Ukweli lazima usemwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli lazima usemwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Feb 2, 2012.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nakumbuka, takriban miaka 4 iliyopita, mtu anayejiita Nabii na Mtume, Josephat Mwingira, ambaye aliwahi kutamka kwamba kabla ya “kuokoka” alikuwa jambazi sugu, aliwafanyia unyama wa kutisha wafanyabiashara, wajasiriamali waliokuwa wamejiajiri wenyewe, kwa kuweka vibanda vyao vya biashara, eneo la Mwenge, nje ya eneo lililokuwa la kiwanda cha umma, Mang’ula Plant Works (jina ni langu, lakini “Mang’ula” ni jina rasmi), ambacho kilibinafsishwa chini ya iliyokuwa Parastatal Sector Reform Commission (PSRC), sasa inaitwa Consolidated Holdings Corporation (CHC).

  Bila taarifa, Mwingira alikodi magari makubwa mawili ambayo ni mitambo ya kutengeneza barabara, aina ya Caterpillar Grader na Caterpillar Scoop, ambayo yalifanya kazi ya kubomoa vibanda hivyo, jambo ambalo liliwasababishia wafanyabiashara hao hasara kubwa SANA. Wengi walifilisika, walipoteza mali na mitaji yao. Waliowahi kuokoa mali zao, walifanikiwa kuondoka mahali hapo salama. Wengi walibaki kutazama, Grader na Scoop, yakifanya maangamizi hayo, bila ya kuwa na nguvu ya kufanya lolote, kwani siku hiyo kulikuwa na magari mawili ya Polisi, aina ya LandRover Defender Pickup, yakiwa na zaidi ya askari Polisi kumi wenye silaha, wakitokea Kituo cha Polisi OysterBay. Askari hao waliitwa hapo baada ya Mwingira kuwasiliana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), ambaye baada ya “maelewano” yao, askari walitinga hapo, kuhakikisha “usalama” unakuwapo.

  Unyama huu wa Mwingira haukuishia hapo. Wamiliki wa viwanda vidogo vilivyo ndani ya eneo hilo la Mang’ula, wanatambua kwamba wao walimilikishwa maeneo yao kihalali na Serikali, kupitia PSRC, baada ya Mang’ula kuvunjwa. Ieleweke kwamba Mang’ula lilikuwa Shirika la Umma, na sio mtu binafsi.

  Kwa sasa, Mwingira anaendesha kampeni ili kuhakikisha kwamba anamiliki (kwa njia yoyote ile, kana kwamba HAKUNA SERIKALI ya KUMWAJIBISHA) eneo lote la Mang’ula! Ameanza na kubomoa na kuharibu mali ya kiwanda cha uchapaji cha AfroPlus, ambacho kiko kwenye eneo hilo. Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa kwenye gazeti la Uwazi, ninanukuu:
  “KIONGOZI wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira amekamatwa na polisi na kupewa kibano katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, akituhumiwa kuharibu mali za mfanyabiashara, Zain Sharifu.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Charles Kenyela, Mwingira alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa kituoni hapo.


  Hata hivyo, Kenyela alisema, Mwingira alidhamiwa baada ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvunja na kuharibu mali ndani ya Kiwanda cha Uchapaji cha Afroplus kinachomilikiwa na mlalamikaji.

  “Tumemkamata kiongozi huyo ili atoe ufafanuzi wa kina baada ya kupokea malalamiko hayo, “ alisema Kenyela alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake.

  Kenyela alisema, mashtaka hayo yalifikishwa polisi na Zain, Januari 8, mwaka huu, akidai kwamba walinzi binafsi wa kiongozi huyo wa kanisa, walivamia kiwandani kwake na kuharibu mali baada ya kufanya fujo.

  Aliongeza kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda eneo la tukio kushuhudia na kukuta mali zilizoharibiwa, hivyo walimtaka Mwingira kufika polisi ili atoe ufafanuzi lakini alikaidi ndipo polisi ikatumia nguvu kumkamata.”


