Ukweli kuhusu kile kinachoitwa Chunusi

Ukweli kuhusu kile kinachoitwa Chunusi

Kwamba kuna ukweli, kuoga ziwani/bwawani mchana haifai???
Kwanini? Hebu nifahamishe make napendaga kwenda huko kuoga mchana
Niliwahi kukutana na kisa kimoja kule Muheza kijiji cha Mlingoti kuna mto ulikuwa unapita hapo kijjini yani pale watu walikuwa hawaendi oga Ijumaa mchana au hata kuchota maji
Jamaa mmoja alileta ujuaji akaenda oga hapo nilimkuta ni chizi na kila Ijumaa mchana alikuwa anaenda kukaa kwenye jiwe moja hapo mtoni

nilishawahi sikia hiyo stor
 
Kwanza Niombe radhi kwa kuahidi mara nyingi kuweka hii post lakini bila kufanya hivyo!

Tunazungumzia chunusi mnyama, shetani, jini au kizuka. Sio chunusi zile za usoni zinazotokana kwa sehemu kubwa kuibana au kuwa domozege! Hapa ni chunusi mtoa roho, majini.

Tumekulia kwenye hizo habari, tumepoteza ndugu jamaa na hata marafiki huko kwenye mito maziwa na hata baharini sababu ikitajwa kuwa ni chunusi.

Ukweli huu hapa

1. Chunusi wa kishirikina - Hapa ni kiumbe jini ndio kinaua kimazingara na binadamu kutafsiri kuwa ni chunusi (nimeshindwa kwa hakika kupata uhalisia na chanzo cha chunusi kuhusishwa na maji)

View attachment 413290

2. Wanyama wa majini(kwenye maji). Wapo wanyama wasiojulikana sana waishio kina kirefu cha maji ambao nao kwa namna moja au nyingine wamesababisha mauaji na kudhaniwa kuwa ni chunusi - hapa hakuna chembe ya ushirikina.

View attachment 413289

3. Chunusi kutokana na mkondo wa maji (strong current) Haya ndio yanaweza kuwa maelezo sahihi zaidi kuhusu chunusi.

Mara nyingi chini ya uso wa maji hupita mikondo ya maji inayoenda kasi sana na inayopita kina kirefu cha maji. Mikondo hii iko ya aina mbili;

- Mikondo ya maji inayoonekana juu ya uso wa maji
- Mikondo ya maji isiyoonekana juu ya uso wa maji.

Hii sasa ndio hatari sana kwa kuwa ukiangalia utaona maji yametulia kabisa lakini kumbe huko chini yake ni habari nyingine

View attachment 413300
View attachment 413301

Wenzetu ambao sio wavivu wa kufikiri waliamua kufanya utafiti wa kwanini kuna baadhi ya maeneo yanaua sana (dhana ya chunusi) na hiki ndicho walichogundua na kuweka tahadhari kwa wasiojua.
View attachment 413302

Sisi tumekuzwa na hulka moja mbaya sana ya kupuuzia mambo hata kama kuna chunusi wa kichawi lakini ufafanuzi wa jinsi hii ungehitajika!

Kumbuka bado tuko kwenye msiba wa ndugu zetu watatu waliopoteza maisha kwa kudhaniwa ni mumiani wanyonya damu. Tungekuwa na matangazo kwenye vyombo vya habari yanayotoa elimu na ufafanuzi kuhusu mambo kama haya wale ndugu pengine wangesalimika.

Kwenye dhana nzima ya chunusi inasemekana kuna chunusi wa aina mbili;

A. Chunusi anayeua na kuondoka na maiti (uhalisia ni mkondo mkali wa maji)

B. Chunusi anayeua na kuacha maiti akinyonya damu tuu (uhalisia ni kifo kinachotokana na viumbe wa majini)

Hizi za mwisho ni picha zinazodhaniwa ni za chunusi ambao wamewindwa na kuuawa na sasa nyama yao iko sokoni (sio Tanzania).

View attachment 413304
hiyo picha ya mwisho ni west africa huko ...hao ni mbwa kama sio nyani ...
 
mshana jr nii inbox nashindwa kiongozi
 
Mshana eti kuna na vile vijitu vifupi pia nimesahau tulikua tunawaitaje eti usiku tu ndio vipo vikiwa mbali huvioni vikiwa karibu vinakuja kuuliza umeniona ukisema hapana nasikia unakula mbata za kutosha hivi ni kweli jamani kuna vipimbi vile vya usiku?
 
Hahhahahaaaa nyingine unajua ni story tu kiuhalisia mbilikimo mbali gizani huwezi kumuona mpaka akukaribie kabisa sasa akikuuliza kama umemuona toka mbali japo ni kweli hujamuona lakini mfariji tu kuwa umemuona ili kuepusha mengine! Watu warefu kwenda chini ni wakorofi by nature
 
Ahahahahaha sawa
 
The King of Msata at his best.

Halafu hizi rip currents hata uwe mwogeleaji kumzidi Michael Phelps ukinasa umenasa aisee. Halafu watu wanabaki wanashangaa mwogeleaji mzuri yule hawezi kuzama lazima atakuwa amechukuliwa kichawi kumbe masikini umeburuzwa na kuwa squeezed na presha kali ya maji kama kimwanasesere tu. Na ukipanick na kujaribu kushindana na mkondo wenyewe ndo kabisa huponi.

Uchawi ndiyo upo lakini tukifikia mahali tukiona tukio tunatafuta kwanza sababu za kisayansi kabla ya kukimbilia ushirikina tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana. Siyo kila kitu ni ushirikina!
Hizi rip current hata huku ziwa victoria zpo
 
Back
Top Bottom