Ukweli lazima usemwe

BY MESS
Wanaowaibia walalahoi ni kama wafuatao: 1. Kakobe 2. Mwingira 3. Mama Lwakatale 4. Mzee wa Upako 5. Gwajima 6. Winners chapel (banana) 7. endelezeni. It is sad wanawaibia pesa zao na wake zao pia mara mia Lowasa anaiibia serikali kuliko hawa mafisadi kupitia jina la Mungu.

Umekosea kumweka kwenye hiyo list ungefanya thorough investigation au umsahau ulikuwa unamaanisha LUSEKELO?
 
Bora wewe usiye ibiwa uwe tajiri sasa na uwe na uwakika wa kufika peponi ungeniambiya kwamba hatutafika
peponi kwa Jina la yesu ninge kuelewa lakini kwa wizi wa mtu ni yeye na MUNGU wake atajibu sike ya mwisho na wewe piya utajibu Matendo yako ni bora uwe safi moyoni na machoni pa MUNGU sio kuangaliya Maisha ya watu wanaishi vipi huo ni uswahili na uswahili Asili yake ni ujinga
 
Ni bora kuhariri maneno ya kweli maana siku ya mwisho utajibu hukumu ni kwa kila mtu jichunguze na wewe je!!!
 
Nakumbuka, takriban miaka 4 iliyopita, mtu anayejiita Nabii na Mtume, Josephat Mwingira, ambaye aliwahi kutamka kwamba kabla ya "kuokoka" alikuwa jambazi sugu, aliwafanyia unyama wa kutisha wafanyabiashara, wajasiriamali waliokuwa wamejiajiri wenyewe, kwa kuweka vibanda vyao vya biashara, eneo la Mwenge

Mwingira akifa leo, kama hao "wachungaji" wenzake, na "kanisa" hilo linakufa pia, kwani hataki mtu mwingine yeyote "ahubiri" madhabahuni kwake. Hafanani kitabia na Kakobe huyu?
Che Mchochezi Excellent!

Mwahahaki, umeeeleza kwa uchache madudu ya mtu anayejiita Nabii Mwingira. Kuna vitu vingi nyuma ya pazia mtu huyu anafanya na vinajulikana kwa watu fulani tu.

Hata hivyo pamoja na hayo madudu yake usijaribu kumlinganisha Kakobe. Kakobe yuko smartmbali sana na huyo mchawi anayejiita nabii.
Maeneo ya mfanano:
  1. Wote wamefungua makanisa Mwenge
  2. Wote ni viongozi wa imani ya "kikiristo" (nimeweka katika vifunga na vifungua usemi kwasababu mmoja siyo imani ya kikristo)
  3. Wote wanatumia Biblia katika mahubiri
Nikupe maeneo machache yatofauti zao:
  1. Mwingira alikuwa jambazi na tapeli kabla ya kuokoka, Kakobe alikuwa mwajiriwa wa serrikali baadaye mjasiriamali.
  2. Mwingira alianzisha Efatha Ministry akiwa muasi wa New Life Crusade(T) baada ya kumshitukia kuwa amekengeuka wakati Kakobe alikuwa mshirika wa Evangelical Assemblies of God Tanzania (EAGT). Wakati Mwingira yuko NLC alikuwa muumini wa Lutheran akiwa katokea RC.
  3. Mwingira anahistoria yenye utata sana hadi kufikia hapo alipo, Kakobe anahistoria inayoeleweka hadi hapo alipofikia.
  4. Mwingira alianza kujiita nabii na mtume kisha ndipo akaanzisha huduma ya Efatha; Kakobe yeye aliitwa Mchungaji,, na hadi leo anaitwa na kujiita hivyo, alipokuwa anaanzisha Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship.
  5. Mahubiri ya Mwingira yana uhuni na viloja vingi, Kakobe katika mahubiri yake hana uhuni wala viloja.
  6. Mwingira katika huduma zake anapunga pepo, Kakobe anfukuza pepo hapungi.
  7. Mwingira kapora eneo alilopo hapo Mwenge, Kakobe hajapora na wala hana mgogoro na majirani zake juu ya maeneo.
  8. Mwingira anauchu wa mali na ni mtu wakujilimbikizia, Kakobe hana mali kama watu wanavyomzushia, anawekeza katika Injili.

Naomba niseme hayo machache. Sitaki tutoke katika mada lakini nilipenda nieleze machache ili Zakaria Kakobe asilinganishwe na tapeli anayejiita Nabii na Mtume Josephati Mwingira.
 
