Ukweli mchungu: Hutavuka mpaka wa Tanzania bila kupata chanjo ya COVID-19

Kukataa isikatae serikali,ila wasubili kwanza (wapewe mda).kwa sababu ugonjwa wenyew na chanjo bado vinaichanganya dunia
 
Mkuu kumbuka hayo ni majaribio ya chanjo,
sio chanjo yenye uhakika.
---hivi mtu akishapata chanjo ,,kama ana uhakika hatopata corona tena ,,,sasa ya nn kujishughulisha na mtu asiyetaka chanjo?
Sia aachwe asiyechanjwa ajifie zake?

Hiyo chanjo ni biashara ya lazima ya Biliget na genge lake la kihuni.

,Na Bado baadhi ya inchi hazijakubaliana na hilo la cheti cha chanjo.

---Maana hawaoni sababu ya kuchanja na chanjo yenyewe ni majaribio .

--- pia chanjo yenyewe itauzwa bei ghali sana kwa inchi husika.

Kwahyo hilo ni jambo la kukubaliana na kulipitisha kwa pamoja ,pengine ni baada ya miezi kadhaa kupita.
 
Ulichoandika hakina mashiko kwa wanaojua maana ya chanjo

Wao wakishapata chanjo maana yake hawawezi tena kupata hayo maambukizi milele.

Sasa wawazuie wengine kwenda huko kwa sababu gani?

Mambo mengine yanahitaji common sense tu na si rocket science!
 
Chanjo ya nini wakati huku kwetu Maralia ni hatari kuliko Corona!! anaetaka kwenda nje ya nchi atapewa masharti husika ya nchi aendayo , kuna mambo ya kuumiza kichwa sio chanjo
 
Tunaweza kushuhudia viongozi wa ngazi za juu wa taifa letu wakizuiliwa airport kwa kutokuwa na vyeti/muhuli/alama za chanjo ya covid 19 tena umetoka Tanzania wanakodai tulipuuzia mbinu zao.
Pole sana.

Asikudanganye mtu kwamba hao unaowaita "viongozi wa ngazi za juu wa taifa letu" wataacha kuchanja. Hawatakutangazia wewe, lakini chanjo wataipata na safari zao hazitaathirika kwa lolote huku wakikulaza usingizi wewe uzidi kukomaza shingo na kukuimbisha wimbo wa "Uzalendo" feki.

Na wakati mwingine watakuhadaa tu kuwa kazi zote wanafanya mabalozi walioko huko nje.

Huu ni utawala wa maigizo, subiri tu utayasikia mengi.

Lakini nikuulize swali, inakuwaje wewe ndie ulete mada kama hii hapa jamvini. Akili zilizokuwa zimekuruka zimerudi?
 
Back
Top Bottom