Fortunatus Buyobe
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 463
- 1,127
Wanajamvi.
Umuofia kwenu....
Jana nimepata habari za ndani juu ya hili sakata la kukamatwa kwa kontena zikisemekana ni mitumba. Kiufupi hapo zamani watu walidanganya sana nature ya mizigo iliyo ndani ya kontena tena ujanja wao wote walikuwa wakifanya kwa kivuli cha transit cargo.
Ujue transit cargo hapo mwanzo zilikuwa hazilipi VAT na hata ukaguzi wake kwenye scanner ulikuwa hafifu kwani ilikuwa haina maslahi kimapato ingawa hii mizigo ilikuwa inabaki humuhumu. Ujio wa scanner mpya na msimamo wa JPM kuwa lazima kila mzigo upite scanner ndio umefumua madudu mengi.
Kulingana na mtoa taarifa wangu anasema "kweli JPM amefanikiwa kuwapoteza wapiga dili wengi bandarini" kwani pale scanner kuna wanajeshi,TISS,TRA na watu wa bandari. Pia port manager ameweka informers kibao. So ili upige dili hawa wote mpaka uwaweke sawa.
Turudi kwenye mada
Inasenekana huyu Bwana ukwaju aliingiza hizi kontena tangu mwezi wa tisa mwaka jana. Ikumbukwe kuwa hii ilikuwa ni kawaida ya bwana ukwaju kukwepa kodi kwa njia hiyo ya kusingizia mitumba na pia kufanya ni transit.
Sasa Bwana ukwaju alimtumia dogo flani aende kwenye kampuni ya clearing( sitaitaja) ili mzigo utolewe mwaka huu February. Ujue agent yeye huwa anafanyia kazi taarifa anazoletewa. Sasa Bill of lading ilionuesha ni mitumba. Hii bill of lading inajazwa ulaya wakati agent hayupo so hapa udanganyifu umeanzia kwa shipping line.
Ok agent akaendelea kufanya kazi yake mpaka akawa amepata release order. Lakini ikaja kugundulika mzigo unadaiwa zaidi ya $80,000 ikiwemo na storage charge(kumbuka mzigo wa tangu September mwaka jana) Bwana Ukwaju alikuwa ameshaanza kunegotiate apunguziwe gharama kwa kuwaandikia TRA bila ya agent kujua.
Sasa TRA wakawasiliana na agent kumjulisha juu ya negotiations alizoanzisha bwana ukwaju. Hapa kengele ya hatari ikalia kwa agent. Kumbuka wakati hili kontena linashughurikiwa tayari bwana ukwaju alishaleta kazi nyingine of the same nature kupitia kwa dogo aliyemtuma mwanzo.
Agent baada ya kuwa na mashaka akamwambia dogo anaomba akutane na mwenye mzigo ndipo bwana ukwaju akaenda kwa agent akamwambia yeye achape kazi tu kwani kila mtu ni wake mle bandarini.
Agent kwa kutotaka kuharibika akawaandikia TRA kuwa anajitoa katika shughuri za kushughurikia huo mzigo na atafutwe agent mwingine. Ikumbukwe haya yote yametokea kabla ya kontena kukamatwa au kupita scanner.
Sasa bwana ukwaju sijui alitafuta agent mwingine au la? Lakini inasemekana mzigo haukupita scanner na tayari alikuwa ameshapanga timu yake ili kutoa mzigo. Nadhani kulikuwa na mazingira ya kuzungukana mzigo ukakamatiwa getini ukiwa katika hatua za mwisho za kutoka. Au ni mainformer ndio walitoa taarifa hilo mie sijui. Ndipo mzigo ukaamuliwa urudishwe scanner na ubainika kumbe sio mitumba bali ni range rover.
Bwana ukwaju alishafanikiwa kutoa gari zingine mfano ile inayoonekana ina namba za zanzibar ilishatolewa ikaenda zanzibar na kupewa namba wakati ile gari documents zilionyesha ni transit to zambia.
Ile gari ilikamatiwa zanzibar na inavyoonekana alikuwa anawatumia agents tofauti tofauti. Ile picha inayooshesha gari yenye namba za Zanzibar ni kwenye kituo cha polisi bandari. Kwa hiyo hakuna uongo katika hilo.
Sema sio sawa kusema JPM alikamata yale magari. Magari yalikamatwa either kwa kuzungukana kwenye pesa au kwa mamlaka husika kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kama haya magari yalikamatwa baada ya kuzungukana. Je, nini maana ya kuwa na taasisi nyingi za usalama pale bandari? Inamaana wameamua kujiunga for common interest? Gari ilifanikiwaje kufika geti la kutoka bila ya kupita scanner? This is a home work for JPM.
TUNDU LISSU
Rais wa TLS ameshaingia katika kumtetea Bwana ukwaju. Naomba hili lisichukuliwe kisiasa kwani anatekeleza majukumu yake ya kutetea hata muuaji. Kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa hata akiwa ni muuaji. Lissu amelalamika kwa nini Bwana ukwaju anashilikiwa na polisi kwa siku 23 bila ya kufikishwa mahakamani au kupata dhamana.
Hili nalo ni la msingi ili haki za watuhumiwa zilindwe. Inasemekana Bwana ukwaju ana ukwasi wa kutisha. Inasemekana polisi wananufaika sana na ukaaji wake pale kituoni kwani ukikaa na waridi lazima unukie waridi.
Wasalaam
Ndimu mkata shombo