Ukweli Kuhusu Electronic Fiscal Devices ( EFDs)

punguzo

Member
Jul 9, 2011
51
0
kwanza kabisa kama ilivyotanabahishwa kwenye website ya TRA(Tanzania Revenue Authority - E-Fiscal Devices (EFD))
kuna aina tatu za EFDs, TRA na Serikali wanatakiwa kuchambua wazi ni aina ipi ya hizo devices ambayo inafaa kwa kwa mazingira yetu ya Kitanzania , aina ipi ni kwa kundi lipi la wafanyabiashara? na ichambue bei ya kila divice(kwa mfano Nchi ya Republic of Georgia ni Georgian Lari GEL350 ( The price of the cash register and its maintenance), ambazo si zaidi ya TSH330,000/-)

Watueleze kwa wamejipanga vipi katika kuwaelimisha wafanyabiashara na wateja, ufuatiliaji, management and controlling ya kodi kwa kutumia hizo mashine.

watuambie kama mtu binafsi anaweza kujinunulia yake binafsi na TRA kuja kuinstall programme zao au kama makampuni binafsi wanaweza kusambaza tofauti na wao TRA kwani ni soko huria.

Anyway,
kama wewe unaujua ukweli wowote kuhusu manunuzi, usambazaji, upatikanaji, njia bora ya usimamizi wa kodi kupitia hizi mashine kulingana na mazingira yetu ya kitanzania( ki-Techolojia ,ki-hulka za wafanyabiashara na wateja na rushwa), tafadhali tuungane pamoja kuweka ukweli na ushawishi wetu hapa kuliko kuingia katika malumbano ya kuwalaumu wafanyabiashara au kuwalaumu TRA na serikali bali tujikite katika kuweka ukweli bayana na data sahihi kuhusu huu mradi wa TRA !

mimi naanza na link za upatikanaji wa EFDs

Daisy Technology - The fiscal devices your business needs

Cash Register Manufacturer, Retail Cash Registers, Restaurant Cash Registers, POS Systems

Home page

CASIO 140-CR ELECTRONIC CASH REGISTER RETAIL SHOP TILL | eBay

pt=LH_DefaultDomain_3&hash=item27c87bfaea

Bora tuwe wawazi na wakweli na tukosoe panapofaa kuliko kuingia katika malumbano kati ya hizi pande mbili

Aksante
 
mkada

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
1,194
2,000
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,309
2,000
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.
 
MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
15,641
2,000
Jamani ndio maana mijadala mingi inakosa lengo kuu.Hapa tuache kujadili tatizo la wafanyabiashara kutolipa kodi maana ni mjadala mpana sana.Mada kuu ni gharama za EFD na sijasikia popote wafanyabiashara wakigoma kulipa kodi zaidi ya uzembe wa TRA tu na mfano mimi nayafahamu makampuni tena makubwa ambayo hata assessment ya kodi haijawahi kufanyika yaani kampuni inajilipia tu kodi itakavyo!

Mjadala ni bei za machine za EFD na sio ukwepaji kulipa kodi. Tusipoteze uelekeo wa mjadala huu.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,162
1,250

Kaka hawa TRA hamna kitu kabisaaaa,hivi wana kitengo cha utafiti kweli????!!!!!
Huwa wanajifunza kutoka kwa wenzao kweli???!!!!
Wana nia ya kuikomboa hii nchi kupitia kodi kweli???!!!!
Waziri wa fedha na wataalamu wake wako aware kweli na uhitaji wa nchi hii katika suala hili??!!!

To hell with it, bora uchaguzi uje tujue la kufanya!!!!
 
Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.
issue sio tulia kodi mkuu, issue ni bei ya efds kuwa juu. umeelewa?
 
Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,445
1,250
Jamani ndio maana mijadala mingi inakosa lengo kuu.Hapa tuache kujadili tatizo la wafanyabiashara kutolipa kodi maana ni mjadala mpana sana.Mada kuu ni gharama za EFD na sijasikia popote wafanyabiashara wakigoma kulipa kodi zaidi ya uzembe wa TRA tu na mfano mimi nayafahamu makampuni tena makubwa ambayo hata assessment ya kodi haijawahi kufanyika yaani kampuni inajilipia tu kodi itakavyo!

Mjadala ni bei za machine za EFD na sio ukwepaji kulipa kodi. Tusipoteze uelekeo wa mjadala huu.
Asante MTAZAMO, maana naona wengine wanatupia tu comments hapa. Wafanyabiashara hawajagomea kodi bali bei ya machine
 
jotohasira

Member
Oct 3, 2013
50
0
Liberal economy. .free market....kibongo bongo haiapply ndio maana Tanesco wamehodhi soko..hilo kama linafanyika huko mbele na ni ishu ya software wanaweza kufanya mtu unanunua mashine then wanaiunganisha..ila hako karushwa principle ndio ishu...
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,132
2,000
TRA inabidi wawe waangalifu hapa ama wanaweza kuibua mapya.

Juu ya kodi falme zimepotezwa.
 
kidole007

JF-Expert Member
Dec 22, 2012
3,096
2,000
wafanyakazi mmeshikia bango hizo device

wafanya biashara hasa wadogo hizo device ni mufilisi
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,162
1,250
Something is behind this mgomo...but the bottom line is TRA ikicheka na wafanyabiashara hakuna kodi itakayokusanywa....hawa sio watu wa kuwachekea kabsa...pamoja na vipato vyetu vya chini wafanyakazi tumelipa kodi sana....tuanze kugawana maumivu sasa na kuongezwa tax base kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii.

Hivi wewe ni mwanaume au mwanamke!!!!!
Hebu weka wazi ujulikane nia yako maana kila unapokuja mjadala wa EFD lazima ulete mada ya ku divert attention kuwa kuna ajenda ya siri,au wafanya biashara hawataki kulipa au kuwa wafanyakazi wanakatwa na mambo kama hayo!!!!!!

Jua kitu kimoja kuwa hawaTRA ndio wanajukumu la kuondoa ambiguities zote hizo unakurupuka nazo kwa kuwekeza wao katika muundombinu huu ili tumalize hili suala tufuate ajenda nyingine za manufaa ya nchi!!!!!!

Umeagizwa na nani na.unalipwa shilingi ngapi,if I may buy you out madam!!!!!!
So that we(without you) can pave the way for a more brighter and sustainable means to build this Nation!!!!!
 
Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
517
500
punguzo umekuja na wazo zuri. Mimi najiuliza swali moja. Je nisababu zipi za msingi zinaziwafanya wafanya biashara wagome kutumia hizo mchine. Je ni kwasababu ya bei zake (initial cost) au kwavile wanajua kuwa utaratibu huu utawafanya wajulikane kipato chao basi hawataki kuzitumia. Je ni kwavile hawaoni faida ya wao kulipa kodi na hivyo kutafuta mwanya wa kuendelea kukwepa kulipa kodi?

