Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Ukweli kuhusu maisha ya ughaibuni

Mkuu, sijui kama umefika US au Canada ila kama haujafika naomba tu linapokuja suala la boarders za hizi nchi usiwaze kama namanga au tunduma.


Sent from my iPhone using JamiiForums

Nimeshawaambia hvyo lakn wanakuwa wabishi
 
Mleta mada ni muongo wa kawaida sana.
Kwa haya aliyoyaandika humu nina uhakika 100% mleta mada hayupo Marekani wala Canada na wala hajawahi kufika huko. Mleta mada ameokoteza blah blah za vijiwe vya Tandale na Tandika. Pia ninahisi kuna issue ya upigaji inatafutwa hapa.

Sababu ni hizi hapa.
1/Mtanzania yoyote aliyefanikiwa kufika Marekani kwa mara ya kwanza, ni vigumu sana kufikiria kwa haraka suala la kukimbilia nchi nyingine kiharamu huku akiiacha Marekani.

2/Kwa mtu aliyekwenda USA kwa njia halali na huku kibindoni akiwa na zaidi ya Dola 3000 (Karibu Milioni Saba za kibongo) hawezi kizembe kizembe kwa haraka haraka kumwamini mtu asiyemjua ili kufanya dili haramu katika nchi ya ugenini.

3/Tabia ya kujilipua kiukimbizi iko kwa baadhi ya watu tu tena katika namna fulani ya kiupekee wala sio mtindo unaofanania kwa kila mtu. (Mara nyingi hufanywa na watu ambao hawana chochote cha kupoteza, wao lolote liwalo poa tu), mleta mada hana chembe za hizo tabia.

4/Hiyo safari ya kuvuka boda ya USA na kisha kuingia boda ya Canada kwa kutumia gari tena kupita vichochoro halafu kujishikisha kwa maafisa wa polisi wa Canada ni uongo wa kitoto wa kutengeneza hapa, hakuna kitu kama hicho. Mleta mada angekuwa amewahi kufika USA asingekuja na hii story hapa. Haijui USA na wala haijui Canada.

5/Sio jambo rahisi kiuhamiaji kujivika utaifa wa nchi fulani ambayo sio asili yako na usigundulike na maafisa wa uhamiaji. Jambo mojawapo ni lugha, pili wajihi na tatu tabia. Wasomali ni watu tofauti sana, sio jambo rahisi kabisa kwa muafrika yoyote kujiigiza msomali. Na usomali sio tiketi ya kupokelewa kuwa mkimbizi huko Canada. Ni rahisi kuhisiwa kuwa ni gaidi kuliko kupokelewa kama mkimbizi wa kisomali.
 
Yaani uende USA kwa njia halali, tena upelekwe na taasisi rasmi kwenda kuhudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa, halafu upotee zako pasipo mtu kujua, waliokupeleka (Tz) wasitoe taarifa ya kupotea kwako, wenyeji wako (USA) wasitoe taarifa ya kutafutwa na mwisho Canada wasizipate taarifa zinazohusiana na wewe!! Huo ni uongo wa kiwango cha chekechea.

Mleta mada ni muongo kwa 100%
 
Yaani uende USA kwa njia halali, tena upelekwe na taasisi rasmi kwenda kuhudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa, halafu upotee zako pasipo mtu kujua, waliokupeleka (Tz) wasitoe taarifa ya kupotea kwako, wenyeji wako (USA) wasitoe taarifa ya kutafutwa na mwisho Canada wasizipate taarifa zinazohusiana na wewe!! Huo ni uongo wa kiwango cha chekechea.

Mleta mada ni muongo kwa 100%

Mimi nishamwambia mleta mada ni muongo ukiangalia stori yake ilivyokaa

Watu wanafikiri wazungu ni wajinga wa kukiubali kirais hivyo.ni bora akuweke mpajani miaka yote apate kujua ukweli
 
Nani aishi kwenye nchi inayonunua ndege wakati dawa hospitali hakuna.Na mnatangaza elimu bure wakati Walimu hakuna watoto watajifundisha wenyewe.Usilazimishe nifikirie Kama unavyofikiria wewe.Tanzania hatuna Serikali tuna kikundi cha watu wachache kinachoamua nani atawale kwa maslahi yao.Njoo Canada uone Raia wenye Serikali yao Kiongozi anaheshimu maamuzi ya Wananchi na havunji Katiba.Watu wanakosa maji Safi na Salama pesa inanunuliwa ndege.Tufike Mahala Watanzania tujitoe Muhanga ili kuokoa Kizazi chetu kinachofata

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu umekwenda Canada wakati nchi imeshatengenezwa. Ulizia historia yao wametoka wapi hadi kufikia hali hiyo. Usitukane nchi yako ilihali umeikimbia we unataka tu uje ukute vinono ule ufaidi, ningekuona wa maana kama ungekuwa sehemu ya kutatua hayo matatizo.
Nchi zilizoendelea kuna watu walijitoa sadaka ndio maana unaona leo vizazi vyao vinafaidi pamoja na wewe mzamiaji. Hakuna maendeleo/manufaa yasiyo na maumivu. Ila kwa kuwa akili yako ni ya kupenda vya bure, endelea na muelekeo uliouchukua.
 
