukweli wa bandarini

Juma wa Juma

Senior Member
Jan 13, 2017
150
221
Jambo la kwanza tumshukuru mungu kwa neema zake then nasikitika kwa wasomi na wanasiasa kutudanganya watanzania na muda mwingine kutupotosha. Yalotokea Bandarini baada ya Magufuli kufika na kuwa anaongea na wanabandari aliruhusu makontena ya mchanga then akaruhusu maswali akaulizwa akajibu.

Kuna afisa wa TRA ndo akatoa taarifa kuhusu Container lenye document linaloonesha mitumba ya nguo na viatu ila limekutwa na MAGARI kwenye kitengo kinaitwa RMG na hukomakontena huwa watakaguliwa na TRA pamoja na polisi ndio tukaenda kushuhudia na kupiga picha.

Kuhusu magodoro huwa yanawekwa kuzuia gari lisijigonge na kuchunika hiyo ni kawaida so watu wasipotoshe kwa maslahi yao ya kisiasa na aina ya ujanja huu huwa unafanywa na wajanja ila safari hii wamenaswa.
 
Kama ni kweli wamekamata hilo container mbona safari hii hawajataja ni la nani.Mbona hayo mengine walitaja ni ya mgodi gani.Kweli kweli container likamatwe kuna magari ndani muhusika mpaka leo asijulikane Yaani angegbewa kama mpira wa corner.
 
Kuna habari nilikuwa naitazama kuhusu wizi wa gari nzuri nzuri ( voque, sports, audi, vw, bmw, benz sedan na s.wagon new model kama sio 2015 basi juu yake.....yaani gari za maana sana) toka UK kuja africa na baadhi zilishafika kenya na uganda na nahisi zipo hata tanzania, usafirishaji wake hauwi wa kawaida. utafichaje gari ndani ya kontena tena inaanza mbele kule then unaiziba na mitumba kama sio ya dili. watu wamepiga sana hii nchi acha hao wanaonaswa wachache wawe mfano.
 
Mkulu analilia font page ..muda c mref ataanzisha skendo za michepuko atokee na kweny udaku
 
Tulikuwa tunataka kumaliza Movie ya Bashite ili wananchi wote waanze kuangalia na kusikiliza Movie mpya ya Bandarini.

Lakini tunawalaani sana waandishi wa magazeti binafsi ambao hawajashiriki kututangazia hii movie mpya na tukatishe ile ya zamani ya Bashite Vs Gwajima. Imekuwa kama ISIDINGO haifiki mwisho ndio maana tulitaka kuikatisha tuanze upya.
 
Wewe nae mleta MAADA ni MPUUZI kamwe haujataka kufikiri.....Hakuna anaekataa ya kuwa NI KWELI magodoro yanaweza wekwa kuzuia GARI lisipolomoke kwenye container...LAKINI JE HIZO DOCUMENT ZA HIZO COINTAINER NI kweli ZIMEANDIKA kuna gari humo au wameandika vinginevyo?????......Haya mambo yapo kabsa mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu mtu anaandika document tofauti kabsa na kilichomo kwenye container.....
 
Hiyo comedy ya bandarini inamdhalilisha sana rais...
Yaani badala ya kutoa maelekezo na yakatekelezwa yeye mguu mguu anaenda kufanya upekuzi..!?
Wenye akili zao serikalini wataendelea kumdharau sana...
"..Hatuchukui hatua hadi aje mwenyewe.."
 
Yaaani magufuli anatafuta kiki kwa nguvu sana,ili aonekane ana uchungu na nchi kumbe hamna kitu.aache ujanja ujanja bana
 
Kama ni kweli wamekamata hilo container mbona safari hii hawajataja ni la nani.Mbona hayo mengine walitaja ni ya mgodi gani.Kweli kweli container likamatwe kuna magari ndani muhusika mpaka leo asijulikane Yaani angegbewa kama mpira wa corner.

Usanii tuu km kawaida yao, hilo lilikuwa pale tangu weeks earlier na hao wazambia walishakamatwa na kupewa dhamana...!! Ni ishu ambayo iliibuliwa na interpool na mengine yalishapita !! Mungu anawaona na atawaadhibu siku moja !
 
Niliona kama container moja ina range rover, kama ile range rover inatokea Europe kwa wakati huu haiwezekani tena kusafirisha container bila ya kudiclear mna nini, kama mna gari lazima iambatane na logbook, makontainer yote yanapigwa scanner kabla ya kuondoka eu, na kama alivyosema mleta uzi magodoro hutumika kuzuia magari yasigongane.
 
Wewe nae mleta MAADA ni MPUUZI kamwe haujataka kufikiri.....Hakuna anaekataa ya kuwa NI KWELI magodoro yanaweza wekwa kuzuia GARI lisipolomoke kwenye container...LAKINI JE HIZO DOCUMENT ZA HIZO COINTAINER NI kweli ZIMEANDIKA kuna gari humo au wameandika vinginevyo?????......Haya mambo yapo kabsa mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu mtu anaandika document tofauti kabsa na kilichomo kwenye container.....
Kama wale walioleta mabasi kibao kwa document za pikipiki, mabasi yakaaza kusafirisha abiria kwa kutumia kadi ya piki piki, mabasi mengine kama matatu kutumia kadi moja ya gari na plate namba zifananazo. HII NDO TZ BWANA.
 
Back
Top Bottom