Ukweli ni kwamba ukristo umevamiwa na majambazi wengi lakini hawataki kukiri hilo hadharani

a. Ukienda RC mapdre wanaongoza kwa kufanya uasherati na nuns, wake za watu, mbaya zaidi watoto wa kiume (sodoma); angalia cases za scotlands, Italy; sijui hali ikoje kwa vijana wetu wanaosoma seminary, sijui kama wameachwa na kina pengo...

b. Ukienda kwa waluthery hao at least uasherati siyo mkubwa kwasababu wanaruhusiwa kuoa; lakini nao wanaongoza kwa kufanya ibada kama biashara...

c. Ukienda kwa walokole hawa wanatia huruma kabisa, biashara majambazi ndio wamejazana hapa..wanajidai wameokoka my foot..above all wachungaji wao ni very incompetent; hawajasoma zaidi ya kukariri misitari kadhaa ya biblia nakuanza kutoa mapofu utafirkiri wamechanganyikiwa

d. Ukienda kwa sabato; hawa kidogo wastaarabu na wanajiheshimu ila kuna kale kundi la masalia linaboa ..

Something must be wrong "garbage in garbage out"

NDUGU

MAANDIKO YAMEANDIKA KUWA "KAMA WEWE UNAJIONA HUNA DHAMBI BASI RUSHA MAWE KAMA HAYA KWA WENGINE"

je wewe umsafi mwenzetu???????????

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
HIvi Mkuu wa JF;

Hii thread inapaswa kuwa katika page hii ya JUKWAA LA SIASA. Tunaomba Ihamishe au ifutwe kabisa kwa ni inaingilia Uhuru wa kuabudu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wote kakobe na hao wanaojiita manabii ni matapeli na wanasababisha umasikini mkubwa kwa watanzania, serikali iache kuwaogopa na iingilie kati masikini na watu waliokata tamaa wanatapeliwa sana. Hili nalo ni janga la kitaifa
 
Afadhali umeona hilo. Huyo ndiye mtume ambaye anadai sadaka kutoka kwa waumini maskini kwa nguvu, namiliki benki kwa manufaa yake, anatumia gari la mamilioni ya fedha huku waumini wakitembea kwa miguu na kulala bila kula-ni mtume huyo-ole wenu mnaomwita sifa asokuwa nayo -jiandalieni mafikio mabaya kwa mwenye Mungu
 
Kila m2 aabudu anachokitaka, ila uovu unaofanywa na viongozi wa makanisa hakuna ubaya ukianikwa. Wanatia aibu sana.
 
Kweli ni janga la kitaifa-wakati watu wanajaribu kujikwamua "mitume na manabii" nao wanazidi kuibuka na kukusanya sadaka kwa nguvu na kuwarejesha watu katika ufukara mkubwa tena wa kutisha-umewahi kushuhudia watu wanaomba lifti pale kwa Kaboke, Mwingira, Mzee wa Upako, Agape baada ya ibada? kama bado fuatilia sehemu hizo. utaona maajabu masiki wanavyotoa fedha kwa waheshimiwa hao. Siyo bure kuna kitu hapo
 
kweli ni janga la kitaifa-wakati watu wanajaribu kujikwamua "mitume na manabii" nao wanazidi kuibuka na kukusanya sadaka kwa nguvu na kuwarejesha watu katika ufukara mkubwa tena wa kutisha-umewahi kushuhudia watu wanaomba lifti pale kwa kaboke, mwingira, mzee wa upako, agape baada ya ibada? Kama bado fuatilia sehemu hizo. Utaona maajabu masiki wanavyotoa fedha kwa waheshimiwa hao. Siyo bure kuna kitu hapo

kwani wanalazimishwa!!!!!!!! Si wanapeleka wenyewe bwana!!!!!!!!!!!!!!!

mizambwa
inaniuma sana!!!
 
Kazi ipo. Mwanahalisi la tarehe 8/2/2012. LINASEMA MWINGIRA ALIMBAKA MKE WA WAKILI MAARUFU JIJINI. NA MKE WA HUYO WAKILI ALIKIRI KWELI.

KUNA TAARIFA NYINGINE ZIMESIKIKA KUWA ALIMBAKA BINTI MMOJA KTK HOTEL MOJA MAARAFU HAPA JIJINI BAADA YA KUMPANGISHA HUKO ETI AKAE SIKU TATU KWA AJIRI YA KUFUNGA NA MAOMBI, KUMBE USIKU ANAKWENDA KUMBAKA.

Haya Mwingira, funguka tukusikie hapa, anza kwanza na gazeti la Mwanahalisi....
 
HIvi Mkuu wa JF;

Hii thread inapaswa kuwa katika page hii ya JUKWAA LA SIASA. Tunaomba Ihamishe au ifutwe kabisa kwa ni inaingilia Uhuru wa kuabudu.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!![/QUOTE

Mods hii ni nini? Au kwa vile haishambulii waislamu basi iachwe? Basi ipeleke jukwaa la dini tutaikuta huko!
 
Mwingira ni Mjasiriamali anayelekea kuwa bepari kama wenzake akina mama Lwakatare!
 
