Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya watanzania walioko ughaibuni

Father x mas uko sahihi mi najua watu waliomaliza darasa la saba toka tz lakin marekan japo wanafanya kazi za kawaida lakin hawakosi million 6 kwa mwezi na wamejenga kwao.

sasa tujiulize hao watu wangekuwa tz hio million 6 wangeipata?


Halafu sasa ughaibuni hakuna kitu utataka kufanya ukashindwa.Unaweza kutoka bongo darasa la saba ila kama una nia ukasoma na degree zako ukapata.Yaani ni ww tu uwe na nia.Bongo mpaka u ufanikiwe jambo utoe rushwa unyanyasike,uzungushwe,ughaibuni sijaona wadada wakitoa rushwa ya ngono ili kufanikisha jambo,bongo huo ushakua utamadun wetu tayar,
 
"ndani ya Bunge la katiba" haturuhusiwi kuingia. Tuliowatuma ni majandaheka, hawajajuwa maana ya "lobbying" ingawa Kikwete alijaribu kuwaelimisha.

Lakini kumbuka, katiba si msahafu, kama si leo kesho, itabadilika tu.

Ikiwa Bibilia wajanja wanaibadilisha na mapunguani wanaikubali, itakuwa katiba?
Hata AYA ZA SHETANI mataahira yanaziamini sana, usishangae kuona yanajilipua! Hicho kipengere kitaingizwa labda baada ya hiki kizazi cha akina Faizafuska kikiwa kimeshapotea!
 
"ndani ya Bunge la katiba" haturuhusiwi kuingia. Tuliowatuma ni majandaheka, hawajajuwa maana ya "lobbying" ingawa Kikwete alijaribu kuwaelimisha.

Lakini kumbuka, katiba si msahafu, kama si leo kesho, itabadilika tu.

Ikiwa Bibilia wajanja wanaibadilisha na mapunguani wanaikubali, itakuwa katiba?

Nikikuuliza tu kusafiri kwako kumekusaidia nini kwakweli huwezi kunijibu. Hivi kwa nini usiende kuishi Uarabuni unang'ang'ania kukaa nchi ya Makafir?

Hapa hoja ni dual citizenship wewe unaleta habari za biblia? Mbona quran ni aya za shetani?
 
Nikikuuliza tu kusafiri kwako kumekusaidia nini kwakweli huwezi kunijibu. Hivi kwa nini usiende kuishi Uarabuni unang'ang'ania kukaa nchi ya Makafir?

Hapa hoja ni dual citizenship wewe unaleta habari za biblia? Mbona quran ni aya za shetani?

Yaani honest huyu sijui ni mmama kweli au mbaba huwa simuelewi akili yake.She is always doing my head in with her comments.
 
umeshawahi jiuliza kwa nini celebrities wanatumia madawa ya kulevya, wana kuwa depressed na wengine hujiua?jiulize utapata jibu kwa nini watu wanazichoka hizo"raha" za majuu.

Wewe maji kutoka 24/7 ni starehe kwa mwengine ni routine, umeme kutokukatika sio anasa, basi kuwepo kituoni ontime, likiwa full airconditioned na linafika linakoenda on time sio mazingaombwe,binafsi hurudi nyumbani kila ninapojisikia nimechoka na routines,Africa kuko random, kuna raha yake.Hao wazungu wanaokuja serengeti, usidhani kwao hakuna Zoo, ila wanapenda kuona vitu katika uasili wake.

mtu kubakia ulaya inategemea anapenda nini kwenye maisha yake, anapenda organisatoin au chaos,kuna wengine wanapenda organiation ila inafika kipindi zinawaboa pia, ndio maana wenzetu wakihit midlife crisis wanafanya vitu vya ajabu mfano kama kununua pikipiki na kusafiri around the world ku-reset.

Alichosema mtoa mada ni sahihi, Tanzania has the best social life for a Tanzanian who grew up here, hata watoto waliozaliwa huku ukiwapeleka kusalimia wajomba zao TZ wakikaa wiki moja wanaboreka wanataka kurudi "kwao",ironically kwa kuwa wako rooted zaidi ughaibuni kuliko TZ.Ni hulka tu ya binadamu usiichukulie serious kihivyo

the only thing i miss in tz ni organised life!!! maisha kama computer game kila kitu kinaenda kwa wakati na namna inayotakiwa
 
Nikikuuliza tu kusafiri kwako kumekusaidia nini kwakweli huwezi kunijibu. Hivi kwa nini usiende kuishi Uarabuni unang'ang'ania kukaa nchi ya Makafir?

