LordJustice1
JF-Expert Member
- Jan 19, 2011
- 2,263
- 530
Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!Hivi kuna faida gani kuingia vitani kugombania mipaka ilhali kwa kiasi kikubwa wakazi wa maeneo husika wanaingiliana kwenye shughuli zao za kila siku? Mmalawi akitaka mafuta ya taa anakuja Tanzania kuchukua, hivyo hivyo kwa mtanzania anayeishi mpakani. Hebu tujifunze kutumia Diplomasia jamani. Nguvu zenyewe za kupigana hatuna, mpaka leo tumeshindwa kupigana na maradhi, na umasikini. Adui ujinga ndiyo anatupiga kila kukicha, hadi Rais wa nchi naye ujinga umemshinda nguvu na sasa ndiyo unaomuongoza kwenye kila analofanya na kusema..