Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Ukweli kuhusu "Kaskazini kuendelezwa na Wanakaskazini"

Mkuu kuna baadhi ya Mikoa watu wake hawakupata na hawana elimu kihivyo lakini wananchi wake wanavipato hakuna mfano-nadiriki kusema katika Mikoa yote Tanzania Mkoa wa Njombe katika wilaya za Njombe,Makambako na Makete wananchi wake wanavipato hakuna mfano hata vijiji vyao ni tofauti kabisa na mikoa mingine.nakuhakikishia pamoja na Mikoa ya kasikazini kuwa na watu wenye Elimu lakini kwa vipato hawafikii hawa viumbe!
pia kumbuka Bukoba Watu wake wana elimu sana karibu kila kaya lakini ni ipo top 5 kwenye Mikoa masikini Tanzania
 
"Mikoa ya Kaskazini iliendelezwa kwa juhudi ya Wanakaskazini"

Huo ni Ukweli unaoleta furaha kwa Wanakaskazini na Maumivu kwa wana mikoa mingine.

Nitaelezea kwa Ushahidi ulio wazi kabisaaa!

Kwanza msingi wa maendeleo ni ELIMU NA MAARIFA.

Ni wazi kuwa mikoa/makabila yenye wasomi wengi ni ile iliyowapokea wamissionary mapema na kuwakabidhi Ardhi. Katika hiyo ardhi kila walipojenga Kanisa basi walijenga na shule au hospitali nzuri.

Mikoa hiyo ni Kilimanjaro, Arusha, Kagera na Mbeya. Hiyo ilitokea hasa katika miaka ya 1885 - 1900

SASA TUKIACHA ERA HIYO:

Wananchi binafsi wa Arusha na Kilimanjaro wana spirit na asili ya utafutaji wa elimu na mali na Maendeleo kwa juhudi sana (Hustles indeed)

Mifano ifuatayo inathibitisha hayo:-

1) KUJALI ELIMU

Kufikia uhuru wa Tanzania, tayari Kilimanjaro ilikuwa na shule (Kongwe) zenye sekondari kabisa zaidi ya 38 na vyuo baadhi Shule hizo ni kama lyamungo, Majengo, Kleruu College, MUCCOBS, Marangu TC n.k

Hizo zilijengwa kwa juhudi ya Wazazi na chama kahawa KNCU

Arusha kulikuwa tayari na shule zilizojengwa kwa Juhudi za wazazi kama Moringe Sokoine, Mringa Middle School, Monduli TC (ingawa pia serikali iliweka nguvu), Arusha Sec.school, Ilboru Sec. School iliyojengwa pamoja na kanisa la KKKT mwaka 1904

Kwa kuwajuza zaidi Ilboru sec.school na kanisa la Ilboru zilijengwa na wanawake (wamama wa kimasai) kutoka Kimandolu, Levolosi na Ilboru yenyewe, na ushahidi upo.

Pia Chama cha kahawa ARCU ilichangia sana maendeleo ya Arusha.

- Miji midogo wakati huo kama Monduli, Marangu, Machame, Ilboru na Akheri zilijengwa na juhudi ya wazee wa huko.

* Mfano tu, Monduli iliamuliwa kuwa mji mahali ilipo na Wazee wachache wa monduli akiwepo Sokoine.

Can you imagine mwaka 1970 tayari Sokoine alishaanzisha jengo kubwa kuwa Halmashauri ya Monduli kabla hata serikali haijaamua halmashauri iwe wapi.

Kina Lowassa na wengine walikuja tu kuendeleza zaidi.

* Kwa Upande wa Kilimanjaro, hasa Marangu akina Mareale walikuwa Mbali tu kiasi cha kuweza kujiongoza bila serikali ya JMT.

Mji wa Moshi ulikuwa mbaali kimaendeleo siku nyingi.

2) UHUSIANO WA KARIBU WA WANAKASKAZINI

Kingine kilichoiendeleza Kaskazini ni Interaction ya kuoana watu wa Kilimanjaro na wenyeji wa Arusha mjini, kwani wali utilize ardhi vizuri kuanzia enzi na enzi.

(Hata leo hii ukichunguza utagundua watoto wengi wa familia hizo ndio wamejaa serikalini, kwenye migodi ya madini, biashara n.k)

3) KUTOKUTEKWA NA USHIRIKINA

Wanakaskazini hawana asili ya "Ushirikina" na ukisikia mchaga, mmasai ama mwarusha analoga basi ujue amenunua uchawi.

Hakuna uchawi wa kutumia paka, Jini au Vifuu bila faida yoyote.

Mikoa kama Tabora chini ya machifu wao walipaswa kuwa mbali sana kimaendeleo kama alivyofanya chief fundikira (wajomba wa Samwel Sitta) na matunda yanaonekana hadi kuwasomesha akina Samwel Sitta (Hayati)

Mikoa mingine imekuja kuamshwa na hizi shule za kata, halafu inalialia kuwa Kaskazini inapendelewa. [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Wengine Dini zao ziliwanyima Fursa ya kuishika Elimu dunia leo wanalialia na kuikumbatia elimu dunia.

