Ukweli kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar - 1964

Mkuu nami nimefuatilia hizi habari na hasa maandiko ya mihangwa tangia zamani. Naona anayoyaandika kwenye Raia mwema ni marudio ya makala alizoziandika kwenye gazeti la Rai hapo zamani. Ni kweli pia kwamba Mihangwa na Ahmed Rajab wametofautiana kuhusu historia hiyo. Kuna siku nilisoma habari za Ahmed nikaona inayofautiana na yaliyoandikwa na Mihangwa ikabidi nimuandikie Mihangwa kumuuliza lakini bahati mbaya hakunijibu. Ila kwa jinsi nilivyofuatilia hizi makala kwangu mimi naona kama Mihangwa ana ukweli mwingi kuliko Ahmed. Naona Ahmed kama anaegemea zaidi kwenye HIZBU ila Mihangwa yupo zaidi upande wa ASP na UMMA party. Pia Mihangwa anaonekana kumkubali Okelo kama kiongozi wa mapinduzi. Ukweli huu unachagizwa zaidi na ile picha ambayo Okelo anaonekana akiwa na wanamapinduzi wengine wakiwa wamemzunguka naye akiwa ameketi kama kiongozi.
 
Mkuu Kimbunga,

Nakubaliana na mtazamo wako kwamba Mihangwa anaweza kuwa na ukweli mwingi. Nilisoma simulizi ya Ahmed Rajab nikakuta ina matobo mengi sana (dots nyingi sana hazijaungana). Mihangwa ametumia reference za vitabu vya simulizi za akina Sheikh Thabit Kombo ili ku-justify simulizi zake, Bwana Ahmed Rajab naona anatupa stori tu ambazo hazina support yoyote.

Nikisoma simulizi ya Ahmed Rajab, ninakuta kuna mapengo mengi na pia kuna maswali mengi. Kama Okello alikuwa "insignificant" kwenye hayo mapinduzi, ilikuwaje akaenda Dar kukutana na Mwalimu? Alipokelewa na Mwalimu akiwa kama nani? Kwamba eti aliyetakiwa kutangaza aligoma/ogopa, then ndipo Okello akaamua kwenda kutangaza kwa kuwa alikuwa na sauti ya kutisha na lafudhi ya ajabu ajabu ndio aachwe na kupewa heshima ya kwenda kukutana na Mwalimu, akiwa kama nani? Mwisho kabisa, kama Okello alikuwa insignificant, kwanini serikali iingie gharama ya kumpeleka Kenya peke yake kwenye ndege kubwa? Ni kipi ambacho serikali ya Marehemu Mzee Karume ilikuwa inakiogopa?

Nikijiuliza hayo maswali, ninafika mahali ninahisi kwamba Okello aliongoza mapinduzi na Mzee Karume kwa kuhofia kupinduliwa aliamua kumuondoa haraka sana ili asije akaleta balaa. Kama angekuwa "insignificant" wala serikali isingeingia gharama/usumbufu wa kumpeleka Kenya na pia asingeenda kukutana na Mwalimu Nyerere.

Few days ago kwenye uzi fulani nilisema kwamba Tanzania tumekuwa na utaratibu wa kuficha ukweli, na hiyo inaanzia kwa waandishi na mpaka kwa watawala. Watawala wetu wanataka waandikwe kwa mazuri tu, wakati kuna mabaya/mapungufu mengi ambayo yanafichwa na hivyo kupotosha historia na ukweli au kuishia kuleta mikanganyiko kama hii na kuwaacha wasomaji wakijiuliza je ni simulizi la nani ambalo lina-make sense?
 
Hapo kwenye red; yale yale ya Mohamed Said na wazee wa Kariakoo. Hii ni syndicate fulani inafanya kazi maalumu kwa malengo maalumu. Silaha kubwa ya kuanzia ni uongo, upotoshaji, na kueneza uvumi badala ya kusimamia ukweli kama ulivyo. Wanataka kuandika historia wanayoijua wao kwa sababu wanazozijua wao. Yetu macho.
 
naiunga mkono simulizi ya Mihangwa kwa kuwa ina supporting evidence. Pia zamani kidogo nilisoma kitabu Field Marshal John Okello ambacho kimezungumzia namna alivyoongoza mapinduzi, alivyokutana na Mwalimu na alivyotokomezwa. Pia nimesoma kitabu cha Masimulizi ya Thabit Kombo Jecha ambacho nacho kimempa credit Okello. Kwa mantiki hiyo, naiunga mkono simulizi ya Mihangwa. Huyo mwingine mpotoshaji tu!
 
Mkuu ni taswhishi ya kukipata kitabu cha Okello. Naweza kukipata wapi mkuu?

Makala za Mihangwa ziko kiukweli zaidi na ukitaka kuijua historia ya Zanzibar na mapinduzi yake hadi muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika basi soma makala za Mihangwa.
 
Mihangwa aunganishe makala zake atengeneze kitabu. Si rahisi kukusanya makala zake zilizosambaa katika magazeti mbali mbali na kwa matoleo tofauti tofauti tena kwa muda mrefu.
 
Mkuu hiyo ni kweli. Ushauri mzuri sana huo. Kuna jamaa mmoja alikuwa akiitwa Lt. Maganga ambaye alishiriki kwenye jaribio la mapinduzi miaka ya 1980. Jamaa alikuwa akiandika simulizi za mpango wa mapinduzi hayo kwenye gazeti la Rai nikakutana naye nikamshauri atunge kitabu tukakubaliana lakini masikini bahati mbaya alikufa kabla hajautekeleza huo mradi.
 
Alichofanya Ahmed Rajab ni upotoshaji wa makusudi wa historia. Alaumiwe mhariri wa Raia Mwema. Alichofanya Joseph Mihangwa ni kuiweka sawa historia hiyo kwa kuandika kitaalamu na ki maadili ya fani. Ashukuriwe Mihangwa. Ni miaka 48 tu imepita tangu mapinduzi hayo, hivyo wazee wengi waliopo leo wanaijua historia hiyo kwa kina maana walikuwepo na wengine walishiriki. Jambo lililowazi ni kuwa Okello alisisitiza Ukristo wakati Zanzibar ilikuwa nchi ya kiislamu, ukichanganya na ushawishi wake kwa vijana unapata jibu la yeye na historia yake kufukuzwa Zanzibar.
 
Mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni Genocide hiyo inajulikana,lakini sioni sababu ya kurejesha mambo yaliyopitwa na wakati, hizo video sio za leo wala jana zimezagaa Europe,lazima tujiulize kuonyesha video hizo zitaisaidia chochote jamii ya wazanzibar ambao wengi wetu hayo mapinduzi tunayasikia tu,tafakari
 
mapinduzi ya zanzibar yalikuwa ni genocide hiyo inajulikana,lakini sioni sababu ya kurejesha mambo yaliyopitwa na wakati, hizo video sio za leo wala jana zimezagaa europe,lazima tujiulize kuonyesha video hizo zitaisaidia chochote jamii ya wazanzibar ambao wengi wetu hayo mapinduzi tunayasikia tu,tafakari

mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi

kwa waliouliwa wazee wao na kwa wanaowaona wazee wao wamepoteza akili kwa kuuliwa waume zao kwa mapinduzi kwa sababu tu ya rangi yao na kwa walioingiliwa dada zao na kwa waliozaliwa kwa wazee wa ubakaji na kwa mateso yaliyotangulia mpaka siku za uchaguzi za hivi karibuni , mapinduzi yanabaki ni jinamizi kubwa lisilosahaulika
 
Mzee
Hii link yako inasema CCM siyo Chama Cha Mapinduzi bali ni ''Christian Church Movement'':

Quote :''This is a clear testimony that the union of Zanzibar and Tanganyika was the creation of Karume, a racist dictator nominal Muslim from Nyasaland (Malawi) and Nyerere, an autocratic devout Christian from Tanganyika. And consequently, Zanzibar has lost her strong Islamicity and sovereignty to Tanganyika since April 26, 1964 when the dictator Karume, signed the Articles of the Union, drafted by British expatriates, Attorney General Roland Brown and Chief Parliamentary Draftsman, P.R.N. Fifoot, to form Tanzania under the clique of the Christian Church Movement (CCM) of Tanganyika''.

Hivi wakereketwa wa CCM mnaikubali hii ? au ni Freemasons na Da Vinci Code?

Ndo naiona leo
 
..tatizo la Zenj linatokana na Sultani wa Kiarabu aliyetawala hapo kujihusisha na biashara ya utumwa.

..upumbavu mwingine waliofanya kuacha makazi yao Uarabuni na kuhamia moja kwa moja hapo Zanzibar.

..Waingereza na Wafaransa hawakuhamia moja kwa moja kwenye makoloni na kuzikana nchi zao za asili. hiyo iliwawezesha kujiondoa na kurudi makwao, na kuepusha shari na mauaji pale wenye nchi yao walipoanza kudai uhuru.

..Waarabu na mzao wao wamewakandamiza Waafrika hapo Zenj miaka na miaka na sijui walikuwa wanategemea mwisho wake utakuwa kitu gani.

..binafsi nasikitishwa na kilichotokea wakati wa Mapinduzi, lakini kwa upande mwingine sishangazwi.

