Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

Ukweli kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi

Kwa maana hiyo Tanzania inakiri kuwa hatuna sehemu kwenye ziwa nyasa OR sorry wenye ziwa lao wanaliita ziwa Malawi.

Wenye kujua historia, neno Ziwa Nyasa tulilitoa wapi? Au tulibatiza mali za watu?

Kama mtu mmoja alivyoshauri, tubadili contents kwenye jiografia ili ieleweke Ziwa Nyasa haliexist!

Mwanzoni hilo ziwa lilikuwa linaitwa lake Nyasa ikiwa ni kutokana na Nyasaland ambayo ndio malawi ya sasa. walipobadili jina na kuwa Malawi wakataka kubadili na ziwa kuwa Lake Malawi
lakini kwa Tanzania tumeendelea na jina lile la mwanzo.

Nafikiri ni sawa na lake Tanganyika, lingebadilishwa kuwa Lake Tanzania.

Olgah alivyosema ni sawa, kuna mazungumzo yanaendelea, ila nijuavyo mimi yameanza siku nying mno, maana toka mdogo nasikia wanaongea, sijui watamaliza lini?
 
Ahsanteni sana walioweza kuibua suala hili bungeni, ni juzi tu katika ile hoja ya Tunapata faida gani niligusia na hili salamu zipelekwe bungeni, naona zimefika.

Sasa nasema kama Mtanganyika, tunataka kuona mpaka unapakwa rangi ya manjano na unakatiza katikati ya ziwa kama ilivyo kwa upande wa msumbiji, hivi vikao hapa si sehemu yake ni kuamuliwa tu na ndivyo ilivyo la si hivyo tutangaze vita vya maji, maana Misri wako tayari kupigana kama maji ya Ziwa Viktoria yatazuiliwa kutiririka kwenye mto Nile, huko kwao wakihisi yanapungua tu wanaulizia kuna nini tunawajibu safari hii mvua sio nyingi.

Sasa hapa kwenye Ziwa Nyasa kuna uhai na mauti kwa Watanganyika wa mikoa inayopakana na ziwa hili, kama Banda alitangaza vita wakati huo sasa ni wakati wa Tanzania kuelekeza mizinga Malawi, maana wazungu wakikosea tu na kusema kuna mafuta na Uranium katika ziwa Nyasa basi Malawi hatowachia uzi tena atadai na ukingo wa ziwa uliopakana na Tanganyika pia ni wa kwake ni bora kukinga kuliko kutibu.
 
Hivi admin,uliongea nini vile kuhususu kutumia alama au picha za Viongozi wa taifa kama logo?
 
Wadau mi huwa naona kuna mkanganyiko wa kuitwa/kutambuliwa kwa jina la Ziwa letu maarufu Nyasa,vyombo vingine(hata ramani) huonyesha Ziwa Malawi. So kipi ni kipi?
 
kuna ramani zinazoonesha ni ziwa nyasa na zingine zaandika ziwa malawi.
Ramani zilizochapwa malawa zinaandika ziwa malawi.
zilizochapwa Tz zaandika nyasa.
 
Mara Nyingi haya maziwa yaliyopewa majina ya nchi ni kiashirio cha kuwa Upande mkubwa wa ziwa upo katika nchi hiyo.

Hilo ziwa Lilikuwa linaitwa Ziwa Nyasa wakati Malawi ikiitwa NyasaLand, Malawi walipopata uhuru na kuiita nchi yao Malawi basi walikuwa kwenye mchakato wa kulibadilisha hilo ziwa kuwa Ziwa Malawi, kwa hiyo kimataifa (Official) hilo ni ziwa Malawi japo ni ngumu sana kwa jamii yote ikubali kwa muda mfupi jina jipya kwakitu kikubwa kama hicho.

Hata Tanzania tulikuwa na Nafasi hiyo ya Kulibadilisha Ziwa Tanganyika na kuwa Ziwa Tanzania lakini ni vitu ambavyo vinasumbua sana

kwa hiyo ya MAlawi sio mara ya Kwanza, maana hata Ziwa Victoria ilikuwa ikiitwa Lake Nyanza
 
Majina yote ni sahihi iwe malawi au nyasa yote yanamanisha kitu kilekile nyasa ni malawi (nyasaland) kwahiyo haijalishi umeita jina gani maana inabaki ileile!.
 