Kwa sasa sina shaka sana na ukristo, labda mpaka nisikie viongozi wa Kanisa Katoliki wanafanya biashara zao kama hao wanaojiita mitume. Siku zote za maisha yangu naliangalia Kanisa hili kama alama pekee ya uwepo wa Kristo Mungu. Haya makanisa ya kisasa, kuanzia Lutheran, ni makanisa yaliyojaa usanii tu hapa duniani, sishangai sana nikisikia kuna jambo baya linatokea katika makanisa hayo. Udhaifu unaotokea katika Kanisa Katoliki ni udhaifu wa mtu binafsi, si wa Kanisa, na Kanisa nalo huwa linalaani kile kibaya kilichotokea. Udhaifu kila mtu anao, lkn kanisa kama taasisi linatakiwa kuulaani huo udhaifu, siyo kuukingia kifua.
Tatizo la makanisa haya ya kisasa ni kwamba yanamilikiwa na watu binafsi, na si jamii kama Kanisa Katoliki.
 
Nakumbuka, takriban miaka 4 iliyopita, mtu anayejiita Nabii na Mtume, Josephat Mwingira, ambaye aliwahi kutamka kwamba kabla ya “kuokoka” alikuwa jambazi sugu, aliwafanyia unyama wa kutisha wafanyabiashara, wajasiriamali waliokuwa wamejiajiri wenyewe, kwa kuweka vibanda vyao vya biashara, eneo la Mwenge, nje ya eneo lililokuwa la kiwanda cha umma, Mang’ula Plant Works (jina ni langu, lakini “Mang’ula” ni jina rasmi), ambacho kilibinafsishwa chini ya iliyokuwa Parastatal Sector Reform Commission (PSRC), sasa inaitwa Consolidated Holdings Corporation (CHC).

Bila taarifa, Mwingira alikodi magari makubwa mawili ambayo ni mitambo ya kutengeneza barabara, aina ya Caterpillar Grader na Caterpillar Scoop, ambayo yalifanya kazi ya kubomoa vibanda hivyo, jambo ambalo liliwasababishia wafanyabiashara hao hasara kubwa SANA. Wengi walifilisika, walipoteza mali na mitaji yao. Waliowahi kuokoa mali zao, walifanikiwa kuondoka mahali hapo salama. Wengi walibaki kutazama, Grader na Scoop, yakifanya maangamizi hayo, bila ya kuwa na nguvu ya kufanya lolote, kwani siku hiyo kulikuwa na magari mawili ya Polisi, aina ya LandRover Defender Pickup, yakiwa na zaidi ya askari Polisi kumi wenye silaha, wakitokea Kituo cha Polisi OysterBay. Askari hao waliitwa hapo baada ya Mwingira kuwasiliana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), ambaye baada ya “maelewano” yao, askari walitinga hapo, kuhakikisha “usalama” unakuwapo.

Unyama huu wa Mwingira haukuishia hapo. Wamiliki wa viwanda vidogo vilivyo ndani ya eneo hilo la Mang’ula, wanatambua kwamba wao walimilikishwa maeneo yao kihalali na Serikali, kupitia PSRC, baada ya Mang’ula kuvunjwa. Ieleweke kwamba Mang’ula lilikuwa Shirika la Umma, na sio mtu binafsi.

Kwa sasa, Mwingira anaendesha kampeni ili kuhakikisha kwamba anamiliki (kwa njia yoyote ile, kana kwamba HAKUNA SERIKALI ya KUMWAJIBISHA) eneo lote la Mang’ula! Ameanza na kubomoa na kuharibu mali ya kiwanda cha uchapaji cha AfroPlus, ambacho kiko kwenye eneo hilo. Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa kwenye gazeti la Uwazi, ninanukuu:
“KIONGOZI wa Kanisa la Efatha, Nabii na Mtume Josephat Mwingira amekamatwa na polisi na kupewa kibano katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, akituhumiwa kuharibu mali za mfanyabiashara, Zain Sharifu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, ACP Charles Kenyela, Mwingira alikamatwa wiki iliyopita na kushikiliwa kituoni hapo.

Hata hivyo, Kenyela alisema, Mwingira alidhamiwa baada ya kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuvunja na kuharibu mali ndani ya Kiwanda cha Uchapaji cha Afroplus kinachomilikiwa na mlalamikaji.

“Tumemkamata kiongozi huyo ili atoe ufafanuzi wa kina baada ya kupokea malalamiko hayo, “ alisema Kenyela alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake.

Kenyela alisema, mashtaka hayo yalifikishwa polisi na Zain, Januari 8, mwaka huu, akidai kwamba walinzi binafsi wa kiongozi huyo wa kanisa, walivamia kiwandani kwake na kuharibu mali baada ya kufanya fujo.

Aliongeza kuwa polisi baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda eneo la tukio kushuhudia na kukuta mali zilizoharibiwa, hivyo walimtaka Mwingira kufika polisi ili atoe ufafanuzi lakini alikaidi ndipo polisi ikatumia nguvu kumkamata.”

Sasa kibano kimegeuka. Kumbe na yeye anaweza kufikishwa Polisi, tena kule kule OysterBay, alikowatumia maafande kuwaharibia mali zao wajasiriamali waliokuwa wakijitafutia riziki zao, tena barabarani, na sio kwenye eneo lake la “kanisa”?