Ukitaka kuelewa vizuri mambo haya, tafadhali anzeni na tangazo la mwingereza kukabidhi madaraka, yaani uhuru wa Zanzibar na hapo tutapata uhalisia maana kama wenyewe walifanya mambo haya na helkopeter ikiwa juu inapiga picha za wanaokufa kwa nini walifanya hivyo???? Kuna jambo la kujiuliza hapa tusikurupukie video tu toka arabuni.
 
mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi

kwa waliouliwa wazee wao na kwa wanaowaona wazee wao wamepoteza akili kwa kuuliwa waume zao kwa mapinduzi kwa sababu tu ya rangi yao na kwa walioingiliwa dada zao na kwa waliozaliwa kwa wazee wa ubakaji na kwa mateso yaliyotangulia mpaka siku za uchaguzi za hivi karibuni , mapinduzi yanabaki ni jinamizi kubwa lisilosahaulika
Let's be fair na tuseme bila kigugumizi, kwa mkakati wa mkoloni hawa jamaa 'waarabu au washirazi na wafrika' walikuwa wanasoma shule za pamoja na walisomeshwa shule za kata yaani za hali ya chini. Lakini kwa nini wauane kwa kiasi hicho kinachosemwa kwenye video hii. Mi nilishaiona video hii ulaya lakini naomba tujihadhari na mbinu chafu za kimagharibi. Huwezi kuwa ulikuwa na helkopta ya kuchukua matukio halafu ukaacha watu wakateketea wakati una silaha. Pili kupiga picha kwa helkopta wakati wa vita isingewezekana hata kama wasingekuwa nayo hapa. Video ni uzushi mtupu wenye lengo la kuchochea uhasama miongoni mwa wazanzibari na watanzania kwa ujumla, tuikatae!
 
kwani walioua na walioendeleza mauwaji baada ya mapinduzi na kwenye chaguzi za hivi karibuni ni nani??

wakoloni wa magharibi au mkoloni wa kiafrika???
 
Kama mpaka sasa hivi waarabu Hapa Zanzibar wanatubagua namna hii, je yasingefanyika mapinduzi maisha ya sisi waZanzibar weusi yangekuwaje?
 
Mzee
Hii link yako inasema CCM siyo Chama Cha Mapinduzi bali ni ''Christian Church Movement'':

Quote :''This is a clear testimony that the union of Zanzibar and Tanganyika was the creation of Karume, a racist dictator nominal Muslim from Nyasaland (Malawi) and Nyerere, an autocratic devout Christian from Tanganyika. And consequently, Zanzibar has lost her strong Islamicity and sovereignty to Tanganyika since April 26, 1964 when the dictator Karume, signed the Articles of the Union, drafted by British expatriates, Attorney General Roland Brown and Chief Parliamentary Draftsman, P.R.N. Fifoot, to form Tanzania under the clique of the Christian Church Movement (CCM) of Tanganyika''.

Hivi wakereketwa wa CCM mnaikubali hii ? au ni Freemasons na Da Vinci Code?

Ahsante bagamoyo , Nikiwa muislam na si mwanachama wa CCM lakini kwa kuisoma tu hiyo Quote uliyo bandika hapa nasita hata ku press hiyo link kwani inaharufu kali ya propaganda za kizushi!
 
Kama mpaka sasa hivi waarabu Hapa Zanzibar wanatubagua namna hii, je yasingefanyika mapinduzi maisha ya sisi waZanzibar weusi yangekuwaje?

Ukitaka kuwajua waarabu na mambo yao angalia picha za watumwa. Yale maminyororo huwa sipendi hata kuyaangalia
 
Marafiki zangu wa karibu sana wapo waraabu na Wazanzibar.. Niliwahi kuwauliza maswali machache tu husiana na video hii ya Mapinduzi ambayo nijuavyo mimi ilitengenezwa kwa minajiri ya sinema lakini wameigeuza kuwa ukweli na matukio halisi. Nawaombeni muitazame tena vizuri na kutafakari ukweli ni upi haswa na nini lengo la hizi filamu..Maswali yangu ni haya:-

1. Ikiwa mapinduzi yale yalifanyika na kundi la wahuni kina Okello inakuwaje ktk video wanaonekana askari Polisi au wanajeshi wenye magari ikiwa jana tu askari hawa walikuwa waajiriwa wa serikali ya sultani?..

2. Tazama vizuri ndege hii (helicopta) kila inapopita inaonyesha watu wakikimbia mashambani (sio Mjini) ambako ndiko yalifanyika Mapinduzi na kufanya mauaji... mara zote mpiga picha kaonyesha askari wakikimbia toka sehemu ya tukio mara baada ya kuua kwa kila kipande (clip) cha video hii ya mauaji, hakuna wakati hata mmoja imeonyesha asklari wakiua ama wako ktk mpango wa kuua isipokuwa huchelewa kama dakika chache tu kwa kila clip.

3. Na ukitazama zaidi hata wale maiti kule ufukwe wa bahari karibu wote wamelala juu ya mawe, ama kwenye muinuko na sio ndani ya maji halafu kwa binadamun waliuawa kinyama namna ile inakuwaje maji yale yasibadilike rangi kuwa nyekundi kwa damu za wale waliouawa?..
4. Inajulikana wazi kwamba Okello aliongoza Mapinduzi na kuwa madarakani kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya Karume na uongozi wake kuchukua, huyu Okello alipata wapi askari wale wenye kuvaa kaptula za khaki.
 
mbona Tanzania inawapenda "genocidaires", hawa mliitikia kuungana nao, FDLR sasa pia mko kitandani nao, nini kibaya na serikali yenu
 
Back
Top Bottom