Fursakibao
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 6,993
- 11,861
Mkuu profession yako ni gani?Sikupigwa ila sitaki kuwaaminisha watu njia hii niliyotumia mimi maana mimi nilikuwa na msimamo wangu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu profession yako ni gani?Sikupigwa ila sitaki kuwaaminisha watu njia hii niliyotumia mimi maana mimi nilikuwa na msimamo wangu
Sent using Jamii Forums mobile app
No. Marekani sio. Unajua nini? Wengi wanakimbilia Marekani. Huyu jamaa amecheza kwenda Canada. Na mpaka kuleta uzi hapa ujue mambo yake tayari yanenyoookaSawa kwa hizo nchi.... Mi naongelea marekani... Kule mambo si mepesi...
Habari za humu wa wadau wa JF,
Nichukue nafasi hii kumshukuru mwenyezi mungu kwa neema na baraka nyingi ambazo ametupa na kikubwa zaidi ni afya njema na maarifa mazuri aliyoturuzuku. Lakini pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Great thinkers wote wa JF ambao walitoa mawazo yao juu ya Mpango wangu wa kuzamia Nchini Marekani mara baada ya kupata Visa ya nchi hiyo.
Nafahamu wapo watu ambao walitamani sana kujua nini kilichojiri baada ya mimi kufika USA na kilichoendelea baada ya kuzamia huku Ughaibuni. Niwakumbushe tu kidogo kuwa nilisafiri tarehe 15 August mwaka huu 2019 kwaajili ya kuhudhuria mkutano ambao ulifanyika na nilihudhuria Nchini Marekani katika mji wa Washington DC ambapo ilinichukua siku 3 kukamilisha kile nilichotumwa na ofisi yangu kukikamilisha.
Nakumbuka watu wengi wa JF walinipa ushauri baada ya kumaliza mkutano nirudi Bongo kwa sababu sina pa kuanzia Marekani ila kwangu mimi hiyo haikuwa sababu ya kunizuia nisizamie Marekani.Kiukweli Marekani ni kuzuri mno japokuwa sijawahi kwenda nchi yeyote hiyo ndio Mara yangu ya kwanza tangu nizaliwe ila sidhani kama kuna nchi nzuri kuliko Marekani hapa duniani,Ni kuzuri nashindwa hata kuelezea kwa kweli.
Mara baada ya kutuma ile Post hapa jukwaani kuna jamaa alinitafuta Private kabla ya kuruka akanipa mchongo akaniambia hapo Marekani hapafai akasema atanipa njia niende Canada ila nikifika nijiripue kama mkimbizi wa Kisomali ndivyo Wazanzibari wengi hufanya hivyo na alinitumia Makaratasi ya Somalia niyasome ili niijue vizuri Somalia kuna maeneo Somalia wanaongea kiswahili.
Nilipomtumia picha yangu akasema nafanana sana na Msomali hivyo nikifika Marekani nimtafute ataniunganisha na mtu nitakayemlipa anivushe upande wa pili yaani Nchini CANADA. Kwa kweli nilikuwa naogopa sana na niliogopa isije ikawa anataka kunipoteza ila nilikuwa na moyo wa ujasiri na nilishachunguza kuwa watu wengi wanatoka Marekani na kuingia Canada kupitia Illegal borders.hivyo nilijipa moyo na kusema ntaweza.
Hivyo nilipomaliza mkutano nikawasiliana na jamaa mvushaji akasema niende New York atakuja kunipokea Airport,kwasababu nilikuwa na Pocket money ya kutosha nilijiamini sana.Baada ya kufika akanipeleka hoteli fulani akasema atakuja kesho asubuhi, Ilipofika majira ya saa 4 asubuhi akafika akiwa yeye na mwenzake ambae alikuwa ni Mmexico na huyo alienipokea alikuwa ni Mzanzibari.
Kwa hiyo tukapanda bus mpaka sehemu ambapo tulishuka na tukachukua Taxi tukawa tunaenda nikaona msitu tu nilipouliza akaniambia kuwa huku sasa ndio tunaelekea CANADA nikashangaa sana tuliposimama sehemu tukashuka na kukutana na watu watano na wale wawili wakawa saba wakaniambia niwape hela tuliyokubaliana yaani Dollar 3000 ikabidi niwape then tukaendelea na safari nikiwa nahofia kuwa nisije nikawa naenda kuchinjwa na kutolewa viungo vya mwili wangu maana hakuna ninaemjua pale na hata huyo Connector wangu nilikuwa simjui ila ilikuwa balaa la hofu limetanda naona sifiki.
Hatimaye nilifika sehemu nikaoneshwa bendera ya Canada na kuambiwa nenda pale na waeleze kuwa wewe ni mkimbizi kutoka Somalia utasaidiwa.Nikaenda na nikavuka mpaka nilipofika nikapigwa pingu palepale kwa kosa la kuvuka kinyume na utaratibu.