Sasa tujiulize, ni Nabii na Mtume gani ambaye:

  1. Anataka kuwaondoa watu wanaomiliki maeneo yao ya kibiashara, kihalali, tena kwa nguvu, kwa kuwaharibia mali zao ili watishike, kwambe yeye ana NGUVU?
  2. Amekwishawaharibia watu, watafutaji, maskini, mali zao, na wengine kuwafilisi kabisa, chini ya mtutu wa bunduki, eti kwa kuwa alikuwa “anasafisha barabara” ya kuelekea kwenye “kanisa” lake?
  3. Anataka kujilimbikizia mali (Ardhi) bila kufuata sheria?

Ieleweke kwamba, (mosi) eneo ilipojengwa Ephata Bank pale Mwenge ni eneo la hifadhi ya barabara, na ipo siku itakuja kubomolewa na TANROADS, anatapozuka Mkurugenzi Mkuu “kichaa” asiyeogopa mtu, bali anayeheshimu na kufuata/kutekeleza sheria!!!

Mwingira hafanani na huo “utume na unabii” wake, kwani matendo yake yanamhukumu. Wafuasi (sio “waumini”) wake hukesha wakiomba na kufunga, wakimwomba “Mungu” alete maafa kwa watu fulani ambo kwa mujibu wa Mwingira ni “maadui” wake, kwa mfano, Mchungaji Ambilikile Mwaisapila (“Babu”), ambaye “wafuasi” wa Mwingira walikesha na kufunga mwezi mzima, wakiomba mauti yamfikie. Mpaka leo, “Babu” anadunda. Ni “Mungu” gani huyo anayeombwa kuwaua watu wasio na hatia? Iweje, “nabii na mchungaji” atake watu wafe kwa amri yake yeye mwenyewe? Huyo sio “Mungu”, bali ni IBLIS!

Eneo ambalo linasomeka kama EPHATA NURU CENTRE, ambao limejengwa kwa upande wa mbele (mabanda ….) unaopakana na Barabara Mpya ya Bagamoyo, bado linahesabiwa, kisheria, ni mali ya Serikali, kwani, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo, eneo hilo HALIJABINAFSISHWA kwa mtu, watu au taasisi yoyote ile. Halikadhalika, eneo ambalo kuna viwanda na kampuni kadhaa, kama vile Simon Engineering, Metal Works, imber Malt Tech, Auto Ran Makongo, Container Global, Simon Engineering, Safe Man, Profession Investigation, Elbe Ltd, Zana za Kilimo Mbeya na Kilimanjaro Machine Tools Ltd, ni eneo linalomilikiwa kihalali kabisa, kwa mujibu wa Sheria, na kampuni hizo tajwa. Iweje leo, Mwingira adai kwamba anamiliki eneo lote hilo “tangu Juni 17, 2005, baada ya kulinunua kutoka kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Mangula, hivyo anasubiri tamko la Mahakama ya Ardhi Tanzania ambako shitaka limepelekwa…”????

Kwanza, hakuna mtu anayeitwa “Mangula”. Eneo lilikuwa mali ya kiwanda cha “Mang’ula”, Shirika la Umma lililobinafsishwa! Pia, Mwingira alikuwa anatumia uhusiano wake na Waziri Mkuu Mstaafu, Sumaye, kuwatishia majirani wake wanaofanya shughuli zao kwenye eneo hilo. HUU NI UHUNI MKUBWA!

Mwingira alipeleka maombi ya kununua eneo lote, lakini akakataliwa na PSRC. Akapewa sehemu ya nyuma, lilipo kanisa lake la EPHATA. Ni eneo kubwa. Amekuwa akitumia uwanja wa mbele wa eneo hilo kuwafanyia semina za “brainwashing” vijana wasiokuwa na ajira, ili wawe watumwa wa kumpelekea pesa, kwa mfumo wa kuwalipisha ada za semina mbali mbali za “kiroho”. WIZI TU! Hakuna lolote!

Mwingira akifa leo, kama hao “wachungaji” wenzake, na “kanisa” hilo linakufa pia, kwani hataki mtu mwingine yeyote “ahubiri” madhabahuni kwake. Hafanani kitabia na Kakobe huyu?

Ninachojiuliza, kwa nini Serikali inakaa kimya ilhali ina taarifa zote kuhusu mambo haya? Wakati ule wale wajasiriamali walipoharibiwa mali zao na “tingatinga” na “kijiko” vya Manispaa ya Kinondoni, wakati ule Mkuu wa Wilaya akiwa Kanali Mstaafu Massawe, Kanali aliahidi kushughulikia suala lile ili wale walioharibiwa mali zao wafidiwe. Sijui nini kiliendekea.

Leo hii, “wafuasi” wa Mwingira wanawapiga watu na kuharibu mali za kiwanda. Hapa hakuna kesi ya jinai? Kwa nini Kamanda Kenyela awaite Mwingira na Zain Sharifu na “kuwapatanisha” ilhali Mwingira ameharibu, makusudi, mali za Sharifu? Kuna nini hapa? Kwa nini Mwingira analindwa huku anavunja sheria kwa makusudi kabisa?

