Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Ununuzi wa Ndege ni Dili la wajanja wachache kuna 10% zao humu ndiyo maana hununua kwa cash ili wachukue chao mapema na hawataki CAG kunusa hesabu za ununuzi wa Ndege kwa hofu ya kuibua ufisadi wao, siyo kwamba hawajui kuwa Ndege hazina faida kwa Nchi bali wameangalia matumbo yao na dhana ya CCM isemayo chukua chako mapema, awamu hii ni tofauti na awamu ya Kikwete na mkapa ambao walipiga Dili zao jioni mwishoni mwa utawala wao, hawa wa sasa wao wanakula mapema chao kisha huko mbeleni ni majaliwa ya mwenyezi mungu, Hakuna sehemu bunge linashirikishwa juu ya ununuzi wa Ndege hata ujenzi wa chato Airport umefanywa kienyeji pasipo idhini ya bunge.

mmebanwa kila pahala wacheni wivu wa pwani
 
Hivi wanasiasa wetu ni watu wa namna gani?
Kwenye manifest ya CDM kuelekea uchaguzi 2015 walizungumzia azma ya serikali itakayoundwa na CDM kufufua shirika la ATC kwa kununua ndege mpya.
Leo hii wakubwa hao hao wanabeza utekelezaji wa suala hilo hilo na JPM. Halafu ni hao hao pia walipinga sana serikali kuzuia makenikia na wakitahadharisha kuwa TZ inawekushtakiwa na mashirika hayo ya kimataifa na mwishowe itabidi mlipa kodi ndiyo abebe mzigo huo. Leo matokeo yake wote tumeyaona. Sasa tumuamini nani?? Wale ambao kila kitu wanaponda au wale ambao hutekeleza kwa vitendo.?
Nadhani ifike wakati wanasiasa watafakari hayo wanayotuambia kwani inafika wakati wanajidhalilisha ni bora watafute mada nyingine za kutudanganya..

Duniani kote hata mashirika makubwa hawanunui Ndege kwa cash bali hukopa kwa kulipa kidogo kidogo, huo ununuzi wa cash kuna ufisadi ndani yake ndiyo maana wapinzani wanapiga kelele.
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Sina jina la kukupa ila ndege hazikununuliwa kwa ajili ya kutoa huduma, zipo kibiashara zaidi ndiyo sababu hazikupelekwa Government Flight Agency ambako ni kwa huduma.
 
Hivi wanasiasa wetu ni watu wa namna gani?
Kwenye manifest ya CDM kuelekea uchaguzi 2015 walizungumzia azma ya serikali itakayoundwa na CDM kufufua shirika la ATC kwa kununua ndege mpya.
Leo hii wakubwa hao hao wanabeza utekelezaji wa suala hilo hilo na JPM. Halafu ni hao hao pia walipinga sana serikali kuzuia makenikia na wakitahadharisha kuwa TZ inawekushtakiwa na mashirika hayo ya kimataifa na mwishowe itabidi mlipa kodi ndiyo abebe mzigo huo. Leo matokeo yake wote tumeyaona. Sasa tumuamini nani?? Wale ambao kila kitu wanaponda au wale ambao hutekeleza kwa vitendo.?
Nadhani ifike wakati wanasiasa watafakari hayo wanayotuambia kwani inafika wakati wanajidhalilisha ni bora watafute mada nyingine za kutudanganya..
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa. Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwahayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!

Yaani Rais wa Nchi ndiyo ana Akili kuliko watanzania wote? au maamuzi yake hutoka mbinguni kwa mungu yeye ni malaika? Acha kusingizia mabeberu, Mbona mkienda kuomba omba misaada kwa wazungu mnawaita wafadhili lakini wakiyakosoa matumizi mabaya ya pesa zao hata za walipa kodi zenye 10% zenu mnakimbilia kuwaita mabeberu, acheni kuishi kwa Fikra za zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM pekee, usijona una Akili kuliko wengine Tambua kuwa Akili ni nywele na kila mmoja ana zake.
 
Kwenye suala wa ndege mimi namuunga mkono Magufuli. Ni kweli gharama zake ni kubwa na biashara ya ndege ni ngumu. Kitu kinachonifanya mimi nimuunge mkono ni kuwa hizi fedha kipindi cha awamu iliyopita zilitumika kwenye mambo ya kijinga kama safari za viongozi nchi za nje, kulipa wafanyakazi hewa, ufisadi kwenye idara mabali mbali za serikali, vikao vya gharama vya wafanyakazi wa serikali kwenye hotel kubwa nk. Sasa kama zilikuwa zinaishia mifukoni mwa watu si bora hata huyu aliyenunua ndege?
 
