#COVID19 Ninachokifahamu sahihi kuhusu Chanjo ya Covid-19, niulize swali nitakujibu

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Kumekua na sintofahamu nyingi mtaani na wengi wanajiuliza maswali kuhusu Chanjo ya Covid, Naomba nieleze kwa jinsi ninavyofahamu na kama una swali niulize nitakujibu kadri ninavyofahamu.

Kwanini Chanjo ya COVID 19 inapigiwa chapuo sana Licha ya kwamba ni hiyari?

- Hii ni kwasababu dunia nzima ipo katika mpango na juhudi za kutokomeza kabisa ugonjwa huu, ndio maana chanjo inasisitizwa sana kwasababu bila watu wote kuchomwa chanjo itakua ni ngumu sana ugonjwa huu kuisha.

Kwanini wanaochoma chanjo wanaendelea kuvaa barakoa? Je nikipata chanjo naweza kuambukizwa na kuambukiza?

- Wanaopata chanjo wanashauriwa kuvaa barakoa kwani wanauwezekano pia wa kupata maambukizi ya korona, iko hivi,
Chanjo Ya korona inapoingia mwilini mwako inaboost immunity, yaani inauongezea kinga mwili wako, kinga hii inayoongezwa inauwezo mkubwa wa kupambana na UVIKO, maana yake wewe uliepata chanjo tayari utakua na kinga utakapopata maambukizi ya UVIKO mwili wako utaweza kupambana na virusi hivyo na hatimaye kutoweka maana tayari una kinga ya kujilinda.

Kwanini baaadhi ya chanjo inatakiwa uchomwe zaidi ya mara moja?

Ni kawaida sana baadhi ya chanjo kuchomwa zaidi ya mara moja ili kuimarisha zaidi kinga mwili, mfano kuna chanjo za Tetanus Taxoid (chanjo ya tetenasi) hii huchomwa mara tatu kwa mwanaume na mara tano kwa wanawake pia zipo chanjo nyingine za watoto ambazo huchomwa zaidi ya mara moja, pia katika chanjo za korona zipo baadhi ambazo unachomwa zaidi ya mara moja na nyingine ni mara moja tu kama Johnson Johnson.

Kwanini baadhi ya mataifa ya magharibi licha ya chanjo ila uginjwa bado upo na watu wanakufa kwa covid?

Ni kwel hata baadhi ya mataifa ambayo chanjo imetengenezwa huko bado wanaugonjwa na watu wanakufa lakini kiuhalisia sio kwa idadi ile kama ya mwanzo.

Mfano mzuri anagalia China ambako ugonjwa umeanzia, kule sasahivi wanaelekea kusahau mambo ya Corona kwasababu zaidi ya 90% wamepata chanjo.

Angalia Ulaya sasahivi hata watu wameanza kufunguliwa angalia michuano ya Euro watu waliruhusiwa kuingia uwanjani na ugonjwa ulienea lakini sasahivi upo very week kwasababu watu wameshapata chanjo.

Angalia nchi ya Italy kipindi cha COVID walikufa sana kwa siku walikua wanakufa zaidi ya watu elfu 6, lakini kwa sasa idadi ya vifo haipo kwasababu wengi wameishapata chanjo hivyo virusi vya korona vimedhoofishwa sana havina nguvu tena.

Kwanini Chanjo ya COVID imechukua muda mfupi sana? je tutaaminije kama haitaleta madhara baadaye?

Hakuna muda malumu uliowekwa wa chanjo kutengenezwa, hata hiyo chanjo ya kifua kikuu ambayo wewe umezaliwa ukaikuta, pia kipindi inatengenezwa wapo watu waliokua wa kwanza kuitumia na haijawadhuru.

Rejea ugonjwa wa Ebora ulilipika Congo, Siera lion, na equatorial Guinea, ugonjwa ule ulilipuka ghafla na utengenezaji wa chanjo yake haukuchukua muda mrwfu na chanjo ilionyesha ufanisi mkubwa mpaka leo hii ebora imebaki kuwa historia.