Hapa hakuna suala la Kesi iliyopo Mahakamani. Hapa kuna uharibifu wa mali. Kuna watu wamepigwa, wameumizwa. Iweje ACP Kenyela awapatanishe? Hapa hakuna suala la KUPATANA. Mwambieni Zain Sharifu afungue kesi ya msingi, JINAI, dhidi ya Mwingira, kwani huyu SIO NABII WALA MTUME! Ni MWIZI TU!

Nimemaliza!

Che Mchochezi Excellent!

Naona unayasema haya yote kwa kuwa hujui ukweli ulivyo. soma taarifa hii hapa chini:

EFATHA FOUNDATION LTD
P.O BOX 32174, MWENGE, DAR ES SALAAM
TELEPHONE: +255732993196, FAX:+255732993196
WEBSITE: www.efathafoundation.org
EMAIL: efathafoundationltd@yahoo.com / info@efathafoundation.org
OUR REF: EFL/ADMN/4/2012
DATE:
11th April, 2012

TAARIFA KWA UMMA

1. UMILIKI WA KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURU CENTRE)
1.1 Utangulizi

Tarehe 9 mwezi April 2012, Jumatatu ya Pasaka,baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza
habari ya umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo hilo. Habari zilizotangazwa ni za
upande mmoja na hazina usahihi. Huduma ya Efatha inapenda kuelezea umma taarifa
sahihi juu ya upatikanaji wa kiwanja na 90, umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo
hilo.

1.2 Upatikanaji na umiliki wa eneo

Serikali kupitia Tume ya Raisi ya Kurekebisha na Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC)
ilitangaza zabuni ya uuzwaji wa eneo la Mang’ula Mechanical and Machine Tools
Company Ltd iliyofilisika, Kiwanja namba 90, Mwenge katika magazeti ya Uhuru na Daily
News ya tarehe 4 mwezi Mei 2005.

Tarehe 18 Mei 2005, huduma ya Efatha kupitia kitengo chake cha uchumi, Efatha
Foundation Ltd, ilipeleka maombi ya zabuni ya kununua eneo hilo PSRC.
Efatha Foundation Ltd ilipokea barua kutoka PSRC yenye kumbukumbu Na.
PSRC/1/13/93 ya tarehe 30 Mei 2005 ikiarifu kwamba zabuni yetu ya kununua eneo hilo
imeshinda kwa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nne.

Masharti ya Malipo ya zabuni yalikuwa asilimia kumi ilipwe wakati wa kupeleka maombi
na asilimia tisini ilipwe ndani ya miezi mitatu baada ya kushinda zabuni.
Efatha Foundation Ltd ililipa shilingi milioni arobaini yaani asilimia kumi ya bei siku ya
kupeleka maombi ya zabuni kwa hundi Na. 000261 ya benki ya Azania na kupewa risiti
ya PSRC Na. 6956 ya tarehe 31 Mei 2005. Na shilingi milioni mia tatu sitini ililipwa kupitia
hundi Na. 000319 ya benki ya Azania ambayo ni asilimia tisini tarehe 10 mwezi Juni 2005
na kupewa risiti ya PSRC Namba 6984 na hivyo malipo yote yakawa yamekamilishwa.

Baada ya kukamilisha malipo Efatha Foundation Ltd ilikabidhiwa hati miliki Namba
41641 ambayo ilipelekwa wizara ya Ardhi ili ibadilishwe jina kutoka mmiliki wa mwanzo
na kuandikishwa jina la Efatha Foundation Ltd. Kwa hiyo Serikali ikahamisha umiliki
kutoka Mang’ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika kwenda
Efatha Foundation ltd tarehe 15 Novemba 2005 saa sita kamili mchana kwa uhamisho
Namba 98648.

Kabla ya Huduma ya Efatha kununua eneo hilo kulikuwa na wavamizi ambao ni
makampuni na watu binafsi kumi na moja ambao walikuwa wamewekwa katika eneo
hilo na Mang’ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika bila kibali cha
mfilisi yaani PSRC. Kwa kuwa hawakuwa wapangaji halali walikuwa wavamizi
(trespassers). Wavamizi hao wakapewa notisi ya kuondoka na PSRC lakini
hawakuondoka. Baadae shughuli za mfilisi, PSRC, zikachukuliwa kisheria na Consolidated
Holding Corporation (CHC). CHC nao wakawapa wale wavamizi notisi kuwa waondoke
kwa sababu eneo hilo limeuzwa lakini hawakuondoka. Efatha Foundation Ltd ilipomiliki
eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondoka mwaka 2005,
wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka
ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd.

Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhama wakafungua kesi mahakamani
dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa.

Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hili thamani yake
ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang’ula Mechanical and
Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro
Plus Industries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali.
Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus
Industries Ltd kama ilivyodaiwa.