Itaendelea...
Nitawaeleza siku nyingine baada ya Pale ila kwasasa nipo Canada.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tuendelee kuwatia moyo wazamiaji ila kiukweli kama huna elimu ya kueleweka Canada utaenda kusota.Hahaha.
Poa kaka kila la kheri.
Sina neno mkuu...Tuendelee kuwatia moyo wazamiaji ila kiukweli kama huna elimu ya kueleweka Canada utaenda kusota.
ataishia kifanya kazi za warehouse ambazi nyingi zinalipa $16 kwa saa ambapo kwa wiki kisheria utafanya masaa 20 tu. na hapa ndipo linapokuja suala la kuwa na multiple Jobs.
Exactly my point kiongozi....sasa msikie huyu jamaa Papi Chulo anavyojidanganya... Kule kama ni mzamiaji na huna mwelekeo mzuri utaelewa maisha ni nini....kuna watu wanazurula daily kule newyork hopeless... Kodi tu room standard $2,600...bado chakula,usafir cjui starehe na ugumu wa kupata kazi huo....kule ukienda jipange...No. Marekani sio. Unajua nini? Wengi wanakimbilia Marekani. Huyu jamaa amecheza kwenda Canada. Na mpaka kuleta uzi hapa ujue mambo yake tayari yanenyoooka
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umesema kweli elimu ndio mkombozi....ukiwa na skill highly needed,wala usihangaike kuzamia...nenda ubalozini kaombe visa... Hili jambo nimelishuhudia sana....Tuendelee kuwatia moyo wazamiaji ila kiukweli kama huna elimu ya kueleweka Canada utaenda kusota.
ataishia kifanya kazi za warehouse ambazi nyingi zinalipa $16 kwa saa ambapo kwa wiki kisheria utafanya masaa 20 tu. na hapa ndipo linapokuja suala la kuwa na multiple Jobs.
HALAFU UJUE MAISHA NA MTAZAMO WA MAISHA TUMETOFAUTIANA SANA. Yupo mtu anasubiri hela za msimu,huyo anaweza kupata hata milioni 200,anahakikisha ameiteketeza yote kwanza ndio anatafuta kazi tena. Wakati huo huo yupo mwenye mtaji wa milioni 50 tu anaendesha maisha yake ya kila siku vizuri sana na anaonekana ni bora kimaisha kuliko yule anaepataga milioni 200,100 mara nyingi. Nakuhakikishia hao wanaolalamika maisha magumu marekani ni wale machinooh kama hao. Hata alipokuwa hapa hataki kazi. AMEFIKA KULE MAREKANI AMEUNGANA NA WENYEJI MAJOBLESS,AMEANZA MAMBO YA MADAWA YA KULEVYA,KUVUTA BANGI,ANATAKA AENDE DISCO,KSBB NDIVYO VIJIWE ALIVYOVIZOEA HATA ALIVYOKUWA HUKU,HAPO ANATEGEMEA/ANASUBIRI HELA YA MIUJIZA. NA HAO NDIO WENGI WANAOSEMA MAISHA MAGUMU MAREKANI NA HAO NDIO WENGI WALIOUAWA HATA SOUTH AFRICA KSBB HATA SEHEMU ZA KUWAKUTA NI RAHISI NI KWENYE MAJUMBA MABOVU WAKIVUTA BANGI,WAKISUBIRI HELA ZA MSIMU. Marekani pia kazi za mashopaz zipo,ila inategemeana wanampatia mtu wa aina gani?. Kama unaonekana umechoka choka,mlevi kila wakati kwa nini wakupe?. Muda mwingine hata hao hao wenyewe hawataki kuomba hizo kazi za mabox,wakiwaiga wenyeji kwamba ni kazi za chini. Uliwahi kuletwa uzi hapa,wapo baadhi ya WaTz wanaoishi au waliofika Marekani wakasema kabisa nani afanye kazi za kujidhalilisha hizo za kubeba mabox kwenye mashoprite?. Lakini ni kazi zenye ujira mkubwa sana UKIJITAMBUA NA UWE NA MALENGOExactly my point kiongozi....sasa msikie huyu jamaa Papi Chulo anavyojidanganya... Kule kama ni mzamiaji na huna mwelekeo mzuri utaelewa maisha ni nini....kuna watu wanazurula daily kule newyork hopeless... Kodi tu room standard $2,600...bado chakula,usafir cjui starehe na ugumu wa kupata kazi huo....kule ukienda jipange...
At least Canada mchomoko upo...
