Kama umekuwa ukivutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) sababu ya kodi inayotokana na uandaaji wa hesabu za shule au chuo chako…Basi soma mpaka mwisho…
UKWELI USIOPINGIKA…Zipo shule pamoja na vyuo mbalimbali hadi leo hii wamelemewa na madeni makubwa yatokanayo na kodi kutoka TRA. Hili siyo kosa la TRA bali tatizo linaanzia kwa shule/vyuo husika kutokana na aina ya uandaaji wa hesabu zao zinazotokana na utunzaji mbaya wa kumbukumbu zao.
Ukumbukwe kuwa biashara ya kuendesha shule/chuo zilizo nyingi zinaendeshwa kwa mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali za kifedha. Hivyo basi kutozingatia sheria za kodi utakuwa unaiweka shule au chuo hali ya hatari ya kufirisika.
Kwa mujibu wa kifungu namba 117 (1) sheria ya kodi ya mapato, 2004 (R.E 2023) kila kampuni, biashara ya ubia na biashara binafsi wanawajibika kuandaa hesabu na kuziwasirisha TRA ndani ya miezi sita tangu mwaka kuisha.
kupitia Makala hii wewe kama mmiliki wa shule/chuo utapata faida hizi;
(a). Makala hii inakupa mwongozo wa kuandaa hesabu za shule yako kwa ufasaha, kwahiyo utaweza kuepuka riba na faini ambazo ungelipa TRA, inamaana hela ambayo ungelipa kama faini utaitumia kuwekeza kwenye miundo mbinu ya shule/chuo.
(b). Itakusaidia kufahamu wapi kuna viashiria vya hatari kwenye shule au chuo, kwahiyo itakuwa rahisi kufahamu wapi pa kuboresha, inamaana ufanisi wa shule au chuo utaongezeka dhidi ya washindani wako sokoni.
(c). Itakupunguzia mgogoro na TRA, kwahiyo utatumia muda wako kujikita ktk kusimamia shule yako, inamaana mapato ya shule yataongezeka maradufu.
(d). Itasaidia kuwajengea uwezo wafanyakazi wako wa kitengo cha uhasibu, kwahiyo utendaji wa usimamizi wa fedha utaongezeka, inamaana itakupunguzia kulipa riba na faini zisizo za lazima kwenda TRA.
NI KAMA BAHATI KWAKO…Hizi ndo njia salama zitakazokusaidia kuandaa hesabu zako ambazo zitaiweka shule yako salama na katika mazingira rafiki ya kiushindani sokoni dhidi ya washindani wako…Soma makala hii MPAKA MWISHO
Mauzo kwenye EFD mashine dhidi ya jumla ya ada,usafiri, mauzo ya uniform na bidhaa nyingine zinauzwa hapo shuleni/chuoni.
BY THE WAY….Unaweza kuwasiliana nasi na tukakusaidia kupata mwongozo namna ya kufuata sheria za kodi ili shule yako iwe kwenye mikono salama ya uwendeshaji. Unachoweza kufanya tuma ujumbe sasa hivi kwenda 0752187434 au info@halaconsultants.co.tz.

- Hakikisha unapoandaa hesabu zako, mauzo ya kwenye mashine ya EFD yawe sawia na jumla ya mapato yatokanayo na ada, usafiri na mauzo ya uniform ambayo yataonekana kwenye hesabu zako. Kwa mjibu wa kifungu namba 86 (1) sheria ya usimamizi wa kodi, 2015 (R.E 2023), endapo kutaonekana kuna tofauti utatozwa riba ya 20% ya thamani ya huduma uliyotoa au Tshs 2,000,000 lakini isiyo zidi 20,000,000 na itachukuliwa ambayo ni kubwa kwa kosa la kutotumia EFD machine inavyostahili.
- Kifungu namba 11 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 inamtaka mfanya biashara kudai na kutoa risiti ya manunuzi au mauzo atakayo fanya. Sambamba na mabadiriko ya kodi ya 2024 ya kifungu husika, inasisitiza kuwa ili manunuzi (gharama) zako zikubaliwe kupunguzwa kwenye mapato ya biashara yako lazima yaambatanishwe na risiti za EFD tofauti na hapo manunuzi yatakataliwa na kutozwa kodi 30% (corporate tax). Kuna yale manunuzi yanayopatikana kwa wauzaji wasiotumia mashine za kielektroniki kama nyanya, vitunguu, mchicha na mengineyo hakikisha unaifadhi taarifa za manunuzi yake kwa usahihi ili wakati wa ukaguzi wa TRA iwe rahisi kutambulika.
- Wakati wa kuandaa hesabu za shule/chuo hakikisha unaweka bayana taarifa za mikopo, kitakachoonekana kwenye hesabu zako ni lile deni la mkopo lililosalia, hii ni kwa mjibu wa kifungu namba 12 (1) (a) sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004. Endapo hutaanisha mikopo yako kwenye hesabu, na TRA wakafanya uchambuzi wa kifedha (cash analysis) itaonesha kuna pesa imeingiza kwenye mzunguko wa shule au chuo lkn haijulikani imetoka wapi. Mwisho TRA wataitafiri hiyo pesa kama ni ada ambayo hukuitolea risti za kielektroniki na itapigwa kodi 30% na kupigwa faini sambamba na kutozwa riba.
- Mishahara inayolipwa kwa walimu na wasaidizi wa kazi hakikisha kiasi husika kimelipiwa PAYE, WCF na NSSF. Vile vile hakikisha unafanya ulinganifu (reconciliation) kati ya mshahara ulioneshwa kwenye hesabu zako pamoja na zile ambazo ulifanya marejesho (return) za PAYE kwenye mfumo wa TRA (Taxpayer’s portal). Kwa mjibu wa kifungu namba 7 (2) sheria ya kodi ya mapato, 2004 kile apatacho mfanyakazi toka kwenye ajira yake inatakiwa kulipia kodi ikiwa mshahara wake unaanzia Tshs 270,000.
- Kuna mali kama majengo, viwanja, samani, komputa na vinginevyo vinavyomilikiwa na shule/chuo, hakikisha taarifa zake ziwe ktk mpangilio wa wazi ujulikanao kama rejista ya mali zisizohamishika. Kuna baadhi ya uongozi wa shule/chuo wanapenda kuwatumia fundi John ktk ujenzi wa majengo au samani za shule/chuo ambao hawatoi risiti za EFD hupelekea kuwa vigumu kupata thamani ya mali hizo. Kama thamani ya majengo au mali zingine hazifahamiki, shule/chuo inaweza kufanya uthamini (valuation) ili kupata thamani ya sasa ya mali hizo ambayo itaioneshwa kwenye hesabu za shule/chuo.
- Kama kuna watoa huduma uliwalipa kwa mwaka wa fedha 2025, mfano wa huduma ni kama ukaguzi (audit), ushauri wa kodi, ushauri wa kisheria, ulinzi, kampuni za usafi, ukarabati na matengenezo na huduma nyingine hakikisha kwenye malipo hayo unakata 5% kabla ya VAT. Hii ni kwa mjibu wa kifungu namba 106 sheria ya kodi ya mapato sambamba na aya ya 4 ya kipengele kikuu (First schedule).
- Katika shughuli za usimamizi wa shule/chuo kuna wale wakurugenzi (Non-executive directors) ambao hawashiriki ktk shughuli za kila siku za uendeshaji wa shule/chuo, endapo shule inaamua kuwalipa gharama za usimamizi wa baadhi ya shuguli za kuutendaji hakikisha umelipia kodi ya zuio ambayo ni 15% ya gharama ya malipo hayo.