2. UVAMIZI WA POLISI NDANI YA KANISA LA EFATHA MWENGE

Tarehe 9 Aprili 2012, jumatatu ya pasaka, majira ya saa kumi na mbili asubuhi waumini
wa Efatha walikuwa katika ibada ya morning glory katika kanisa la Efatha Mwenge
wakiongozwa katika ibada hiyo na Mchungaji David Mwakisole ndani ya kanisa. Kanisa
limezungushiwa ukuta pande zote nne na lina mageti ya kuingilia kanisani ambayo
yanafungwa. Polisi walipanda ukuta wakachungulia wakasikika wakisema hawa huku
ndani. Baadae polisi wakarukia ndani kupitia ukutani. Wakati ibada inaendelea ghafla
waumini walivamiwa kutoka nje na watu ambao baadae walitambuliwa kuwa ni polisi.
Walipoingia kwa nguvu wakatupa mabomu ya machozi ndani ya kanisa huku wakifyatua
risasi za moto wakati ibada ikiendelea. Kwa kitendo hicho ibada ilivurugika na kusimama
na waumini wakaanza kukimbia ovyo ndani ya kanisa. Risasi na mabomu ya machozi
yalitupwa kuelekea madhabahuni na kuelekea kwa waumini waliokuwa katika ibada.
Waumini wengine waliokuwa wakija kwenye ibada walizuiliwa nje na kukamatwa.
Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia na polisi wakiwapiga kwa virungu,
vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu
mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ulitapakaa damu. Pia polisi walivunja
madirisha, viti, milango na spika kama ilivyoonyeshwa katika baadhi ya vyombo vya
habari hasa ITV. Kabla hawajavamia, mmoja wa askari aliwatahadharisha wenzake kuwa
wasipige mabomu na risasi kwa kuwa hapo ni kanisani lakini wenzake walipinga
wakisema kuwa huyu mtu ana kiburi na watu hawa ni wakorofi. Wakati risasi na
mabomu yakipigwa baadhi ya askari walikuwa wakiokota maganda ya risasi na mabaki
ya mabomu ya machozi ili kuondoa ushahidi. Hata hivyo baadhi ya risasi za moto,
maganda ya risasi za moto na mabaki ya mabomu yalibaki kanisani na yamehifadhiwa
mahali maalum kwa hatua zaidi.

Kanisani kulikuwa na idadi ya waumini kati ya sitini na sabini waliokuwa wanaabudu.
Polisi waliwakamata jumla ya waumini 53 pamoja na wachungaji waliokuwa wakiongoza
ibada wakiwapiga na kuwasweka katika magari ya polisi kuwapeleka kituoni pamoja na
kuvuta gari zilizokuwa zimeegeshwa nje ya kanisa kwa breakdown. Tumepata habari
kuwa walikuja na baadhi ya waandishi wa habari walioandaliwa kabla ili kurekodi tukio
hilo na ushahidi tunao. Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwa makusudi
ili likatekelezwe katika kanisa la Efatha. Tukio hili linatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa
kwa Huduma ya Efatha.

Kitendo cha polisi kuvamia na kuvuruga ibada ni kinyume na sheria na katiba ya jamhuri
ya Muungano wa Tanzania iliyoweka uhuru wa kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza
kwamba ibada ziheshimiwe na zisiingiliwe. Tunajiuliza kulikuwa na tatizo gani polisi
wasisubiri nje ibada iishe na wawachukue watu wanaotaka kuwachukua. Ndani ya
kanisa hakukuwa na vita, wala mtu mwenye silaha, wala mtu anayeuawa ambaye polisi
walilazimika kwenda kumwokoa. Sisi tunaliona hili kuwa ni kumdharau Mungu,
kuvuruga ibada na kuwadhalilisha waumini wa Efatha waliokuwa wakitumia uhuru wao
wa kuabudu. Leo wamefanya hivyo kwa dharau ndani ya kanisa la Efatha, kesho
tutegemee watakwenda kufanya nini kwa dhehebu jingine, Msikiti, Dini nyingine au
watu waliokusanyika kihalali na kwa sababu halali?

3. MAJUMUISHO

Vielelezo vyote kuhusu umiliki wetu halali wa eneo hili vilishawasilishwa polisi mkoani
na wilayani. Kutokana na maelezo haya Efatha Foundation Ltd inapenda kuuthibitishia
umma kuwa EFATHA FOUNDATION LTD ndiyo mmiliki halali wa KIWANJA NA. 90, ENEO
LA MWENGE (NURU CENTRE) na si vinginevyo.

KATIBU
EFATHA FOUNDATION LTD
 
Hii ya ufufuo nashauri ajiunge na mbunge wa arusha kufufua walio wafu
OTIS
 
Mwingira ni Mjasiriamali anayelekea kuwa bepari kama wenzake akina mama Lwakatare!

soma ukweli huu upate kuelewa na kuongea ukiwa na data:

EFATHA FOUNDATION LTD
P.O BOX 32174, MWENGE, DAR ES SALAAM
TELEPHONE: +255732993196, FAX:+255732993196
WEBSITE: www.efathafoundation.org
EMAIL: efathafoundationltd@yahoo.com / info@efathafoundation.org
OUR REF: EFL/ADMN/4/2012
DATE:
11th April, 2012

TAARIFA KWA UMMA

1. UMILIKI WA KIWANJA NA. 90, ENEO LA MWENGE (NURU CENTRE)

1.1 Utangulizi

Tarehe 9 mwezi April 2012, Jumatatu ya Pasaka,baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza
habari ya umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo hilo. Habari zilizotangazwa ni za
upande mmoja na hazina usahihi. Huduma ya Efatha inapenda kuelezea umma taarifa
sahihi juu ya upatikanaji wa kiwanja na 90, umiliki na matukio yaliyotokea katika eneo
hilo.