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.
 
Segerea 2026 watakwenda wengi jela juu ya hizo Ndege tu kwani hata ukarabati wake umejaa ufisadi wa kutisha sana, mda utaongea waache wajimwambafy sasa huko mbeleni mwenye kinga ni mmoja pekee.
 
Mkuu, usilidhalilishe shirika letu la ndege. Nalo liko kibiashara, si kihuduma. Unapochangia mada kama hizi, jiulize mara mbilimbili kabla ya kuandika. Kwahiyo, kwako wewe, ndege za ATCL zinatoa huduma kama ilivyo kwa shule, zahanati na mabomba? Bure kabisa wewe!

Mkuu kwenye vikao mbali mbali vya ccm ndivyo wanavyoaminishwa!
Na pengine kuna asilimia kadhaa za ukweli...
Ujue hizi ndege tangu zimenunuliwa zinazurura tu humu nchini!
Ila kwa jinsi nijuavyo hizo 30 bilions ni makusanyo ghafi wala si faida!
 
Kuna kitu watu hamjui ni kua magu anapiga cha juu kwenye madili karibia yote ya serikali siku hizi, ni ukweli mchungu ambao hamtaki kuusikia maana mnamuona ndugu yenu kama malaika kua hawezi fanya kitu kama hicho.

Hakukua na haja ya kununua ndege hizi kwa cash, tena kwa fujo ndege 11. Kafunga mashirika ya ndege mengine kama fastjet siku hizi kila mtu anapanda ATCL, ila cha kushangaza pamoja na yote hayo kuingiza 30Bil peke yake miaka yote hiyo inamaanisha hadi hiyo hela ije kurudi ni miaka zaidi ya 70. Hapo ni vizazi vingi vimepita.

Sasa tuacheni kugombana na kutukanana tujaribu kufikiria, kitu ambacho return yake ni 70 years (assuming tutaendelea hivi) hiyo hela si bora ingewekwa kwenye elimu na vitu vingine vya muhimu kama healthcare? Au kama tuna shida sana na ndege basi tungenunua angalau haat 5 mwisho, kuagiza ndege 11 kwa cash huku nchi yenyewe maskini na sehemu nyingine zote hazijadevelop ni kitu cha ajabu. Huo utalii mnaosema tunakuza tusijidanganye hata watanzania tu wataruka na Emirates, Qatar au mashirika mengine ambayo yana competitive prices, hakuna mtu atapanda ATCL bei za kijinga kwa sababu tu ya uzalendo, the market always win.

Ukweli hizo hela kwenye ndege zimetupwa tu, hizo ndege subiri ziange kupata matatizo tuinvest hela nyingine tena kuzifix. Wakati mashirika mengine duniani yanapunguza ndege sisi ndo tunaongeza tena kwa cash. Lol
 
Hivi wanasiasa wetu ni watu wa namna gani?
Kwenye manifest ya CDM kuelekea uchaguzi 2015 walizungumzia azma ya serikali itakayoundwa na CDM kufufua shirika la ATC kwa kununua ndege mpya.
Leo hii wakubwa hao hao wanabeza utekelezaji wa suala hilo hilo na JPM. Halafu ni hao hao pia walipinga sana serikali kuzuia makenikia na wakitahadharisha kuwa TZ inawekushtakiwa na mashirika hayo ya kimataifa na mwishowe itabidi mlipa kodi ndiyo abebe mzigo huo. Leo matokeo yake wote tumeyaona. Sasa tumuamini nani?? Wale ambao kila kitu wanaponda au wale ambao hutekeleza kwa vitendo.?
Nadhani ifike wakati wanasiasa watafakari hayo wanayotuambia kwani inafika wakati wanajidhalilisha ni bora watafute mada nyingine za kutudanganya..
Tofautisha manifest na manifesto. Anyways, mi sijasoma hizo nyaraka, lakini walisemaje kuhusu CAG na ukaguzi wa manunuzi ya ndege na uendeshaji wa shirika la ATCL?
 
Je, zina faida gani economically?