Hapa hoja ni dual citizenship wewe unaleta habari za biblia? Mbona quran ni aya za shetani?

Usikasirike kwenye ukweli, jee, unakataa kuwa Bibilia haibadilishwi?
 
Nimekupata ila huwezi kuchukua uraia huko uliko kwenda ukavuna za kutosha alafu baadae ukirudi nyumbani ukakaa miaka kadhaa ukaomba uraia wa Tz au ukiukana uraia wa Tz sheria inasemaje kuhusu kuutaka tena uraia wako? Ila hapa mie nachoona hata kama utakuwa raia wa nje ukaja Tz kuishi kama mgeni bado nafsi yako itakuwa unajiona kama mbongo tu hivyo inawezekana pia ukafanya mambo yako tu na mwisho wa siku maisha yanakwenda, unless kama na ajira za wabongo unazimezea mate au unakuwa unatamani kuwa kiongozi (ila kama huko haupo nadhani maisha yatakwenda vizuri tu

Hapo kwenye bold ni kasumba ya Watanzania wengi ili mradi maisha yanaenda hakuna tabu hata kama umevunja sheria.

Ni sawa na kuniambia kuwa sheria za Tanzania zinapiga marufuku ushoga lakini mwisho wa siku maisha ya mashoga yanakwenda. What's the point of having a law you can't enforce?

Kwa stahili hii tutakuwa tunajenga taifa ambalo watu wake hawana nidhamu. Taifa ambalo watu wake hawazingatii na kufuata sheria za nchi.

Kama tuko radhi kuwa na taifa la aina hii basi tusimsute Mtanzania yoyote atakayefanya mambo kinyume na sheria so mwisho wa siku maisha yanakwenda.
Hapo bold nilikuwa ninamaanisha just in case umebadili uraia alafu ukarudi bongo ukawa unafanya maisha yako kama mgeni kikubwa usikimbilie kwenye ajira ambazo ni kwa ajili ya watz pia usikimbilie kwenye uongozi kikubwa fursa mbalimbali za kiuchumi unazipata kama raia wa nje hivyo pamoja na kwamba ni raia wa nje lakini nafsi yako itauwa ya kibongo bongo kutokana na shina lako kuwa hapa bongo
 
Usikasirike kwenye ukweli, jee, unakataa kuwa Bibilia haibadilishwi?

kulikuwa hakuna haja ya kutamka neno biblia au mtu atamke quran.....yakiahaaemwa hayo basi mada yote inabadilikaaa inaingia ktk udinI sasa
 
Hapo bold nilikuwa ninamaanisha just in case umebadili uraia alafu ukarudi bongo ukawa unafanya maisha yako kama mgeni kikubwa usikimbilie kwenye ajira ambazo ni kwa ajili ya watz pia usikimbilie kwenye uongozi kikubwa fursa mbalimbali za kiuchumi unazipata kama raia wa nje hivyo pamoja na kwamba ni raia wa nje lakini nafsi yako itauwa ya kibongo bongo kutokana na shina lako kuwa hapa bongo

Yaani una maana kuwa kwa mfano mtu aachane na uraia wake wa Tanzania na kuchukuwa uraia wa Marekani halafu aje Tanzania kama Mmarekani na kuendesha maisha yake hapa kama mgeni?

Kama ulikuwa unamaanisha hivi sidhani kama mgeni ana benefits na privileges kama alizo nazo Mtanzania. Kwenye sekta ya uchumi sidhani kama mgeni anaruhusiwa kumiliki ardhi kirahisi hivyo kama ilivyo kwa Mtanzania.

Halafu kuna Watanzania wako nje lakini wanamiliki ardhi kubwa tuu Tanzania sasa wakiwa raia wa nchi nyingine, kuna uwezekano mkubwa wa kunyang'anywa hiyo ardhi kwa vile siyo Mtanzania tena.

Sheria inasema kuwa anayechukuwa uraia wa Tanzania ana-cease kuwa Mtanzania hata kama nafsi yake itauwa ya kibongo bongo kutokana na shina lake kuwa hapa bongo. Huyo siyo mbogo tena, ni mgeni hata kama anaishi kibongo bongo.

