Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Lissu biashara hajui ila kakalia kishabiki shabiki tu

kuna biashara unaweza tumia Mil.50 kuifungua ila faida ikaja robo au hata robo isifike kwa mwezi m1

Biashara imegharimu 50mil ila faida per day 100k ukipiga kwa mwaka unapata 36,000,000M

Unaweza ukaona ndani ya mwaka mzima Hata hela ya biashara(mtaji haijarudi) ila huwezi sema hii biashara MBAYA

au HAILIPI
BADO safari inaendelea kwenye biashara kuna miaka inaendelea kwenda Faida itaonekana TU

Tatizo la watu waliozoea mishahara ya mwisho wa mwezi ni 1 tu wao UVUMILIVU kwao ni ZERO.

Yani lissu anataka anza leta siasa kwenye Biashara (huyu mtu huyu aseeee) yani iko hivi bwana Lissu

Hizo ndege hata zikifanya kazi kwa miaka 20 hazijrudisha hiyo hela Bado siwezi sema eti Tulifanya makosa zinunua

Ila tu hizo ndege ningekuona wamaana kama ungesema zimetengeneza HASARA kiasi fulani au zimetengeneza MADENI

kiasi fulani Ndio tungepima Mizani sasa HASARA vs FAIDA ila usitupimie biashara kwa kipimo chako cha CAPITAL vs FAIDA

Faida zipo indirect way na Direct way

Lissu usitake jitoa ufahamu hujui ni watalii wangapi wameshaletwa nchini na kuacha pesa tofauti na Hela(faida) walizosema ATCL

ki ufupi bwana Lissu TUACHE KIDOGO.
 
Kwenye suala wa ndege mimi namuunga mkono Magufuli. Ni kweli gharama zake ni kubwa na biashara ya ndege ni ngumu. Kitu kinachonifanya mimi nimuunge mkono ni kuwa hizi fedha kipindi cha awamu iliyopita zilitumika kwenye mambo ya kijinga kama safari za viongozi nchi za nje, kulipa wafanyakazi hewa, ufisadi kwenye idara mabali mbali za serikali, vikao vya gharama vya wafanyakazi wa serikali kwenye hotel kubwa nk. Sasa kama zilikuwa zinaishia mifukoni mwa watu si bora hata huyu aliyenunua ndege?
Siyo kila anayekuja JF lazima achangie hoja. Wengine muwe mnasoma na kujifunza tu. Yaani kwa akili yako unaamini kweli matumizi ya Serikali yamepungua kwa sababu safari za watumishi wa umma zimepungua?

Na unaamini ndiyo zilizonunua ndege? Pole sana, Serikali hii ndiyo ina matumizi makubwa ya kutisha kuliko zote. Kama una elimu ya kawaida tu nenda kasome CAG Report, ukielewa ndiyo urudi hapa
 
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.
Dotto kama kitaalamu alipaswa mwambie mjomba wake namna taratibu za fedha zinavyotaka kwa kuwa yeye ndiye mtaalamu.
 
Sasa ndege sita zimekusanya bil 30 kwa miaka 3 hapo bado service makadilio itakuwa bil 10
Kwahiyo hapa makusanyo halali ni bil 20 inakusanya bill 7 kila mwaka
Ili tuweze kurudisha trillion 1.7 inatuhitaji miaka zaidi 100 nda ndege sina hakika kama zitaendelea kutumika sipingi ununuzi wa ndege ila aliyefikiria ununuzi wa ndege tena kwa cash halikuwa hana plan lengo lake watu waone tu kafufua shirika la ndege
Hebu tupige hesabu....... Mapato Bil 30 - Uwekezaji 1.7 Trilion ( Bil 1700 )

% Interest after 3 years = 30//1700 times 100 = 1.76 Billion. (Hii si Faida bali ni Gross)

Ukifanya kwa kila mwaka inakuwa 1.76 divice by 3 = 589 milion. (Hii nayo ni Gross).

Kifupi unawekeza 1.7 Trillion then unapata Gross income ya 589 mil kwa mwaka.

au ni sawa na kusema unakusanya Tshs Million moja kama Gross kwa uwekezaji wa Billion 2.9
 
Siyo kila anayekuja JF lazima achangie hoja. Wengine muwe mnasoma na kujifunza tu. Yaani kwa akili yako unaamini kweli matumizi ya Serikali yamepungua kwa sababu safari za watumishi wa umma zimepungua?

Na unaamini ndiyo zilizonunua ndege? Pole sana, Serikali hii ndiyo ina matumizi makubwa ya kutisha kuliko zote. Kama una elimu ya kawaida tu nenda kasome CAG Report, ukielewa ndiyo urudi hapa
Pole sana wewe unayeumia roho. Ulizoea kula vya bure kama nzi awamu iliyopita. Fanya kazi.
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Heeeee!!! Mkuu yaani hizo ndege ni kwa ajili ya kutoa huduma? Ipi hiyo vitu vingine sio lazima kuchangia,
 
Dotto kama kitaalamu alipaswa mwambie mjomba wake namna taratibu za fedha zinavyotaka kwa kuwa yeye ndiye mtaalamu.
Inaelekea wewe hufahamu serikali inavyofanya kazi. Hivyo basi wazaramo wanasema 'karaga baho'
 
Siyo kila anayekuja JF lazima achangie hoja. Wengine muwe mnasoma na kujifunza tu. Yaani kwa akili yako unaamini kweli matumizi ya Serikali yamepungua kwa sababu safari za watumishi wa umma zimepungua?

Na unaamini ndiyo zilizonunua ndege? Pole sana, Serikali hii ndiyo ina matumizi makubwa ya kutisha kuliko zote. Kama una elimu ya kawaida tu nenda kasome CAG Report, ukielewa ndiyo urudi hapa
Naiunga mkono hoja yako kwa 100%
 
Wananunuzi wa Ndege wao wanataka 10% yao kwenye ununuzi na pia kwenye matengenezo service zake, wao wanaangalia matumbo yao kwanza mengineyo ni mbele kwa mbele huko
Tuna tabia ya kuzungumzia mambo ambayo hatuna weledi nazo . Na hizo tunazikuza kiasi kwamba hata ukweli unapotolewa kwa vile haupendezi basi ni wachache tu wanaweza ku-appreciate hayo.
 
CHADEMA mnajidhalilisha sana kwenye Ilani yenu ya uchaguzi 2015 mliandika kuhusu ndege ukurasa wa 53 hivi mnadhani watu hatusomi au hatukumbuki mliyokuwa mkiyanadi sasa yamefanywa na CCM mnaona mabay au mnadhani watanzania ni wote mazuzu.

Hapo kwenye huo ukurasa walisema watanunua ndege kwa cash bila hata bunge kushirikishwa?
 
Kuwa na ndege za serikali kuna manufaa mengi sana achilia mbali faida halisi itakayokuwa inatengenezwa na uendeshaji wa shirika hilo. Baadhi ya manufaa ya kufufua shirika la ndege ni:
a. Ajira ndege moja mfano hii Dreamliner inaporuka huwa ina wafanyakazi wasiopungua 12 yaani wakiwemo mapilot wawili, flight engr mmoja, flight technician mmoja, cabin crews ( air hostess) wasiopungua 8. Hapo awali ndege za kampuni binafsi zilikuwa na watumishi hata kutoka nje ya Tanzania. Kwa hiyo hata kama ndege haitakuwa na faida kubwa bado kuna ajira zinatengenezwa kwa watanzania.
b. Kodi, biashara inayofanywa na ATCL hukatwa kodi mfano unaponunua ticket kodi ya kununua ticketi (VAT) hunufaisha faida, lakini zipo kodi nyingi zinatokana usafiri wa anga mfano kodi za PAYEE kwa wafanyakazi. Hapo awali unakuta mfanyakazi wa fast jet tuseme pilot ni raia na mkazi wa Kenya kwa malipo yake hulipwa kupitia bank nchini Kenya kwa hiyo PAYEE italipwa Kenya.
c. Kushusha gharama za usafiri, Tangu ATCL imefufuliwa gharama za usafiri wa anga hapa nchini zimeshuka. Kwa asiye tumia usafiri wa anga anaweza kuona hamna lolote, kabla ya ATCL kufufuliwa usafiri wa anga ulitawaliwa na makampuni binafsi ambapo kuna wakati yalikuwa yakisoma msimu wa abiria wengi na kupandisha bei kuna wakati nauli ya kwenda mwanza tu one way mtu analazimika kulipia zaidi ya 400,000 ambapo kwa sasa kwa ATCL ni chini ya gharama ya kwenda na kurudi Mwanza wakati wote.
d. Ufufuaji wa ATCL umesababisha kuibuka fursa za biashara na ajira. Kulikuwa na viwanja vya ndege vilivyokuwa vimekufa au havipo kabisa. Viwanja hivyo vimepelekea watu kupata ajira za kuhudumia viwanja, mfano huduma za zimamoto, usafi, uhakiki wa mizigo, ulinzi, biashara katika viwanja vya ndege.
e. Zipo faida nyingi sana achilia mbali za kuleta watalii, kuitangaza nchi kimataifa.