Hizi hela ni zaidi ya mtaji wa viwanda vya Bakhresa. Angalia impact ya viwanda vya Bhakresa na ndege za Magufuli in terms of mzunguko wa hela, ajira na services. Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli. By the way, hata hayo makampuni makubwa yanapata hasara na biashara ya ndege si biashara ya kutegemea kujenga uchumi. Je, Bunge limepitisha manunuzi ya ndege saba?

Hivi unaachaje kuwekeza kwenye kilimo, madini, elimu, gesi,maji, umeme then unaenda kuwekeza kwenye ndege kwa taifa changa kama hili ambalo watoto hawana madawati na hospitali mama wajawazito wanalala chini?

Hapo hatujagusa demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Huu uongozi umechafua sana picha ya taifa hili; this is one of the worst leaderships. By the way, kila chenye mwanzo kina mwisho, walikuwepo wakina Mobutu, wapo wapi now? Tusibiri muda wake utafika tu.

View attachment 1250571
Alijibiwa aisee
Screenshot_20191031-183853_Twitter.jpeg
Screenshot_20191031-183153_Twitter.jpeg
Screenshot_20191031-183143_Twitter.jpeg
 
Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli.
Hapa ndipo mnapodhihira kuwa wapinzani hamna akili sawa sawa... Mkuu umeshawahi kwenda AirPort ukaona lile Dreamliner linavyoshusha watu? Kwani lazima kila kitu mpinge?
 
Kwenye suala wa ndege mimi namuunga mkono Magufuli. Ni kweli gharama zake ni kubwa na biashara ya ndege ni ngumu. Kitu kinachonifanya mimi nimuunge mkono ni kuwa hizi fedha kipindi cha awamu iliyopita zilitumika kwenye mambo ya kijinga kama safari za viongozi nchi za nje, kulipa wafanyakazi hewa, ufisadi kwenye idara mabali mbali za serikali, vikao vya gharama vya wafanyakazi wa serikali kwenye hotel kubwa nk. Sasa kama zilikuwa zinaishia mifukoni mwa watu si bora hata huyu aliyenunua ndege?

Kikwete licha ya hayo mapungufu yake kila mwaka aliwaongezea nyongeza ya mishahara watumishi wa umma, na Deni la Taifa halikuwa kubwa kama sasa ambapo wanajinadi kudhibiti wizi safari za nje lakini Deni la Taifa limepaa kuwa maradufu huku watumishi wa umma wakibuni Mbinu za kisayansi kufanya ufisadi pasipo kugundulika kirahisi kwa haraka, Ndege wanunue kwa mikopo lakini vitu vinginevyo vya maendeleo vifanyike kwa kasi ikiwemo kujenga miundominu bora zaidi isiyo haribiwa na mvua kirahisi
 
Eti muda si mrefu mtatamani kuziuza na hakuna wa kuzinunua'
Huu ni uchawi sasa, wewe unasema hivyo kama nani na unajua nini kuhusu biashara ya ndege mzee!?
Ndio kwanza vitendea kaz vnaendelea kuletwa na kuboreshwa wewe tayari ushaanza kuleta nuksi. Kuna biashara gani ya haraka ivo
Hizo ndizo tope zenyewe, biashara ya Ndege sio kuleta blah blah na kujifanya unatoa huduma, gharama za kuendesha hizo ndege ni kubwa kiasi kwamba muda sio mrefu mtatamani kuziuza na msipate wa kuzinunua, na bahati mbaya mnaharibu mahusiano na jamii ya kimataifa kila siku, na biashara inahitaji watu, ipo siku mtaanza kuzibebea mashudu, endeleeni na uzwazwa.
 
Hapa ndipo mnapodhihira kuwa wapinzani hamna akili sawa sawa... Mkuu umeshawahi kwenda AirPort ukaona lile Dreamliner linavyoshusha watu? Kwani lazima kila kitu mpinge?

Kukosoa ndiyo kazi ya upinzani huwezi kuwapangia vya kukosoa lazima wakosoe kuanzia dogo mpaka kubwa
 
Kwenye suala hili Dotto anaingiaje?
Tujikite kwenye maada maana ndugu zangu nyingi mkitoa hoja na kujibiwa kwa hoja badala ya kuendelea na mjadala mna tabia ya ku-diverge issue yenyewe na hivyo kupoteza maana.

Doto ni mmowapo wa waidhinishaji wa malipo ya cash , utakuja kujua huko mbele pindi CAG akituhusiwa kuingia humo.
 
Back
Top Bottom