Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Nashangaa sana wazawa kuponda jitihada za serikali ya awamu ya 5 kununua ndege. Mbona awamu ya 1,2 na 3 kama sikosei shirika la ndege lilikuwepo??

Kwa uelewa wangu mdogo wa biashara aiku zote mwanzo huwa mgumu. Ndio maana wanaofanikiwa kwnye biashara ni wale wenye roho ngumu na uthubutu.

Sikutarajia kabisa shirika letu la ndege kufufuliwa bada ya mwaka 1 faida ikaja..

Kuendesha kampuni ya ndege siyo biashara rahisi kama kuuza machungwa.

Mwisho: Taifa lolote linaloendelea ili likue na kujiitangaza lazima liwe na shirika lake la ndege ili kujinadi kibiashara..

Nawaza kwa sauti tu..

Sent using Samsung S6 Edge

Hakuna anayepinga kununua ndege za ATCL, tunachohofia na jinsi huu uwekezaji unavyofanywa. Wakati mashirika ya ndege ya jirani zetu yanapata hasara na mengine hata kuuza ndege zao; Sisi ujasiri wa kuagiza ndege mpya unatokana na upembuzi yakinifu wa sampuli gani?

Biashara ya ndege hivi sasa inahitaji substantial resources as subsidies to keep them afloat, je on top of buying new planes do you as a country have the muscle to cushion ATCL amidst this economic crunch?
 
Je, zina faida gani economically?

Hizi hela ni zaidi ya mtaji wa viwanda vya Bakhresa. Angalia impact ya viwanda vya Bhakresa na ndege za Magufuli in terms of mzunguko wa hela, ajira na services. Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli.

By the way, hata hayo makampuni makubwa yanapata hasara na biashara ya ndege si biashara ya kutegemea kujenga uchumi. Je, Bunge limepitisha manunuzi ya ndege saba?

Hivi unaachaje kuwekeza kwenye kilimo, madini, elimu, gesi,maji, umeme then unaenda kuwekeza kwenye ndege kwa taifa changa kama hili ambalo watoto hawana madawati na hospitali mama wajawazito wanalala chini?

Hapo hatujagusa demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Huu uongozi umechafua sana picha ya taifa hili; this is one of the worst leaderships. By the way, kila chenye mwanzo kina mwisho, walikuwepo wakina Mobutu, wapo wapi now? Tusibiri muda wake utafika tu.

View attachment 1250571
Bil 10 kwa mwaka kwa mwez karibia milioni 830 je gharama za uendeshaji zikoje 'overhead expenses,wages,training,maintenance just to mention a few'
 
Mkuu Ndinani acha kuwa mwoga, chloroquine inatiba corona, na virusi huyo hana uwezo wa kuishi mahali penye joto lenye kuzidi 25, kuanzia June mpaka August sehemu ya juu ya dunia itakuwa na joto kali, huyu virus atapotea jumla. Anatamba muda huu kwa sababu sehemu nyingi za dunia joto lipo chini.

Kuwekeza kwenye ndege ni kuwekeza kwenye utalii, na pesa ya utalii ndio hiyo inayojenga zahanati, vituo vya afya na kusomesha wanafunzi kuanzia la kwanza mpaka kidato cha sita.Ondoa wasiwasi hakuna suala la laana kwani uwekezaji kwenye ndege unayo tija kwa maisha ya watu wa kila rika.

Watu kama wewe ndio maadui wakibwa wa vita hii dhidi ya covid-19, kwasababu mnataka kuwaaminisha wananchi kuwa ugonjwa huu una tiba ilihali wataalam wanasema hauna tiba mpaka hivi sasa!! Wananchi wakiwaamini nyie mavuvuzela ugonjwa utasambaa kwa kasi kubwa na nchi kuangamia!! Kumbuka nchi hii ni maskini sana haina uwezo wa kukabiliana na hili janga linalowasumbua hata nchi tajiri.
Acheni siasa kwenye mambo hatarishi kwa uhai wa nchi.
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa.

Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwa hayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!
Dah!! Sikuhizi ili uonekane unajua kitu flani au una point ya muhimu, ni lazima kwanza umtoe akili mwenzio, tujifunze tu kutoa hoja, bila ya kuweka maneno ya maudhi..
 