Ni kweli mkuu..... Nidhamu ya maisha na kujipanga vyema ndo vitakufanya uishi vizuri popote pale.HALAFU UJUE MAISHA NA MTAZAMO WA MAISHA TUMETOFAUTIANA SANA. Yupo mtu anasubiri hela za msimu,huyo anaweza kupata hata milioni 200,anahakikisha ameiteketeza yote kwanza ndio anatafuta kazi tena. Wakati huo huo yupo mwenye mtaji wa milioni 50 tu anaendesha maisha yake ya kila siku vizuri sana na anaonekana ni bora kimaisha kuliko yule anaepataga milioni 200,100 mara nyingi. Nakuhakikishia hao wanaolalamika maisha magumu marekani ni wale machinooh kama hao. Hata alipokuwa hapa hataki kazi. AMEFIKA KULE MAREKANI AMEUNGANA NA WENYEJI MAJOBLESS,AMEANZA MAMBO YA MADAWA YA KULEVYA,KUVUTA BANGI,ANATAKA AENDE DISCO,KSBB NDIVYO VIJIWE ALIVYOVIZOEA HATA ALIVYOKUWA HUKU,HAPO ANATEGEMEA/ANASUBIRI HELA YA MIUJIZA. NA HAO NDIO WENGI WANAOSEMA MAISHA MAGUMU MAREKANI NA HAO NDIO WENGI WALIOUAWA HATA SOUTH AFRICA KSBB HATA SEHEMU ZA KUWAKUTA NI RAHISI NI KWENYE MAJUMBA MABOVU WAKIVUTA BANGI,WAKISUBIRI HELA ZA MSIMU. Marekani pia kazi za mashopaz zipo,ila inategemeana wanampatia mtu wa aina gani?. Kama unaonekana umechoka choka,mlevi kila wakati kwa nini wakupe?. Muda mwingine hata hao hao wenyewe hawataki kuomba hizo kazi za mabox,wakiwaiga wenyeji kwamba ni kazi za chini. Uliwahi kuletwa uzi hapa,wapo baadhi ya WaTz wanaoishi au waliofika Marekani wakasema kabisa nani afanye kazi za kujidhalilisha hizo za kubeba mabox kwenye mashoprite?. Lakini ni kazi zenye ujira mkubwa sana UKIJITAMBUA NA UWE NA MALENGO
Sent using Jamii Forums mobile app
USA (Boston), UK (London & Birmingham).Sina neno mkuu...
Una experience yoyote nje ya nchi? Ulishaishi wapi mzee....
Tatizo ndugu zetu humu watabisha sana kwa hili. wanaona kama wanakatishwa tamaa.Mkuu umesema kweli elimu ndio mkombozi....ukiwa na skill highly needed,wala usihangaike kuzamia...nenda ubalozini kaombe visa... Hili jambo nimelishuhudia sana....
Then kuna sehemu unapwaya.USA (Boston), UK (London & Birmingham).
In the bucket List for the coming year.- France & Belgium Huku natakiwa nikawakilishe taifa kwenye uwanja wa 6X6![]()
![]()
NB: Siendi kuzamia huko anytime nikitaka kwenda napeleka tu kitabu nagongewa tu mhuri.
Hizo nimekutajia nilizokaa mwezi na kundelea.
Zile ambazo nimekaa not more than a week kwa safari za kikazi ziko kibao.
Naomba usiwe tomaso tafadhali
Sure mkuu.....bila hivyo mtu utaishi kwa bahati nasibu tu....Tatizo ndugu zetu humu watabisha sana kwa hili. wanaona kama wanakatishwa tamaa.
MAmbo si mepesi kivip mkuu?! Mbona unataka kutukatisha tamaa?Sawa kwa hizo nchi.... Mi naongelea marekani... Kule mambo si mepesi...
Baadhi ya watu wana akili mbovu sana.Wewe ni mmoja wao wakati ile ni biashara haramu ya watu wanachohitaji ni pesa tu sio lingine.Na Wamexico ndio waliokuwa na wanaovusha watu wengi kutokea kwao Mexico kuingia Marekani.Halafu usichokijua ni kwamba Canada na Marekani hakuna Ukuta au uzio wowote sehemu kubwa ipo wazi unaweza hata kuvuka bila kukamatwa,Utakamatwa ukishavuka ukawa upo Canada.Ila Mexico na Marekani kuna Ukuta Mkubwa sana huwezi kuvuka kirahisi lakini still Wamexico ukiwapa pesa Wana njia zao wanakuvusha kutokea Mexico kuingia Marekani ila border Patrol ni kubwa sana Upande wa Marekani.Nimejifunza mengi hapa Canada nimekutana na Wazanzibari kibao na Wasomali kibao nao wamevushwa kutokea Mexico mpaka Canada
Sent using Jamii Forums mobile app