Ukweli mchungu: Hutavuka mpaka wa Tanzania bila kupata chanjo ya COVID-19

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,884
22,601
Biblia inaonya ashupazae shingo ikivunjika haitapona tena.

Sawa hatukuweka lockdown tukavuka ila sio chanjo, hili sio swala la kidola ni suala la dunia (WHO) linasimamiwa na dunia na mataifa yenye nguvu duniani na uwezo mkubwa.

Wazungu corona inewapa kichapo kikali hawatataka wewe uwapelekee tena ugonjwa huo, USA inapitisha billion 900$ hii pesa itawauma sana hawatakubali uwapelekee tena gonjwa hili baya.

Tunaweza kushuhudia viongozi wa ngazi za juu wa taifa letu wakizuiliwa airport kwa kutokuwa na vyeti/muhuli/alama za chanjo ya covid 19 tena umetoka Tanzania wanakodai tulipuuzia mbinu zao.

Tunagomea kinga kwa sabau gani mbona hatukugomea za ndui, mabusha, tetenasi, polio, tezi na hata kinga za mimba inamaana hii ndio yenye madhara tu.

USSR
 
Kama Tanzania hawahitaji chanjo logic ni kwamba huo ugojwa siyo tishio kwao, wazungu wanatoa hadi chanjo za mafua na hii siyo kwa watoto na akina mama wajawazito pekee, kwa hiyo swala la chanjo litabaki kwa nchi husika kuamua..
 
Mkuu hakuna aliekuzuia wewe kupata chanjo ukiitaka itaifuata sehemu inapotolewa Ila siyo kwa hapa Tanzania taifa teule.

Kila la kheri katika kuipata hiyo chanjo.
Mimi na familia yangu hatuna hata mpango wa kupata huo upuuzi unaosadikika ni chanjo ya Corona.
 
48 Reactions
Reply
Back
Top Bottom