Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Ukweli kuhusu ndege za Serikali

wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Huduma kwa wote au kwa matajili pekee? Mimi huku nanjilinji hayo mandoto liner ntayapandia wapi na lini?
 
Hakuna ufisadi kwenye ununuzi wa ndege, wapinzani achene kupotosha kwa kichaka cha CAG, price za ndenge hizi ziko wazi kwenye website za mashiraka hayo ingawaje inaweza kushuka kulingana na majadiliano ya pande mbili. Lissu tofauti na siasa hajawahi fanya biashara, hiki ni kipindi cha investments from 2015-2020 hautegemei faida kubwa wakati huu, objective should be rebranding, and better service provisions ili waweze kuvutia wateja wengi Zaidi na hatimaye baadae kupata profit, ROI haiwezi kuwa ndani ya miaka mitatu, hakuna biashara ya hivyo duniani kwa large scale, labda biashara ndogo ndogo za kununua karanga sh 10 unauza same day sh 20. Tuwape muda wa kutosha ATCL na management ili wafanye kazi, siasa hizi za kusema hivi kesho vile ndo tutaua shirika.
 
Hela za matanuzi ya Dubai na kule bondeni za kwenye masemina na warsha ndizo hizi zinazonunua ndege.

Hawa akili zao wamezitegesha katika kupinga kila jambo, halafu serikali inawajibu kwa vitendo.

Vitendo vipi wanajibu? Mwaka wa nne watumishi wa umma hawana nyongeza za mishahara na Deni la Taifa limezidi kuwa kubwa zaidi, kwani ndege lazima zingenunuliwa kwa cash? na kwa nini hawakukopa kisha hizo pesa zitumike kujenga miundo Mbinu kufufua viwanda mlivyogeuza magodauni huku kilimo kwanza kikiwa kimetelekezwa kabsa
 
Hakuna ufisadi kwenye ununuzi wa ndege, wapinzani achene kupotosha kwa kichaka cha CAG, price za ndenge hizi ziko wazi kwenye website za mashiraka hayo ingawaje inaweza kushuka kulingana na majadiliano ya pande mbili. Lissu tofauti na siasa hajawahi fanya biashara, hiki ni kipindi cha investments from 2015-2020 hautegemei faida kubwa wakati huu, objective should be rebranding, and better service provisions ili waweze kuvutia wateja wengi Zaidi na hatimaye baadae kupata profit, ROI haiwezi kuwa ndani ya miaka mitatu, hakuna biashara ya hivyo duniani kwa large scale, labda biashara ndogo ndogo za kununua karanga sh 10 unauza same day sh 20. Tuwape muda wa kutosha ATCL na management ili wafanye kazi, siasa hizi za kusema hivi kesho vile ndo tutaua shirika.

Ufisadi upo hata Ndege ya mkapa bei zilikuwa wazi lakini wajanja walipiga humo humo hata sasa bei zipo wazi na wajanja wamepiga humo humo lakini kwa kuwa sasa CAG hana ruhusa kuingia huko itakuwa vigumu kujua wamepiga ngapi lakini mwaka 2026 akiingia Rais mwingine ikulu vyote vitaanikwa wazi atapona mwenye kinga yake wengine wataelekea segerea tu.
 
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
Umemaliza yaani. Eti mtu anasema kuna mapato ya us dollar mil.14 halafu audit imezuiwa lakini watu wanashangilia!
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Kwahiyo ATCL in taasisi ya umma yenye malengo ya kutoa huduma?
Lah, sijui huyu bwana katumia nini kuingiza akili ya Watanzania wengi kwenye matope na kukwamia hapo.
KARLO MWILAPWA ukijadili mambo mengine nje ya matendo ya magu unakuwa uko smart sana, lakini kwenye hayo ni kama umefungwa kitambaa machoni na unaongoza njia. Pole sana, tiba ya tatizo hilo ni kuruhusu brain ifanye kazi na sio moyo
 
Tuanzie na hilo la akina mama wajawaziyo kulala chini ni hospitali gani hapa tanzania with vivid example?
Ushahidi gani unataka mkuu ? au tuibebe hospitali ambayo wamama wajawazito wamelala chini tukuletee nyumbani kwako ndio uamini ?!
 
