Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,468
Hivi kaka huko ghorofani kuko sawa?Kikwete licha ya hayo mapungufu yake kila mwaka aliwaongezea nyongeza ya mishahara watumishi wa umma, na Deni la Taifa halikuwa kubwa kama sasa ambapo wanajinadi kudhibiti wizi safari za nje lakini Deni la Taifa limepaa kuwa maradufu huku watumishi wa umma wakibuni Mbinu za kisayansi kufanya ufisadi pasipo kugundulika kirahisi kwa haraka, Ndege wanunue kwa mikopo lakini vitu vinginevyo vya maendeleo vifanyike kwa kasi ikiwemo kujenga miundominu bora zaidi isiyo haribiwa na mvua kirahisi
Kwa akili ya kawaida tu huoni kuwa kuna miradi mingi tena ya maana imeibuliwa na awamu hii kuliko hiyo awamu unayoisema? Hivi ulikuwa unatarajia deni la taifa lishuke? Ingawa deni letu limeongezeka lakini linalipika kwani hivi sasa jirani zetu wamefikia mahala wanashauriwa wasikope tena. Lakini kwetu pesa zetu zinatumika kwenye miradi ambayo inatarajiwa kulipa maradufu.