  Sasa kibano kimegeuka. Kumbe na yeye anaweza kufikishwa Polisi, tena kule kule OysterBay, alikowatumia maafande kuwaharibia mali zao wajasiriamali waliokuwa wakijitafutia riziki zao, tena barabarani, na sio kwenye eneo lake la “kanisa”?

  Sasa tujiulize, ni Nabii na Mtume gani ambaye:


  1. Anataka kuwaondoa watu wanaomiliki maeneo yao ya kibiashara, kihalali, tena kwa nguvu, kwa kuwaharibia mali zao ili watishike, kwambe yeye ana NGUVU?
  2. Amekwishawaharibia watu, watafutaji, maskini, mali zao, na wengine kuwafilisi kabisa, chini ya mtutu wa bunduki, eti kwa kuwa alikuwa “anasafisha barabara” ya kuelekea kwenye “kanisa” lake?
  3. Anataka kujilimbikizia mali (Ardhi) bila kufuata sheria?

  Ieleweke kwamba, (mosi) eneo ilipojengwa Ephata Bank pale Mwenge ni eneo la hifadhi ya barabara, na ipo siku itakuja kubomolewa na TANROADS, anatapozuka Mkurugenzi Mkuu “kichaa” asiyeogopa mtu, bali anayeheshimu na kufuata/kutekeleza sheria!!!

  Mwingira hafanani na huo “utume na unabii” wake, kwani matendo yake yanamhukumu. Wafuasi (sio “waumini”) wake hukesha wakiomba na kufunga, wakimwomba “Mungu” alete maafa kwa watu fulani ambo kwa mujibu wa Mwingira ni “maadui” wake, kwa mfano, Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (“Babu”), ambaye “wafuasi” wa Mwingira walikesha na kufunga mwezi mzima, wakiomba mauti yamfikie. Mpaka leo, “Babu” anadunda. Ni “Mungu” gani huyo anayeombwa kuwaua watu wasio na hatia? Iweje, “nabii na mchungaji” atake watu wafe kwa amri yake yeye mwenyewe? Huyo sio “Mungu”, bali ni IBLIS!

  Eneo ambalo linasomeka kama EPHATA NURU CENTRE, ambao limejengwa kwa upande wa mbele (mabanda ….) unaopakana na Barabara Mpya ya Bagamoyo, bado linahesabiwa, kisheria, ni mali ya Serikali, kwani, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, eneo hilo HALIJABINAFSISHWA kwa mtu, watu au taasisi yoyote ile. Halikadhalika, eneo ambalo kuna viwanda na kampuni kadhaa, kama vile Simon Engineering, Metal Works, imber Malt Tech, Auto Ran Makongo, Container Global, Simon Engineering, Safe Man, Profession Investigation, Elbe Ltd, Zana za Kilimo Mbeya na Kilimanjaro Machine Tools Ltd, ni eneo linalomilikiwa kihalali kabisa, kwa mujibu wa Sheria, na kampuni hizo tajwa. Iweje leo, Mwingira adai kwamba anamiliki eneo lote hilo “tangu Juni 17, 2005, baada ya kulinunua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Mangula, hivyo anasubiri tamko la Mahakama ya Ardhi Tanzania ambako shitaka limepelekwa…”????

  Kwanza, hakuna mtu anayeitwa “Mangula”. Eneo lilikuwa mali ya kiwanda cha “Mang’ula”, Shirika la Umma lililobinafsishwa! Pia, Mwingira alikuwa anatumia uhusiano wake na Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye, kuwatishia majirani wake wanaofanya shughuli zao kwenye eneo hilo. HUU NI UHUNI MKUBWA!

  Mwingira alipeleka maombi ya kununua eneo lote, lakini akakataliwa na PSRC. Akapewa sehemu ya nyuma, lilipo kanisa lake la EPHATA. Ni eneo kubwa. Amekuwa akitumia uwanja wa mbele wa eneo hilo kuwafanyia semina za “brainwashing” vijana wasiokuwa na ajira, ili wawe watumwa wa kumpelekea pesa, kwa mfumo wa kuwalipisha ada za semina mbali mbali za “kiroho”. WIZI TU! Hakuna lolote!

