Ukweli kuhusu ndege za Serikali

Pablo Blanco

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
7,328
6,589
Je, zina faida gani economically?

Hizi hela ni zaidi ya mtaji wa viwanda vya Bakhresa. Angalia impact ya viwanda vya Bhakresa na ndege za Magufuli in terms of mzunguko wa hela, ajira na services. Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli.

By the way, hata hayo makampuni makubwa yanapata hasara na biashara ya ndege si biashara ya kutegemea kujenga uchumi. Je, Bunge limepitisha manunuzi ya ndege saba?

Hivi unaachaje kuwekeza kwenye kilimo, madini, elimu, gesi,maji, umeme then unaenda kuwekeza kwenye ndege kwa taifa changa kama hili ambalo watoto hawana madawati na hospitali mama wajawazito wanalala chini?

Hapo hatujagusa demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Huu uongozi umechafua sana picha ya taifa hili; this is one of the worst leaderships. By the way, kila chenye mwanzo kina mwisho, walikuwepo wakina Mobutu, wapo wapi now? Tusibiri muda wake utafika tu.

Screenshot_20191101-095822~2.jpeg
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Mkuu, usilidhalilishe shirika letu la ndege. Nalo liko kibiashara, si kihuduma. Unapochangia mada kama hizi, jiulize mara mbilimbili kabla ya kuandika. Kwahiyo, kwako wewe, ndege za ATCL zinatoa huduma kama ilivyo kwa shule, zahanati na mabomba? Bure kabisa wewe!
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Ndege zinatoa huduma kwa watanzania wa kati na chini? Achilia mbali nauli za ndege, Watanzania wengi hawajawahi kupanda ndege na wengi tu watafariki bila kupanda ndege.
 
wapinzani mnapokosa mambo ya msingi ya kujadili mnakuwa vituko sana. kwa hiyo unalinganisha makampuni ya Bakhresa ambayo yanatafuta faida kubwa na taasisi za serikali ambazo ni kwa ajili ya kutoa huduma?
Hizo ndizo tope zenyewe, biashara ya Ndege sio kuleta blah blah na kujifanya unatoa huduma, gharama za kuendesha hizo ndege ni kubwa kiasi kwamba muda sio mrefu mtatamani kuziuza na msipate wa kuzinunua, na bahati mbaya mnaharibu mahusiano na jamii ya kimataifa kila siku, na biashara inahitaji watu, ipo siku mtaanza kuzibebea mashudu, endeleeni na uzwazwa.
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa.

Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwa hayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!
 
Hizo ndizo tope zenyewe, biashara ya Ndege sio kuleta blah blah na kujifanya unatoa huduma, gharama za kuendesha hizo ndege ni kubwa kiasi kwamba muda sio mrefu mtatamani kuziuza na msipate wa kuzinunua, na bahati mbaya mnaharibu mahusiano na jamii ya kimataifa kila siku, na biashara inahitaji watu, ipo siku mtaanza kuzibebea mashudu, endeleeni na uzwazwa.
walikuwa wanabebea nyama ya mbuzi,na hii ndo shida ya nchi kuongozwa na washamba,raisi msukuma makamu wa rais msukuma,matokeo yake ndo haya
 
Kwa upeo wako wa mtindio wa ubongo unajiona unaakili saana kuliko rais wa nchi? Usafiri ni usafiri tu kwa nchi kubwa kama Tanzania lazima tuwe na usafiri wa anga kwa kukidhi angalau soko la ndani tu inatosha hata tusipofanya international flight. Kwa akili zako za kipimbi tutegemee barabara tu kusafiri? Usafiri wa anga lazima ukidhi vigezo vya kimataifa kwahiyo ubora na hadhi ya ndege zetu ni sawasawa na ubora na hadhi za ndege zoote za kimataifa. Hatukununua ndege kwa kuangalia faida ya moja kwa moja bali kuboresha mazingira rafiki ya uwekezaji, utalii n.k. Ulishawahi kujiuliza gharama za kujenga mtandao wa barabara za lami nchini gharama yake kiasi gani? Gharama ya kilometa moja ya barabara ni bilioni moja kwa wastani zidisha mara kilometers za Barbara zoote utapata matrilion ya hela mbona hamhoji hizo gharama ambazo in zaidi mara ngapi ya gharama za kununua ndege? Mleta uzi na Tundu Lissu ni vibaraka wa Mabeberu! Kwahayo ndo yanakutosha kulingana na akili zako ndogo maana nikichambua zaidi hutanielewa!
Linganisha idadi ya Watanzania wanaotumia barabara na wanaotumia ndege.
 