Pia kuna raia wa nchi nyingine wamepewa uraia wa Tanzania na wanaishi kibongo bongo hapa nchini huku wakiendelea na uraia wa nchi zao original.

Pomoja na kuwa na uraia wa nchi mbili hawa wanaruhusiwa kwa mfano kumiliki ardhi kama wabongo, lakini wabongo wazawa waliochukuwa uraia wa nchi nyingine hawaruhusiwi tena kumiliki ardhi kama Watanzania wengine. Kwani nini?
 
Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula. Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi. Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini, hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji. Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa. Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi. Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa, sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa, sijawahi ona watoto wenye utapiamlo, sijawahi ona watu wakitembea pekupeku, sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL, sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa, ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence. Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe. Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.


Tunahitaji kusikia simulizi za wenzetu mnaoishi nje ya Tanzania. Tunakushukuru sana kwa kufunguka.

Hata hivyo, kwa kuwa wewe mambo yalikuendelea vyema, haimaanishi kwamba hali iko hivyo kwa wote. Huwezi kuzungumza kwa niaba ya wote waishio ughaibuni, can you? Aliyeko Ufaransa au Urusi mambo yanaweza kuwa tofauti sana kwake. Huko Scandinavia pia inaweza kuwa ngumu mno kupata kibarua kama lugha yao haujai-master.

Wanasema "Usione vyaelea ...". Scandinavia bustani ni kijani leo kwa kuwa kuna walioitolea jasho/damu kuupata ukijani huo!

Umejitahidi sana kutaja yaliyo mazuri huko ulikoishi. Ila naona kama umeweka chumvi hivi bila kujishtukia. Hujawahi kuwaona waokota chupa za bia/soda majalalani au night clubs?
 
Yaani una maana kuwa kwa mfano mtu aachane na uraia wake wa Tanzania na kuchukuwa uraia wa Marekani halafu aje Tanzania kama Mmarekani na kuendesha maisha yake hapa kama mgeni?

Kama ulikuwa unamaanisha hivi sidhani kama mgeni ana benefits na privileges kama alizo nazo Mtanzania. Kwenye sekta ya uchumi sidhani kama mgeni anaruhusiwa kumiliki ardhi kirahisi hivyo kama ilivyo kwa Mtanzania.

Halafu kuna Watanzania wako nje lakini wanamiliki ardhi kubwa tuu Tanzania sasa wakiwa raia wa nchi nyingine, kuna uwezekano mkubwa wa kunyang'anywa hiyo ardhi kwa vile siyo Mtanzania tena.

Sheria inasema kuwa anayechukuwa uraia wa Tanzania ana-cease kuwa Mtanzania hata kama nafsi yake itauwa ya kibongo bongo kutokana na shina lake kuwa hapa bongo. Huyo siyo mbogo tena, ni mgeni hata kama anaishi kibongo bongo.

Pia kuna raia wa nchi nyingine wamepewa uraia wa Tanzania na wanaishi kibongo bongo hapa nchini huku wakiendelea na uraia wa nchi zao original.

Pomoja na kuwa na uraia wa nchi mbili hawa wanaruhusiwa kwa mfano kumiliki ardhi kama wabongo, lakini wabongo wazawa waliochukuwa uraia wa nchi nyingine hawaruhusiwi tena kumiliki ardhi kama Watanzania wengine. Kwani nini?

Yes ndio nilikuwa nina maanisha hivyo mkuu, in this case nimepata picha kwanini jamaa wanadai uraia pacha
 
Naona kumekua na maneno meengi kuhusu watanzania waishio ughaibuni.
Mimi nimeishi Scandnavia kwa muda mrefu ila baada ya kutimiza malengo yangu nilirudi nyumbani for good.Kwa sasa huwa ninakwenda mara kwa mara kwa sababu ya kibiashara kisha ninarudi nyumbani.

Kusema ule ukweli wa Mungu,kwa watoto wa maskini kama mimi ulaya ni bora kuliko bongo.Hapa nitaiongelea ulaya kama ninavyoifahamu mimi.Mimi mzee wangu hakua tajiri kama mzee wa Le mutuz,Tanzania niliyozaliwa mimi na kukulia ni tofauti sana na Tanzania aliyozaliwa na kukulia kaka yangu Le Mutuz.Mim Mungu alinijalia sana akili za darasani lakini kutokana na umaskini wa wazee nilishindwa kuendelea na chuo.

Ikatokea zali nikaenda scandinavia,nilienda kule nikiwa na malengo mawili,kusoma na kutafuta mtaji wa maana wa kijiajiri.Mungu alinisaidia,nimesoma,nina masters yangu,nina nyumba sita nimepangisha,nyumba moja ninafanyia biashara zangu na moja ninaishi na wadogo zangu na moja iko mkoani wazee wamejisitiri.Nina viwanja na mashamba.Vyote hivi nisingekuwa navyo leo kama nisingeenda ughaibuni.

Pia Mungu alinisaidia nikakusanya pesa ambazo nilitumia kujiajiri.

Mimi niliajiriwa kwenye kampuni ya kutengeneza magari.Huko nilikua na waafrika wengine wengi tu.

Sio kweli kwamba sehemu pekee wabongo waliyo nayo ni kwenye birthday za sebuleni tu LOL.Ulaya kuna viwanja vya maana bana za kula bata bongo itasubiri sana tu.Kitu kinachofanya wabongo wakusanyike kwenye hivyo vipati hadi nadhani ni ile hali ya kufurahia kukutana na wabongo wengine.Pia sio kila mtu anapenda kuwa kwenye hiyo mikusanyiko ya wabongo,mimi ni mmoja wa watu ambao nilikua sipendi kujimix na wabongo wenzangu.

Suala la kwamba wabongo walioko ughaibuni wana maisha magumu sikubaliani nalo.Kwanza kabisa idadi ya watanzania walioko tanzania wenye access ya internet inayowawezesha kusema wabongo wa ughaibuni wanateseka ni ndogo sana ukilinganisha na watanzania walioko bongo wasiojua hata internet ni nini.

Mimi kwa sasa ninaishi Tanzania na ninafurahia maisha ya hapa sababu ughaibuni imenisaidia leo hii sihitaji kwenda kujambiana kwenye madaladala,leo hii nikipata ugonjwa usio na tiba ya kueleweka bongo naenda zangu kutibiwa Scandinavia,mm nina uraia wa scandinavia tayari.

Hakuna binadamu yeyote awe muafrika au mzungu au muarabu hata awe amechoka vipi financialy aliyeko scandinavia anayelala njaa eti kisa hana hela ya chakula.Kwa Tanzania kila jua linapokuchwa kuna mamilioni ya watoto na watu wazima wanalala njaa.

Scndinavia inaongoza kwa uchache wa vifo vya watoto na wazazi,kwa Tanzania hebu tuchukue sekunde tano kuwaombea R.I.P dada na mama zetu watakaokufa wakati wakijifungua usiku wa leo.Tanzania mama zetu wanajifungua huku wakitzabwa makofi na manesi.Dada zetu waliko ughaibuni wanajifungualia katika mazingira kama mtu yuko hotelini,hata wanaojifungulia Aghakhan watasubiri sana compare na wanaojifungulia hospitali za serikalini ughaibuni.

Tokea nimeishi ughaibuni sijawahi shuhudia umeme ukikatika wala maji.Huwa wanayafunga tu kwa masaa au kuukata umeme kwa masaa na hapo mnapewa taarifa kuwa saa fulani mpaka saa fulani maji au umeme utazimwa.Sijawahi kuona watoto wanaotembea peku na kaptura zimechanika kwenye masaburi.Sijawahi ona mtoto akishindwa kusoma kwa sababu mzazi hana pesa,sijawahi ona mtu anakufa kwa kukosa elfu mbili ya kununua dawa,sijawahi ona watoto wenye utapiamlo,sijawahi ona watu wakitembea pekupeku,sijawahi ona ambulance za vibajaji LOL,sijawahi ona wakulima masikini kama hawa wa Tanzania.

Scandinavia maji huchemshi,unafungua bombani unakunywa,ukitaka ya baridi au ya moto kila wakati yapo.