Kwahiyo ATCL in taasisi ya umma yenye malengo ya kutoa huduma?
Lah, sijui huyu bwana katumia nini kuingiza akili ya Watanzania wengi kwenye matope na kukwamia hapo.
KARLO MWILAPWA ukijadili mambo mengine nje ya matendo ya magu unakuwa uko smart sana, lakini kwenye hayo ni kama umefungwa kitambaa machoni na unaongoza njia. Pole sana, tiba ya tatizo hilo ni kuruhusu brain ifanye kazi na sio moyo
Mkuu Chakaza. Hivi na yeye Mwilapa amesoma kabisa shule au ni kama Bashite ?.
 
Sasa ndege sita zimekusanya bil 30 kwa miaka 3 hapo bado service makadilio itakuwa bil 10
Kwahiyo hapa makusanyo halali ni bil 20 inakusanya bill 7 kila mwaka
Ili tuweze kurudisha trillion 1.7 inatuhitaji miaka zaidi 100 nda ndege sina hakika kama zitaendelea kutumika sipingi ununuzi wa ndege ila aliyefikiria ununuzi wa ndege tena kwa cash halikuwa hana plan lengo lake watu waone tu kafufua shirika la ndege
 
Ushahidi gani unataka mkuu ? au tuibebe hospitali ambayo wamama wajawazito wamelala chini tukuletee nyumbani kwako ndio uamini ?!

Muhimbili bado kuna msongamano mkubwa hata zile word zingine waganjwa wanalala chini
 
Ufisadi upo hata Ndege ya mkapa bei zilikuwa wazi lakini wajanja walipiga humo humo hata sasa bei zipo wazi na wajanja wamepiga humo humo lakini kwa kuwa sasa CAG hana ruhusa kuingia huko itakuwa vigumu kujua wamepiga ngapi lakini mwaka 2026 akiingia Rais mwingine ikulu vyote vitaanikwa wazi atapona mwenye kinga yake wengine wataelekea segerea tu.

CAG amewahi kagua ATCL ikiwa na ndege mbili, concerns yake ilikuwa ni madeni makubwa yaliyokuwa yanaikabili ATCL, pili uzembe na pesa za operations kupotea bila kuwa vibali, sio ununuzi wa ndege.

Kumbukeni watu wanasema serikali iandae mazingira ya wawekezaji waje wawekeze kwenye shirala la ndege, hayo mazingira yanatakiwa yaandaliwe kwa miaka mingapi? kama toka mkapa hatuna shirika, kaja kikwete hatuna shirika, hiyo ni Zaidi ya miaka 20, wawekeaji mbona hawaji au kuliona hilo shirika la ndege? kwani miaka ya nyuma ATCL ilikuwa haina wawekezaji ambao wanaijua hii biashara kutoka SA mbona tulizidi kupata hasara? kuna vitu vingine serikali lazima ifanye kwanza ndipo wawekezaji waje, mfano ATCL hadi 2022 itakuwa na ndege Zaidi 11, hapo hata mkiongea na wawekezaji wanaweza kukusikiliza maana wanajua wakuja kuwekeza kwenye kitu cha kuleta faida, au wanaweza serikali wakatoa share, watu wakanunua likuwa shirika linaendeshwa makampuni, watu + serikali.