  Mwingira akifa leo, kama hao “wachungaji” wenzake, na “kanisa” hilo linakufa pia, kwani hataki mtu mwingine yeyote “ahubiri” madhabahuni kwake. Hafanani kitabia na Kakobe huyu?

  Ninachojiuliza, kwa nini Serikali inakaa kimya ilhali ina taarifa zote kuhusu mambo haya? Wakati ule wale wajasiriamali walipoharibiwa mali zao na “tingatinga” na “kijiko” vya Manispaa ya Kinondoni, wakati ule Mkuu wa Wilaya akiwa Kanali Mstaafu Massawe, Kanali aliahidi kushughulikia suala lile ili wale walioharibiwa mali zao wafidiwe. Sijui nini kiliendekea.

  Leo hii, “wafuasi” wa Mwingira wanawapiga watu na kuharibu mali za kiwanda. Hapa hakuna kesi ya jinai? Kwa nini Kamanda Kenyela awaite Mwingira na Zain Sharifu na “kuwapatanisha” ilhali Mwingira ameharibu, makusudi, mali za Sharifu? Kuna nini hapa? Kwa nini Mwingira analindwa huku anavunja sheria kwa makusudi kabisa?

  Hapa hakuna suala la Kesi iliyopo Mahakamani. Hapa kuna uharibifu wa mali. Kuna watu wamepigwa, wameumizwa. Iweje ACP Kenyela awapatanishe? Hapa hakuna suala la KUPATANA. Mwambieni Zain Sharifu afungue kesi ya msingi, JINAI, dhidi ya Mwingira, kwani huyu SIO NABII WALA MTUME! Ni MWIZI TU!

  Nimemaliza!

  Che Mchochezi Excellent!
   
 2. nkawa

  nkawa Senior Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwisho wake umefika...kuna mama mmoja alinipa habari ya kuchekesha eti Mwingira anafufua wafu, walimpeleka mtoto mdogo alyekufa kuombewa afufuke, waliomba kuanzia asubuhi hadi jioni, jasho linamtoka hakuna lolote hadi ndugu wakaingilia kati wakamnyang'anya maiti wakaenda kuzika, maiti imeshaanza kuharibika...hii ni hatari
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh, hivi ni Mungu gani wanamwabadu hawa wakina mwingira?
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  It's sad. To me religions are a waste of time.
   
 5. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hii issue ya UFUFUO naona inapamba moto siku hadi siku...hata mbunge wa Arusha alishajaribu kufanya UFUFUO!
   
 6. t

  tenende JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nashukuru kwa uchambuzi wako mzuri. Ili watu wengi wasome ujumbe huu weka maneno yako ya mwisho kuhusu Mwingira, yaani rusha upya mada hii - wengi wangependa kujua.

  "Mwingira SIO NABII WALA MTUME! Ni MWIZI TU!"
   
 7. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pesa za sadaka zinampa wazimu.
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Siku zote maji hayasahau ubaridi hata uyachemshe vipi. Kama alikuwa jambazi mnadhani ameacha? Atakuwa ameacha kuvizia usiku au kunyang'anya kwa kutumia silaha sasa anachukua uso kwa macho.
  Jana nimekutana na mtu amevaa fulana imeandikwa ati mtoto wa Mwingira wa Ephata. Nikashangaa nikajiuliza hizi kufuru zinatoka wapi au ndio unabii unatimia?
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba ukristo umevamiwa na majambazi wengi lakini hawataki kukiri hilo hadharani

  a. Ukienda RC mapdre wanaongoza kwa kufanya uasherati na nuns, wake za watu, mbaya zaidi watoto wa kiume (sodoma); angalia cases za scotlands, Italy; sijui hali ikoje kwa vijana wetu wanaosoma seminary, sijui kama wameachwa na kina pengo...

  b. Ukienda kwa waluthery hao at least uasherati siyo mkubwa kwasababu wanaruhusiwa kuoa; lakini nao wanaongoza kwa kufanya ibada kama biashara...

  c. Ukienda kwa walokole hawa wanatia huruma kabisa, biashara majambazi ndio wamejazana hapa..wanajidai wameokoka my foot..above all wachungaji wao ni very incompetent; hawajasoma zaidi ya kukariri misitari kadhaa ya biblia nakuanza kutoa mapofu utafirkiri wamechanganyikiwa

  d. Ukienda kwa sabato; hawa kidogo wastaarabu na wanajiheshimu ila kuna kale kundi la masalia linaboa ..