Yaani uende USA kwa njia halali, tena upelekwe na taasisi rasmi kwenda kuhudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa, halafu upotee zako pasipo mtu kujua, waliokupeleka (Tz) wasitoe taarifa ya kupotea kwako, wenyeji wako (USA) wasitoe taarifa ya kutafutwa na mwisho Canada wasizipate taarifa zinazohusiana na wewe!! Huo ni uongo wa kiwango cha chekechea.

Mleta mada ni muongo kwa 100%



Mimi nishamwambia mleta mada ni muongo ukiangalia stori yake ilivyokaa

Watu wanafikiri wazungu ni wajinga wa kukiubali kirais hivyo.ni bora akuweke mpajani miaka yote apate kujua ukweli

Sijaelewa mnabisha nini wakurugenzi....

Mbona haya mambo ya kawaida saana kwa wanaojilipua. Simtetei mtoa mada ila mnakikataa kinafanyika. Sina experience na USA na Marekani ila Ulaya haya mambo yafanyika.

Ujerumani watu kibao wanajilipua kama wasomali. Na interview zinafanyika kama mtoa mada alivyoeleza. Sasa hapo kuna kushinda au kurudishwa. Halafu bado hajakubaliwa kuishi Canada kesi yake inaendelea...ataenda pewa matokeo ya aidha kubaki au kurudishwa.
 
Kama ni jobless ni vyema ukafikiria kufanya mambo mengine tu ndugu.
Gharama ya kufika huko hautaweza kuimudu.

Mzee kitaeleweka tu, ninacho amini hakuna kinacho shindikana chini ya jua, utakiwi kukata tamaa.. i will


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Acha kumkatisha tamaa mwenzako,A3M ameshauri kwa mwenye kazi na uhakika Wa kipato asiende huko,waende watu wasio na ajira,elimu na maisha magumu...umebahatika kupata m7 unajiripua Canada au US haahaahaaahaa!!!!

Tatizo mtu anajua, ukiwa jobless ndio hauna pesa..


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mimi toka mwanzo anavyoandika kuomba ushauri azamie au arudi nilimuambia kuwa aache ubinafsi na amechelewa sana kishakuwa na familia.
Unapokuwa na familia lazima uwafikirie wenzako.
Na kwa jinsi alivyojibu hayo maswali atarudishwa aje aungane na familia yake eti under age lakini ana mke na mtoto.


Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu ni tapeli lipo humuhumu bongo linajifunza kuuzia watu chai! Ati kawaambia ni under age lakini ana mke na watoto 3. Daah! Kwanza mtu ambaye kampuni inaweza kumpeleka hadi US kwa ajili ya workshop au training ni mtu anayejielewa, composed na atleast senior kwa hiyo hawezi kuzamia hata kidogo. Afterall kama umesoma vizuri kwanini uzamie? Si ufuate utaratibu ukafanye kazi kama expert? Halafu linajisifu ati limepata kazi ya uhotelia. Terrible! Yaani mtu uzamie ughaibuni, uache familia Tanzania halafu unakuwa hotelia huku ukitegemea kutoboa maisha? Ujinga.
 
Kama ni jobless ni vyema ukafikiria kufanya mambo mengine tu ndugu.
Gharama ya kufika huko hautaweza kuimudu.

Hujui kuna kitu kinaitwa scholarship , au hilo neno jobless umeli define vipi??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ukuje kieleweke
Daby Mrs Bishanga canada haina sheria ngumu za uhamiaji kama ilivyo USA Na Australia . pia ni nchi ambayo inahamasisha watu wenye ujuzi mbali mbali kuhamia huko kufanya kazi zipo nyingi watu wanahitajika kwa wingi ,hivyo wana program mbali mbali kwa ajili ya watu wanaopenda kwenda kuishi Canada ,hapa chini ni baadhi ya program ambazo unaweza ku apply na kupata kibali cha kuishi huko ,

Express Entry is an electronic management application system for immigration to Canada. It facilitates the selection and processing of Canada’s economic immigration programs:
- Federal Skilled Worker Program,
- Federal Skilled Trades Program,
- Canadian Experience Class,
- Provincial Nominee Program

Ingia google na uchimbe mwenyewe kujua ni namna gani uta apply na njia ipi inaweza kukufaa zaidi wewe,lakini endapo una ndugu au jamaa anaishi Canada basi inakuwa rahisi zaidi kupata kibali,google pia kama una ndugu unafata process gani ktk izo program za ku apply
 
Back
Top Bottom