Ukweli ni upi "Rais kafanya" au "Serikali imefanya"?

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,542
2,172

Maneno haya yanamaana sawa kimantiki " Rais kafanya X " " Serikali imefanya Y " au " " Tumefanya Z " tumia lolote utakuwa sahihi tu.​


Kunabaadhi ya wenzetu wameishiwa hoja hasa huku mitandaoni kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipinga kwa nguvu zote kutumika kwa sentesi " Rais X kafanya mradi Y".

Watu hawa mara zote wanahoji niwapi huyu Rais X kapata huu ukwasi wa kutekeleza mradi Y? Jambo ambalo kisiasa wanadhani linamuinua zaidi huyu Rais X kwa kupewa endorsement ya mradi "Y".

Wakati wote watu hawa ambao wengi wao ni watu kutoka Upinzani wamependekeza itumike sentesi " Serikali X imetekeleza mradi Y".


UFAFANUZI WANGU
____________________

Kwanza, Kisiasa :
Sote tunafahamu ili tuweze kushinda Uchaguzi wowote ule popote tunahitaji mambo matano makubwa ambayo ni,

1. Mgombea Mzuri


2. Mtandao au Chama

3. Agenda|Ilani ya Uchaguzi

4. Organization au timu kampeni

5. Rasilimali, fedha, vitu na watu


Sasa kwahoja hii naomba tuangazie hitaji la tatu la kushinda Uchaguzi ambalo ni " ILANI YA UCHAGUZI " Ilani ya Uchaguzi inaweza kuwa yakuandikwa au yakutamkwa,

ILANI YA UCHAGUZI maana yake ni ahadi za mgombea au chama kwa Wapigakura au wananchi.
Tuelewane vizuri hapa tumesema Ilani ni ahadi ya mgombea au Chama wala sio ahadi ya Serikali kwa wapigakura au wananchi, nadhani hapa tunakubaliana wote,

Tukubaliane pia huyu mgombea baadae anaweza kushinda na kuwa Rais X, Sasa bila kusahau kuna ahadi aliwaahidi wapigakura wake yeye kama yeye yaani akishinda atafanya miradi X,Y,Z.

Kwaufafanuzi huu wa Ilani ya Uchaguzi kama miradi X,Y,Z ikitekelezwa na aliyekuwa Mgombea wa nafasi X ambae alishinda Uchaguzi huo kwa ahadi hizo na sasa anazitekeleza kama alivyoahidi ubaya unatoka wapi tukisema " Rais X katekeleza miradi X,Y,Z? "

Pili kimuundo :
Rais wa JMT ndio Raia namba moja wa JMT ndie mkuu wa Serikali ndio afisa manunuzi mkuu, ndie mshauri mkuu wa bajeti ndie mtia saini wa mwisho wa sheria ya bajeti unakataaje hajafanya wakati kila kitu kinaanzia na kuishia kwake!!


Tatu, Rais ndie mwenye mamlaka ya kusimamia pesa yote ya nchi kabla na baada ya bajeti kwenye kutekeleza miradi ya nchi kwani ndie aliyepewa dhamana na ndio atakayeulizwa ifikapo mwaka 2025 kulingana na Ilani yake iliyopita hivyo anafanya kwa niaba yetu

Nne, Urais ni taasisi, Sisi sote tuko chini ya Rais wa JMT akiwa kama Raia namba moja wa nchi, Hivyo tuvifanyavyo tunavifanya kwa niaba ya Nchi na Rais wetu ndio maana likitokea baya lawama zote kwa Rais wa nchi kwanini linapotokea jema mnasita kusema kafanya hili Jema iweje Rais apokee mabaya tu mema asipokee?

||Serikali inafanya kwa niaba ya Rais na Rais anafanya kwa niaba ya wanachi||
 
Duuuh kweli we Jabali

Hapo kwenye Ilani nimepapenda zaidi,
Awamu hii CHADEMA kazi mnayo,
 
CHADEMA wanataka useme ni mabeberu yamefanya au wananchi wamefanya, Wanaogopa sana jina Samia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom