Mpende kila mtu, mheshimu na jua ana mchango fulani kwenye maisha yako

Theofrey Theofrey

New Member
Jul 30, 2022
4
10
Dunia yote ni kitu kimoja, sisi binadamu ni kitu kimoja. Huu ndiyo ukweli ambao ukiuelewa na kuuishi kila wakati utakuwa na maisha bora. Tumekuwa tunaambiwa na jamii zetu, kwamba kundi letu ni bora kuliko la wengine, kwamba rangi yetu ni bora au asili na kabila letu ni bora kuliko nyingine.

Wote huu ni uongo ambao umeleta machafuko makubwa hapa duniani. Sisi sote ni kitu kimoja na tunategemeana sana ili tuwe na maisha bora hapa duniani. Mpende kila mtu, mheshimu na jua ana mchango fulani kwenye maisha yako.

Hata kama mtu anafanya mambo mabaya kwako, bado kuna mchango mkubwa unaoupata kupitia mabaya anayokufanyia. Kumbuka uzuri na mabaya ni pande mbili za shilingi moja. Be calm.
 
Back
Top Bottom