Feedback
JF-Expert Member
- Mar 14, 2011
- 7,988
- 4,507
Mimi nimemshangaa sana TANMO eti anasema haina haja kugombea mipaka kwa vile tuna mambo mengi ya kushughulikia, tukiwa na viongozi watano tu wenye kichwa kama chake nafikiri Mwanza, Shinyanga Kagera zote zingekuwa sehemu ya Uganda, Kilimanjaro, Arusha, Mara zingekuwa za Kenya, Kigoma na Rukwa zingekuwa za Burundi, Mbeya yote wangekuwa wamewapa Malawi kwa huruma yao, Dar, Pwani, Mtwara na Tanga zingekuwa za Zanzibar. Labda Dodoma na Tabora tu ndizo zingebaki.Wewe kichwa chako kibovu sana! Tukiwa wajinga wataendelea kumega mipaka kama akina Iddi Amini alivyodai kwamba Kagera Salient iko Uganda! Sasa hivi nako Warundi wameumega mpaka wetu! Kamuzu Banda naye aliwahi kudai kuwa Wilaya yote ya Kyela iko Malawi! Kwa hiyo wewe kwa akili yako finyu tukae kimya tu ili "kuogopa malumbano na vita?" Open your mind please!