Hii nchi nimegundua ina wananchi wa ajabu sana, 20+ yrs bila shirika la ndege tulibenefit na nini? Maisha yetu yalikuwa bora pasipo shirika la ndege? hatua zipi tulipiga kama taifa pasipo shirika la ndege? uwepo wa shirika hili au ununuzi wa ndege hizi kumetufanya hatua tulizopiga miaka 20 iliyopita kurudi nyuma? Jibu ni no, kuna nchi yeyote duniani itaendelea bila serikali ku invest? hizo ajira kwa wananchi wake mtazipata wapi, uchumi utakuwa vipi, shida kuwa kila mtanzania kwa sasa ni politicians, hebu tuwasikilizeni watalaam wa uchumi wanasema nini kuhusu ununuzi wa ndege hizi, from there we discuss positively, hii ni nchi yetu sote.
 
Mkuu, usilidhalilishe shirika letu la ndege. Nalo liko kibiashara, si kihuduma. Unapochangia mada kama hizi, jiulize mara mbilimbili kabla ya kuandika. Kwahiyo, kwako wewe, ndege za ATCL zinatoa huduma kama ilivyo kwa shule, zahanati na mabomba? Bure kabisa wewe!
Wewe Bw.Mselewa unaamini kabisa investment kama hiyo inaweza kuwa na payback period ya miaka 3??Kama unakubaliana na huo ujumbe basi naanza kuwa na wasi wasi na wewe.Kuna investment zinachukua miaka 15 hadi 20 nk kubreak even.Acheni siasa hapa
 
Sasa ndege sita zimekusanya bil 30 kwa miaka 3 hapo bado service makadilio itakuwa bil 10
Kwahiyo hapa makusanyo halali ni bil 20 inakusanya bill 7 kila mwaka
Ili tuweze kurudisha trillion 1.7 inatuhitaji miaka zaidi 100 nda ndege sina hakika kama zitaendelea kutumika sipingi ununuzi wa ndege ila aliyefikiria ununuzi wa ndege tena kwa cash halikuwa hana plan lengo lake watu waone tu kafufua shirika la ndege

Wananunuzi wa Ndege wao wanataka 10% yao kwenye ununuzi na pia kwenye matengenezo service zake, wao wanaangalia matumbo yao kwanza mengineyo ni mbele kwa mbele huko
 
Muhimbili bado kuna msongamano mkubwa hata zile word zingine waganjwa wanalala chini
Sasa huyo jamaa aliyekuwa anapinga yeye anaishi wapi katika nchi hii ambapo vitanda hospitalini vinawatosha wagonjwa wote ?, kama dar ni hivyo ujue huku mikoani hali na mbaya zaidi, hata wakilala kitandani basi wanalazwa watatu, ni mapopoma pekee ndio wanaweza kushangilia uzwazwa wa serikali hii ya awamu ya tano
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa. Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwahayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!
Sifa kuu ya kuwa rais nchini ni akili kuliko wote?Ingekua hvyo Jiwe angekosa uraisi. Mmekua wajinga mpk mnatia aibu. Nyambafu
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?

Rudi shule ukajifunze kufanya utetezi. Ndege za ATCL zinatoa huduma? Fast jet ilikuwa ndege za wafanyabishara lakini walikuwa wanacharge nauli ndogo kuliko hao ATCL. Au hujui maana ya huduma?
 
Vitendo vipi wanajibu? Mwaka wa nne watumishi wa umma hawana nyongeza za mishahara na Deni la Taifa limezidi kuwa kubwa zaidi, kwani ndege lazima zingenunuliwa kwa cash? na kwa nini hawakukopa kisha hizo pesa zitumike kujenga miundo Mbinu kufufua viwanda mlivyogeuza magodauni huku kilimo kwanza kikiwa kimetelekezwa kabsa
Kutokuwepo kwa nyongeza ya mishahara au deni kuongezeka sio kigezo cha chochote kutofanyika.

Mkuu tunapanua bandari, tunatengeneza meli kwenye maziwa yetu makuu, tunajenga zahanati, yapo mengi yanafanyika.

