soma hapa ili ujue kweli na uweze kusema ukweli:
EFATHA FOUNDATION LTD
P.O BOX 32174, MWENGE, DAR ESSALAAM
TELEPHONE:+255732993196, FAX:+255732993196
WEBSITE:www.efathafoundation.org
EMAIL: efathafoundationltd@yahoo.com /info@efathafoundation.org
OUR REF: EFL/ADMN/4/2012
DATE: 11[SUP]th[/SUP]April, 2012
TAARIFAKWA UMMA
1.1 Utangulizi
Tarehe 9 mwezi April 2012,Jumatatu ya Pasaka,baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza habari ya umiliki namatukio yaliyotokea katika eneo hilo. Habari zilizotangazwa ni za upande mmojana hazina usahihi. Huduma ya Efatha inapenda kuelezea umma taarifa sahihi juuya upatikanaji wa kiwanja na 90, umiliki na matukio yaliyotokea katika eneohilo.
1.2 Upatikanaji na umiliki wa eneo
Serikali kupitia Tume ya Kurekebishana Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC) ilitangaza zabuni ya uuzwaji wa eneola Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika, Kiwanjanamba 90, Mwenge katika magazeti ya Uhuru na Daily News ya tarehe 4 mwezi Mei2005.
Tarehe 18 Mei 2005, huduma yaEfatha kupitia kitengo chake cha uchumi, Efatha Foundation Ltd, ilipelekamaombi ya zabuni ya kununua eneo hilo PSRC.
Efatha Foundation Ltd ilipokeabarua kutoka PSRC yenye kumbukumbu Na. PSRC/1/13/93 ya tarehe 30 Mei 2005 ikiarifu kwamba zabuni yetu ya kununua eneohilo imeshinda kwa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nne.
Masharti ya Malipo ya zabuniyalikuwa asilimia kumi ilipwe wakati wa kupeleka maombi na asilimia tisiniilipwe ndani ya miezi mitatu baada ya kushinda zabuni.Efatha Foundation Ltd ililipashilingi milioni arobaini yaani asilimia kumi ya bei siku ya kupeleka maombi yazabuni kwa hundi Na. 000261 ya benki ya Azania na kupewa risiti ya PSRC Na.6956 ya tarehe 31 Mei 2005. Na shilingi milioni mia tatu sitini ililipwakupitia hundi Na. 000319 ya benki ya Azania ambayo ni asilimia tisini tarehe 10mwezi Juni 2005 na kupewa risiti ya PSRC Namba 6984 na hivyo malipo yote yakawayamekamilishwa.
Baada ya kukamilisha malipoEfatha Foundation Ltd ilikabidhiwa hati miliki Namba 41641 ambayo ilipelekwawizara ya Ardhi ili ibadilishwe jina kutoka mmiliki wa mwanzo na kuandikishwajina la Efatha Foundation Ltd. Kwa hiyo Serikali ikahamisha umiliki kutoka Mang'ula Mechanical and Machine Tools CompanyLtd iliyofilisika kwenda Efatha Foundation ltd tarehe 15 Novemba 2005 saa sitakamili mchana kwa uhamisho Namba 98648.Kabla ya Huduma ya Efathakununua eneo hilo kulikuwa na wavamiziambao ni makampuni na watu binafsi kumi na moja ambao walikuwa wamewekwa katikaeneo hilo na Mang'ula Mechanical andMachine Tools Company Ltd iliyofilisika bila kibali cha mfilisi yaani PSRC. Kwakuwa hawakuwa wapangaji halali walikuwa wavamizi (trespassers). Wavamizi haowakapewa notisi ya kuondoka na PSRC lakini hawakuondoka. Baadae shughuli zamfilisi, PSRC, zikachukuliwa kisheria na Consolidated Holding Corporation(CHC). CHC nao wakawapa wale wavamizi notisi kuwa waondoke kwa sababu eneo hilolimeuzwa lakini hawakuondoka.
EfathaFoundation Ltd ilipomiliki eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizinotisi ya kuondoka mwaka 2005, wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka ambaoni pamoja na Afro Plus Industries Ltd. Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhama wakafungua kesimahakamani dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa. Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hilithamani yake ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang'ula Mechanical and Machine Tools CompanyLtd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro PlusIndustries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali.Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro PlusIndustries Ltd kama ilivyodaiwa.