Wkati naishi ughaibuni nilikua sina gari binafsi,japo magari ni bei chee sana kila mtu anaweza kuwa nalo cha muhimu tu uwe na vibali vya kukuwezesha kupata driving licence.Sikuhitaji gari binafsi kwa sababu usafiri wa public ni wa starehe.Baada ya kurudi bongo imenibidi tu niwe na usafiri sababu daladala kusema ukweli ni hiyo shida tu lakini ni mateso.

Wabongo walioko ughaibuni wanabezwa kwa kazi wanazofanywa,fine,hata mimi huko kwenye kampuni ya magari sikuwa nafanya kazi niliyosomea,ila ukweli ni kwamba nilikuwa nalipwa vizuri,wakati naanza nilikua nalipwa kama milioni sita za madafu kwa mwezi.Baadae waliniongeza,sasa kwa mtoto wa maskini kama mimi ukiniambia nilivokua ughaibuni nilikua nateseka nakuona unaongea kichini maana mdingi wangu angekua nazo hizo nisingeshindwa kwenda chuo bongo wakati kichwani kuko vizuri.

Hata wanaosafisha wazee hakuna anayepokea chini ya milioni nne za madafu kwa mwezi.Hapo nimetaja kima cha chini.

Kitu ambacho ambacho kwangu kilikua kinanipa stress enzi naishi ughaibuni ni kwamba sijawahi kufeel at home.Hii hali ndiyo ilinifanya kusave na kufanya kazi kwa bidii hadi nikatimiza malengo yangu nikarudi home.Kwa kifupi social life ya ughaibuni sucks(,huu ni mtizamo wangu).

Inshort kwa upande wangu mimi hata wale watanzania wanaoishi ughaibuni bila vibali mateso yao hayafikii hata theluthi ya mateso ya watanzania masikini walioko Tanzania.

Ughaibuni ni kweli kuna maisha ya ghali,ila ukiishi kwa malengo yako hakuna asiyefanikiwa.Pia ukiamua kuwa mtu wa bata ughaibuni utakula bata za maana kuliko wala bata wa bongo.

Ni kweli wahamiaji wengi(sio wabongo tu) wanafanya kazi za wazee,kusafisha na nyingine kama hizo ila ni ukweli pia kuwa wapo wapo wengi tu wenye kazi zao za maana.
Pia wewe secretary au mfanyakazi kwenye kampuni ya simu bongo na nyingine kama hizo hebu jiulize unapata shilingi ngapi kwa mwezi hadi umcheke mwenzio anayesafisha wazee na kupata milioni zake nne kwa mwezi?

Kitu ambacho wabongo wamewazidi walioko ughaibuni ni good social life tu.

Sijui kama una uhakika na unachoKINENA.
Leo unasema ukiumwa unakula pipa unaenda kutibiwa kwenu Scandinavia,
we hujapatwa na tumbo la kuhara lile ambalo halichukui hata sekunde ushakaukiwa mma mwilini.
By the tym unakumbuka Scandinavia yako uko hoooiiiii bin taaban.
Luku vere aisee.
Huku kwetu Mungu anatusaidia kule kwenu Scandinavia hospitali ndo msaada wenu wa 1.
Kwa mtazamo wangu mimi itakuchukua mda kujikubali hapa Tz before you forget Scandinavia yako.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Halafu sasa ughaibuni hakuna kitu utataka kufanya ukashindwa. Unaweza kutoka bongo darasa la saba ila kama una nia ukasoma na degree zako ukapata. Yaani ni ww tu uwe na nia. Bongo mpaka u ufanikiwe jambo utoe rushwa unyanyasike,uzungushwe,ughaibuni sijaona wadada wakitoa rushwa ya ngono ili kufanikisha jambo,bongo huo ushakua utamadun wetu tayar,

Hata na wewe ni Mtanzania lakini kwa KUJISIFIA umevuka kiwango kwani vitu ambavyo umeviandika haviendani na umri wako kabisa .
  • umepata zali,​
  • ukaenda chukua Master​
  • hapohapo ukapata muda wa kutengeneza magari (Kuunganisha nuts assembly) sijui ni kuunda Volvo​
  • ukaanza biashara​
  • nina nyumba sita Ndugu yangu nyumba za Bongo sio km zamani ukasimamishe tembe Kijijini uiite nyumba, siku hiti kuna kulipia ardhi ya Tanzania kwa sq meter na kiwanja ni zaidi ya 4,90,000.00 hapa Dodoma sasa wewe una viwanja 6 bado nyumba ya chini ni 36M​
    • nyumba 6 za 36M ni sawa na 216,000,000.00​
    • Na kwa jinsi unavyohadithia Hadithi za Shigongo umeweza kukaa nyumba 4 mbili umeacha Sadaka​
Kajipange tena kuwa Mwandishi wa UDAKU kazi Rudini tu Tanzania km Le Mutuz tupo naye hapa Dodoma na Dar huyu Diaspora mwenye uhakika, Blog na mashamba na nyumba Dodoma na Mvumi tunajua ni zake sasa hizo 6 hiyo abaru sikuimalizia