Ndugu zetu wa kyela tunawapenda sana lakini msipokaa sawa mtachukuliwa na wamalawi kwakuwa watasema bonde la nyasa ni lao nanyi mnaishi katika bonde la ziwa malawi (malavi).
 
Mwaka jana kuna chi 2 za Amerika Kusini; Nicaragua/Honduras, nusura waingie vitani baada ya mojawapo kufuata ramani ya Google na kutangaza kuwa ndio mpaka wao rasmi.

Hawa jamaa wa Google, msitari wa mpaka wamechora na rangi nyekundu kisha wanaonyesha LAke Nyasa yote imebaki Malawi, hii imekaaje? Nadhani hili la ugomvi wa mpaka halina itikadi, nakumbuka miaka ya nyuma enzi za Hayati Mwalimu nusura tuzipige na Malawi wakati wa Dr. Banda kwa ajili ya mpaka huu.

attachment.php
 
Je, Mh. Membe aliliongelea hili kwenye mawasilisho yake Bungeni? au kama liliwahi kusemewa wadau tuleteeni hapa maelezo ya serikali yenu na hatua gani zimechukuliwa kurekebisha mpaka.
 
Nitashangaa kama Jenerali Shimbo na JWTZ yake watakuwa hawalijui hili na kama wanalijua ni hatua gani wamechukua so far. Hii ndio kazi yao ya msingi waliyoajiriwa na watanzania kuifanya na si kuingilia siasa za ndani au kutisha wananchi.
 
Je, Mh. Membe aliliongelea hili kwenye mawasilisho yake Bungeni? au kama liliwahi kusemewa wadau tuleteeni hapa maelezo ya serikali yenu na hatua gani zimechukuliwa kurekebisha mpaka.
Jana Membe amedai eti kuna kamati imeteuliwa kuhusu suala hilo! Pinda pia aliwahi kudai eti kuna timu ya wataalamu imepelekwa kukutana na wenzao wa Malawi! Hata hivyo niliwahi kusoma kitabu kimoja kilichoandikwa "Boundaries of East Africa" mwandishi aliandika ku-suggest kwamba kisheria Tanzania haina hata tone la la maji Ziwa Nyasa (wamalawi huliita Lake Malawi)! Wamalawi wamekuwa wajanja sana kusambaza Ramani hapa nchini zinazoonesha upuuzi kama huo! Mimi nionavyo, hakuna haja ya kujadiliana na wamalawi, ni vema tukakaa kwenye "state of conflict" tukawa na sehemu ya Ziwa kuliko tukaingia kwenye mjadala na kulikosa kabisa lile Ziwa!
 
Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani.

Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..
 
Hao google wana yao uku mambo shwari wamalawi wanakwao nasi kwetu.Uku ritui,mbambabay,manda na itungi operation zaendelea hawa jamaa hatuna kwele nao kabisa.
Kwanza karonga yote wanaoishi apo ni watz so suala la mpka kwao sio issue kabsaaa
 
Jana Membe amedai eti kuna kamati imeteuliwa kuhusu suala hilo! Pinda pia aliwahi kudai eti kuna timu ya wataalamu imepelekwa kukutana na wenzao wa Malawi! Hata hivyo niliwahi kusoma kitabu kimoja kilichoandikwa "Boundaries of East Africa" mwandishi aliandika ku-suggest kwamba kisheria Tanzania haina hata tone la la maji Ziwa Nyasa (wamalawi huliita Lake Malawi)! Wamalawi wamekuwa wajanja sana kusambaza Ramani hapa nchini zinazoonesha upuuzi kama huo! Mimi nionavyo, hakuna haja ya kujadiliana na wamalawi, ni vema tukakaa kwenye "state of conflict" tukawa na sehemu ya Ziwa kuliko tukaingia kwenye mjadala na kulikosa kabisa lile Ziwa!

Labda wanalindwa na hawa hapa:

Ruhanjo , Ex-TISS Bosi Mr. EM, Waziri Mkulo ............!
 
Back
Top Bottom