1.2 Upatikanaji na umiliki wa eneo

Serikali kupitia Tume ya Kurekebisha na Kubinafsisha Mashirika ya Umma (PSRC)
ilitangaza zabuni ya uuzwaji wa eneo la Mang'ula Mechanical and Machine Tools
Company Ltd iliyofilisika, Kiwanja namba 90, Mwenge katika magazeti ya Uhuru na Daily
News ya tarehe 4 mwezi Mei 2005.

Tarehe 18 Mei 2005, huduma ya Efatha kupitia kitengo chake cha uchumi, Efatha
Foundation Ltd, ilipeleka maombi ya zabuni ya kununua eneo hilo PSRC.
Efatha Foundation Ltd ilipokea barua kutoka PSRC yenye kumbukumbu Na.
PSRC/1/13/93 ya tarehe 30 Mei 2005 ikiarifu kwamba zabuni yetu ya kununua eneo hilo
imeshinda kwa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nne.

Masharti ya Malipo ya zabuni yalikuwa asilimia kumi ilipwe wakati wa kupeleka maombi
na asilimia tisini ilipwe ndani ya miezi mitatu baada ya kushinda zabuni.

Efatha Foundation Ltd ililipa shilingi milioni arobaini yaani asilimia kumi ya bei siku ya
kupeleka maombi ya zabuni kwa hundi Na. 000261 ya benki ya Azania na kupewa risiti
ya PSRC Na. 6956 ya tarehe 31 Mei 2005. Na shilingi milioni mia tatu sitini ililipwa kupitia
hundi Na. 000319 ya benki ya Azania ambayo ni asilimia tisini tarehe 10 mwezi Juni 2005
na kupewa risiti ya PSRC Namba 6984 na hivyo malipo yote yakawa yamekamilishwa.

Baada ya kukamilisha malipo Efatha Foundation Ltd ilikabidhiwa hati miliki Namba
41641 ambayo ilipelekwa wizara ya Ardhi ili ibadilishwe jina kutoka mmiliki wa mwanzo
na kuandikishwa jina la Efatha Foundation Ltd. Kwa hiyo Serikali ikahamisha umiliki
kutoka Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika kwenda
Efatha Foundation ltd tarehe 15 Novemba 2005 saa sita kamili mchana kwa uhamisho
Namba 98648.

Kabla ya Huduma ya Efatha kununua eneo hilo kulikuwa na wavamizi ambao ni
makampuni na watu binafsi kumi na moja ambao walikuwa wamewekwa katika eneo
hilo na Mang'ula Mechanical and Machine Tools Company Ltd iliyofilisika bila kibali cha
mfilisi yaani PSRC. Kwa kuwa hawakuwa wapangaji halali walikuwa wavamizi
(trespassers). Wavamizi hao wakapewa notisi ya kuondoka na PSRC lakini
hawakuondoka. Baadae shughuli za mfilisi, PSRC, zikachukuliwa kisheria na Consolidated
Holding Corporation (CHC). CHC nao wakawapa wale wavamizi notisi kuwa waondoke
kwa sababu eneo hilo limeuzwa lakini hawakuondoka. Efatha Foundation Ltd ilipomiliki
eneo hili kihalali na kisheria wakawapa wavamizi notisi ya kuondoka mwaka 2005,
wavamizi nane wakatii amri wakaondoka na wavamizi watatu walikaidi kuondoka
ambao ni pamoja na Afro Plus Industries Ltd.

Baada ya hapo wavamizi watatu waliokataa kuhama wakafungua kesi mahakamani
dhidi ya Efatha Foundation Ltd wakipinga kuhamishwa.

Ni vyema ieleweke kuwa Efatha Foundation Ltd iliponunua eneo hili thamani yake
ilijumuisha majengo yaliyokuwa yamejengwa humo na Mang'ula Mechanical and
Machine Tools Company Ltd iliyofilisika. Hii ni pamoja na jengo alilokuwa anatumia Afro
Plus Industries Ltd ambalo linalalamikiwa kubomolewa na kwamba tumeharibu mali.
Jengo lililobomolewa ni mali ya Efatha Foundation Ltd na siyo mali ya Afro Plus
Industries Ltd kama ilivyodaiwa.