Je, chanjo ya Covin ndiyo Alam ya 666?

Hayo mambo yamekaa kiimani zaidi na sio kisayansi na kusema kwamba chanjo ni chapa ya 666 ni sababu zisizo na mashiko kwani hata kwenye maandishi chapa ya mnyama hadi itokee tayari dunia itakua imeshapitia kipindi cha kuabudu siku moja na kuwa na serikali moja pia chapa ya mnyama itakua inahusisha moja kwa moja mpinga kristo.

Je, Wazungungu wanataka kutuua kupitia chanjo?

Wakuue kwa lipi, wangetaka kukuua wasingeruhusu nchi mbalimbali zitengeneze chanjo chanjo ingekua ni moja dunia nzima, lakini mpaka sasa nchi nyingi zimetengeneza chanjo ikiwemo Africa kusini China na India kama mpango ungekuwa ni kuuwa watu basi ingetumika chanjo moja dunia nzima.

Lakini vilevile ieleweke kwamba Mzungu akiamua kukuua, hauna ujanja wa kukwepa.

Kwanini kwenye fomu ya chanjo, serikali ilijitoa kuwajibika kwa lolote litakalotokea?

- Chanjo kazi yake ni kuboost immunity ili mwili wako uwe na uwezo wa kupambana na Covid pale unapoipata,

Sasa basi kipaumbele cha kwanza ni wenye magonjwa sugu, na wenye magonjwa sugu wengi immunity zao ziko chini sana so serikali ikisema iwalipe.

Ikitokea mtu yytr amepiga chanjo na akafa hata kwa ugonjwa mwingine watadai fidia,

Means mimi niwe na Chronic heart diseases nikaamua kuchoma chanjo, mwezi mmoja ukipita nikafa kwa ugonjwa wa moyo au mwingine wwte ule lazima ndugu waidai serikali fidia.

Sasa serikali italipa wangapi? Maana hapa ingesema ihusike watu wangeenda kuiangushia serikali jumba bovu, mtu anakufa kwa TB ila kwakua alipiga vaccine ya covvid atataka alipwe.
 
78asilimia y waliogua newca ktk jimbo flan Marekani wamepata chanjo je hii imekaaje Je ninkirusi kimpenya au chanjo imefail ikamletea ugonjwa? Kwa maana chanjo ni kukizubisha kirusi
 
Majibu yako yapo poa, ila hapo kwa China pana walakini, lengo la China ni kwamba hadi December mwaka huu 70% ya population yao (1.4 bil) wawe wamechanja, kwa takwimu walizotoa karibuni may be wapo kwenye 50% kwa sasa. Hiyo 90% umeitoa wapi?
 
Jimbo na Nanjing china lipo lockdown wiki hii na uchina imepiga hatua kwa mujibu wa maelezo yako ni 90%. Je kwa uchumi wetu unadhani inawezekana kutegemea chanjo kufikia herd immunity ambayo itatuweka salama maana chanjo yenyewe haizuii maambukizi ya Corona
 
Vipi aina madhara kwa watu wenye umri mkubwa kama wenye kisukari, pressure?

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
kwa asilimia kubwa chanjo ni muhimu sana kwa wazee na wale wenye magonjwa ya kudumu/sugu hao ndio kwa kiasi kikubwa body immunity yao imeshapungua hivyo ni muhimu sana kupata chanjo kwaajili yavkuboost immunity ili hata wakipata kirusi kinga ya mwili iwe na nguvu ya kukishambulia
 
Je Chanjo ya covid Ina faida za ziada mfano kuimarisha Kinga mfumo wa Koo dhidi ya virus wengine mafua, tonsils?
 
Umesema chanjo inasaidia kuongeza uwezo wa kinga ya mwili kupambana na hivyo virusi na hatimaye mtu anapoumwa huweza kupona, swali, kwa sisi tuliokwisha kuumwa na kupona kuna haja gani ya ku boost immunity zetu (kuchoma chanjo) wakati zilishaprove kuwa ziko thabiti kabisa kupambana na virusi hivi?
 
Back
Top Bottom