Ukweli na uwazi kwenye mapenzi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Waafrica HIV/UKIMWI tunafanya ni siri. Ukosefu wa kinga mwilini unachangia muamko wa magonjwa mengi kwenye mwili, kuanzia cancer, TB, magonjwa ya akili ect. Lakini ni kwa Afrika ni kumvunjia heshima mtu kwa kusema anaumwa cancer lakini pia aligundulika na HIV.

Tunapokuja kwenye swala la mapenzi. Mzungu ni mwepesi sana kusema by the way I can not have unsafe sex since I am HIV+. Mwanaume wa kiafrica atajua kabisa status yake lakini hasemi akwambie kwani wewe dada yake?

Tubadilike jamani.
 
Hata wewe dada unaye kubali kupigwa bila kinga na mtu ambaye hujamjua hata historia yake vizur wewe ndiyo shida...Hali ya afya ni siri ya mtu tena ukichukulia umepata mtu kwa kumtamani tu na unataka 1 night stand kwanini umweleze siri ya afya yako..Ngono salama ni lazima sana kwa mtu usiye mjua vizur na kama mko na serious relatn muende mkapime kwa pamoja mjue status zenu...
 
Hata hivyo kaka zangu wengi hawapendi mipira. Ndiyo maana nimeona niliseme hili hapa.
 
Nikulizwa mimi kama mwanaume nitajibu..Wanawake wengi ndiyo hawapendi kutumia Kinga kwa vigezo kadhaa..Kuna wanaosema wanapataga Fungus pindi wanaposhiriki tendo na mwanaume alievaa mpira...Kuna wengine wanaosema ndom huwapunguzia ladha ya tendo....Ila kwa sababu hizo toka kwa mwanamke haziwezi nibadilsha msimamo wangu kama mwanaume wa kutumia kinga..
 
Hata wewe dada unaye kubali kupigwa bila kinga na mtu ambaye hujamjua hata historia yake vizur wewe ndiyo shida...Hali ya afya ni siri ya mtu tena ukichukulia umepata mtu kwa kumtamani tu na unataka 1 night stand kwanini umweleze siri ya afya yako..Ngono salama ni lazima sana kwa mtu usiye mjua vizur na kama mko na serious relatn muende mkapime kwa pamoja mjue status zenu...
Umejibu mambo mengi kwa pamoja lakini nimekuelewa kuwa swala la afya kwetu bado ni siri yako kubwa hii inatokana na tabia ya kunyanyapaa wenye VVU.
 
Nikulizwa mimi kama mwanaume nitajibu..Wanawake wengi ndiyo hawapendi kutumia Kinga kwa vigezo kadhaa..Kuna wanaosema wanapataga Fungus pindi wanaposhiriki tendo na mwanaume alievaa mpira...Kuna wengine wanaosema ndom huwapunguzia ladha ya tendo....Ila kwa sababu hizo toka kwa mwanamke haziwezi nibadilsha msimamo wangu kama mwanaume wa kutumia kinga..

Hii inatokana na ukosefu wa uelewa katika umuhimu wa kulinda afya. Ninadhani hii dhana ya kutoongelea vitu kwa uwazi inachangia. Nilikuwa ninaongea na rafiki kutoka Ghana aliniambia walifeli sana katika kuinua public health miaka ya 2000. Walikwenda sehemu za wazi na kuwaelimisha wakina mama matumizi ya mipira(condom).

Waliwaeleza zitawalinda na magonjwa pia uzazi usio na mpangilio, kutokana na tabia zetu za kutoongelea mambo wazi wale public health officers walionyesha uvaaji wa ndomu kwenye kidole gumba. Baada ya mwaka mmoja waliporudi kuonana na wamama wengi walikuwa na watoto wadogo na walilalamika ile mipira haikusaidia, waliulizwa mliitumia? Walisema ndiyo wakati wa tendo husika tulivaa mipira kwenye vidole gumba.

Ilitakiwa wademonstrate na kwenye artificial manhood ili walengwa waelewe sasa ile posho yote iliyotolewa kwa promotion ya public health ni kama ilimwagwa mferejini.
 