2. UVAMIZI WA POLISI NDANI YA KANISA LA EFATHA MWENGE

Tarehe 9 Aprili 2012, jumatatu ya pasaka, majira ya saa kumi na mbili asubuhi waumini
wa Efatha walikuwa katika ibada ya morning glory katika kanisa la Efatha Mwenge
wakiongozwa katika ibada hiyo na Mchungaji David Mwakisole ndani ya kanisa. Kanisa
limezungushiwa ukuta pande zote nne na lina mageti ya kuingilia kanisani ambayo
yanafungwa. Polisi walipanda ukuta wakachungulia wakasikika wakisema hawa huku
ndani. Baadae polisi wakarukia ndani kupitia ukutani. Wakati ibada inaendelea ghafla
waumini walivamiwa kutoka nje na watu ambao baadae walitambuliwa kuwa ni polisi.
Walipoingia kwa nguvu wakatupa mabomu ya machozi ndani ya kanisa huku wakifyatua
risasi za moto wakati ibada ikiendelea. Kwa kitendo hicho ibada ilivurugika na kusimama
na waumini wakaanza kukimbia ovyo ndani ya kanisa. Risasi na mabomu ya machozi
yalitupwa kuelekea madhabahuni na kuelekea kwa waumini waliokuwa katika ibada.
Waumini wengine waliokuwa wakija kwenye ibada walizuiliwa nje na kukamatwa.
Kilichofuata ni vurugu huku waumini wakikimbia na polisi wakiwapiga kwa virungu,
vitako vya bunduki na mateke. Baadhi ya waumini walijeruhiwa vibaya sehemu
mbalimbali za mwili na ukumbi wa kanisa ulitapakaa damu. Pia polisi walivunja
madirisha, viti, milango na spika kama ilivyoonyeshwa katika baadhi ya vyombo vya
habari hasa ITV. Kabla hawajavamia, mmoja wa askari aliwatahadharisha wenzake kuwa
wasipige mabomu na risasi kwa kuwa hapo ni kanisani lakini wenzake walipinga
wakisema kuwa huyu mtu ana kiburi na watu hawa ni wakorofi. Wakati risasi na
mabomu yakipigwa baadhi ya askari walikuwa wakiokota maganda ya risasi na mabaki
ya mabomu ya machozi ili kuondoa ushahidi. Hata hivyo baadhi ya risasi za moto,
maganda ya risasi za moto na mabaki ya mabomu yalibaki kanisani na yamehifadhiwa
mahali maalum kwa hatua zaidi.

Kanisani kulikuwa na idadi ya waumini kati ya sitini na sabini waliokuwa wanaabudu.
Polisi waliwakamata jumla ya waumini 53 pamoja na wachungaji waliokuwa wakiongoza
ibada wakiwapiga na kuwasweka katika magari ya polisi kuwapeleka kituoni pamoja na
kuvuta gari zilizokuwa zimeegeshwa nje ya kanisa kwa breakdown. Tumepata habari
kuwa walikuja na baadhi ya waandishi wa habari walioandaliwa kabla ili kurekodi tukio
hilo na ushahidi tunao. Kwetu sisi inaonyesha kuwa tukio hilo liliandaliwa kwa makusudi
ili likatekelezwe katika kanisa la Efatha. Tukio hili linatupa hisia kuwa kuna chuki kubwa
kwa Huduma ya Efatha.

Kitendo cha polisi kuvamia na kuvuruga ibada ni kinyume na sheria na katiba ya jamhuri
ya Muungano wa Tanzania iliyoweka uhuru wa kuabudu na sheria za nchi zinazoeleza
kwamba ibada ziheshimiwe na zisiingiliwe. Tunajiuliza kulikuwa na tatizo gani polisi
wasisubiri nje ibada iishe na wawachukue watu wanaotaka kuwachukua. Ndani ya
kanisa hakukuwa na vita, wala mtu mwenye silaha, wala mtu anayeuawa ambaye polisi
walilazimika kwenda kumwokoa. Sisi tunaliona hili kuwa ni kumdharau Mungu,
kuvuruga ibada na kuwadhalilisha waumini wa Efatha waliokuwa wakitumia uhuru wao
wa kuabudu. Leo wamefanya hivyo kwa dharau ndani ya kanisa la Efatha, kesho
tutegemee watakwenda kufanya nini kwa dhehebu jingine, Msikiti, Dini nyingine au
watu waliokusanyika kihalali na kwa sababu halali?

3. MAJUMUISHO

Vielelezo vyote kuhusu umiliki wetu halali wa eneo hili vilishawasilishwa polisi mkoani
na wilayani. Kutokana na maelezo haya Efatha Foundation Ltd inapenda kuuthibitishia
umma kuwa EFATHA FOUNDATION LTD ndiyo mmiliki halali wa KIWANJA NA. 90, ENEO
LA MWENGE (NURU CENTRE) na si vinginevyo.

KATIBU
EFATHA FOUNDATION LTD
 
Sheria itafuata mkondo wake kama ni kweli.Kumiliki eneo inaonekana mwingira yupo smart.Ttatizo ni kutokuwa na subira na kutumia nguvu.Hayo maengineyo ya uzinzi na uchafu katika imani yake mjijue wenyewe.
 
Back
Top Bottom