2. UVAMIZIWA POLISI NDANI YA KANISA LA EFATHA MWENGE
Tarehe 9 Aprili 2012, jumatatuya pasaka, majira ya saa kumi na mbili asubuhi waumini wa Efatha walikuwakatika ibada ya morning glory katika kanisa la Efatha Mwenge wakiongozwa katikaibada hiyo na Mchungaji David Mwakisole ndani ya kanisa. Kanisa limezungushiwaukuta pande zote nne na lina mageti ya kuingilia kanisani ambayo yanafungwa.Polisi walipanda ukuta wakachungulia wakasikika wakisema hawa huku ndani. Baadae polisi wakarukia ndani kupitiaukutani. Wakati ibada inaendelea ghafla waumini walivamiwa kutoka nje na watuambao baadae walitambuliwa kuwa ni polisi. Walipoingia kwa nguvu wakatupamabomu ya machozi ndani ya kanisa huku wakifyatua risasi za moto wakati ibadaikiendelea. Kwa kitendo hicho ibada ilivurugika na kusimama na waumini wakaanzakukimbia ovyo ndani ya kanisa. Risasi namabomu ya machozi yalitupwa kuelekea madhabahuni na kuelekea kwa wauminiwaliokuwa katika ibada. Waumini wengine waliokuwa wakija kwenye ibadawalizuiliwa nje na kukamatwa. Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia napolisi wakiwapiga kwa virungu, vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemumbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ulitapakaa damu. Pia polisi walivunjamadirisha, viti, milango na spika kama ilivyoonyeshwa katika baadhi ya vyombovya habari hasa ITV. Kabla hawajavamia, mmoja wa askari aliwatahadharishawenzake kuwa wasipige mabomu na risasi kwa kuwa hapo ni kanisani lakini wenzakewalipinga wakisema kuwa huyu mtu ana kiburi na watu hawa ni wakorofi. Wakatirisasi na mabomu yakipigwa baadhi ya askari walikuwa wakiokota maganda yarisasi na mabaki ya mabomu ya machozi ili kuondoa ushahidi. Hata hivyo baadhiya risasi za moto, maganda ya risasi zamoto na mabaki ya mabomu yalibaki kanisani na yamehifadhiwa mahali maalum kwahatua zaidi.Kanisani kulikuwa na idadi yawaumini kati ya sitini na sabini waliokuwa wanaabudu. Polisi waliwakamata jumlaya waumini 53 pamoja na wachungaji waliokuwa wakiongoza ibada wakiwapiga nakuwasweka katika magari ya polisi kuwapeleka kituoni pamoja na kuvuta garizilizokuwa zimeegeshwa nje ya kanisa kwa breakdown. Tumepata habari kuwawalikuja na baadhi ya waandishi wa habari walioandaliwa kabla ili kurekoditukio hilo na ushahidi tunao. Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hiloliliandaliwa kwa makusudi ili likatekelezwe katika kanisa la Efatha. Tukio hililinatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa kwa Huduma ya Efatha.
Kitendo cha polisi kuvamia nakuvuruga ibada ni kinyume na sheria na katiba ya jamhuri ya Muungano waTanzania iliyoweka uhuru wa kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza kwamba ibadaziheshimiwe na zisiingiliwe. Tunajiuliza kulikuwa na tatizo gani polisiwasisubiri nje ibada iishe na wawachukue watu wanaotaka kuwachukua. Ndani yakanisa hakukuwa na vita, wala mtu mwenye silaha, wala mtu anayeuawa ambayepolisi walilazimika kwenda kumwokoa. Sisi tunaliona hili kuwa ni kumdharauMungu, kuvuruga ibada na kuwadhalilisha waumini wa Efatha waliokuwa wakitumiauhuru wao wa kuabudu. Leo wamefanya hivyo kwa dharau ndani ya kanisa la Efatha, kesho tutegemee watakwenda kufanya nini kwa dhehebu jingine, Msikiti, Dininyingine au watu waliokusanyika kihalali na kwa sababu halali?
3. MAJUMUISHO
Vielelezo vyote kuhusuumiliki wetu halali wa eneo hilivilishawasilishwa polisi mkoani na wilayani. Kutokana na maelezo haya EfathaFoundation Ltd inapenda kuuthibitishia umma kuwa EFATHA FOUNDATION LTD ndiyommiliki halali wa KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURU CENTRE) na sivinginevyo.
KATIBU
EFATHA FOUNDATION LTD