Faida ni nyingi mno;
Aione TL kwenye Jalada
 
Inaelekea wewe hufahamu serikali inavyofanya kazi. Hivyo basi wazaramo wanasema 'karaga baho'
Kati ya mimi na wewe nani anajuwa Serikali? Wewe ni mshabiki tu wa huu utawala mbovu mimi ni muumini wa Good Governance and rule of law.
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Sijui kama unajua vipau mbele vya taifa, na sidhani kama utavijua kama hutakaa uwaze vyema na kufikiri kwa kutumia akili ya kichwani.
 
JF siku hizi imekuwa kama tumbo la fisi, kila uchafu unaingia na kutoka. Natamani JPM aendelee kupiga kazi mpaka 2035 ili Tanzania iendelee kuinuka katika nyanja zote. Tulikuwa tumedhauliwa sana na mataifa ya nje, yaani resources zote zilizopo tulikuwa omba omba, fedha za mikopo na misaada zinatumika isivyo, wapiga dili kila mahali, sekta binafsi iliyokuwa inafanya biashara chafu, uzembe na kutowajibika katika sekta ya umma pamoja. Leo Taifa limepata mzalendo bado watu wanalalama vijiweni, please, tuwe na busara kidogo. Duniani hakuna Serikali inayoajiri kila mtu, tujifunze kujiajiri. Tunataka Serikali ipite mtaani kugawa hela, tuache akili za matope, tuache kulia lia, opportunities zipo nyingi sana Tanzania.

Mzalendo ananajisi box la kura au mimi ndio sijui maana ya uzalendo? Sasa hivi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
 
Je, zina faida gani economically?

Hizi hela ni zaidi ya mtaji wa viwanda vya Bakhresa. Angalia impact ya viwanda vya Bhakresa na ndege za Magufuli in terms of mzunguko wa hela, ajira na services. Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli.

By the way, hata hayo makampuni makubwa yanapata hasara na biashara ya ndege si biashara ya kutegemea kujenga uchumi. Je, Bunge limepitisha manunuzi ya ndege saba?

Hivi unaachaje kuwekeza kwenye kilimo, madini, elimu, gesi,maji, umeme then unaenda kuwekeza kwenye ndege kwa taifa changa kama hili ambalo watoto hawana madawati na hospitali mama wajawazito wanalala chini?

Hapo hatujagusa demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Huu uongozi umechafua sana picha ya taifa hili; this is one of the worst leaderships. By the way, kila chenye mwanzo kina mwisho, walikuwepo wakina Mobutu, wapo wapi now? Tusibiri muda wake utafika tu.

View attachment 1250571
Kupanga ni kuchagua ndege ni muhimu pia,lkn tungeanza na vigusavo wengi mfano miradi igusayo watu ili kukuza ajira na kuongeza idadi ya walipa kodi,kisha ziada ndo tukimbilie kwenye miradi hii mikubwa bila kuwasomesha watu namba kwa kuathiri shughuli zao. Hicho kilichokusanywa ni kidogo sana kulinganisha na thamani za ndege hizo kama tungewekeza kwenye miradi mingine ya kukuza ajira za vijana nchini.
 
Mzalendo ananajisi box la kura au mimi ndio sijui maana ya uzalendo? Sasa hivi ni ngumu kutofautisha uzalendo na ujinga.
Neno Uzalendo limebadili maana siyo ile tunayoijua. Kwa mfano hapa Tanzania hakuna mtu amepigania haki za madini kutoka kwa wawekezaji kushinda Tundu Lissu. Halafu Meko anasema Tundu Lissu siyo mzalendo auliwe. Ridiculous!!

Wanaijiita wazalendo ndiyo akina Bashite, Meko na Ole Sabaya wakati kazi yao ni kujitajirisha kwa fedha za unyang'anyi wa wazi wazi.
 
Pablo Blanco,

Ununuzi wa ndege ni dili la wajanja wachache kuna 10% zao humu ndiyo maana hununua kwa cash ili wachukue chao mapema na hawataki CAG kunusa hesabu za ununuzi wa ndege kwa hofu ya kuibua ufisadi wao, siyo kwamba hawajui kuwa Ndege hazina faida kwa nchi bali wameangalia matumbo yao na dhana ya CCM isemayo chukua chako mapema.

Awamu hii ni tofauti na awamu ya Kikwete na mkapa ambao walipiga dili zao jioni mwishoni mwa utawala wao, hawa wa sasa wao wanakula mapema chao kisha huko mbeleni ni majaliwa ya mwenyezi mungu, hakuna sehemu bunge linashirikishwa juu ya ununuzi wa ndege hata ujenzi wa Chato Airport umefanywa kienyeji pasipo idhini ya bunge.
Hata kama wanapiga dili si watazitapika ukiingia awamu nyingine maana madaraka ni sawa na koti la kuazima.Maana huwezi ficha Mali au pesa zitataifishwa tu.
 
Back
Top Bottom