Silaa aagiza kukamatwa kwa aliyesababisha mgogoro eneo la maegesho ya bajaji Gongo la mboto!!

franckkimm

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
440
852
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi Gongo la Mboto kumkamata bwana mmoja aliyefahamika kwa majina ya Bakari Shingo na wenzie akiwemo msimamizi wa eneo hilo kutokana na kudaiwa kusababisha mgogoro wa eneo la maegesho ya bajaji katika mtaa wa Gongo la Mboto Ilala jijini Dar Es Salaam.

Aidha Silaa amemtaka mkuu wa mipango miji halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam kumilikisha eneo hilo la maegesho ya bajaji kwa mkurugenzi wa jiji na kumtaka aweke utaratibu mzuri wa malipo kwa madereva wa waliokuwa wakipaki eneo hilo ikiwemo kuwapunguzia ushuru kutoka shilingi elfu 2500 waliyokuwa wakilipa awali hadi kufikia shilingi elfu moja 1000.

Waziri Silaa ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo hilo baada ya kuwepo mgogoro huo ambao umezua taharuki hasa kwa madereva bajiji waliokuwa wakifanya kazi eneo hilo kutolewa na anayedai kuwa ndiye mmiliki.
 
Back
Top Bottom