Ukweli kuhusu kile kinachoitwa Chunusi

Ukweli kuhusu kile kinachoitwa Chunusi

Mshana eti kuna na vile vijitu vifupi pia nimesahau tulikua tunawaitaje eti usiku tu ndio vipo vikiwa mbali huvioni vikiwa karibu vinakuja kuuliza umeniona ukisema hapana nasikia unakula mbata za kutosha hivi ni kweli jamani kuna vipimbi vile vya usiku?
Vibwengo.
 
Haya mambo huwa yananisumbua sana umejaribu kunieleza maana kuna rafiki yangu aliwai kufa Ziwa victory kuna bichi inahitwa Mamba beach, yaani alikuwa anajua kuogelea balaa mpaka wingereza alifika kwa ajili ya kuogerea lakini alikufa hapo mamba beach mwanza maeneo kama unakwenda airport ya mwanza baada ya kuliwa na maji kuna mtu alisema huyu mwezenu mtampata kesho muda kama huu aliozama, tuliita watu wa kuzamia majini wa aina zote lakini hatukumpata mpaka ilipofika kesho yake mida kama ile ndio wazamiaji kutoka South Africa walimkuta amenasa kwenye tope yaani tulilia sana huwa kitu icho uwa kinanisumbua sana kwakweli wenyeji walituambia ameliwa na chunusi.

Mkuu huyo alinasa kwenye matope - na matope ni hatari unanasa miguu na mikono.
 
Kote salama na kote si salama Inategemea na mkondo
Hii inajustify my reasons kwanini nayaogopa maji. Nikiendaga beach mm huwa naangalia tuuuuuuuu na kuwashangaa wadada! Kifo cha maji kibaya. Hii inanikumbusha mwaka juzi kijana mmoja kahitimu pale Ardhi University aliposomea kozi ya General Architecture miaka mitano, kusherehekea mahafali yake akaamua kwenda kuogelea pande za Mbalamwezi Beach. Na huo ndo ukawa mwisho wa yule ndugu. RIP
 
Mkuu miaka ya 90 maeneo ya mbagala mimi nilishuhudia tulienda kuoga kwenye Bwawa tena huwa lina jaa msimu wa mvua tu kiangazi kaji yote yanakauka kuna kijana mwenzetu alizama kwa masaa mengi kidogo ila alipoibuka alikuwa maiti tayari.

Hizo sababu za kisayansi naona zinaelezea zaidi kwenye mito au bahari so vipi kwenye haya maji yaliyotuama ambayo hayatembei tena?
Inawezekana hilo bwawa lilikuwa na matope mengi chini sasa huyo ndugu alinaswa na hayo matope, muda aliokuwa amepotea inawezekani ni muda aliokuwa unatumia kujinasua kwenye hilo tope hivyo hadi mauti kumkuta, mara nyingi mtu akishakufa kwenye maji huelea juu hivyo alionekana akiwa marehemu
 
Mshana ushaomba kazi Kwenye kile chuo cha SA courses za Witchcraft?? Hope u will make a hell of a Lecturer....
 
Nakumbuka ata yule Bosi wa viwanja vya uwanja wa ndege alifariki akiwa anaogelea
 
ktk ubora wako mshana unajua meng sana. mzee mshana kuna kreta ipo mkoa wa mbeya wilaya rugwe kata ya isongole ktk kjij cha mchangan, inaitwa kreta ngozi au lake ngozi iko juu ya mlima. vjana weng wamepotea pale, kuna wanafunz watatu walipotelea mle, naamin kupotea kwa kuna uhusiana na ulichokieleza. 2liingia weng lakn wa3 hawakutoka iliuzunsha sana
 
Mkuu miaka ya 90 maeneo ya mbagala mimi nilishuhudia tulienda kuoga kwenye Bwawa tena huwa lina jaa msimu wa mvua tu kiangazi kaji yote yanakauka kuna kijana mwenzetu alizama kwa masaa mengi kidogo ila alipoibuka alikuwa maiti tayari.

Hizo sababu za kisayansi naona zinaelezea zaidi kwenye mito au bahari so vipi kwenye haya maji yaliyotuama ambayo hayatembei tena?
hakukuwa na tope kwenye hilo bwawa kweli ?
 
The King of Msata at his best.

Halafu hizi rip currents hata uwe mwogeleaji kumzidi Michael Phelps ukinasa umenasa aisee. Halafu watu wanabaki wanashangaa mwogeleaji mzuri yule hawezi kuzama lazima atakuwa amechukuliwa kichawi kumbe masikini umeburuzwa na kuwa squeezed na presha kali ya maji kama kimwanasesere tu. Na ukipanick na kujaribu kushindana na mkondo wenyewe ndo kabisa huponi.

Uchawi ndiyo upo lakini tukifikia mahali tukiona tukio tunatafuta kwanza sababu za kisayansi kabla ya kukimbilia ushirikina tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana. Siyo kila kitu ni ushirikina!
Kweli
 
ktk ubora wako mshana unajua meng sana. mzee mshana kuna kreta ipo mkoa wa mbeya wilaya rugwe kata ya isongole ktk kjij cha mchangan, inaitwa kreta ngozi au lake ngozi iko juu ya mlima. vjana weng wamepotea pale, kuna wanafunz watatu walipotelea mle, naamin kupotea kwa kuna uhusiana na ulichokieleza. 2liingia weng lakn wa3 hawakutoka iliuzunsha sana
Naomba direction vizuri nitafanya mpango nifike huko
 
Naunga mkono hoja namba tatu strong current hatari sana,kuna maeneo baharini meli hazipiti kukiwa na strong current noma sana hy kitu.
 
Back
Top Bottom