Upo sawa kabisa Uwazi katika maswala yote ya kujamiana na Elimu ya uzazi inachukuliwa kuwa ni kitu cha siri sana na kisichofaa kuzungumzwa hadharani kwa uwazi wake....Kitu kingine pia ni mapenzi yaliyopitiliza mtoa mada yawezekana una Elimu ya kutosha jinsi ya kujilinda na maambukizi yanayosababishwa na Ngono zembe...Inakuja tokea umempata mwenza ambaye umempenda mno na hauku tayar kumpoteza kabisa kwan amekizi vigezo vyake vingi shida jamaa huyo anakuambia mimi nataka nipige mzigo tena bila Ndom na kama nikupima afya hakuna shida panga siku tutaenda tu lakini leo nimezidiwa naomba game...Hapo ndipo kina mama wengi wanaposhidwa kufanya maamuzi sahihi. ama wanakuja shtuka too late..
 
Mtu makini anajilinda mwenyewe, ukitaka kulindwa inakula kwako!

Ni mpaka uwe na uwelewa huo. Kuna watu bado wanafanya ngono zembe kwa kutokuelewa. Ni dhahiri elimu na maarifa uliyonayo ndiyo yamepelekea wewe kuwa na uelewa ulionao.
 
Upo sawa kabisa Uwazi katika maswala yote ya kujamiana na Elimu ya uzazi inachukuliwa kuwa ni kitu cha siri sana na kisichofaa kuzungumzwa hadharani kwa uwazi wake....Kitu kingine pia ni mapenzi yaliyopitiliza mtoa mada yawezekana una Elimu ya kutosha jinsi ya kujilinda na maambukizi yanayosababishwa na Ngono zembe...Inakuja tokea umempata mwenza ambaye umempenda mno na hauku tayar kumpoteza kabisa kwan amekizi vigezo vyake vingi shida jamaa huyo anakuambia mimi nataka nipige mzigo tena bila Ndom na kama nikupima afya hakuna shida panga siku tutaenda tu lakini leo nimezidiwa naomba game...Hapo ndipo kina mama wengi wanaposhidwa kufanya maamuzi sahihi. ama wanakuja shtuka too late..

Nono labda kwa uelewa nilionao lakini 5 minute pleasure na kunywa vidonge kila siku, nonono a big no.
 
Kama tungekuwa tunanasema No no no nyingi hivi kasi ya maambukizi ya ukimwi ingekuwa imepungua sana kama si kwisha kabisa...
 
Ukijielewa kuwa wewe binafsi unathamani ya pekee katika maisha yako, wewe binafsi unawajibu wa kutunza afya yake, afya. Kuzaliwa na afya njema ni zawadi ya pekee na unaweza kuipoteza hiyo zawadi kwa uzembe wa dakika tano. Ni mifano tu ya kukufanya umkache handsome boy asiyetaka mpira.
 
Kama tungekuwa tunanasema No no no nyingi hivi kasi ya maambukizi ya ukimwi ingekuwa imepungua sana kama si kwisha kabisa...

Umenikumbusha binti wa rafiki yangu alipata mchumba, tuliambiwa ni mtoto wa kigogo fulani wa serikalini ndiyo amerudi alikuwa anasoma Europe, siwezi kutaja nchi. Hakuna aliyeweza kufikiria wale wawili wapime afya zao, tulicheza chereko harusi ya nguvu.

Akiwa mjamzito ndiyo yule binti aligundua ameambukizwa, taharuki ndiyo tunaletewa file la jamaa kumbe alikuwa anaishi na mama mashangingi huko majuu kwa kukwepa gharama za maisha.

My take, don't judge the book by it's cover.
 
Utamaduni katika jamii ni suala la msingi katika kukuongoza ni jinsi gani utachukua maamuzi yako.

Ukipanda basi mara nyingi kama sio zote utakuta wameandika "abiria chunga mzigo wako". Ukiingia kwenye nyumba za watu Kuna jumbe zinasema "ya humu tuachie wenyewe". Tukiwa kwenye chumba cha mitihani haturuhusiwi kuonyeshana majibu au kujadili. Kwa maana hiyo mfumo wa makuzi na malezi yetu umejengwa katika "usiri (ubinafsi?)

Kwa maana hiyo Tatizo sio sisi wanaume bali ni makuzi na malezi tuliyopewa na kurithi katika jamii.
 
Back
Top Bottom