nina nyumba sita ​
​

Ha-hah-haah
 
Yes ndio nilikuwa nina maanisha hivyo mkuu, in this case nimepata picha kwanini jamaa wanadai uraia pacha

Lakini kama nilivyoandika kwenye uzi mwingine, sababu za kiuchumi zinaweza ku-play part lakini siyo kubwa sana.

Zipo sababu nyingine za msingi ambazo hazijatiliwa maanani katika haya madai.

Nyani Ngabu kaiandika vizuri haki ya uraia wa kuzaliwa. Mfano, mimi na wewe tumezaliwa Tandahimba kwa wazazi ambao ni Watanzania.

Ninaenda Finland kutafuta maisha lakini katika kuyatafuta maisha vizuri ikanilazimu kuomba na kupewa uraia.

Nikiwa huko bado tunaendelea kuwasiliana, tunatumiana picha na utani Whatsup, na wakati mwingine labda ukipata ka-trip ka kuja Finland lazima tuonane au unashukia kwangu.

Au kama kuna ndugu/rafiki anakuja Finland, unamwambia kuna jamaa yangu yuko kule ngoja nikupe namba zake ukifika huko atakupokea.

Karibia Krismasi narudi Tanzania (kama wachaga wanavyoenda kwao kula Krismasi) kusalimia ndugu na jamaa kule kijijini kwetu.

Nakukuta uwanja wa ndege unafanya kazi kama afisa uhamiaji. Tena nilikuambia in advance nitakuja Kirsmasi anyway.

Tunapiga story tena kwa lugha ya kabila letu, nakuonyesha passport zangu mbili za Tanzania na Finland, zote zinaonyesha kuwa nimezaliwa kijiji kimoja na wewe kule Tandahimba.

Halafu unaniambia oh sorry, wewe siyo Mtanzania tena na unaninyang'anya passport yangu ya Tanzania kwa vile mie siyo raia tena wa Tanzania kwa sababu nina passport ya Finland.

Lakini hapo hapo kuna wahindi na wapakistani wana uraia wa Tanzania na nchi zao za kuzaliwa wanapita hapo airport kila wakati bila tatizo.

Mimi unaniambia nikalipie dola 50 paleee ili nipate visa kuingia Tanzania na kwenda kusalimia ndugu na jamaa kule kijijini kwenu Tandahimba.

Nadhani labda wengi tunatumia maneno (uchaguzi wetu wa maneno) kimakosa.

Haki ambayo wengine tunaizungumzia ni haki ya uraia wa kuzaliwa.

Kwamba, hata iweje Mtanzania mzawa asipoteze haki yake hiyo ya msingi.

Kwa hiyo, tuseme kuna Mtanzania alienda kutafuta maisha huko majuu labda na akaoa na kuanzisha familia na kupewa uraia wa huko lakini Tanzania bado ana mizizi na kadhalika.

Mtu kama huyo si haki kumlazimisha aukane Utanzania wake kwa sababu Utanzania huo ni haki yake ya kuzaliwa, ni haki yake ya msingi.

Sina tatizo kabisa na kumwekea mtu kama huyo vizuizi kadha wa kadha vya kisheria. Lakini kumlazimisha aikane haki yake ya kuzaliwa si haki kabisa na hakuna mwenye haki ya kumlazimisha mwingine afanye hivyo.

Kwa hiyo mimi kwa maoni yangu naona kwamba, labda lugha inayotumiwa ikibadilishwa (tuache kutumia sijui uraia pacha au uraia wa nchi mbili) hili suala zima litakuwa 'palatable'.

Tuzungumzie haki: haki ya kuzaliwa, haki ya msingi kabisa badala ya uraia pacha.
 
Back
Top Bottom