Watuhumiwa 7 wa upotevu wa makontena bandarini waliokuwa wametoroka wamekamatwa

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wafanyakazi saba kati ya wanane wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) waliotuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandarini ambao walitoroka, wamepatikana na tayari wanaendelea kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma hizo.

Watumishi hao ni kati ya watuhumiwa 15 wa TPA waliotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa wameshiriki kuondosha makontena na magari hayo kutoka katika bandari kavu saba bila kulipa ushuru wa Bandari.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi alisema jana kuwa mfanyakazi mmoja kati ya hao wanane, hajapatikana; na anaendelea kusakwa na polisi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Wote walishapatikana kasoro mtumishi mmoja, Happygod Naftali, ambaye huyu alishaacha kazi siku nyingi baada ya viongozi kuanza kufuatilia suala hilo; lakini bado polisi wanaendelea kumsaka,” alisema Ruzangi.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha watuhumiwa hao, kukamatwa na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

“Ni kwamba tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Sirro licha ya kuwa hakutaka kutaja idadi ya wafanyakazi wa TPA ambao wamepatikana. “Kwa kweli idadi nitaitoa siku nitakapozungumza na waandishi wa habari wiki hii,” alifafanua.

Watumishi waliokuwa wanasakwa na polisi waliopatikana kwa mujibu wa Ruzangi ni Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonasweet Kimaina, Zainab Bwijo na Nathan Edward.

Watumishi hao wanaungana na watumishi wengine saba John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman na Benadeta Sangawe waliokamatwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Watumishi hao saba, kwa mujibu wa Sirro, tayari walishapelekwa mahakamani.

“Ukiacha wale saba ambao tumeshawafikisha mahakamani, hawa wengine bado tuko nao tunaendelea kufanya upelelezi,” alieleza.

Wafanyakazi hao wanatuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,884 na magari 2,019 ambayo yalitoroshwa kutoka katika Bandari Kavu (ICD) saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na hivyo kuipotezea Serikali mapato ya Sh bilioni 48.55.

Kuhusu mawakala 280 waliopewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo yao makao makuu ya TPA namna ya walivyohusika kulipia makontena hayo, Ruzangi alisema mamlaka yake inajipanga kutoa taarifa kamili juu ya suala hilo.

“Tunaendelea kuandaa taarifa ya kilichotokea na kilichobainika kuhusu mawakala hao, tutatoa taarifa hivi karibuni,” alisema Meneja Mawasiliano huyo.

Tangu Rais John Magufuli aingie madarakani, uongozi wake umeibua ufisadi wa kutisha ambao ulikuwa unafanywa Bandari ya Dar es Salaama kwa kuwashirikisha wafanyakazi wa TPA na mawakala pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Kwa mara ya kwanza upotevu wa makontena 349 uligundulika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutinga bandarini na kubaini makontena hayo kutolewa bandari kavu bila kulipiwa kodi.

Upotevu huo ulifanya vigogo wa TRA, akiwemo Kamishna Mkuu Rished Bade na makamishna wengine kusimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Baadaye Majaliwa alibaini upotevu wa makontena 2,431 yaliyoondolewa bandari kavu bila kulipiwa ushuru wa Bandari.

Katika sakata hilo, baadhi ya mawakala wa forodha walifungiwa kufanya biashara na TPA Sakata la mwisho ni la kupotea kwa makontena 11,019 na magari 2,019, ambayo yaliondolewa kwenye ICD saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na kuipotezea serikali mapato ya Sh bilioni 48.
 
Mpaka mnawakamata hao wafanyakazi wa bandarini maana yake mnakiri kuwa wamefanya kosa tena kosa la uhujumu uchumi na rushwa. Lakini mbona wanashughulikiwa peke yao tu?au hizi sheria dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi zinawahusu peke yao tu?Vipi kuhusu wale wafanyabiashara wamiliki wa hayo makontena mbona hawaguswi?hii vita ya kupambana na ufisadi haitakuwa na maana yoyote kama hayo mapambano mtayaelekeza kwa watumishi wanaoshawishiwa lakini hamtaki kuwagusa wanaoshawishi hizi rushwa yaani wafanyabiashara,watu binafsi na hata viongozi wa serikali.
 
Mbona katika list hii wale wa Kaskazini wako wengi?
Ndio waliosoma na kujipatia nafasi nyeti tangu siku nyingi. Kihistoria, hakuna ubishi ni eneo ambalo lilikuwa na shule nyingi sana ikilinganishwa na maeneo mengine. Kuna vijana wengi tu kutoka Kanda ya Ziwa tulisoma katika shule za Kaskazini na kufundishwa na walimu wengi kutoka Kaskazini mfano Mosha, Mushi, Malle, Mbuya, Shayo n.k. Hakuna anayewakamata eti kwa sababu ni wa Kaskazini bali ni kwa sababu 'wamepiga fedha' kupitia nyadhifa zao.
 
Serikali ina mkono mrefu ila tungependa kuona hao jamaa wanachukuliwa hatua za kisheria. Ikiwezekana wafilisiwe kabisa ili kurejesha theamani ya hela walizochukua na jela inawahusu.
 