  Something must be wrong "garbage in garbage out"
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hajamiminwa sawasawa
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhh
   
 12. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #12
  Feb 13, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Wadau kuna tetesi eti Mwingira majuzi kabaka mtoto zina ukweli? Si vizuri sana kutoa tuhuma dhidi ya watumishi wa kanisa, lakini pia tuna haki ya kufuatilia na kujua ukweli
   
 13. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180

  My friend, people (including you) have made sex the only sin whereas in fact it is linked to human weakness and frailty and perhaps, therefore, it is the least of all the sins!

  Mwingira's case is unique, naona huyu ni nabii wa ibilisi. Nakumbuka alishawahi (miaka ya nyma) kukusanya vijana waliokuwa wamemaliza form six akiwaahidi scholarship USA na kuwa changisha kila mmoja $ 2,500 amabzo alichukua na USA hawakwenda. Dhuluma iko ndani ya damu yake.

   
 14. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,430
  Likes Received: 12,699
  Trophy Points: 280
  Hata ukisikiliza mahubiri yake utajua tu anaongozwa na shetani wala si mungu,maneno mpumbav , mjinga na maneno mbofumbofu yote yake! Simwamini hata kidoogo
   
 15. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wewe tuwe tunaheshimiana ktk imani. Suala la Mwingira na uvamizi linahusianaje na mapadre? Unao ushahidi kuwa mapadre na masista wanafanya uasherati?

  Kuna uasherati mkubwa kama aliofanya mtume wako ambaye alifikia kuwalala hata watoto wa miaka 9? Sio huyu mudi alikuwa akiwanyinya watoto denda? Tukiachilia mbali ya kiongozi wenu, yule mtoto aliyelawitiwa msikitini dodoma alilawitiwa na Padre?

  Mna matatizo mia kidogo lkn ubize kuzungumza ya watu. Nendeni mkajipange matokeo ya form 4 mmechezea namba mbaya.
   
 16. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  We tulia tu, time will tell.

  Kuna gazeti lilitoa picha zake akiwa na mama ambaye anasemekana ndio kambandua sasa maadam yameanza kuruka kwenye media, tega masikio na macho weka wazi.

  Haya makanisa yenye kuitwa 'kanisa la Mchungaji .....' yana mambo makubwa kuliko unavyoweza kuona kwa nje.
   
 17. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  wenzetu mna matatizo mengi kupita hata ya huyo mwingira lakini kilolomo cha kuponda dini nyingine mnacho sana...hivi huwa inawasaidia nini?
   
 18. m

  m'monga JF-Expert Member

  #18
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba ukristo ume vamiwa kweli anaye fanya dhambi ni mtumwa wa dhambi hao watu wapo katika dini zote ila
  wasemwe wanao chafua ukristo sababu haistaili ni dini itayo wapeleka watu pazuri
   
 19. m

  m'monga JF-Expert Member

  #19
  Feb 13, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ukristo ni njia safi Haitakiwi Kuwa na dosari pale dosari inapojitokeza huonekana bila kuchelewa ni lazima wawekwe wazi wanao chafuwa dini yoyote na kumbuka hakuna hawezae kuja kwa Baba bali kwa njia ya yeye(yesu)kwa kufika lazima tuache madhambi na kumtii yeye
   
 20. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #20
  Feb 13, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wanaowaibia walalahoi ni kama wafuatao: 1. Kakobe 2. Mwingira 3. Mama Lwakatale 4. Mzee wa Upako 5. Gwajima 6. Winners chapel (banana) 7. endelezeni. It is sad wanawaibia pesa zao na wake zao pia mara mia Lowasa anaiibia serikali kuliko hawa mafisadi kupitia jina la Mungu.
   
Loading...