Watu kama wewe ndio maadui wakibwa wa vita hii dhidi ya covid-19, kwasababu mnataka kuwaaminisha wananchi kuwa ugonjwa huu una tiba ilihali wataalam wanasema hauna tiba mpaka hivi sasa!! Wananchi wakiwaamini nyie mavuvuzela ugonjwa utasambaa kwa kasi kubwa na nchi kuangamia!! Kumbuka nchi hii ni maskini sana haina uwezo wa kukabiliana na hili janga linalowasumbua hata nchi tajiri.
Acheni siasa kwenye mambo hatarishi kwa uhai wa nchi.
Covid-19 ni tatizo la muda tu, tatizo la kupita. Juzi Trump kasema Chloroquine inatibu huu ugonjwa, na cha muhimu ni kuzingatia kunawa mikono kikamilifu na kuepuka usafiri wenye watu wengi kama vile mwendokasi.
 
wewe unamuamini Trump ambaye hata wataalam wake hawamuamini? Chroquine ingekuwa dawa kwanini WACHINA wasiitumie kuponya watu wao? Tumia akili kidogo!
Trump anafahamika kwa kutokuwa mkweli(spin doctor) hiyo dawa alioisema haitibu bali inapumguza makali ya covid-19!!
 
Mkuu kumbuka kuwa Chloroquine ilikuwa imesahauliwa, ilitumika miaka ile ya 1970-2000 halafu yakagunduliwa madawa mengine, hivyo wameijaribu na kuona inafaa.

Unaleta siasa za Trump kutoaminiwa na wataalam wake, yule ni rais wa dunia sio sawa na katibu tarafa ya sehemu unayoishi.
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa.

Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwa hayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!
we ndo pumbavuuu kabisa. wangapi wanatumia ndege? wangapi wanatumia bara bara? linganisha mzunguko wa hela unaoletwa na mabasi ya abiria + malori na mzunguko wa hela unaoletwa na hizo ndege

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hatimaye ndege zimeipa hasara serikali na dikteta uchwara naye hayupo
Jamaa aliishi maisha ya kutamani vitu vya utotoni bila kuangalia uhalisia wa mambo. Angeweza kununua ndege nne tu tatizo alikuwa extremist mno halafu very toxic hataki ushauri hata kidogo na wajinga wakamtia kichwa sasa wanamgeuka.
 
alikuwa hajui ethics za uongozi
 
Wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Sidhani kama unajua ulichoandika! Jitahidi kushirikisha 'vidole na akili' wakati wa kuandika.
 
Sidhani kama unajua ulichoandika! Jitahidi kushirikisha 'vidole na akili' wakati wa kuandika.
Alichoandika kina ukweli. Impact ya wanaotumia usafiri huo kwa ajili ya kuboresha shughuli zao kiuchumi kwao na nchi ipo kubwa tu. Bahati mbaya hilo hatuna jinsi ya kulipima moja moja kama tunavyoweza kupima hasara ya kampuni.
 
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
Awamu ya 6 imefika,ni muda muafaka Dotto kuenguliwa kupisha uchunguzi
 
hatimaye ndege zimeipa hasara serikali na dikteta uchwara naye hayupo
Kazi ipo
Screenshot_20210328-162203.jpg
Screenshot_20210328-145853.jpg
 
Watu hawapingi ufufuaji wa ATCL bali modus operandi. Yaani kwenye Ilani ya CCM na CDM wote walisema watafufua lakini siyo kwa namna anayofanya Meko. Yeye Meko anakaa na mpwa wake Dotto James Katibu Mkuu Hazina wanaamua kununua ndege na kulipa. Hawana business plan, hawana procurement plan wala hawatangazi zabuni.

Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2015 na Kanuni zake na Sheria ya Fedha zimevunjwa zote kwa 100% na CAG haruhusiwi kukagua shughuli za ATCL kwa vile zimehamushiwa kasma #20 ya Ikulu kutoka kasma ya Mawasiliano na Uchukuzi.

Hapo kinachoendelea ni ufisadi na rushwa tu kwenye manunuzi. Tusubiri awamu ya 6, tutakuja kufufua uzi huu na sintoshangaa kumuona Dotto James akipelekwa Segerea.
Anyway CAG kasema kuna loss ya Tsh 60 Bilion kwa mwaka 2019/20
 
Back
Top Bottom