Mpaka mnawakamata hao wafanyakazi wa bandarini maana yake mnakiri kuwa wamefanya kosa tena kosa la uhujumu uchumi na rushwa. Lakini mbona wanashughulikiwa peke yao tu?au hizi sheria dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi zinawahusu peke yao tu?Vipi kuhusu wale wafanyabiashara wamiliki wa hayo makontena mbona hawaguswi?hii vita ya kupambana na ufisadi haitakuwa na maana yoyote kama hayo mapambano mtayaelekeza kwa watumishi wanaoshawishiwa lakini hamtaki kuwagusa wanaoshawishi hizi rushwa yaani wafanyabiashara,watu binafsi na hata viongozi wa serikali.

Hii ndio Tanzania. Kama kweli kinachofanyika ni kwa nia njema, naamini hao wafanyabiashara pia watakamatwa vinginevyo tunatafuta sifa kwa kuwaumiza waajiriwa wa serikali tu.
 
Hata ya kufukuza na kukamata watunishi wa umma mnataka yatangazwe kwa mbwembwe kuonyesha serikali inafanya kazi. Lakini kutuonyesha upande wa pili Mawaziri na serikali ikihojiwa na kuelezwa uchafu na madhaifu yake live hamtaki na mpaka mnatumia majeshi kuzuia hilo kwa nini?
Ni wazi hapa kuna maigizo ya aina Fulani na hawataki kuumbuka. Ila ukweli usiooangalia mzee Pombe utaumbuka mapena sana haijapata kutokea kwa kiongozi mwingine
 
t
Mpaka mnawakamata hao wafanyakazi wa bandarini maana yake mnakiri kuwa wamefanya kosa tena kosa la uhujumu uchumi na rushwa. Lakini mbona wanashughulikiwa peke yao tu?au hizi sheria dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi zinawahusu peke yao tu?Vipi kuhusu wale wafanyabiashara wamiliki wa hayo makontena mbona hawaguswi?hii vita ya kupambana na ufisadi haitakuwa na maana yoyote kama hayo mapambano mtayaelekeza kwa watumishi wanaoshawishiwa lakini hamtaki kuwagusa wanaoshawishi hizi rushwa yaani wafanyabiashara,watu binafsi na hata viongozi wa serikali.
unaanza na watumishi ndio waliopewa dhamana. mfanyabiashara hakushikii bunduki kupokea rushwa.
 
Jikite katika kujadili
Huo uchafu Wa upande Wa pili ili usemwe ni lzm TBC tu iwe live ,kwa hiyo mitambo ya TBC ikigoma uchafu hautasemwa tena. Sikutarajia kama upinzani una akili fupi kiasi hiki.!!!

Mbowe ana magazeti yake ni kwa nini asitumie hayo kuwaeleza watz?!.?

Mbona anapobadili gia angani anatumia ,ITV, Azam, Eatv kuwaelezea watz , sasa hivi anashindwa nini
mada wewe umekalia siasa tuu mara Mbowe mara gia hebu jikite kwenye huu uzi kwanza...Tanzania Kwanza then vyama vyenu baadae
 
Na
Ndio waliosoma na kujipatia nafasi nyeti tangu siku nyingi. Kihistoria, hakuna ubishi ni eneo ambalo lilikuwa na shule nyingi sana ikilinganishwa na maeneo mengine. Kuna vijana wengi tu kutoka Kanda ya Ziwa tulisoma katika shule za Kaskazini na kufundishwa na walimu wengi kutoka Kaskazini mfano Mosha, Mushi, Malle, Mbuya, Shayo n.k. Hakuna anayewakamata eti kwa sababu ni wa Kaskazini bali ni kwa sababu 'wamepiga fedha' kupitia nyadhifa zao.
Kusoma kuna uhusiano gani na kuwa mwizi? Luna faida gani kuwa msomi mwizi?
 
Mpaka mnawakamata hao wafanyakazi wa bandarini maana yake mnakiri kuwa wamefanya kosa tena kosa la uhujumu uchumi na rushwa. Lakini mbona wanashughulikiwa peke yao tu?au hizi sheria dhidi ya rushwa na uhujumu uchumi zinawahusu peke yao tu?Vipi kuhusu wale wafanyabiashara wamiliki wa hayo makontena mbona hawaguswi?hii vita ya kupambana na ufisadi haitakuwa na maana yoyote kama hayo mapambano mtayaelekeza kwa watumishi wanaoshawishiwa lakini hamtaki kuwagusa wanaoshawishi hizi rushwa yaani wafanyabiashara,watu binafsi na hata viongozi wa serikali.
yaani mkuu hiii nchi sheria zinawahusu watu wadogowadogo wale wahusika wakuu huwez kuskia kes zao zinaishaje,...
wao huwa wapo juu ya sheriaa,..
kes ya masamaki haipo hot now chek it bro,..
ndo problem la hii nchi watu wanaanza kwa mbwembweeeee
mwsho wa cku nothing happen
 
“Ni kwamba tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Sirro licha ya kuwa hakutaka kutaja idadi ya wafanyakazi wa TPA ambao wamepatikana. “Kwa kweli idadi nitaitoa siku nitakapozungumza na waandishi wa habari wiki hii,” alifafanua.
upelelezi,...
upelelezi ganiiii wakati watu hadi wanakamatwa tayari na ushahidi upo,...
tatzo la nchiiiii ndo hilooo,...
longolongo nyingi,.
hapo watu washapata mianya ya rushwa tyr kupiga ela za watuhumiwaa
 
Back
Top Bottom