Kuna asilimia kubwa kabisa inayonifanya nihisi kwamba kuna watu wametengeneza hiki kipande cha sinema kuchochea udini, katika kipindi cha Uchaguzi suala la udini lilitawala sana, japokuwa Uchaguzi umeisha lakini bado linaota mapembe, hivi karibuni tulisikia waislamu kubomoa bucha za Kitimoto Morogoro, baada ya hapo Mchungaji alipoteza maisha kwa sababu ya mabishano baina ya dini, Leo tena mnatutengenezea Video kama hii, hamuoni kama ndio mnazidi kuuwasha moto, kuna watu wengine hawana uelewa wa teknolojia, akiangalia tu basi anajua ni kweli yametendeka.
Wewe Majimshindo Mwanzo kabisa ulianza kwa kumtaka Nyerere kuhusika na mauaji ya waZanzibar lakini Conclusion yako ni tofauti kabisa na ni ya kichochezi maradufu, hili suala la kusema Waislamu wanatengwa Kielimu si kweli. Waislamu wanapata elimu kama raia wengine, kuna Shule nyingi tu za Kiislamu zinazotoa elimu kwa waislamu. Ukitazama leo hii kwenye serikali ya kikwete kuna Wasomi wengi sana wa Kiislamu wenye nyadhifa za juu kabisa. niambie, Elimu hii waliipata Wapi na Lini? usiwe mbayuwayu jaribu kuangalia hali halisi sababu hili suala linatumika kisiasa zaidi, tunaumia sisi lakini manufaa wanapata Wanasiasa, siwezi kujua, pengine labda na wewe Unanufaika na mpango huu. tuambie!!