Pablo Blanco,

Hivi wanasiasa wetu ni watu wa namna gani?

Kwenye manifest ya CHADEMA kuelekea uchaguzi 2015 walizungumzia azma ya serikali itakayoundwa na CHADEMA kufufua shirika la ATC kwa kununua ndege mpya.

Leo hii wakubwa hao hao wanabeza utekelezaji wa suala hilo hilo na Rais Magufuli halafu ni hao hao pia walipinga sana serikali kuzuia makenikia na wakitahadharisha kuwa TZ inawekushtakiwa na mashirika hayo ya kimataifa na mwishowe itabidi mlipa kodi ndiyo abebe mzigo huo. Leo matokeo yake wote tumeyaona. Sasa tumuamini nani? Wale ambao kila kitu wanaponda au wale ambao hutekeleza kwa vitendo?

Nadhani ifike wakati wanasiasa watafakari hayo wanayotuambia kwani inafika wakati wanajidhalilisha ni bora watafute mada nyingine za kutudanganya.
 
Pablo Blanco,

Ununuzi wa ndege ni dili la wajanja wachache kuna 10% zao humu ndiyo maana hununua kwa cash ili wachukue chao mapema na hawataki CAG kunusa hesabu za ununuzi wa ndege kwa hofu ya kuibua ufisadi wao, siyo kwamba hawajui kuwa Ndege hazina faida kwa nchi bali wameangalia matumbo yao na dhana ya CCM isemayo chukua chako mapema.

Awamu hii ni tofauti na awamu ya Kikwete na mkapa ambao walipiga dili zao jioni mwishoni mwa utawala wao, hawa wa sasa wao wanakula mapema chao kisha huko mbeleni ni majaliwa ya mwenyezi mungu, hakuna sehemu bunge linashirikishwa juu ya ununuzi wa ndege hata ujenzi wa Chato Airport umefanywa kienyeji pasipo idhini ya bunge.
 
Je, zina faida gani economically?

Hizi hela ni zaidi ya mtaji wa viwanda vya Bakhresa. Angalia impact ya viwanda vya Bhakresa na ndege za Magufuli in terms of mzunguko wa hela, ajira na services. Watalii hawawezi wakaacha kupanda ndege za makampuni makubwa yenye muda mrefu kwenye biashara pamoja na usalama wa uhakika waje wapande ndege za Magufuli. By the way, hata hayo makampuni makubwa yanapata hasara na biashara ya ndege si biashara ya kutegemea kujenga uchumi. Je, Bunge limepitisha manunuzi ya ndege saba?

Hivi unaachaje kuwekeza kwenye kilimo, madini, elimu, gesi,maji, umeme then unaenda kuwekeza kwenye ndege kwa taifa changa kama hili ambalo watoto hawana madawati na hospitali mama wajawazito wanalala chini?

Hapo hatujagusa demokrasia na ukiukwaji wa haki za binadamu. Huu uongozi umechafua sana picha ya taifa hili; this is one of the worst leaderships. By the way, kila chenye mwanzo kina mwisho, walikuwepo wakina Mobutu, wapo wapi now? Tusibiri muda wake utafika tu.

View attachment 1250571

hapo meshadanganywa na huyu anayekula raha ughaibuni mmekurupuka kutuletea uozo ni lini mtabadilika acheni siasa za maji taka wandugu
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom