Habari za leo Wana JF,Natumai mko poa sana na wale ambao hawako vizuri kwa namna moja au nyingine namuomba mwenyezimungu awaondoe katika hali hiyo na awapeleke katika hali nzuri zaidi ili waweze kuendelea na mapambano ya maisha ya kila siku.Nichukue nafasi hii kipekee kabisa kuweza kumshukuru mwenyezimungu,Mwenyezimungu ambae anatupenda sana sisi Wanaadamu na ametuumba umbile zuri kuliko kiumbe mwingine yeyote yule na ametufanya kuwa na akili ya kufikiria na kuamua na kuchagua kile ambacho tunakitaka hivyo hatuna budi kumshukuru.Ntakuwa mchoyo wa Fadhila kama sitawashukuru wana JF ambao wamesoma na kucoment hadithi yangu ya ukweli na sio ya kutunga hivyo nawashukuru sana.
Inaendelea...........
Baada ya kuvuka ile border ya USA na Canada nilikutana na polisi na bila ya kunihoji walinipiga Pingu jambo ambalo lilinishitua sana na moyo wangu ukaanza kwenda mbio nikaona sasa nimejiingiza kwenye matatizo maana sikuambiwa kuwa ntapigwa Pingu niliambiwa ntasaidiwa tu.Nikasachiwa mwili mzima then nikapelekwa kwenye kituo cha polisi,Nilipofika mule ndani nikafunguliwa pingu kisha kikafunguliwa chumba kidogo sana ambacho kilikuwa na Choo chake nikaingizwa ndani kisha nikaambiwa na Polisi wawili wa CANADA nivue nguo zangu zote hivyo kubaki uchi kama nilivyozaliwa kisha wakanifungia mlango wakaondoka.Walipoondoka nikaanza kukiangalia kile chumba huku nikiwa na wasiwasi mkubwa na mawazo nikaona heater na Camera nne nikawasha heater maana kulikuwa na baridi kiukweli nilikuwa katika wakati mgumu sana nilikumbuka nyumbani hasa mama yangu,Watoto wangu,mke wangu na ndugu zangu nikaanza kutokwa na machozi nikikumbuka nilivyosoma kwa shida na kupata kazi na nikawa namudu maisha yangu na kusaidia ndugu zangu nikajiona katika watu wapumbavu mimi ni mpumbavu kwelikweli.Chumba hakikuwa hata na kigodoro hivyo sikuweza kulala Usiku mzima.
Ilipofika asubuhi majira ya saa tatu mlango ukafunguliwa na Polisi wawili wakafungua mlango kisha wakaingia ndani ya chumba changu wakanipa nguo zangu na kisha wakaniambia niwafuate.Tukaingia chumba kingine mulemule ndani nikakutana na Afisa mwengine wa Polisi akaniuliza kwa ukali "Why did you cross the border Illegally?" Nikamwambia kuwa mimi ni mkimbizi kutoka Somalia nimeletwa na Agent Marekani na amenipokea mtu ambae amenileta mpaka hapa akaniambia nivuke ntasaidiwa hivyo wakaniuliza tangu naianza hii Safari nimetokea wapi na nimepita wapi mpaka nimefika hapa,Waliniuliza maswali mengi sana ambayo sitaweza kuyaandika yote humu Pia waliniuliza kwanini nisiombe Asylum USA nikawaambia kuwa nimeambiwa USA hawapokei wakimbizi na uzuri nilishapangwa cha kusema hivyo nilikuwa naigiza vilevile nilivyofundishwa kujibu na wakati wananiuliza walikuwa wanaandika kwenye computer walipomaliza tu wakatoa Karatasi ambayo ilikuwa inaonesha maswali niliyoulizwa na nilichojibu kisha nikaambiwa nitie Signature yangu.
Baada ya hapo nikaambiwa niwafuate Polisi wale wawili walionitoa mule chumbani kisha tukatoka nje nikaambiwa nipande gari hivyo nikaingia kwenye gari ikiwa na Polisi wengine wapya watatu .Gari ikaanza mwendo ambapo nakumbuka ilituchukua masaa matatu mpaka Kufika mji mkubwa kidogo nakumbuka unaitwa Québec ambapo mji huo wanazungumza Sana Lugha ya Kifaransa.Nilipofika Quebec nikapelekwa sehemu kwenye mjengo mkubwa Sana ulivyo kama Hotel nikakabidhiwa kwa Ofisa mmoja mwanamke na akapewa karatasi zangu huku akiaambiwa kwa Kifaransa kisha wakaniaga wale walionileta wakaniambia wananitakia kila la kheri
Mwanamke huyo akaniuliza Je nkilichoandikwa kwenye zile karatasi ni kweli au uongo nikajibu ni kweli,Akatoka akaniletea kitambulisho kinachoonesha kuwa mimi Mkimbizi kutoka Somalia kisha ikapigwa simu kwa Security wakanipeleka sehemu humohumo ndani nikapewa Lotions,Sabuni za kuogea,Shuka na Blanket kisha nikapelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa na watu wawili tu ila kilikuwa ni chumba kidogo ambacho kilikuwa na vitanda vya Double decker viwili yaani kitanda kimoja mmoja analala juu na mwingine chini kwahiyo chumba kimoja hulala watu wanne japo nilikuta watu wawili tu ila ikiwa mtu na mkewe wanapewa chumba kimoja peke yao na kitanda kikubwa.Nilikaa pale mwezi mmoja huku nikapata breakfast na lunch na dinner kwenye Kantini kubwa iliyokuwa na watu wengi Sana ikiwa wengi wao ni Waarabu wa Syria,Yemen na Afghanistan pia kulikuwa na Wasomali wengi na Watanzania ambao wengi walikuwa Wazanzibari na Kutoka Dar ilikuwa nipo peke yangu ila hawakunibagua.
Niliiishi pale kwa miezi miwili huku nikiutembea mji maana tulipewa ticket za bure kwa mwezi mzima na ikiisha muda unapewa nyingine na tulikuwa tunalipwa kwa mwezi pesa kidogo bila ya kufanya kazi.Kwa kweli nilipata marafiki wengi wa Kizanzibar pale kambini na kupeana hope kuwa tutashinda kesi na kupata Papers za kuishi na kukubalika kisheria.Na tulipeana Technic nyingi za kushinda case maana kuna Wazanzibari walijiripua kuwa ni Wasomali na walipoulizwa kwenye Interview ya kesi zao walisema kuwa Walitoa rushwa ili wapate Passport za Tanzania na wengine walisema wao ni mashoga kwahiyo jamii zao zimewatenga na wanataka kuuliwa maana jambo hilo halikubaliki kisheria kwetu na wengine walisema wao ni Wanasiasa hivyo Serikali inawaua na kuwapoteza na wengine walisema kuwa ni Waandishi wa habari na vyeti feki wametengeneza vya Uandishi wa habari kwa kweli Wazanzibari uzamiaji upo kwenye Damu.
Baada ya mwezi mmoja niliitwa kwenye Interview yangu ya kwanza ya kuhojiwa kilichonikimbiza Somalia na nikienda nikahojiwa kwa muda wa masaa 6 na maswali niliyoulizwa ni mengi sana..........
ITAENDELEA................
Ntataja maswali yote niliyoulizwa kwasababu dhamira yangu sio kuwafundisha watu kuzamia ila wayajue maisha halisi ya kuzamia ili mtu akiamua kuja ajue nini kitakachotokea hivyo Kujiandaa kisaikolojia mapema
Sent using
Jamii Forums mobile app