Huwezi kupata vyote kwa wakati mmoja, chagua kipi kifanyike kwa gharama ya mengineyo kusubiri. Ukitazama maslahi ya wachache utakuwa na uchumi mzuri kwa maana ya vitu hivyo vichach kuonekana lakini ni kwa hasara ya mengine kutooneka..

Unayo shilingi elfu kumi mfukoni sasa chagua moja uinywe yote usiku au unywe chupa moja ya 1500 ili kesho uamke na 8500 mfukoni, hiyo ndio dhana ya opportunity cost.
 
Kuwa na ndege za serikali kuna manufaa mengi sana achilia mbali faida halisi itakayokuwa inatengenezwa na uendeshaji wa shirika hilo. Baadhi ya manufaa ya kufufua shirika la ndege ni:
a. Ajira ndege moja mfano hii Dreamliner inaporuka huwa ina wafanyakazi wasiopungua 12 yaani wakiwemo mapilot wawili, flight engr mmoja, flight technician mmoja, cabin crews ( air hostess) wasiopungua 8. Hapo awali ndege za kampuni binafsi zilikuwa na watumishi hata kutoka nje ya Tanzania. Kwa hiyo hata kama ndege haitakuwa na faida kubwa bado kuna ajira zinatengenezwa kwa watanzania.
b. Kodi, biashara inayofanywa na ATCL hukatwa kodi mfano unaponunua ticket kodi ya kununua ticketi (VAT) hunufaisha faida, lakini zipo kodi nyingi zinatokana usafiri wa anga mfano kodi za PAYEE kwa wafanyakazi. Hapo awali unakuta mfanyakazi wa fast jet tuseme pilot ni raia na mkazi wa Kenya kwa malipo yake hulipwa kupitia bank nchini Kenya kwa hiyo PAYEE italipwa Kenya.
c. Kushusha gharama za usafiri, Tangu ATCL imefufuliwa gharama za usafiri wa anga hapa nchini zimeshuka. Kwa asiye tumia usafiri wa anga anaweza kuona hamna lolote, kabla ya ATCL kufufuliwa usafiri wa anga ulitawaliwa na makampuni binafsi ambapo kuna wakati yalikuwa yakisoma msimu wa abiria wengi na kupandisha bei kuna wakati nauli ya kwenda mwanza tu one way mtu analazimika kulipia zaidi ya 400,000 ambapo kwa sasa kwa ATCL ni chini ya gharama ya kwenda na kurudi Mwanza wakati wote.
d. Ufufuaji wa ATCL umesababisha kuibuka fursa za biashara na ajira. Kulikuwa na viwanja vya ndege vilivyokuwa vimekufa au havipo kabisa. Viwanja hivyo vimepelekea watu kupata ajira za kuhudumia viwanja, mfano huduma za zimamoto, usafi, uhakiki wa mizigo, ulinzi, biashara katika viwanja vya ndege.
e. Zipo faida nyingi sana achilia mbali za kuleta watalii, kuitangaza nchi kimataifa.
 
Nadhani serikali ilifaa isifanye biashara ya ndege bali ingeweka mazingira mazuri kwa sekta binafsi ikakua huku yenyewe ikibaki kama msimamizi. Pesa iliyotumia ni zaidi ya trillion 1 kwenye ununuzi wa ndege ambayo kama ingewekezwa kwenye miondimbinu ya kilimo cha umwagiliaji mambo yangekua super.

Mfano tu serikali ingevuta maji toka ziwa Nyasa mpaka bonde la usangu/madibila,,ziwa rukwa mpaka kamsamba .Haya ni mabonde ya mpunga ambayo shida kubwa ni mvua lakini wangepata maji ya kutosha uzalishaji ungekua mkubwa. Pia kuna mkoa wa morogoro ambako wanalima mpunga mpaka wa kiangazi japo maji mateso, serikali ingechimba mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya umwagiliaji . Sijui kuhusu maeneo mengine amabayo yanaweza kuzalisha japo shida ni maji.
 
Back
Top Bottom