Kumbukeni...Azimio la Arusha likija Arusha tyr Arusha ilikuwa na majengo makubwa na shule za kuwatosha watoto wa Chuga.

Someni Historia, Fanyeni tafiti kabla ya kuanza kulialia.
mkuu, usipate shida, we ukiona kaskazini kunaendelea, tz ni yetu sote. ondoka nenda kaskazini katafute kiwanja ujenge na wewe uishi huko. kwani tatizo liko wapi?
 
hivi na sisi wa Mkoa wa Mara ni wana kasikazini au ??? Nyerere angekuwa akina JPM na Kikwete Mara sa hivi ingekuwa New york
 
Unat

Unataka kumlinganisha Trump Na Bakhresa? Wote matajiri au Bill Gates na Mengi? Angalia hawa wanaochukia watu wa Kaskazini hawana nini kama wao?
Rafiki yangu sisi LDC country. Hamna kitu zaidi ya mbwembwe Tu. Ki uhalisia hatuna hizo hela za kuringishiana subiri Magufuli aendele kukata miraji ya wizi labda ndipo mtastuka in reality sisi maskini.
 
Mtoa thread ana inculcate spirit ya ukanda na Ukabila bila kujitambua. Mpishano wa kimaendeleo ni mlundikano wa factors nyingi sana! Mtoa mada anamawazo ya Kikoloni Tena yanauono wa Kibaguzi sana! Hana tofauti na wale wanaoamini ktk Hamitic Myth kuwa watu wa race fulani ni superior na ndio wenye fikra za kimaendeleo kuliko wengine! My friend, Kaskazini na Wanakaskazini ni Watanzania na they have nothing unique except favour due to colonial regionalism which favoured that part of the country basing on their own colonial reasons and marginalising other areas. Nani alichagua kuzaliwa mahali au Kabila hilo hata apate courage ya kujinasibu mbele za watu Timamu? Stop being mkoloni ktk fikra zako za kiafrika! North is nothing out of JMT
 
Kama mkuu alivyo elezea kupitia tafiti yake... Mimi ni mkazi wa kaskazini na ofcoz nimetembelea mikoa mingi nchini mikoa ya pwani na kanda ya ziwa tofauti ya IQ za watu wa mikoa hii ukilinganisha na kaskazini kiujumla.. Watu wa mikoa iyo upenda kuridhika wanaridhika na hata maendeleo kidogo bt northern we didn't.. Alaf Mikoa ya Arusha na moshi ofcoz Arusha tuna infraction na wakenya so many ideas of life we share mfano kama mm ni mmasai bt ninandugu zangu wanaishi Kenya na kule ni wazawa wa uko so watu wengi wa kaskazini wana ndugu na wakenya dat why we share some ideas to use our brain to make a better day...
Hata hiyo mikoa mingine utakuta kati ya matajiri kumi huwezi kukosa wawili mpaka watatu wana asili ya kaskazini
Ktk post yote umenifurahisha hapo uliposema marangu(wachaga)waliweza kujiongoza bila JMT.Niliwahi kusikia wachaga walikuwa na Rais wao na serikali yao je hii ni kweli?Nijibu ili niendelee kudadisi
 
Fuatilia historia vizuri kabla ya uhuru wa Tanganyika wakati Nyerere alipoenda UN kutafuta uhuru wa Tanganyika alionana na Mareale akiwa UN pia kutafuta uhuru wa eneo lake lakini Nyerere alimzidi ujanja akadai kuwa uhuru anaoutafuta unahusisha hata eneo lake (Mareale), hivyo uhuru ukatolewa mmoja kwa Tanganyika badala ya nchi mbili. Baada ya hapo ili kuondoa mgongano Nyerere alimpeleka UK kuendeleza maisha huko ili asilete chokochoko.
Maendeleo yalikuwa Moshi kwa muda mrefu sana kabla ya uhuru. Ukifuatilia utakuta kuwa hata ikulu ya Moshi ilijengwa kabla ya ile ya Dar (Walikuwa wamejipanga mapema kuwa nchi).
Ukweli watu hii kaskazini Moshi-Arusha wanapenda kwao sana na wanajijali, %ge kubwa ni wajanja kubwa (comparatively); naturally aliyekuzidi amekuzidi tu, kumfikia wewe uliyechelewa kwa sababu moja au nyingine, uwezekano upo but siyo kwa majungu na kupiga domo but kutambua udhaifu wako na kujipanga bila kinyongo. Ukianza wivu na kulipiza visasi hutafika popote ila utaambulia vumbi tu na watu wako kama unao!
Kama unafuatilia historia pia eitha wajua aua hujui tafuta facts kuhusu Dodoma.
Nitakumegea kidogo:- Nyerere alimpa jukumu Malecela kuendeleza Dodoma ili iwe makao makuu mapema sana akidhani kuwa kwa sababu ilikuwa kwao angefanya vizuri but outcome siri anaijua Malecela mwenye alivyo mdisappoint Mzee mwenzake na ninadhani it was a serious disappointment ilyofanya mpango wa Nyerere kuhamia Dom kuwa kama ulivyokuwa.
Mambo ni mengi yanayofanya maeneo mbalimbali ya nchi yetu kuwa na tofauti kimaendeleo. Zipo issue za kisiasa, kidini(aina ya misionaries walioingia eneo husika na namna walivyopokelewa), location, nk
Sorry nimeandikannikiwa sijatulia sana!!!
Itaendelea...
Na mmeru alikuwepo alieenda kudai Uhuru wa wameru
 
Soma thread vzr uelewe, inahusu Tz na wanaolalamika kuwa kaskazini inapendelewa kimaendele.
Wote wanaolalamika na kujisifia ni wapumbavu kwasababu bado wanaishi kwenye nchi uchumi mdogo duniani na karibia asimilia zaidi ya 40 wanaishia chini ya dola moja kwa siku, watu wa kaskazini wakiwemo kwenye Hilo kundi.
 
lami hadi machame
Aisee ni njia panda ya kwenda kwa Babu yangu Kyalia Nkweseko hahahahahaa nimepamis sshv npo mbali bt soon nikirudi tu tour ya kwanza Marangu namalizia Nkweseko thn Arusha moja thn narudi makazi yangu Dar moja ingawa itakuwa cyo hollyday nitatimba tu kuangalia ndg na jamaa zetu
 
arusha.jpg

Inajieleza
braeburn_imani-550x200.jpg

Hapa ni Arusha .(Kaskazini)
braeburn_garden_estate-550x200.jpg

Oooh Kaskazini,kaskazini,
SOMENI HAMTAKI
6.jpg
6.jpg

Hahahaha...Unaweza sema hapo ni Newyork..Kumbe ni Arusha Tanzania..
 
Mwaka 1926-1928 wachaga tayari walikuwa na gazeti likiitwa Kwakya kama sijakosea likiwa na maana ya kumekucha.
Shule alizotaja ni chache sana zipo shule za kale 1,000 zaidi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro shule kama Makumira na Enaboishu ni za zamani sana. Pia shule zote za serikali hasa zile za zamani zilikuwa mali ya makanisa. Angalia kwa sasa kila wanafunzi 100 walio Universities hapa Tz basi 35 hadi 40 wanatoka kaskazini.
 
Vya kuandika ni vingi mnooo. Nenda pahala popote hapa Tz utakutana na mtu wa kaskazini anafanya biashara fulani hivi. Nenda university yoyote hapa Tz utakuwa wakufunzi wengi ni hao hao[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
mimi sio wa kaskazini,lakini sio siri napenda spirit ya watu wa kaskazini mwa Tz ktk kutafuta maendeleo.pia nakuwa inspired na spirit ya wahaya ktk kutafuta elimu.

huu ni mtizamo wangu,simlazimishi mtu yoyote asiye wa kaskazini kukubaliana nami.

With due respect, nakubaliana na wewe mkuu kwa 2000%....

Mimi siyo wa huko lakini nimeishi na kufanya kazi mkoa wa Arusha na Kilimanjaro kwa takribani miaka 10 mijini na vijijini.....nawapenda na kuwakubali sana natives wa mikoa hiyo especially wa mkoa wa Kilimanjaro!!

Wanajituma, wanajitambua na kujielewa kweli kweli pamoja na kwamba wana kasoro zao ndogo ndogo za hapa na pale kama binadamu lakini ambazo si kikwazo kusonga kwao mbele kimaendeleo...

Mfano mzuri waangalie watu kama Edward Ngoyai Lowassa na Freeman Mbowe kama viongozi wa kijamii wanaotukanwa na kupigwa vita kweli kweli tena kwa kudhalilishwa utu wao....

Lakini kamwe hawarudishi baya na hawana visasi kabisa.....Hili ni ngumu sana isipokuwa kwa mtu aliyestaarabika pekee, mtu aliyekwisha jitambua na kuelewa maana ya ustaarabu ni nini....!!

Hili ni tofauti sana kutoka kwa watu wa jamii zingine isipokuwa wachache tu toka miongoni mwa jamii hizo ndiyo ambao sasa ustaarabu unawavuvia ikiwemo jamii yangu mimi mwenyewe!!
 
Sifa za Kijinga vitu vimejengwa na Wakoloni and then mtu anasema kimejengwa na kina mama wa Kimasai au Kimachame n.k Hizo Shule ukienda zitizama zina majengo ya kale ya tawala za Wajerumani Nenda Kolila Old Moshi n.k Shule Nyingi zilikuwa za Dini
Acha uongo mkuu

Ukitaka ushahidi kuhusu shule na kanisa la Ilboru nitakupa.

Tena sio hizo tu kuna shule sijazitaja kama Minha secondari

Ilboru ilijengwa na wanawake wa Arusha mwaka 1904 ikawa chini ya KKKT na baadaye ikataifishwa kuwa ya serikali.
 
Baada ya JK kuwachinjia baharini na ninyi kupewa pepo mmefika wapi??? Viwanda na Majengo alowaletea had uani yamekuwa magofu
Hawa watu wanashangaza sana mkuu
 
Back
Top Bottom