Kuna vitu viko wazi ambavyo mimi naviona. Ukusanyaji wa kodi kwa TRA bado upo kwa kiwango cha chini, cha kusikitisha hata hicho kidogo kinachokusanya ni kiwango kidogo kinachofanya kazi za maana/kinachotumiwa kwa maendeleo. Kiasi kikubwa kinaishia mikononi mwa wachache kwa njia za deal deal. Na hiyo inawafanya watu wasione umuhimu wa kulipa kodi.
Pili hata wale wenye EFD tayari bado hawazitumii inavyotakiwa. Utakuta bado wanatumia risti zao za zamani au hatoi risti kabisa. Na mara nyingi sana na hii imenitokea mara kibao wafanya biashara anakwambia bei ya kifaa hiki ni mfano laki 7 ukitaka risti au laki 5.5 bila risti. Mteja yoyote atakimbilia kuchukua bidhaa bila risti na mwisho wa siku mfanya biashara ananufaika kwa kukwepa kodi. Lakini ki u-halisia huwa wanaongeza bei kumtisha mteja na hivyo kusababisha mteja akubali kutochukua risti. TRA needs to workout that, vinginevyo mtakuwa na hizo EFD lakini bado efficiency yenu ya kukusanya kodi itakuwa ndogo. Usahauri wangu kama zipo machine zinazoweza kupatikana kwa bei ndogo kama ulivyo pendekeza itakuwa ni jambo zuri. Lakini pia wanaweza kuwakopesha wafanya biashara na wakawa wanawakata hela yao kidogo kidogo hadi itakapo isha. Tusilazimishe kununua machine hizo kwa hela ndefu hivyo. Si kila mfanya biashara anahela ya kutoa kwa haraka na hasa anapogundua kuwa hicho kifaa hakimsaidi kama wanavyoelezwa eti kutunza kumbukumbu. Ingekuwa kweli wao wanaona kitawasaidia basi wangekimbilia, kumbukumbu zao wanazo ila huwa wanajaribu kuzificha na kwasababu TRA hawanauwezo wa kuzipata hujikuta wakiwakadilia malipo kidogo ya kodi licha ya kwamba utaona wengi wanalalamika kama vile wamekadiliwa kwa kiwango cha juu.

Wito wangu: Serikali ijitahidi kutumia vizuri kodi za wananchi, hii itawafanya wananchi ambao ndo walipa kodi waone kwamba kodi yao inatumika vizuri. Binafsi huwa nasikitika naposikia watu wamepiga hela za miradi flani, au wanafanya ubadhilifu, au wanatumia vibaya magari ya serikali. Wanafanya uchakachuzi katika sekta mbalimbali huwa nasikitika sana. Najua mwisho wa siku sisi ndo tunaumia maana hizo ni kodi zetu. Ukweli ni kwamba kama wafanyakazi wa nchi hii nao wangekuwa na option ya kukwepa kulipa kodi ya mapato (pay as you earn) watu wasingelipa. Hakuna mtu anayegoma kulipia huduma na hasa anapoona huduma zinzotolewa ananufaika nazo.
Watu hawana hospitali, viongozi wanakimbizwa nje wanapougua, shule zetu zinakwisha watoto wa viongozi wanasomeshwa nje au shule private nzuri. Barabara mbovu, tembelea maeneo wanapokaa wao. Huduma za maji na umeme mbovu kwao wanapata masaa yote. Sasa mtu anajiuliza kwanini nilipe kodi. Kwanini nami nisifanye saving itakayo nisaidia baadaye nitakapo ihitaji.
 
Last edited by a moderator:

FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,083
1,225
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.
Pasco,

Sijui na wewe unaanza kuchanganya mambo. Issue hapa sio kukataa au kukwepa kodi, ila ni ulanguzi unaofanywa na TRA kwa kisingizio cha kufuatilia kodi. Na wafanyabiashara wa Kariakoo hawako peke yao kwenye hili. Ni hivi majuzi tu Mbeya nako kulikuwa na sintofahamu.

Tukumbuke hizi sio zama za RTD, kwamba taarifa zinapatikana kupitia RTD na wakina Uhuru/Dailynews. Zama za utandawazi zinampa raia wa kawaida uwezo wa kupata habari anayotaka na kwa muda anaoutaka yeye.

Bei ya hizi machine ni wizi mtupu na TRA wanataka kuleta maujanja kwenye huu ulanguzi. Hata hapo Kenya, pamoja na unyang'au wao, watu wanauziwa machine kwa bei nafuu. Hizi za TRA zina almasi ndani yake?

Kumbuka, kama kuna watu wanye uwezo wa kufuatilia bei za hizi machine basi wafanyabiashara wa Kariakoo watakuwa wa kwanza. Kila kukicha wanaenda China kununua bidhaa, wanajua hizi machine zinauzwa bei gani, leo hii mtu mzima anasimama na kuwaambia machine laki 8?

Na hata kama TRA watakuja na kisingizio kwamba wao wanatumia models za ghali, bado swali la msingi linabaki, kwanini wawachagulie watanzania machine za ghali? Hivi ni kweli machine zinazouzwa na TRA ni za viwango vya juu sana hivyo kufanya bei ya sasa kuwa sahihi?

Mh. Zambi ameongea bungeni baada ya kufanya uchunguzi binafsi, na anakubaliana na madai ya wafanya biashara kuwa bei za hizo machine si sawa. Kwanini TRA wanaendelea kungang'ania huu ulanguzi? Na kwanini waziri wa Fedha anakuwa bubu? Si ajabu huyu waziri na mawani yake wala hana habari ni kiasi cha fedha Tanzania imepoteza kwa kufunga maduka? Uchumi hauendeshwi kwa mtindo huo!
 
NasDaz

JF-Expert Member
May 6, 2009
11,275

Hoja ya kwamba bei ni kubwa hata mimi nakubaliana nayo lakini tatizo wafanyabiashara wenyewe hawana kauli moja kuhusu ni kwanini hasa hawataki hizi mashine!!! Hizi kauli mbili mbili ndizo zinazotia shaka; kwamba mara huwezi kumpunguzia mteja coz' hata ukimpunguzia utalazimika kulipa kodi ya original price, ukiongea na mwingine anakuambia kodi kupitia hizi mashine ni nyingi; ukisogea upande wa pili wanakuambia wao hawakatai kulipa kodi na wapo tayari kulipa kodi kwa mfumo wa zamani....ukikutana na mwingine yeye ndo atakueleza suala la bei ya mashine kuwa kubwa!!!

BInafsi, nakubaliana na hoja kwamba hizi mashine bei yake kwa wengi ni kubwa especially kule mikoani lakini tutake tusitake; hizi mashine hata kama ingekuwa zinatolewa bure bado wafanyabiashara wengi wasingezipenda...wabongo tumeshazoea maisha ya ujanja ujanja! Hata wakati LUKU zinakuwa introduced, watu walikuwa wanazipinga ile mbaya coz' walifahamu ule ujanja ujanja wa bili imefikia laki 7 lakini msoma mita unampa elf 20 anakausha; ndo basi tena! Hapa ndipo ulipo msingi wa tatizo; hizi zingine zote ni kutafuta public sympathy!!
 
bulama

JF-Expert Member
Dec 13, 2012
576
225
Kwa hizo mashine zimefungwa kamera ili kujua ni kitugani kimetok na kipi kimeingia? Kama jibu ni hapana wizi utakuwa palepale watauza na hawatatoa risti.
Wabongo tumezoea sana wizi na kukwepa, wafanya biashara wamezoea super profit, kwa vile sasa mashine zitaonyesha kila kitu, nanataka kuzigomea!. Mbona wahindi wanazitumia na hawagomi?!.

Anayelipa kodi ni end user, hivyo anayepaswa kugoma ni mteja baada ya kupandishiwa bei kufuatia wafanya biashara kulipa kodi!, na sio wafanya biashara wagome kuuza, kisa kodi iko juu!. Huu sasa ni mwanzo mzuri wa hivi vibiashara mchoro mchoro vifungwe zibaki biashara halali tuu!.

Kwa upande wa EFD, nako ni wizi mtupu!, mashine inauzwa dola 100, hapa unauziwa dola 1000!.
Ukiamua kununua mwenywe, wale maajent wa TRA hawakubali ku install!.
Mijimashine yenyewe approved kwa Tanzania yote inatumia windows only kwa sisi tunaotumia mac, tunalazomika kununua computer ya window kwa ajili ya EFD tuu!.
Huu pia ni nyanyasaji!.
Pasco.
Pasco.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom